Zitto alipuka posho za wabunge kuongezeka kimya kimya

[h=1]Zitto na Demokrasia[/h] Zitto na Demokrasia

[h=2]Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi[/h] with 9 comments
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho. Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.

Tukumbuke hapo hapo cdm Joseph selasini anataka posho iongezwe halafu shibuda akitaka posho iongezwe watu wanakaa kikao wanataka kumfukuza lakini kwa selasini hamna kikao wala nini wacheni unafuki cdm
 
Hiyo 200000 kwa siku wangepeleka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.hii sio haki na wengi wao wanasinzia tu.serikali iwe makini .kuna watu wanajali matumbo yao tu.
 
Katika hili nakuunga mkono Zitto kwa 100%. Chama kiende mbele na kukemea tabia ya wabunge kama Selasini wanaolia kuwa mshahara na posho za wabunge ziongezwe. Tunataka kujenga chama ambacho watu wanaweza kuona kuwa kweli kinaweza kuwakomboa.
 
hivi Zitto si aliacha kuchukua posho hizi, vile vile nakumbuka na CDM walikataa. status ikoje kwenye kikao kilichoisha?
 
Suala hili la posho za wawakilishi wetu kamwe haziendani na dhana ya uwakilishi,kwa kiongozi yoyote anaye wakilisha wananchi wenzake,ni lazima avae viatu vya wale anao wawakilisha,Taifa la Tanzania lina wananchi maskini ambao ndiyo asilimia kubwa ya Taifa zima.
Hivyo suala la umaskini wa wananchi halijalishi itikadi ya chama chochote cha siasa,kwa maana ya kwamba hakuna mbunge anaye wakilisha matajiri jimboni kwake bali wananchi.
Nina pata picha mbaya kwamba kumbe Itikadi za Vyama vya siasa na wabunge wake huwa zinakuwa sawa pale ambapo hoja inayo wasilishwa inakuwa inahusu Mswaada wa Maisha ya ubunge wa kifalme,maisha ya anasa ya kibunge katikati ya kilindi cha mskini,hapo naona itikadi sawa,hoja sawa,hakuna walk out ya kukataa posho,hakuna walk out ya kukata ongezeko,no!!!no!!!!!!!!!no!!!!!!!!!!!
Ninategemea chama changu kitoe msimamo wa vitendo,nategemea chama changu kiitishe maandamano kupinga maisha ya ufalme ya kibunge juu ya anasa hizi katikati ya umaskini wa kiuwiano wa vipato,kama wabunge wanawawakilisha wananchi mbona sioni kama wana uchungu na vipato vya wananchi wao?walimu,madaktari,hospitali,shule,ajira kwa vijana,hizo nyongeza wange zikataa zingewasaidia vijana wasio na ajira wanao hitimu vyuo kila uchao.
Haya ndiyo mambo ya wabunge wangu kuyasimamia kwa kujipeleka gerezani kupinga malipo ya ufalme na siyo vinginevyo.
Nina udhika na kukemea siasa za ujima,siasa za usaliti,siasa za uzandiki,sitegemei wabunge wa chama kikuu cha upinzani nchini kuingia kwenye mkumbo wa ufisadi wa anasa za kifalme,sasa tutasimamia uwajibikaji wa kiitikadi,uwajibikaji wa kisera na uwajibikaji wa kimfano katika kuwa na uchungu na maisha ya watanzania wenzenu.
Kadinali pengo aliwahi kusema isiwe tukawa tunachukia ufisadi eti kwa sababu tunawaonea wivu wanao faidika na ufisadi kwa sababu hatuna fursa hiyo,.Sasa hatuwezi tukaikemea serikali katika kukalia maisha ya anasa kwasababu pengine ya wivu wa uroho.
Natoa wito kwa wale wote walio viongozi,wanachama na mashabiki lakini kikubwa wazalendo wa kitanzania tuwakatae wale wanaokomba posho hizi,kwasababu hiyo siyo sera ya chama cha Demokrasia na Maendeleo[CHADEMAS],Mtu anaye kwenda kinyume na hiyo ashughulikiwe.
 
Watanzania tumekuwa wabinafsi, kila mtu anajiangalia mwenyewe tu lakini maandiko yamenena siku za mwisho watu watakuwa ni wenye kujipenda wenyewe na wenye kupenda fedha, wabunge nao ni watu....
 
Unajua huu unaweza kuwa mtego toka kwa muhimili wa executive kwenda kwa Bunge au lah ni namna moja ya kunyamazisha hasira za wabunge juu ya serikali na madudu yake.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
[COLOR=#00ff00 said:
Nyani Ngabu[/COLOR];2897412]Zitto anatafuta sifa tena.


kwa hiyo wewe ulitaka afanyeje...??? huwa nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri
 
Bwana zito kabwe amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa anamwomba katibu mkuu wa chadema Dr. Slaa kuitisha kikao cha dharura kulizugumzia swala hilo la posho kupandishwa kinyamela kwa kuwa sera ya CDM ya mwaka 2010 inakataa posho kubwa za watumishi wa serikali. Zitto amesema watajadili hizo posho na kutoa tamko kwani posho za wabunge zimepanda kimya kimya.

Hivi wale wanaotajwa tajwa kuutaka Uprezidaa, nao wamelamba posho hii mpya? nazungumzia EL na Mamba!

 
hii serikal c sikivu kabisa serikal inayoendeshwa kwa mabavu nchi ya watu maskin leo mshaarA kwA watumish wanalilia at least frm 135000 to 300000bt wameongeza sh 15000yani sasa ni sh 150000 bt wao watunga sheria wanajongezea kwa kufullu nw posho yA cku moja ni mshAara wa mtu hii c dhalau ipo cku isio nA jina vilio vya maskin mungu atavisikia
 
Unajua huu unaweza kuwa mtego toka kwa muhimili wa executive kwenda kwa Bunge au lah ni namna moja ya kunyamazisha hasira za wabunge juu ya serikali na madudu yake.

Mkuu nami nimefikiri juu ya hilo wazo. Pengine serikali imeamua kuwalisha unga wa ndele wabunge ili wazidi kuwa mazezeta katika kuisimamia serikali. Na serikali inaelewa kwamba wengi wa wabunge wapo bungeni kimaslahi binafsi zaidi; hivyo ongezeko la posho kwa asilimia zaidi ya 100 ni furaha kwa wabunge wa aina hiyo.
 
ama kweli chadema munafahamu kutukana, mmemshambulia hapa nyani ngabu kwa matusi ya kila aina.....!!

Basi na mimi nasema tena kuwa zitto zuberi kabwe anatafuta sifa.

Sasa anayejua kutukana anitukane tuone maana atakuwa hana akili na busara kwa kutukana kwake.......!!!
 
ama kweli chadema munafahamu kutukana, mmemshambulia hapa nyani ngabu kwa matusi ya kila aina.....!!

Basi na mimi nasema tena kuwa zitto zuberi kabwe anatafuta sifa.

Sasa anayejua kutukana anitukane tuone maana atakuwa hana akili na busara kwa kutukana kwake.......!!!

Unaposema anatafuta sifa ainisha basi ni katika nadharia ipi? Eleza kiufasaha sio kuropoka ru zungumza unishiwishi nikuelewa
 
Back
Top Bottom