Zitto aisumbua chadema; Chama chafikiri namna ya kumdhibiti?

Status
Not open for further replies.
Box_front.gif


Guilty until proven innocent? au
Innocent until proven Guilty?

Wengine mnaitikia vibwagizo tu as if ni kasuku.
Think!

Mabadiliko ya kweli Tanzania hayatakuja kwa majungu, dhana na hearsays!

Kubenea, Kibanda na Ngurumo wanakiua chadema, wanaaandika habari za Zito wauze magazeti. I am telling you guys! haiwezekani watu mnaowaita wanamapinduzi, wafichua ufisadi issues kama hizi za kuigawa chadema wanaziandika pasi uoga wala detailed info, udaku tu!!!

kwa heri chadema!!
 
huyu ni wa kufukuzwa kwenye chama..aende huko CCM..hatuwezi kulea watoto wapuuzi wa level hii hata kidogo
 
mi nafikiri wala haina usumbufu kikubwa ni kumtoa kwenye madaraka kwenye chama abaki mbunge wa kawaida asipewe madarka ya juu kwenye chama ili asiweze kupata tena habari za ndani ya chama akazitumia vibaya,ila utaratibu ufuatwe kama vikao vikifanyika hizi tuhuma ziwekwe mezani wapige kura kuchagua mtu mwingine au kama huwa wanateua basi wateuwe muhimu chadema wafuate utaratibu party displine procedure wa chama uliopo haina haja ya kuharakisha mambo,kumfukuza uanachama sidhani kama ni nzuri sana labda kama kuna ukiukwaji mkubwa umefanyika wa tararibu za chama nafikiri chadema watakuwa na taratibu zao za makosa yanayostahili kumfukuza mtu uanachama
 
Kubenea, Kibanda na Ngurumo wanakiua chadema, wanaaandika habari za Zito wauze magazeti. I am telling you guys! haiwezekani watu mnaowaita wanamapinduzi, wafichua ufisadi issues kama hizi za kuigawa chadema wanaziandika pasi uoga wala detailed info, udaku tu!!!

kwa heri chadema!!
Mimi nadhani wote wangenyamaza sasa kitu kidogo wanataka kukikuzaa weeeeeeeeee wrong strategy Zitto anyamaze na hao wengine wanyamaze kwa sasa
 
mnapeana moyo tu na kupotezeana muda

wenyewe wamempa cheo, wenyewe mnataka wamfukuze! kma hawana akili walimpa Zito cheo, je ina maana hawana akili ya kuongoza nchi, kwa makosa hayahaya?/

hivi nyie huwa mnafikiri kweli au?
 
Kuweni macho na mafisadi katika chadema Lissu na Mbowe tunajua njama zenu kwa Zitto hamumuwezi kabisa.
Huyu ameiva kisiasa sio Lissu hata kesi kila wakati anashindwa mahakamani sasa siasa ataweza.
Mbowe rudia kazi yako ya kuuza bar na kupiga disco
 
Kuweni macho na mafisadi katika chadema Lissu na Mbowe tunajua njama zenu kwa Zitto hamumuwezi kabisa.
Huyu ameiva kisiasa sio Lissu hata kesi kila wakati anashindwa mahakamani sasa siasa ataweza.
Mbowe rudia kazi yako ya kuuza bar na kupiga disco
Haya maneno ni uchonganishi inaelekea una nia ya kufuel motto kwa manufaa zaidi Zitto ni mtovu wa nidhamu wananchi wote tunajua lakini tunasema kwa vile wananchi wengi wamemueleza ukweli apewe nafasi ya kujirekebisha nadhani anajua lakini la kutokumuweza halina maana manake yeye si zaidi ya chama
 
Yeye ni maarufu tayari ila umaarufu wake ndo tishio kwa vigogo wa chama ndio maana inaelekea hata wamewahonga baadhi ya wanajf ili kumshugulikia zitto.ninasema mmehongwa kwa sababu mfano mimi nilivyo bize sijui kama naweza pata muda wa kuanza kuhangaikia imposibles
Kitu kimoja tuu kimeshusha umaarufu wake kama kasi ya umeme kuropoka siri ya chama kwenye TBC! ambao aliwaita mwenyewe wamhoji na itachukua miaka mingine mitano kuziba pengo hilo mtaji wake siku zote ulikuwa wananchi sasa hatumwamini tena imemgharimu sana swala la kukurupuka anaingiza na vitu vya kishetani kama udini hafai kiujumla anatakaiwa ajifunze kupiatia njia ngumu nidhamu katika maisha ni jambo la bure
 
Some chadema fans never cease to amaze me!!

kwa akili yako ndogo mleta maada humu, hakuna mwenye uwezo wa kumtimua Zitto ndani ya chadema huyo hayupo!!!! hata wakae kikao na Mtei deliberately wamtimue hakuna!!!! unapoandika maada kama hizi uwe mwangalifu sana

Halafu kumbuka childish ideas kwenye siasa ni kujitukana, hujasema zito amekosea kitu gani na kwa nini afukuzwe! kama ni kutoenda bungeni walikuwa wengi tu hawakwenda bungeni!!! hupo hapo??

Akina Mbowe na Slaa hawatamweza Zitto walishamkosea na kijana kafyatuka sasa! mtatumia wee magazeti ya tz daima na mwanahalisi hamtaweza!!! ukishukutana na mtu anajiita mwanaume anashindwa ku-mface Zito na kwenda gazetini, wakati mko chama kimoja na wote mna vyeo ni weakness!!!

chadema naona mmepania sana kujiimarisha kwa style ya kutafuta mchawi nani, kupigana na Cuf, to me I am curious, this makes you guys aidha vilaza wa siasa, au hamjui mnaongea nini, yaani mnachefua, unajiona ukija tu JF unaweza andika lolote, wenye akili wanawaangalia

Lissu hajasema swala la kufukuzwa ila vikasuku vimerukia na kujipa moyo, na mwingine anaanzisha maada iko digrresive!!! what a shame!!

Taratibu Mkuu, kwa tone yako, unaweza ukahatarisha afya yako zaidi kuliko kumuathiri mtoa mada. mada haina tatizo lolote hasa ukiangalia context, historia ya Zitto katika CDM, vituko vilivyojitokeza huko nyuma, na mazingira ya tuhuma. huyu ni mtu mwenye madaraka makubwa katika chama na bungeni, pamoja na hadhi kubwa kabisa hata mbele ya jamii. sasa kwa kitendo alichofanya, huwezi kumlaumu mtoa mada kwa kwenda mbele zaidi na kutoa ushauri kwa CDM wakati wana-contemplate wafanye nini na Zitto. ni kweli kuna wabunge wengine wanatuhumiwa kwa hili lakini tukubaliane kwamba Zitto ana uzito wa aina yake, na mtoa mada ameamua kumzungumzia Zitto, kwa definition ya mipaka ya mada yake. hilo nalo halina tatizo. CDM ni chama kikubwa na penye wengi pana mengi. mgombea wao wa urais alipata kura nyingi, zaidi ya watanzania milioni 2 wanampa sapoti, ukiachilia waliopigia kura wabunge na madiwani wake. CDM hata kama sio chama tawala, kinabeba maslahi na matakwa ya mamilioni ya watanzania, na hiyo yote ni kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii. kwa hiyo ni halali kabisa kutoa ushauri katika hadhara kama hii, hasa kwa wale wenye mapenzi mema na CDM, au wanaofuatilia mambo ya CDM. kama wewe wanakuchefua, haina sababu kubwa sana kuwaandikia namna hii. ndio maana haina lazima ya kuchangia kila post, hasa zile ambazo unaona zinakuchefua. kitu ambacho kwa maoni yangu kinafaa, ili tujenge nchi yetu, ni kutoa constructive criticism, ili hawa CDM ambao wanabeba dhamana ya watanzania wengi, waweze kufanya vizuri kazi yao kwa maslahi ya nchi yetu pia.
 
Hivi Jamani huyu Zitto si alishakuja hapa jamvini kwenye live session na akajibu hii hoja ya yeye kutokwenda bungeni siku ile kuwa hakukubaliana na mawazo ya kuwalk-out ila akapologize kwa wapenzi na wanachama kwa kitendo chake kuongea na media maana hicho ndicho kilitibua mambo??

Tusiwe wepesi wa kusahau mchango wa Zitto mazee, na hizi hoja za kutengana au kutengwa si hoja sahihi. Hatuhitaji kutengana wala kubaguana hasa wakati huu ambao tunahitaji kukusanya nguvu kama watanzania kuokoa nchi yetu kutoka hapa ilipo, tunapaswa kujadili tofauti zetu za kimawazo na kukubaliana kwenye common goal na kumwelewa mwenzetu anaposema sory kwa kukosea kidogo na wote tukamove on.

JF isiwe mahali ambapo watu wanakuja kuhubiri habari za kutengana na kunyanyapaana.
 
Kuna thread moja ililetwa hapa ilikuwa inamzunguzia kwa kiini dhamira za Godfather Edwin Mtei na Chadema lakini kwa bahati mbaya mods waliifutilia mbali. Kwa kifupi mwandishi ameandika kwa kirefu mikakati ya Chadema na kuwagusia waandishi wa habari wawili ambao wapo kwenye mkakati huo pengine kwa kutumiwa bila kujua au kwa malengo maalum na majina yao yalitwajwa kuwa ni Jenerali Ulimwengu na Saed Kubenea. Kwa mikakati yake sishangai kuona Zitto anaandamwa na nani anajua who next? Arfi? Slaa? or Tundu Lissu? Tuombe uhai tuone. Na nitashukuru kama kuna mtu aliwahi kucopy yale maelezo maana mie ninayo in hard copy.
hawajui... na wakija kujua watakuwa wameshachelewa. walio na akili hilo uliloliongelea wanalijua na ndio maana ZITO wala hawamuumizi kichwa.
just a hint'''''' hivi unamjua mke wa Jenerali Ulimwengu???????'''''''' anaitwa JOSEPHINE MARREALE mtoto wa mangi MAREALLE.
Kalagabahoooooooooooooooooooooooo
 
Wandugu,
Sinauzoefu sana na mambo ya siasa, ila kwa mwenendo wa huyu kijana mwenzetu Zitto kabwe inanipa mashaka...Kwa kweli anaonekana kuwa msaliti wa chama chake cha Chadema kwa kujipendekeza kwa chama tawala. haiingii akilini kusema yeye awe na ukaribu zaidi na kuona yanayofanywa na chama tawala kwa sasa ni bora na yamefanyika mengi...Wapi yule Kabwe wakutetea haki za wanyonge?

TETESI: (chanzo mitaani na kwa wachambuzi tofauti) Amenunuliwa na Serikali ya Jei kei kwa kuahidiwa mustakabali mnono wa maisha, alichoombwa ni afanye mbinu ya kuhamia NCCR na agombee uraisi kwa mwaka 2015 ili kuzigawa kura za CHADEMA
Zitto ni kijana anaekubalika, akitangaza uraisi wengi watamfuata na kuzigawa kura za chama machachari kinachoisumbua kichwa CCM.

WanaJF hili limekaaje jamani?

... rais Mkara??? Hata sifa hanazo na hatakuwa nazo. Hawa jamaa ambao ni DOUBLE AGENTS hatari sana. Nakumbuka kisa cha jamaa mmoja kwa jina Kim Philby aliesambaratisha Soviet Union kwa kiaina. even though, once a traitor, always a traitor! au?
 
Tatizo anajulikana Kigoma(Dubai ya Tanzania) tu.

Kwingineko anakubalika kwa sababu ya Chadema.

Akienda CCM atawekwa kitengo cha Tambwe Hiza.
 
CHAMA CJA DEMOKRASIA NA MAENDELEO KIMEFIKIA MAAMUZI YA KUMFUKUZA CHAMANI NAIBU KATIBU MKUU WAKE ZITTO ZUBERI KABWE KUTOKANA NA TABIA YAKE YA KIFISADI NA TAMAA ZA HELA CHAFU ZA MAFISADI.TAARIFA HII IMELETWA KWANGU NA KIGOGO MMOJA WA CHAMA AMBAYE YUKO KWENYE KIKAO KINACHOENDELEA SASA CHA KUJADILI MWENENDO WA WABUNGE WAPYA,UONGOZI WA CHAMA NA TATHMINI YA UCHAGUZI WA URAISI KILICHOANZA JANA,SIJAAMBIWA KINAFANYIKIA WAPI.

MJUZAJI AMENIAMBIA KUWA WAKATI WANAJADILIANA ISSUE YA MWENENDO WA WABUNGE ILIBIDI WAMTOE NJE NAIBU KATIBU MKUU HUYO KWA KUWA AJENDA HII ILIMHUSU SANA YEYE KAMA KIONGOZI WA WABUNGE WASIO NA MAADILI NA WASIOHESHIMU VIONGOZI WAO.BAADA YA KUTOKA HUKU AKISONYA KUONYESHA DHARAU KUBWA MKUU MMOJA ALISEMA HAMNA HAJA YA KUTOKA AKAE NA ASIKIE MAAMUZI YETU KWA UWAZI.

BAADA YA ZITTO KUKAA TENA KWENYE KITI CHAKE NDIPO MMOJA WA WAJUMBE AKASEMA ZAIDI YA DHARAU NA MAKOSA YOTE ALIYOFANYA ZITTO KITENDO CHA KUTUSONYA WOTE HAPA NI DHARAU KUBWA NA NAOMBA TUPIGE KURA YA KUMFUKUZA NDANI YA CHAMA ,WAJUMBE WOTE WALISHANGILIA NA MWENYEKITI ALIPOULIZA WANGAPI WANASEMA ZITTO AFUKUZWE WOTE WALISIMAMA WAKISHANGILIA NA KUSEMA KIWAVI JESHI KIFUKUZWE.

LAKINI KWA UPANDE MWINGINE ZIITO HAKUONYESHA KUSHTUSHWA NA HALI HIYO NA BADALA YAKE ALINYANYUKA NA KUSEMA ATAENDA MAHAKAMANI NA HUKO NDIO WATAKAPOKUTANA.

VIONGOZI HAO WAMEKUBALIANA MMOJA WAO ALIYETANGAZA KUPEWA BARUA YA ONYO ATAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI BADAE LEO KUTANGAZ TERMINATION YA ZITTO CHAMANI NAAMINI ATAKUWA AMEPOTEZA UBUNGE WAKE PIA

CHAMA KINAKUA HAYAKWEPEKI HAYA

hii ni tetesi kutoka kwa mtu wa kuaminika CHADEMA.
 
Kuweni macho na mafisadi katika chadema Lissu na Mbowe tunajua njama zenu kwa Zitto hamumuwezi kabisa.
Huyu ameiva kisiasa sio Lissu hata kesi kila wakati anashindwa mahakamani sasa siasa ataweza.
Mbowe rudia kazi yako ya kuuza bar na kupiga disco

Du...!!! Una hasira kama mbogo aliyejeruhiwa!!! Umepenyeza vichaka vya Simba nini!:hungry:
 
chama cja demokrasia na maendeleo kimefikia maamuzi ya kumfukuza chamani naibu katibu mkuu wake zitto zuberi kabwe kutokana na tabia yake ya kifisadi na tamaa za hela chafu za mafisadi.taarifa hii imeletwa kwangu na kigogo mmoja wa chama ambaye yuko kwenye kikao kinachoendelea sasa cha kujadili mwenendo wa wabunge wapya,uongozi wa chama na tathmini ya uchaguzi wa uraisi kilichoanza jana,sijaambiwa kinafanyikia wapi.

Mjuzaji ameniambia kuwa wakati wanajadiliana issue ya mwenendo wa wabunge ilibidi wamtoe nje naibu katibu mkuu huyo kwa kuwa ajenda hii ilimhusu sana yeye kama kiongozi wa wabunge wasio na maadili na wasioheshimu viongozi wao.baada ya kutoka huku akisonya kuonyesha dharau kubwa mkuu mmoja alisema hamna haja ya kutoka akae na asikie maamuzi yetu kwa uwazi.

Baada ya zitto kukaa tena kwenye kiti chake ndipo mmoja wa wajumbe akasema zaidi ya dharau na makosa yote aliyofanya zitto kitendo cha kutusonya wote hapa ni dharau kubwa na naomba tupige kura ya kumfukuza ndani ya chama ,wajumbe wote walishangilia na mwenyekiti alipouliza wangapi wanasema zitto afukuzwe wote walisimama wakishangilia na kusema kiwavi jeshi kifukuzwe.

Lakini kwa upande mwingine ziito hakuonyesha kushtushwa na hali hiyo na badala yake alinyanyuka na kusema ataenda mahakamani na huko ndio watakapokutana.

Viongozi hao wamekubaliana mmoja wao aliyetangaza kupewa barua ya onyo atakutana na waandishi wa habari badae leo kutangaz termination ya zitto chamani naamini atakuwa amepoteza ubunge wake pia

chama kinakua hayakwepeki haya

hii ni tetesi kutoka kwa mtu wa kuaminika chadema.

aende kwa amani naamini huyo aliyemuita kiwavi jeshi atakuwa bob makan
 
hawajui... na wakija kujua watakuwa wameshachelewa. walio na akili hilo uliloliongelea wanalijua na ndio maana ZITO wala hawamuumizi kichwa.
just a hint'''''' hivi unamjua mke wa Jenerali Ulimwengu???????'''''''' anaitwa JOSEPHINE MARREALE mtoto wa mangi MAREALLE.
Kalagabahoooooooooooooooooooooooo

So!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Acha fikra potofu
 
he salalaaaaaaaaaaaaa mbuyu kijana puuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu chini,alale mbele kiazi yule anataka kuleta tabia za Marando Chadema,bado Marando na yeye soon atachapishwa lapa
 
kama habari hizi ni za kweli basi ni dhahiri kwamba HATAONDOKA NA MTU HATA MMOJA.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom