Zitto ajieleza mbele ya Sekretariat ya CHADEMA kwa masaa 3, kukutana na vyombo vya habari

Hakika ukweli utajulikana na sidhani kama mambo ya urais yana husika hapa!
 
Bado hujaeleza chochote juu ya Zitto zaidi ya udaku.
Na Swai ni nani?
Zitto should watch his steps!
 
swai ni nani hasa? najua Zitto hawezi fanya Press Conference kwani baadhi ya magazeti yameshamchimba na tunamuomba aachane na hayo mavitu yatamharibia hata km atajakuwa mgombea Binafsi anyamaze kwanza mwambieni.
kachokoza mahali Nyeti sana Urais!!!!
 
We kweli mshakunaku, umejuaje kama wenzio hawajalala? ina maana nawe hujalala, unapiga chabo?

Kama hupigi chabo nini mchango wako kwenye hayo mazungumzo?
 
Ambacho unaweza kuwa sahihi ni kuwa zito kuahirisha press conference jana, mengine ni tungo na haiuzi.
 
Hao waliotangulia kutoa maoni wameniwakilisha vizuri SANA. Nashukuru wameonesha METHODICALLY kwamba JF is a place of Great Thinkers.

KWELI CCM MMEFILISIKA! MTAKE MSITAKE KIFO KINAWASUBIRI! R.I.P. CCM.
 
Wandugu,Nipo dodoma kuanzia asubuhi ya leo,Gumzo kubwa la hapa dodoma ni kuhusu press atakayoifanya Mbunge wa chadema Mhh.zitto kabwe hapo kesho kutokana na kuahirishwa kwake hii leo tar:31/07/2012 baada ya kuombwa na kushawishiwa na wabunge wa chadema pamoja na wabunge rafiki toka vyama vingine. Usiku huu hadi nakuja hewani hapa ni kwamba vikao vinaendela chini kwa chini kwa wabunge wa CCM na baadhi wa CHADEMA (nalinda majina yao) vikao vyao vimeanzia wazi maeneo ya canteen za bunge ambapo baadhi ya wabunge wa CCM (WALIKUWA 4) ambao mmoja wao alitajwa jana kuhusika na rushwa wamesikika wakisema ZITO KABWE hata akiundiwa tume na Rais ya kumchunguza hawawezi kuja na jibu lolote la kwamba zito anakula rushwa,kwa sababu watanzania wanaimani naye sana pia amekuwa mtasri wa mbele kusisitiza uzalendo Wakati huohuo nikiwa naelekea dodoma Hotel,nimeongozana na wabunge wa ccm na mmoja wa NCCR wamekuwa wakisisitiza kuwa ZITTO KABWE nachomwa na wabunge wenzake wa CHADEMA kutokana na tofauti zao,mmoja wao akajibu kuwa ZITTO amkuwa tishio kwa sababu ametangaza kuutaka URAIS mapema hivyo basi amefunga milango ya Viongozi wake wa juu kutangaza nia ya Urais ndani ya chama. Hapa nilipo nipo Hitelini ambako kuna baadhi ya waheshimiwa wapo ndani ya Hoteli hii,lakini hawajalala wanaendela na mazungumzo ya kutaka kushawishi zito asifanye press kesho kwa sababu hajatajwa sehemu yoytote kwamba anahusika na rushwa.. Nitaendela kuwajuza,hasa swala la SWAI kuonekana maeneo flani nje ya viwanja vya bunge akiwaagiza wabunge wa chadema kuonana na zitto mapema kabla hajafanya press hapo kesho.sijui Swai anatakakuomba msamaha au la?
Mkuu endelea ku2 update japo hausomeki cijui u miongoni wa waheshimiwa au usalama wa taifa!!https://www.jamiiforums.com/images/styles/JamiiForums/smilies/A S 465.gif
 
hv kwa wenye akili mmekosa mtu wa kumfikiria kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tz mpaka mnawazia zitto? mnafikiri fifa ya urais ni unafiki? hakuna mtu hapo wenye kuona mbali naomba muachane na mawazo hayo.
 
Zitto ahojiwa kwa rushwa

Monday, 30 July 2012 21:02

zitto-kabwe-top-safi.jpg
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe​
Waandishi Wetu, Dar na Dodoma
SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

"Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe," inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.

Lissu ataja wengine
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

Wabunge wengine watatu tumeshindwa kuwataja kwa kuwa hawakupatikana kuzungumzia tuhuma dhidi yao.

Katika orodha hiyo wamo wawili wa Viti Maalumu na mmoja wa jimbo na Lissu alidai kwamba wamekuwa wakishiriki vikao vya Kamati ya Nishati na Madini huku wakijua kuwa wana maslahi binafsi na wengine kutumia fursa hiyo kujinufaisha.
"Kwa takriban juma moja sasa kumekuwa na mjadala mzito wa ufisadi hapa bungeni, sasa Kambi Rasmi ya Upinzani imejitathmini na kuona kwamba wabunge wake hasa walioko kwenye Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, John Mnyika, David Silinde na Mwanamrisho Abama hawahusiki," alisema Lissu na kuendelea:

"Ila uchunguzi wetu umefanikiwa kupata majina ya wabunge wanaohusika moja kwa moja na mgongano wa kimaslahi ambao tunaona tuwataje kwa maslahi ya umma."
Lissu alikwenda mbali zaidi na kutaja tuhuma zinazowahusu wabunge hao akisema wawili ambao gazeti hili halikuwaja, wamejihusisha kufanya biashara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo wana mgongano wa kimaslahi.

Alisema Mwijage ana mgongano wa kimaslahi katika mchakato mzima wa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kampuni ya Puma Energy kwa kuwa yeye ni mtalaamu mwelekezi wa kampuni hiyo inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 50.
"Nasir Abdalah na Mariam Kisangi; Hawa wanamiliki vituo vya mafuta. Sasa kwa namna yeyote ile kuwa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini hawawezi kutenda haki katika mchakato wowote unaohusu suala la mafuta," alisema na kuendelea;

"....(jina limehifadhiwa) hana mgongano wa moja kwa moja wa maslahi, lakini kwa kadri tunavyofahamu, yeye ndiye aliyekuwa akiyafanyia kampeni ya kupata zabuni makampuni ya mafuta ya Oryx na Camel na ....(jina limehifadhiwa), suala lake ni complicated kidogo. Maslahi aliyonayo katika suala hilo ni kuwa ana uhusiano wa Kimapenzi na kigogo mmoja katika Wizara ya Nishati na Madini."

"Hawa ndiyo wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini ambao sisi Kambi ya Upinzani tunawafahamu kuwa ndiyo waliojihusisha na mgongano wa kimaslahi. Tumewaangalia wabunge wetu wote watatu hawamo ila kama kuna mtu ana taarifa zinazowahusu, aseme na tutazifanyia kazi."

Lissu alisema kitendo cha wabunge kujihusisha na mgongano wa kimaslahi na taasisi za umma ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 na ni kinyume na maadili ya kibunge.
Katika hatua nyingine Lissu amemshauri Spika wa Bunge Anne Makinda kuzivunja pia kamati za Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) akisema nazo zina madudu mengi.

"Hili lisiishie tu kwa kuvunja Kamati ya Nishati na Madini, tunataka pia kamati za POAC na LAAC zivunjwe, uchunguzi ufanyike na wahusika waitwe kujitetea na hatimaye wenye hatia watajwe hadharani bungeni na majina yao yachapishwe kwenye magazeti ili haki itendeke," alisema.

Alipoulizwa Chadema imefanya nini dhidi ya Mbunge wake, Zitto Kabwe kutajwa katika orodha hiyo, alijibu: "Nikiri kwamba sisi taarifa tunazo ila hatujamwita kumwuliza. Naomba ieleweke kwamba kama chama au Kambi Rasmi ya Upinzani hatuna maslahi na mbunge yeyote anayeonekana kujihusisha na masuala hayo."
"Katika hili tunaomba uchunguzi ufanyike na matokeo yake yatangazwe ili tupate msingi wa tuhuma hizo na ninaahidi kwamba tutazifanyia kazi ipasavyo."

Majibu ya tuhuma
Alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo, Kisangi alikiri kumiliki kituo cha mafuta lakini akasema sheria haimzuii mtu kama mambo yake anayafanya kwa uwazi.

"Nimekuja bungeni nikitokea kwenye ualimu, nilikuwa nafundisha Shule ya Msingi ya Mianzini na biashara hii ni ya familia. Inaendeshwa kwa uwazi na mwanangu wa kwanza ndiye anayeisimamia. Kutokana na uwazi katika shughuli zangu, mwaka jana Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilinipongeza. Mimi ni msafi na siko huko wanakofikiri wao (Chadema)."

Kwa upande wake, Mwijage alikanusha kuwa mtaalamu mwelekezi wa Kampuni ya Puma, badala yake akasema ni mtaalamu wa petroli anayefanya kazi ya kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu nishati hiyo.

"Siyo kweli, hawa wanadandia hoja. Mimi ni mtaalamu wa petroli ambaye mchango wangu kimsingi una faida kubwa bungeni na hata kwa jamii kwa ujumla. Sijafanya maamuzi yeyote ya kulihujumu taifa hili na hata kwenye Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini pekee, nilitoa mchango wa kurasa 10 kuhusu masuala hayo ya petroli," alisema

Aliishauri kambi hiyo ya upinzani kuvuta subira, akieleza kuwa jambo lililoko bungeni linahusu ufisadi na uhujumu uchumi hivyo kauli zinazotolewa bila utafiti zinaweza kuvuruga mchakato mzima uliokwishaanzwa na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Awali, Abdallah alipoulizwa kuhusu tuhuma za kumiliki vituo vya mafuta hivyo kuwa na maslahi binafsi, alicheka na kuahidi kwamba angepiga simu baadaye, lakini hakufanya hivyo na alipopigiwa baadaye alikata simu. Hata hivyo, alizungumza na waandishi wa habari na kukanusha kumiliki vituo vya mafuta.

Kamata kwa upande wake alisema: "Kuna kamati maalumu imepewa kazi ya kuchunguza mambo hayo, hivyo yote yanayoulizwa yatakuwa wazi na ukweli utajulikana tu. Nina maslahi au sina ukweli mtaujua, haraka ya nini?.

Mjadala Bungeni
Mjadala huo wa wabunge kuhusishwa na mgongano wa kimaslahi ulianza kulipuka bungeni jana asubuhi baada ya wabunge watatu; Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Salum Barwany (Lindi Mjini) na Mbunge wa Nkasi Kaskazni, Ali Kessy kutaka wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi watajwe bungeni ili kuisafisha taasisi hiyo ya kutunga sheria.

"Mheshimiwa Naibu Spika juma lililopita Mheshimwa (Vita) Kawawa alitoa hoja kutaka suala la ufisadi lishughulikiwe kwa kuvunjwa Kamati ya Madini na Spika akaridhia na kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili. Kwa nini Kamati nyingine zilizohusishwa na ufisadi huo nazo zisivunjwe?" alihoji Nassari na kuendelea:

"Kuna Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Mheshimiwa Mrema na Kamati ya Mashirika ya Umma (POAC) inayoongozwa na Zitto. Kuna tabia ya wabunge kuzikimbia kamati zisizokuwa na mikataba kama Kamati ya Huduma za Jamii na wanazikimbilia kamati zenye mikataba."

Barwany alitaka Bunge litajiwe majina ya wabunge waliotuhumiwa kwenye kashfa hiyo mpaka wakapelekwa kwenye Kamati ya Maadili, akieleza kuwa hili litasaidia kulisafisha... "Tumeambiwa Kamati ya Maadili inajadili suala hilo, lakini hatujatajiwa ni wabunge gani waliopelekwa huko, tunaomba mtutajie ili Bunge lijisafishe."

"Mimi naungana na wazo la Barwany na Nassari. Majina yatajwe wabunge tunadhalilishwa na wananchi huko mitaani. tuwataje hadharani,' alisema Kessy.

Akitoa mwongozo wa hoja hiyo, Ndugai aliiagiza Kamati ya Uongozi ya Bunge kutoka kwenye ukumbi wa Bunge ili wakajadili suala hilo na baadaye apelekewe taarifa.
"Naamini wenyeviti wote wa kamati mmo humu ndani, naomba sasa hivi mwende kwenye Ukumbi wa Spika mkajadili suala hilo halafu nipate majibu sasa hivi," alisema.

Baadaye jioni, Ndugai alisema kuwa Spika hawezi kuwataja kwa majina wabunge ambao wanajihusisha na rushwa kwa kuwa hawajui.

Alisema Kamati ya Uongozi iliyokutana jana mchana ilikubaliana kuwa ufanyike uchunguzi wa kina kwa ajili ya kuwabaini wale wanaoshukiwa na kwamba ikibainika Bunge litawaanika hadharani.

"Kamati imerejea kumbukumbu za hansard ya Jumamosi kuwa ufanyike uchunguzi wa kina juu ya jambo hilo na wabunge mtaitwa kwa ajili ya kutoa ushirikiano, ikumbukwe kuwa mbunge akiitwa siyo kwamba ndiyo amekuwa mtuhumiwa, bali pale itakapothibitika majina yatawekwa hadharani,'' alisema Ndugai.
Naibu Spika alitahadharisha kuwa ndani ya Kamati hiyo utafanyika uchunguzi wa kutosha kubaini kama kuna mjumbe mwenye maslahi kwa wale wahusika basi ataondolewa ili kutoa nafasi kwa kamati kufanya kazi yake ipasavyo.

Aliwatahadharisha wabunge kuwa Kamati hiyo haitaingilia utaratibu wa vyombo vya dola ambao wamekuwa wakiufanya ikiwemo wa Takukuru wa kuwahoji baadhi ya wabunge
http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/25163-zitto-ahojiwa-kwa-rushwa
 
Kilaza wa jimbo la Tabora, Rage mzee wa bastora ameomba muongozo wa spika kuwa kwa nini Mh. Tundu Lissu kataja majina ya wabunge wala rushwa wa CCM pekee na ameacha wa CHADEMA. Sasa anataka muongozo ili na Zitto atajwe.

Sasa yeye si angemalizia hiyo orodha!!
 
Baada ya kuhojiwa kwa masaa matatu na Kamati Kuu ya chama, wajumbe wengi hawajaridhishwa na majibu ya utetezi wa mheshimiwa Zitto.
Hivyo basi Zitto ameombwa apime uzito kati ya tuhuma zinazo mkabili na KUJIUZULU.
Zitto yuko karibu sana na watu wa CCM, pia ana urafiki mkubwa na Kafulila wa NCCR.
Zitto yuko mbioni kuondoka Chadema, je ni wapi atakako enda kugombea urais 2015?
 
JF sasa inataka kugeuzwa kijiwe cha porojo. msitupeleke huko Tafadhali, huna habari soma thread za wenzako hutopungukiwa na kitu.
 
the day will come and the truth will come out...ikumbukwe zitto ndiye aliesapoti kupandishwa kwa bei ya mafuta yataa kwa kisingizio cha uchakachuji.....pia ndiye aliepiga kelele serekali inunue mitambo iliyo tumika ya iliyokuwa dowans huku akijua ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya uma....kwamba serekali hairuhusiwi kununua kitu kilicho tumika....sasa ni kwavipi tusiseme ana maslahi binafsi na tanesco? pia hana vipao mbele maana kupambana na mafisadi yeye,kupigania maslahi ya wasnii yeye,poac yeye..nikwanini sula kama la wasnii asimpe ushauri sugu jinsi ya kudeal nalo alafu yeye aendelee na masuala aliyo anza nayo tangu 2008?
 
zitooooo(7).jpg

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe


Tuhuma za rushwa kuibuka bungeni na baadhi ya wabunge kudaiwa kuhongwa zimemuibua Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe na kusema yupo tayari kubebeshwa mzigo badala ya kuhusisha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati yake.

Aidha, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alisema wananchi wasishangae baadaye kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.

Madai ya kuwepo kwa rushwa bungeni yaliibuka katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma wakati wa kuchangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambapo ilidaiwa kuwa baadhi ya wabunge walihongwa fedha kwa lengo la kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).

Zitto katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari jana na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, alisema kuwa zipo hoja pandikizi za kutaka POAC ivunjwe na hasa zikimlenga yeye (Zitto) kama mwenyekiti wa kamati hiyo.

“Kwa maoni yangu, Kamati ya POAC isihusishwe na tuhuma hizi kwa vyovyote vile. Niko tayari nihukumiwe, mimi kama mimi na sio kuhusisha wajumbe wengine ambao hawatajwi mahala popote katika tuhuma hizi mbaya sana katika historia ya Bunge letu,” alisema Zitto.

Alisema wapo watu wenye kiu, wasioitakia mema Tanzania kuiona POAC ikivunjwa au sura zikibadilishwa kwa kuwa kamati hii imekuwa mwiba kwa mikakati yao ya kifisadi.

Zitto, alisema atakuwa tayari kuinusuru POAC isivunjwe kwa maslahi ya Taifa kwa kuchukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu uenyekiti iwapo itathibitika pasipo shaka kuwa amehongwa hasa ikizingatia kuwa kamati hiyo ni muhimu zaidi kuliko yeye (Zitto).

Alisema anafahamu kuwa kuna wanasiasa hasa wa upinzani ambao wanautaka sana uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha, lakini hawajui kuwa anayepanga wajumbe wa kamati ni Spika wa Bunge.

“Ni lazima tufike mahali kama viongozi kwamba utaratibu unapokiukwa na yeyote yule, au uongo unapotolewa hadharani tuseme bila kuogopa. Hili ndio jukumu letu kama wabunge na viongozi,” alisema Zitto.

Alisema taarifa za rushwa dhidi yake kama kawaida ya uzushi mwingine wowote zimesambazwa kimkakati na kwa kasi kubwa kiasi cha kuukanganya umma.

Aliongeza kuwa anafahamu kuwa anabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yake ya uongozi daima imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa, jinsia zao, makabila yao na rika zao.

“Nawajibika kupitia kwenu kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea Watanzania wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa taifa,” alisema Zitto.

Alisema mkakati wa kumuunganisha na baadhi ya wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea rushwa unatekelezwa kutokana na kuwepo kwa kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zake (Zitto) zinatokana na ushawishi wa rushwa.

Alisema baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco chini ya uenyekiti wa Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kuwasimamisha viongozi wa Tanesco, POAC ilimuandikia Spika kumuomba aridhie ili kamati iweze kuiita bodi hiyo.

Alisema wengine walioombwa kuitwa na kamati hiyo ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ili kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa.

Alisema kamati kujiridhisha na hatua za bodi ni sehemu ya msingi ya utekelezaji wa majukumu ya kamati yaliyowekwa kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge na pia Tanesco ni moja kati ya mashirika ambayo yanawajibika kwa kamati yake kwa hesabu zake na pia ufanisi wake kwa ujumla.

Hata hivyo, alisema yupo tayari kuchunguzwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyombo vya dola na ikiwa itathibitika amepokea rushwa atawajibika kisiasa.

“Sina bei, sijawahi kuwa nayo na sitarajii kuwa nayo huko mbeleni...ninawaahidi sitarudi nyuma katika mapambano dhidi ya rushwa katika nchi hii pamoja na mikakati ya aina hii ya kunidhohofisha na kunivunja moyo,” alisema.

Zitto alisema kamati yake inasimamia mashirika 259 ya umma na kwamba wanaoibua tuhuma za rushwa dhidi yake ni kutaka kuivuruga kamati hiyo ili kufanikisha nia ya wanaotaka kukidhi kiu ya tamaa zao za kupora rasilimali za nchi.

Alisema hakuna sababu ya kuihusisha POAC na tuhuma zinazoelekezwa kwake na badala yake alitaka ahukumiwe yeye binafsi na anasubiri uchunguzi ambao kama utathibitisha tuhuma hizo atajiuzulu nafasi ya uenyekiti kwenye kamati.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Zitto aliongozana na wabunge wengine wa chama chake ambapo pia aliwatuhumu wabunge wa upinzani kwamba wanataka POAC ivunjwe ili warithi nafasi yake ya uenyekiti.

Wakati huo huo, Zitto amesema serikali imeingia mkenge mwingine wa kulipa 'capacity charge' ya Sh. milioni 152 kila siku kwa Kampuni ya Symbion ambayo ilinunua iliyokuwa mitambo ya Richmond/Dowans fedha zinazolipwa hata kama kampuni hiyo haizalishi umeme au la.

Kadhalika, alisema kuwa Tanesco linatumia Sh. bilioni 42 kwa mwezi kulipa gharama mbalimbali kwa makampuni ya Songas, Aggreko na IPTL ikiwemo kununua mafuta mazito ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme wa kampuni hizo.

Zitto alisema gharama hizo zinachangia kuidhohofisha Tanesco kiutendaji na kifedha.

Alisema malipo hayo yanatokana na mikataba ya kinyonyaji baina ya serikali/Tanesco na kampuni hizo ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wabunge kwa muda mrefu bila mafanikio.

Alisema inashangaza kuona Symbion ikilipwa mamilioni ya fedha kila siku; miezi michache baada ya serikali na wanasiasa wenzake kupinga wazo lake la kutaka serikali inunue mitambo ya Dowans ili iweze kuzalisha umeme wa gesi ambao ungeuzwa kwa gharama ndogo kwa wananchi.

Zitto alisema taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Tanesco inaonyesha kwamba shirika hilo limekuwa likitumia asilimia 86 ya mapato yake kulipia gharama kwenye kampuni zinazozalisha umeme, hali ambayo inatokana na mikataba ya kinyonyaji.

Alisema ni katika kupinga ufisadi huo kumepelekea yeye (Zitto) kuzushiwa kwamba amepokea rushwa ili atetee mafisadi wanataka kuihujumu Tanesco.





CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom