Zitto airarua serikali; abeza Rais kulalamikia matatizo badala ya kuyatatua

Hivi hizi kamati za bunge ni kamati za ushauri au kamati za utendaji? Mbona kila siku wanaongea na sisikii serikali wakichukua hatua yoyote? Kuhusu hili la NSSF kuzalisha umeme mimi siamini kama ni njia sahihi ya matumizi ya fedha za wafanyakazi. Hawa NSSF kazi yao ya kimsingi ni kubiresha maisha ya wafanyakazi ya sasa na ya baadaye na kwa mtazamo wangu wangewekeza zaidi kwenye miradi ya kuwajenga nyumba nafuu na kuwakopesha wafanyakazi ili waondokane na hizi nyumba za kwenye makazi yasiyopimwa. Suala la umeme lingeachiwa shirika na NDC ambao tayari wana miradi ya uwekezaji kwenye umeme inayosubiri maamusi ya wizara ili ifanyike.
 
Kubiresha = kuboresha
Maamusi = Maamuzi
 
Zitto anaanza kurudi kwenye form yake acheni kumkatisha tamaa,with mass support atakuwa fiti haraka.

Ni kweli JK aache kulalama
 
zittto anatafuta umaarufu kwa kutumia shida ya umeme. Sasa anashindana na makamba. Wao serikali lolote jema. Ikosaini mkataba baraka watasema wafisadi hao. Wakichelewa wazembe hao.

Huh urais 2015 sijui utaipeka wapi tz!!!

mtetezi wa mkwere na serikali yake hupo kazini
 
selikali tunasubiri ushauri wa mwisho toka kwa Rostam Aziz na bwana Lowasa kuweni wavumilivu! Mbona mmevumilia toka 1992?
 
Wanasiasa wenye malengo ya kugombea urais kwa kufadhiliwa na Mafisadi ndio waliopatiwa uongozi wa Kamati za Bunge, kila kukicha Kamati na vyombo vya habari. Wote Mafisadi tuu!!
 
Kazi nzuri Zitto ila usiishie tu kutoa mapendekezo na kuacha serikali itekeleze "itakapoamua",hapo inabidi serikali ibanwe hasa la sivyo yatakuwa yale yale ya IPTL,Richmond na Dowans na mwisho wa siku ndo kuanza oh mi nilisema hiki,yule hakufanya kile and so on!so you don't seat back and relax until it's done!!!
 
Zitto uraisi 2015 ni wako hata kama chadema wakikuwekea zengwe wakampitisha yule kasisi wao ambae by 2015 atakuwa ashachuja we njoo NCCR kwa bwana mdogo wako Kafulilia kwani uwezo unao na unaweza gombea jimbo lolote hapa TZ na ukashinda kwanini ushindwe na uraisi
 
Ulitaka asemeje ili asionekane anatafuta urais? Watu waache kufanya kazi zao kisa wasije onekana watafuta urais-huo ni uzube mwingine!
bora umeliona, maana wakati huu mtu akiongea kitu chochote anaambiwa anatafuta uraisi, kwani waja mnatakaje? watu wasifanye kazi katika sekta walizopangiwa? tuachane na coments za 'anataka uraisi 2015' coz tushazichoka humu.
 
ni tatizo la kitaifa ikifikia kiongozi mkuu wa nchi naye analialia kama wananchi, mimi si mshabiki wa Zitto Kabwe lakini kwa hili nduguyangu nimekubeba mgogoni.

Imefikia hatua Mkuu wa nchi awe na kauli nzito hata kama zitakiuka baadhi ya vipengere ili kunusuru taifa kwa mfano hili la Giza mamlaka anayo kwa mfano:
1. Nataka Jumatatu mitambo yoyote inayoweza kuzalisha umeme iiwe imewashwa, waziri hakikisha unanipigia simu saa mbili
asubuhi kunipa confirmation.
2. Wote mlioiba pesa za umma namwagiza mwanasheria mkuu wiki moja wawe mahakamani -- nitakuwepo mwenyewe
kushuhudia
3. Nakuagiza wewe kamishina wa TRA - wiki moja nisione mizigo imerundikana hapa bandalini kama unataka nije nikusaidie kazi
nitakuja
4. etc.....

Wakuu kauli kama hizi ndizo tunazitaka kuzisikia , siyo kuanza kulalamika maandano ya CHADEMA kwamba eti wanataka kuiangusha serikali.

Bravo Zitto mwendo mdundo:
 
Zitto uraisi 2015 ni wako hata kama chadema wakikuwekea zengwe wakampitisha yule kasisi wao ambae by 2015 atakuwa ashachuja we njoo NCCR kwa bwana mdogo wako Kafulilia kwani uwezo unao na unaweza gombea jimbo lolote hapa TZ na ukashinda kwanini ushindwe na uraisi

Sorry to say Zitto haruhusiwi kikatiba kugombea urais 2015,kigezo cha umri kinamzuia labda uombe by then katiba iwe imerekebishwa!plus kuja NCCR.....mmh!sijui.
 
Zitto uraisi 2015 ni wako hata kama chadema wakikuwekea zengwe wakampitisha yule kasisi wao ambae by 2015 atakuwa ashachuja we njoo NCCR kwa bwana mdogo wako Kafulilia kwani uwezo unao na unaweza gombea jimbo lolote hapa TZ na ukashinda kwanini ushindwe na uraisi

Usimdanganye mwenzako wewe.....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom