Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

Timbilimu ulikuwa hujui kuwa nchi yetu iko mikononi mwa mafisi? Pale bungeni ni sawa na gulio la Katerero ambapo kila mtu huanika vyake na kuuza kwa bei yake. Tumo msambweni na tusipoamka na kujikomboa kama wenzetu wa Misri Libya na Tunisia tutaendelea kuumia sana na kudanganywa na hawa wachumia tumbo wanaowakilisha mtumbo yao kwa kisingizio cha kutuwakilisha. Ukitaka kujua tuna balaa gani rejea maneno ya mbunge wa Rombo Joseph Selasini aliyedhukuriwa akisema, "Mheshimiwa mwenyekiti baadhi ya makampuni ya mafuta yalikuwa hapa Dodoma na kutoa chochote kwa wabunge na hili si kwa upande wa serikali ya CCM bali wabunge wa pande zote tukiwemo wapinzani. Msione watu wanazungumza kwa nguvu hapa kutetea, hawa wamepewa chochote,”
 
Nadhani huu ni uamuzi wa busara sana badala ya kusubiri maneno yazidi kukua ni vizuri kumaliza udhia mapema.
Nadhani sasa sekretariati imepata mengi kutoka kwake na hivyo kuinufaisha sana kamati kuu itakapokutana kwa ajili ya kutafakari tuhuma hizo dhidi yake.

Narudia tena kumshauri kamanda Zitto ajiepushe na tabia ya kupenda kuwa msemaji wa kila kitu kinachojitokeza mbele yake, afanye hivyo pale anapolazimika tu. Kama anajitambua kwamba yeye ni "presidential hopeful" lazima ajilinde kwa kauli na matendo yake. Hii vita baridi ccm wanayopigana nae yeye hajaijua kwakuwa wamekuwa wakimpamba na yeye akaanza kujisahau kumbe walikuwa wanamlia timing wammalize.

Kutoa maelezo ni hatua mojawapo ya kuanza safari ya uwajibikaji

Tuhuma hizi zikiendelea kuaminika haimchafui Zitto peke yake bali chama kizima kinakosa moral authority ya kukemea ufisadi.

Naamini he's innocent hadi hapo hiyo tume ya kuchunguza itakapotoa ripoti.Hatuwezi kupigia kelele kuhusu kuhongwa kwa wengine halafu sisi ya kwetu yawe upako.
 
kama Zitto alipokea fedha za Rostam itakuwa ngumu sana kujinasua nakumbuka Mtikila na yeye alipokea mchango wa Rostam kwa ajili ya kanisa lake Rostam alikuja kumuanika wazi mpaka leo Mtikila haongei kitu kuhusu Rostam anyway ngoja tumsikilize hiyo kesho atasemaje huyo Zitto
 
dr slaa ni mmoja wa wanaosemekana kuusaka urais 2015
je zitto ana imani dr slaa anaweza kuongoza sekretarieti? ukizingatia wanaomchafua zitto ni wabunge wapenda posho na wasaka urais kutoka vyama vyote, (hii ni kutokana na maelezo ya zitto mwenyewe)

Zitto ana imani sana na Katibu mkuu wake Dr. Slaa na ndio maana yeye(zitto) ameomba kuonanana naye na kuzungumza naye. Bahati nzuri Chadema hakuna mambo ya kukolimbana kama huko kwenu thatz why zitto amekuwa na jeuri ya yeye mwenyewe kwenda kutoa maelezo kwa kiongozi wake wa chama.

Mambo ya uraisi sio hoja ya msingi kwa sasa, hususan muda huu tunapotaka kuona bunge likijisafisha na tope la rushwa pamoja na makandokando yake.
 
Last edited by a moderator:
Zitto aache kutapatapa asubiri majina yakiwekwa wazi kule mjengoni ndo aseme. Mbona anapaniki hivyo?
 
Unajua kama Nilivyowahi kusema ya Kwamba imeshaonekana Kuiangusha Chadema ni kupitia a weak link na ikaonekana ni Zitto baada ya Marehemu Chacha...Kwanza wakajaribu sana kumkosanisha na Mbowe, Ikashindikana ila kuharibu mahusiano yao wenyewe lakini haikukigawa chama.

Ya pili wakamtumia tena Zitto ktk Ukaskazini na Udini ikafanya kazi kubwa sana na lawama zikaanza kuingia vichwani mwa watu lakini ajabu chama ndio kikapata umaarufu zaidi ujio 2010..Baada ya kushindwa kote njia nyingine imejitokeza ambayo ni Zitto mwenyewe kuwa sababu achukiwe ndani na pengine kujitenga na chama hivyo kuwagawa ktk makundi mawili. Na hakika hii imeonekana inafanya kazi maana kweli Zitto anachukiwa na wanaChadema. Naye anaanza kuamini kama hana nafasi ndani ya Chadema na wanaChadema nao wanafunga uwezekano wa Zitto kufikia ambition yake.. In fact it's working japo very slow lakini inafanya kazi..

Halafu, Zitto hana makosa kujibu tuhuma hizi mbona Dr.Slaa alikuwa akizijibu nyingi tu hadi wakaenda personal na watu walikuwa nyuma yake hata kaa wanajua kweli tuhuma ni nzito...Kwa nini Zitto asijibu, isipokuwa kosa la Zitto ni kutojipanga nyuma ya chama ktk majibu yake. Kila kitu anachukulia personal kama wanavyotaka, badala ya kutumia kofia ya chama kujikinga. Niliwashtua both Zitto, Mbowe na Wanachamema hapa toka mwaka 2009 lakini watu hawaniamini.. Ninaujua mji wa Dar kama kiganja cha mkono na najua mengi yanayofanyika nyuma ya pazia japo niko nje ya nchi.

Hii tabia ya Zitto kujifanya independent (kwa sababu haamini mtu) wakati akitumia jukwaa la CDM ndio inayomweka bayana zaidi kisiasa. Anatakiwa kujifunza zaidi siasa, maana ndipo imani na uzalendo huanzia ili mawazo binafsi kuongoka. Let them say maadam mnaelewa malengo yao, nia zao haitawaumiza vichwa..

Mkuu Mkandara sijui ni Kwa nini CDM na Vijana wa CDM hawapendi kusoma Busara zako hizi. Mabandiko yako ni Moja ya Mabandiko ambayo hayapendwi kabisa na CCM kwa Sababu wanatambua kwamba siku CDM wakikiuelewa Basi CCM watakimbia hapa jamvini. Ndio Maana nikauliza kwamba Thread ya Wabunge kutuhumiwa na Rushwa haikuwavutia Rejao, wala Ritz wala Zomba.

Mwenye Macho haambiwi Tazama
 
Last edited by a moderator:
Unajua kama Nilivyowahi kusema ya Kwamba imeshaonekana Kuiangusha Chadema ni kupitia a weak link na ikaonekana ni Zitto baada ya Marehemu Chacha...Kwanza wakajaribu sana kumkosanisha na Mbowe, Ikashindikana ila kuharibu mahusiano yao wenyewe lakini haikukigawa chama.

Ya pili wakamtumia tena Zitto ktk Ukaskazini na Udini ikafanya kazi kubwa sana na lawama zikaanza kuingia vichwani mwa watu lakini ajabu chama ndio kikapata umaarufu zaidi ujio 2010..Baada ya kushindwa kote njia nyingine imejitokeza ambayo ni Zitto mwenyewe kuwa sababu achukiwe ndani na pengine kujitenga na chama hivyo kuwagawa ktk makundi mawili. Na hakika hii imeonekana inafanya kazi maana kweli Zitto anachukiwa na wanaChadema. Naye anaanza kuamini kama hana nafasi ndani ya Chadema na wanaChadema nao wanafunga uwezekano wa Zitto kufikia ambition yake.. In fact it's working japo very slow lakini inafanya kazi..

Halafu, Zitto hana makosa kujibu tuhuma hizi mbona Dr.Slaa alikuwa akizijibu nyingi tu hadi wakaenda personal na watu walikuwa nyuma yake hata kaa wanajua kweli tuhuma ni nzito...Kwa nini Zitto asijibu, isipokuwa kosa la Zitto ni kutojipanga nyuma ya chama ktk majibu yake. Kila kitu anachukulia personal kama wanavyotaka, badala ya kutumia kofia ya chama kujikinga. Niliwashtua both Zitto, Mbowe na Wanachamema hapa toka mwaka 2009 lakini watu hawaniamini.. Ninaujua mji wa Dar kama kiganja cha mkono na najua mengi yanayofanyika nyuma ya pazia japo niko nje ya nchi.

Hii tabia ya Zitto kujifanya independent (kwa sababu haamini mtu) wakati akitumia jukwaa la CDM ndio inayomweka bayana zaidi kisiasa. Anatakiwa kujifunza zaidi siasa, maana ndipo imani na uzalendo huanzia ili mawazo binafsi kuongoka. Let them say maadam mnaelewa malengo yao, nia zao haitawaumiza vichwa..
Mkuu umelenga penyewe,siasa ina mbinu nyingi sana hasa katika nchi zenye demokrasia changa.Ikumbukwe kuwa nchi yetu ndiyo imeingia kwenye siasa za ushindani,hivyo vitu vingi vinafanywa kwa majaribio.Katika hali kama hii,kuna wanasiasa wengine wanatumia mbinu za kificho na hila kuharibu wapinzani wao.Nimefuatilia mwenendo wa kisiasa wa nchi yetu hasa kutokea suala la Buzwagi lilipoibuliwa bungeni na Zitto.Baada ya hapo likafuatia suala la ufisadi lililoibuliwa mwembeyanga tarehe 15 Septemba,2007.Baada ya hapo lilifuatia suala la Richmond na kusababisha serikali kuvunjika.
Inaelekea wapanga mikakati wa CCM walikuja na mipango mingine ikiwa ni pamoja kuwakaribia kwa njia za hila viongozi wa CHADEMA ili kudhoofisha mshikamano wa viongozi.Njia hii ilitumika kwa mbinu za hali ya juu ambazo wanachama na viongozi wa CHADEMA walishindwa kubaini mapema kuwa ni mkakati wa kuwachonganisha ili wasiaminiane.Mtindo huu hujitokeza kwa kumkaribia Kiongozi mmoja mmoja na kumpa sifa za kumlewesha ili ajione ni muhimu mno kuliko chama kama jumuia na kutumia baadhi ya wanahabari.Katika hali kama hii inatokea sintofahamu na wanachama kumtenga kiongozi na hatimaye mahasimu wake kumshambulia kirahisi na kumhujumu kisiasa.
 
wale waroho wa posho bungeni kina selasini na kundi lake,wapenda rushwa kina msigwa na kundi lake ndio wanaoinjinia hii ishu ili kamanda zitto achafuke,tumewashtukia mchezo wenu mchafu,waelewa wa mambo bado tuna imani na zitto.l
 
Zito umeshauriwa sana, chukua huo ushauri ufanyie kazi. Safari yako bado mbichi tawala tamaa zako na uwe na kiasi.

Kuhusu wewe kula rushwa, hii imesemwa sana tangu mapema sana lakini kwa wakosoaji wako (ambao wewe unaona maadui zako) wewe ni kama bata mzinga anayeficha kichwa wakati uchi ameufunua, lakini bado kuna walio na imani na wewe. Sasa safari hii namna ya kuponyoka binafsi ni vigumu sana bila msaada kutoka magongoni.

Mimi ningekushauri uwe mwangalifu sana hasa katika maneno yako, na kama utaamua kuzungumza jibu hoja na wajibu wote waliokutuhumu kama una weza au kaa kimya. Ulalamishi wa kusema kuwa wanakuchafua, eti posho, eti urais hiyo inawafanya wengi wachukie zaidi jibu hoja siyo sababu.

Zaidi mwombe rafiki yako Pasco wa jamii forums akushauri lakini akubali akuambie ukweli asikupake mafuta kwa mgongo wa chupa.

Hata hivyo unanafasi kubwa ya kujificha na hata kushinda kwa vile CCM na serikali yake na hasa mkuu wa kaya hatapenda suala hili liendelee na hasa ikuguse wewe. Japo majeruhi wa mtandao watapenda iendelee na wazalendo.

Ninaamini kuwa hili suala litachakachuliwa na CCM mafisadi ili kipande kiwageukie maadui zao na hasa CDM.
Tusubiri tuone itakuwaje
 
I find almost everything with Zitto to contain some itching elements. In fact some takes it as genius while others consider it hypocrisy.

Myself, I hope he's not in it. Zitto need to be provided with every opportunity of a fair hearing.

I want to deduce my conclusions from such a process.
 
Freema una akili sana najua jf siku hizi kumeingiliwa na waimba mduara huwezi amini kama hii ni web page ambayo ilijengwa na sifa njema na busara za wanachama bt nw napata shaka watu wa facebook.com wamesha kuja huku. Watu wanahukumu bila ushahidi tuhuma hizo ni ndogo kwa zitto najua wana jf hawa wanao mtuhumu leo kesho atakuwa ndio shujaa wao go go zito
 
Cwezi kujudge ila kilichonitia hasira ni hili la kuagiza vipuri vya Pound elfu 50.. Kilichowafikia TANESCO ilikuwa magunia ya MISUMARI... Achilia mbali hili la kuvuna nguzo IRINGA na kuzipeleka MOMBASA kisha zinarudi BONGO zikiwa zinanesha zimetokea kwa WAZULU...
Kuuza mafuta..na kufunga mitambo ya GAS ili wafanye BIASHARA.... Mmmh!!! Ctaki cma cna
 
Mkuu Mkandara sijui ni Kwa nini CDM na Vijana wa CDM hawapendi kusoma Busara zako hizi. Mabandiko yako ni Moja ya Mabandiko ambayo hayapendwi kabisa na CCM kwa Sababu wanatambua kwamba siku CDM wakikiuelewa Basi CCM watakimbia hapa jamvini. Ndio Maana nikauliza kwamba Thread ya Wabunge kutuhumiwa na Rushwa haikuwavutia Rejao, wala Ritz wala Zomba.

Mwenye Macho haambiwi Tazama
Mkuu wangu sielewi kwa nini inatokea hivi. Nimejaribu sana lakini naaminishwa kwamba Zitto ni mzigo habebeki japokuwa zote hizi ni tuhuma ambazo hazina ukweli isipokuwa kwa reaction ya Zitto dhidi ya madai na kwa kujua udhaifu wake hawachoki kumchokonoa wakijua Wanachadema wataamini maanake ndiye the weakest link. Zitto ni mtu wa Action na anazipenda Actions kwa sababu ndipo ukweli hupatikana. CCM ni mabingwa wa kupika fitna tena hujisifia na kupongezana wanapoona mdudu kaingia ndani ya kokwa..

Ni kazi kubwa sana kwa Wadanganyika kutoa tongo ikiwa hakuna maji..Ni vigumu kufikiria kilimo kama hakuna mvua na Ndivyo Tulivyo. Kinachonisikitisha tu ni kwamba imefikia mahala watu wote ndani ya Chadema wamefikia kusema - NA LIWALO LIWE!...

Kuna makosa mawili makubwa sana yanayofanywa na Chadema hivi sasa ktk ulinzi wa chama kisiasa. 1. Udini 2. Zitto. Hizi ndio sehemu ambazo ngome ya Chadema imelegalega, hawakuweka majeshi ya kutosha. wakishambuliwa ktk Udini halafu ukisikia majibu ya Wanachadema wakitupa pinde za mishale, nasema sii rahisi kabisa kwa mtu aliyeko nje kutoamini kuna Udini mkubwa ndani ya CDM. Watu wengi sana wanakiogopa chama hiki kutokana na tuhuma hizi maana imetafutwa sehemu dhaifu na kuishambilia japokuwa hawana ushahidi na wala hawahitaji ushahidi maana majibu yao tu yanatosha. Japokuwa hoja hii ililengwa kupoteza kura za Dr.Slaa ktk uchaguzi mkuu wa 2010, lakini sasa hivi imekuwa mdudu ndani ya kokwa..

Pili, upande wa Zitto ukisikia lawama zake halafu jinsi Zitto mwenyewe anavyojitetea, lazima utaamini Zitto ni mharibifu na inatokana na Mazingira yaliyojengwa. Yeye mwenyewe kwanza hujitenga na lawama za chama kutokana na picha alowekewa usoni..Muda wote sasa vita kubwa ya Zitto it's about him against Chama na viongozi wake na sio CCM na viongozi wabaya. Na maadam wamemtenga ktk hili huwa haogopi upweke pale anapofikiri anasimamia haki hata kama inatoka kwa shetani, kisiasa hii anajichimbia kaburi na kuongeza wigo na utengano.

Ni rahisi sana kwa mtu kusema mbona Zitto hakuwepo Arumeru au mbona Zitto hakufanya hili ama lile pasipo kujua kwamba Zitto mwenyewe haaminiki sasa kweli ataalikwa Arumeru? Na kwa kutomwalika Zitto akichukia, ataona mbona kuna vikao muhimu vya chama haalikwi?.. inaanza kumjaza ujinga kwamba hapendwi na hapendwi kweli kwa msimamo wake as independent. na wakati huo huo anaamini chama hiki kina wenyewe na imani hiyo inaongeza mtengano.. Hapa Mshindi ni CCM, na kusema kweli sina hakika kama tutafika 2015 salama kama tusipojipanga mapema sana kuweka tofauti zetu pembeni na kuhakikisha chama kinajilinda ipaswavyo ktk sehemu hizi mbili.
 
Ndugu wana Jf
Ni takribani siku ya 5 sasa uvumi wa Mh.Zito zuberi kabwe Mbunge tegemeo/bendera ya chama anayewakilisha Jimbo la Kigoma kaskazini kuhusishwa na Upokeaji wa rushwa ndani ya kamati yake(POAC).
Sakata lote hili ni mchezo ulioanza takribani miezi kadhaa tangu uchaguzi wa Wa wabunge wa Afrika mashariki(EALA),Katika uchaguzi huu Mh.zito Zuberi kabwe aliwakamata wabunge wa chadema wakipokea Rushwa toka kwa shy rose Banji na wagombea wengine waliokuwa wanacointest nafasi ya ubunge huo.Wabunge waliokamtwa ni Mh.Peter Msigwa na Joseph selasini wote wa CHADEMA.
Mh.zito nanukuu"ndugu wabunge wenzangu inakuwaje mnapokea rushwa ilihali sisi chadema msimamo wetu nikuzia rushwa na aina yote aya ufisadi" wabunge wale hapohapo hawakuweza kutoa jibu.
Mh.Zito Zuberi kabwe akaona haitoshi akalipeleka kamati kuu ya chama iliyofanyika Mbezi Garden mwezi wa tano akiomba taratibu zifuatwe kwa wabunge waliohusika na kupokea rushwa.
Lakini kwa kushangaza,hilii swala lilipigwa danadana na halikujadiliwa
SASA kuanzia hapo Mh zuberi zito kabwe alijijengea uadui na wabunge hawa.Ulikuwa ni mwendelezo wa chuki ile ya kipindi cha kudai posho Bungeni ambapo Mh zito aliomba kufutwa kwa posho huku Mbunge selasini aliomba kuongezwa kwa posho.
Swala la zito Zuberi Kabwe Kudaiwa anahusika na Rushwa Nyuma yake kunanguvu inayosukumwa na Wabunge wa chadema tajwa hapo juu,wakati huohuo swala la Mh.zito kutangaza kuutaka Urais ndilo linalozidikumjengea maadui wanaodai anahusika na Rushwa
Tujikumbushe hakuna,Sehemu alipotajwa zito kuhusika na Rushwa,hata Leo katika orodha ya Tundu Lissu ya wabunge wala rushwa Zito hayupo.Zito anashutumiwa kwa kumtetea Mhando mkurugenzi wa Tanseco akisimamia kuwa hatua hazijafuatwa.
Kimsingi Hii ndiyo picha halisi,Kuna wabunge wengi na viongozi wa CHADEMA waliomstari wa mbele kuhakikisha Zito anapatikana na hatia,wakti huohuo Mh.zito zuberi kabwe ameiagiza CHADEMA kumfanyia uchunguzi wa kina kubaini shutuma hizo alizobambikiwa.
Zaidi tunaomba Tumsikilize kesho akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Asante,Nitakuja tena,
 
Hii pesa watu hawaridhiki nayo? Ina mana zitto nae ni mla rushwa? Mmmh kama ni kweli basi tena, pesa sabuni ya roho
 
Back
Top Bottom