Zitto, akiwasilisha ushahidi, Serikali itakubali kujiuzulu?

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
Zitto, alituhumu Baraza la Mawaziri kushawishiwa na watu fulani ili kulifuta Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa faida ya wachache ambao wana maovu yao katika taasisi za fedha na wengine kesi zao zipo mahakamani zikiendelea. Kimsingi suala hili lililoibuliwa na Zitto ni zito sana. Na halipaswi kujibiwa 'kishabiki-shabiki'. Yanahitajika majibu ya kina na yenye upana wake kwa upande wa Serikali.

Tuhuma hizi si za kubezwa hata kidogo, nisingependa wabunge hasa Spika wao, Anne Makinda, aizime kwa stahili aliyoizoea hasa katika masuala yanayoonekana kuiweka pabaya serikali.Watanzania tumeelezwa kwamba Baraza la Mawaziri limeshawishiwa na watu fulani ili CHC linalokusanya madeni life na wachache wenye madeni waendelee kunufaisha matumbo yao bila kujali athari za jambo hilo kwa taifa.

Ingawa sina ushahidi wa hili, lakini sipingi hata kidogo hoja hii ya Zitto. Huenda ni kweli Baraza letu la Mawaziri chini ya mwenyekiti wake, Rais Kikwete limeshawishiwa kutaka hili shirika life ili watu wachache 'watunishe matumbo yao'.

Zitto, kwa nafasi aliyonayo ya Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, na Waziri Kivuli wa Fedha, inawezekana anachokisema ni sahihi ingawa sina uhakika katika hili.

Lakini kulingana na 'harufu chafu' inayolikumba taifa na Serikali yetu ya 'ufisadi’, jambo hili nina hakika litafungwa fungwa na Watanzania tusielewe ukweli wa jambo lenyewe.Kama huyu Msajili wa Hazina ameshindwa kuyashughulikia mashirika 25, inakuwaje apewe mashirika mengine kuyashughulikia? Ni vipi hizi hati za mashirika mbona hana?

Nikimnukuu tena Zitto hapa tulimsikia bungeni akisema kwa uchungu mkubwa kwamba: “Nasisitiza kwamba Baraza la Mawaziri limepitiwa na kufanyiwa lobbying (ushawishi). Ila, ninachosema ni wabunge kuwa makini na kutokubali kupitisha azimio hili kwa kuwa tunawapa ulaji watu.”Spika huyu ametoa agizo hili kwa Zitto lakini ameshindwa kuuleza umma juu ya ushahidi aliopelekewa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambaye alimtaka ampe mwongozo wa nini kinaweza kufanywa na mbunge iwapo amebaini kuwa waziri mkuu hakusema ukweli bungeni.

Makinda inaonekana kakalia ushahidi huo kwa masilahi anayoyajua yeye, Watanzania tunatakiwa majibu kwa kila jambo linalotokea bungeni.
......... JE SPIKA ATAKUBALI ZITTO KUTOA USHAHIDI MAONI YAKO TAFADHALI.....
 
......... JE SPIKA ATAKUBALI ZITTO KUTOA USHAHIDI MAONI YAKO TAFADHALI.....

Makinda anaweza kupewa ushahidi wote anaotaka, ngoma ni kuuweka hadharani. Tunasubiri hukumu ya ushahidi wa Lema sijui watautoa lini hadharani.
 
Nafikiri ushahidi wa ukweli ndio umfanya mtu kuwa huru. Vithitisho ndio ushahidi tosha hivyo tusubiri maana ushahidi huwasilishwa palepale bungeni.
 
Back
Top Bottom