Zitto aifagilia CCM kwa Mabadiliko kwa kuwapatia Vijana nafasi katika Uongozi ndani ya CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Israel Mgussi,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, amekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapatia vijana nafasi katika uongozi wa sektretarieti na kamati kuu ya CCM.

Akichangia hoja ya muswada wa marekebisho ya sheria ya mauzo ya nje (EPZs) na maeneo maalumu kiuchumi (SEZs) bungeni jana, Zitto alisema vijana ndio mhimili wa maendeleo ya kwa nyanja zote kwa taifa lolote duniani.

“Nianze kwa kusema,nimefurahishwa na mabadiliko katika Chama Cha Mapinduzi,nimefurahi vijana kupewa fursa ya kushika nyadhifa hizo kubwa katika chama," alisema Zitto na kuongeza,

“....Sisi Chadema tulishaanza hilo muda mrefu, vijana ndio wanapewa nafasi kubwa ya uongozi katika Chama maana ndio mhimili wa maendeleo, nampongeza Januari Makamba, Nape Nnauye kwa nafasi walizochaguliwa, naahidi sisi Chadema tutashirikiana nao katika kuhakikisha tunaliletea taifa hili maendeleo.”

Katika mchango wake wa muswada wa marekebisho ya sheria ya SEZs na EPZs, Zitto alisema ni vizuri kwa sheria hiyo kuwaangalia watu wanaozalisha bidhaa maalumu kama saruji kwa kuwaondolea kodi ya kusafirisha bidhaa hizo hadi kwa mlaji.

Mbali na hilo alisema suala la vivutio kwa wawekezaji ni muhimu, lakini akapinga kitendo cha mwekezaji kupewa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 akisema hiyo haina tija kwa faida, maana wawekezaji hao huzalisha ajira ndogo kwa wazawa na kwamba taifa hupoteza mapato bure.

“Vivutio wanavyopewa wawekezaji viangaliwe kama vina faida, mwekezaji anaposamehewa kodi ya mapato kwa miaka 10,msamaha wa kodi ya mapato kwenye gawio, riba na pango kwa miaka 10, misamaha wa ushuru wa forodha, VAT na kodi nyingine kwenye malighafi na mitambo ya uzalishaji haina faida kwa nchi, maana mwekezaji anaweza kuondoka mara tu miaka 10 inapoisha," alisema Zitto.

Kauli ya Zitto iliungwa mkono na mbunge wa Jimbo Sorwa(CCM), Ahamed Salum ambaye pamoja na mambo mengine yeye alitaka serikali iviwezeshe viwanda vidogo vidogo vya ndani kupitia SIDO.

Mbuge huyo wa Sorwa alisema endapo viwanda vya ndani vitapewa fursa na misamaha hiyo ya kodi wanaopatiwa wawekezaji wakubwa iwe pia kwa wawekezaji wadogo, wazalishaji wa ndani wanaweza kutoa tija kubwa kwa taifa.

Salum alisema hata nchi ya China ambayo kwa sasa inaonekana uchumi wake kukua kwa kasi, asilimia 70 ya wazalishani ni kutoka viwanda vidogo vidogo na wawekezaji wakubwa ni asilimia 30 tu.Alisema ni vema kama Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuviwezesha viwanda vya ndani na kwamba kauli ya kilimo kwanza iendani na uwekezaji wa ndani katika viwanda vidogo vidogo..
 
ni mawazo yake, lakini ni mtu mwenye "influence" kubwa sana ndani ya chama chake na hata kwa wananchi wasio wanachama wa Chadema. Nimesoma maelezo ya Katibu Mkuu mpya wa CCM kuhusu upinzani, ni kama vile mpaka sasa haoni upinzani wa maana. Hii si kweli lakini ni njia moja ya kunadi chama chake kwa wapiga kura. Ni vigumu sana kusikia kiongozi wa chama tawala akisifia Chadema, hata kwa mazuri yote yote wanayofanya (kupinga ufisadi, katiba mpya etc). sasa kiongozi wa chama makini kama Chadema naona ni vizuri akae mbali na mambo ya ndani ya chama chengine. Kama ni mambo ya kiserikali/kitaifa hapa hana budi kuongea.
 
Israel Mgussi,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, amekipongeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwapatia vijana nafasi katika uongozi wa sektretarieti na kamati kuu ya CCM.

..

...Ooh Yes
VIJANA HASA HAWA WAWILI

- Nape Mnauye - mwakilishi wa wale wanaojiita wapambanaji wa mafisadi walio ndani ya ccm
-January Makamba - Mwakilishi wa mafisadi

very interesting music
 
ZK NA YEYE PIA NI WA CCM,TUNAMSUBIRI TUU TIME WILL TELL,YUKO CHADEMA KUN KAZI ANATUFANYIA

he is our comming Katibu Mkuu
 
Nice words Zitto... upinzani sio vita!!! cha maana ni kujenga nchi na sio ushabiki wa kijinga
 
siasa za chuki hazina tija kwa taifa kitu cha msingi ni dhamira ya dhati ya mtu kwenye kuleta maendeleo we as young generation kitu ambacho tunatakiwa kukifanya sasa popote tulipo kwa kuwa soon taifa litabaki mikononi mwetu nikuwa vichocheo vya maendeleo .huu ni ukweli usiopingika ccm wameshasaturate hata wafanye any kind of adjustment hawawezi kujisafisha kwa sasa kwani sura yao kwenye society sio nzuri
cha msingi sisi kama wanaharakati wa maendeleo tujipange this individual acttack technically is not effeciency mwaacheni zitto afanye kazzi yake muda utaongea kama ana dhamira ya dhati taifa hili tutamjua

Cruel leaders are replaced only to have new leaders turn cruel.-che the great


 
Hilo la kawaida zitto kupongeza CCM sio mara ya kwanza

Anyway ZITTO hope Jumamosi utatema cheche zako kama zamani ARUSHA na kuvua gamba
 
Kwa jinsi alivyo handle issue ya dowans, nina shaka kama ujana wa Januari Makamba ni wakushangiliwa!
 
yeah ni kweli hata mimi namuunga mkono,kwani kijana kama NAPE anafaa kupata nafasi kama hiyo,ni mtu mwenye msimamo na hana longolongo ktk jambo linalohusu maslahi ya Taifa,hebu angalia ule mchakato wa wajengo la VIJANA LA CCM,alisimama kidedea na kusimamia ukweli,ingawaje Mzee makamba alipiga debe atemwe ila wenye akili walitambua hila iliyopo

Cha muhimu ni hao vijana kuichapa kazi kwa nguvu na kwa maslahi ya chama chao na Taifa kwa ujumla
 
Upinzani si kutazama mabaya tu ya mwenzio...nI PAMOJA NA KUPONGEZANA KWA mazuri!
Sioni tatizo na alichofanya Zitto, ili mradi wajibu wake kwa cdm anaujua.
 
Zitto anafanya kazi nzuri sana ndani ya mjengo... kwa hilo lazima tumpe kuddos jamani, hayo mengine ya kupongeza wale wa kijani nadhani its just natural
 
ZK NA YEYE PIA NI WA CCM,TUNAMSUBIRI TUU TIME WILL TELL,YUKO CHADEMA KUN KAZI ANATUFANYIA

he is our comming Katibu Mkuu

Huko kujidanganya tu, hakuna lolote analowafanyia, Zitto ni mtu wa kanuni na mwenye fikra thabiti. Nakumbuka alipokuwa anachangia hotuba ya raisi katika mkutano uliopita alisema, nanukuu "vijana ni lazima tuungane kwa maendeleo ya taifa, regardless tofauti za itikadi za vyama, tuungane ili tulikomboe taifa letu." huyo ndiye Zitto Kabwe
 
Hilo la kawaida zitto kupongeza CCM sio mara ya kwanza

Anyway ZITTO hope Jumamosi utatema cheche zako kama zamani ARUSHA na kuvua gamba
Ha haa haa! Karibu tena Chadema Mh. ZK, naona magamba yanavuliwa kila mahali sasa!
 
Huu ni wakati muafaka kwa Zitto kuamia CCM. Hili dirisha la fursa ni la kwake. Wenzake wengi (Kabourou, Bagenda, Lamwai, Ngawaiya, Hiza, CUF, TLP, n.k.) wamesha fanya taiming zao na kuamia CCM kwa nyakati zilizowafaa.
 
Huu ni wakati muafaka kwa Zitto kuamia CCM. Hili dirisha la fursa ni la kwake. Wenzake wengi (Kabourou, Bagenda, Lamwai, Ngawaiya, Hiza, CUF, TLP, n.k.) wamesha fanya taiming zao na kuamia CCM kwa nyakati zilizowafaa.

Ni lazima ufahamu kuwa upinzani sio uadui au kukosoa tu pale mwenzako anapokosea bali pia kusifia pale mwenzako anapofanya vizuri.

Zitto ni mahiri sana na anajua namna ya kusoma alama za nyakati.

Msijenge chuki katika vyama kwani wote nia yenu ni ile ile kuwatumikia wananchi na kuleta ahueni ya maisha.
 
Kweli CCM imefanikiwa kupandikiza siasa za chuki. Sababu yenyewe haijawahi kukubaliana waziwazi na mambo mazuri/hoja za wapinzani basi tuelewe upinzani ni kupinga kila kitu. Lazima tubadilike kimtazamo hasa sisi vijana. Ni kweli Zitto anamapungufu yake kama binadamu, ila kwenye hili sijaona kosa, kwanza tungemsifu maana ameonyesha ukomavu kwenye siasa na inabidi vyama vingine viige huu utamaduni. Tukumbuke kuwa, viongozi wenye uwakilishi kwa watanzania Bungeni wanatoka vyama mabimbali, hivyo nia ya bunge ni kuleta tija kwa wananchi wote. Tusikariri kuwa Bunge ni la kuendesha itikadi ya chama tawala tu, hivyo unapochangia ni vyema kuwa na mtazama wa Kitaifa. Bahati mbaya vyama vingi Afrika wanapokuwa watawala hupenda kubeza wapinzani ili kuwaondolea credut mbele ya jamii na kupunguza kukubalika kwao kwa wananchi a kuwezesha watawala kuendelea kutawala hata kama hawana uwezo mzuri. Hivi kile kisa cha Rais na Warekani Clinton enzi hizo na mwanadada Monica, ilipofikiwa kupigiwa kura ya kuwa na imani naye kuendelea na utawala, licha ya member wa Democtratic (chama chake) kuwa wachache lakini alishinda. Tuache siasa za chuki na tuangalie mantiki na tija kwa Taifa katika kila jambo.
 
Back
Top Bottom