Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
huo ni wivu na ndio kinacho watia upofu wa wasiko na akili.

Kweli Taifa hili haliwezi kuendelea tukiwa na watu wenye mentality kama yako, badala ya kuhoji huyo mtu kapata wapi mali zote hizi huku kazi yake ikifahamika na mshahara wake hali kadhalika, wewe unasema watu wanamwonea wivu, halafu baadae mnakuja kulalamikia ufisadi wakati mkiwa mitaani mnawasifia mafisadi na kulamba miguu yao. Wewe huna tofauti na wale wasukuma waliopelekea malori ya bia na Chenge baada ya kashfa ya dollar 1.2 bil nao wakasema kijana wao kaonewa. Mwizi ni mwizi tu, mnafiki ni mnafiki tu! ni takataka kwenye jamii no matter his intellectual capacity!
 
zitto kabwe wa 2005,
zitto kabwe aliyefukuzwa bungeni
zitto kabwe aliyekuwa na uchungu mkubwa na nchi hii kwenye dowans,richmond,epa etc

HAWEZI KUONGEA NA ROSTAM.....!WATAONGEA NIN?

halaf mifano tunayo.....mtikila ilikuwaje?

Usiwe na wasiwasi hayo ya Mtikila yatatokea tu very soon...usishangae sura na signature zitakazoonekana zikawa za wateule wenu waliojivika kilemba cha umiliki wa chama wakati hawana support hata ya kulazimisha katika kikao chochote kile cha uongozi wa chama....
 
Hivi kiongozi kuzungumza na Rostam ama Afisa Usalama wa Taifa ni kukiuka maadili? Lakini pia ni lini uliwahi kukemea wanayofanya wengine dhidi ya Zitto zaidi ya kushabikia tu na kuhalalisha?

Hapana kaka mimi sishabikii chochote ila am a great believer kwamba we need upinzani mkubwa katika siasa ili nchi iweze kuendelea (politicians are all alike and they need to be checked) therefore all is happening now is upinzani inside chadema which is not healthy.... another point Chadema moja ya their trade mark is fighting against ufisadi.... therefore zitto talking to one of the major accussed Fisadi I think he has some clarification to make of what he was talking about or to tell us maybe he does not believe the said is a fisadi...... I dont follow politics like a football team, but i need upinzani wa kweli and right now Chadema is the only Party who can provide that...
 
Wewe utasutwa. fuatilia mambo kwanza kabla ya kuropoka. Zitto hajwahi kumiliki Hammer. Hammer aliyokuwa nayo ilikuwa ni ya Kaka yake ambaye ni mfanyabiashara wa magari iliuzwa mika minne iliyopita. Gari pekee la gharama ambalo Zitto amewahi kununua halizidi shilingi milioni 30 na yote ni second hand tena second hand za hapa Tanzania. Zitto alipopewa fedha zake za ubunge mwanzoni aislimia kuwa alisurrender kwa Mbowe kama kumpunguzia mzigo wa michango yake katika kampeni kumbe fedha alizokuwa Mbowe anadai ni zake ni za kutoka kwa Rostam...zaidi ya milioni 100.

Lakini pia kumbuka Zitto sio mbunge wa vikao vya bunge tu. Anatumia sana eleimu yake kama consultant na hivyo kujipatia mapato zaidi ambayo yote huishia katika matumizi ya kibunge na chama. Zitto miaka yote hii amekuwa akijitolea kusaidia chama ama viongozi wenzake bila ya kuomba kulipwa kama wafanyavyo viongozi wenzake.

Huyo Anthony Komu mwenyewe ambaye ndio mpika majungu gatika gazeti lake la Mwanahalisi lilioanzishwa kwa msaada mkubwa wa Zitto, Zitto alimpa PRADO bure bila ya kutoa senti....

By the way acha ushamba, hivi unajua thamani ya used hammer? Its less than 25,000USD na kama Zitto angetaka kumiliki he could afford just kwa kutumia mkopo wa lazima wa magari wanaopewa wabunge....
ha ha ha ha!
wewe ndo mshamba sasa!hiyo nani kaizungumzia USED HAMMER?....kwanin haujaopt for a BRAND NEW HAMMER ambayo ni zaid ya mil 200?-jibu ni rahisi,itakusumbua kufanya mchanganuo wa kazi za consultancy na kazi za ubunge ili udanganye vizuri kwamba INAWEZEKANA KUNUNUA HAMMER kwa hizo kazi mbili(ubunge na consultancy firm).infact hapa tunazungumzia zaid ya magari matano ya kutembelea
 
Hii ndo kazi ya wale nusu ya usalama Wa taifa wanao ripoti kwa Slaa ambao walishindwa kumjuza Slaa namna ya kuzuwia kuibiwa kura?

Hebu tufumbe macho tufikiri simu ya Slaa itatoka na majina ya watu gani anaowasiliana nao?

Mwanahalisi linajua fika kuwa inachofanya ni uchonganishi lakini ni wazi kuna kitu kinapikwa na CDM(since gazette limefungamana na chama)

Nionavyo "'akufukuzae hakwambii toka"
 
Too much predictions!
Kubenea kama kweli anataka kujenga hizo data angezitoa kwa uongozi wa CDM ili ZITO aulizwe.
Naye ajibu ili akionekana anahatia basi asulubiwe lakini si hiki anachofanya kuchapisha chapisha tuu (uchochezi)
mi mwenyewe namuona anaganga njaa tuuu na anabomoa zaidi kuliko kujenga.
 
Mhhh,

Haya mambo yanatisha. Hivi ingeandikwa kuwa hayo maongezi ya Zitto kayafanya na Osama Bin Laden ingekuwa issue au tungeona poa?
 
basi wewe kumbe hujasoma msimamo wangu. Mimi ni mzalendo wa uwazi na ukweli tupu miaka yote. Ila sipendi dharau kwenye mambo ya msingi....... Ukinisoma utaona nimeshasema zaidi ya mara tatu kwamba mbowe is not the best one for chadema

Kaka ,

Uzalendo una sura nyingi sana na kila mtu anastyle yake ya kusimamia uzalendo wake.....
 
Too much predictions!
Kubenea kama kweli anataka kujenga hizo data angezitoa kwa uongozi wa CDM ili ZITO aulizwe.
Naye ajibu ili akionekana anahatia basi asulubiwe lakini si hiki anachofanya kuchapisha chapisha tuu (uchochezi)
mi mwenyewe namuona anaganga njaa tuuu na anabomoa zaidi kuliko kujenga.

Mhhhh,

Kubenea awapelekee CHADEMA kwani yeye ni agent wao au kaajiriwa na wao kuwafanyia ushushu?
 
Too much predictions!
Kubenea kama kweli anataka kujenga hizo data angezitoa kwa uongozi wa CDM ili ZITO aulizwe.
Naye ajibu ili akionekana anahatia basi asulubiwe lakini si hiki anachofanya kuchapisha chapisha tuu (uchochezi)
mi mwenyewe namuona anaganga njaa tuuu na anabomoa zaidi kuliko kujenga.

Kwani unadhani haya yanatoka wapi? Ni huko huko lakini hawana guts za kuyazungumza katika vikao vya chama na wala kuyazungumza mbele yake......Wanabaki tu na longolongo lao walilozoea eti "tuna ushahidi" wakiambiwe leteni hapa wanapiga danadana....
 
Hivi hata kama Zitto alipigiwa na Rostam nae Zitto akawa anakata simu bila ya kuongea chochote sie tutajuaje?
 
Naomba tujikumbushe kidogo kuhusu "King Maker"

Tumeingiliwa, tusimame imara kulinda usalama wetu

Padri Privatus Karugendo

HABARI zilizotangazwa na vyombo vya habari kwamba mafisadi walijitahidi kutumia fedha ili kuuingilia uchaguzi wa KKKT, ili kuhakikisha hata na kwenye dini wanaweka viongozi wanaowataka wao, imetushtua sana na kuthibitisha wasi wasi wetu wa kuingiliwa na mafisadi katika kila nyaja.

Inatisha! Iwe mikataba mibovu wamo, iwe siasa wamo, iwe michezo wamo na sasa wanataka kuingilia dini?

Wanataka kumwondoa Askofu Alex Malasusa, ili wamsimike nani huyo watakaye mwendesha na kuwasikiliza na kuwasaidia katika kampeni za uchaguzi wa 2015?

Ni mchungaji gani anayeweza kukubali mtego huu wa kumziba mdomo na kumzuia kufanya kazi zake za Kinabii? Haiwezekani mafisadi wakajiingiza kanisa kichwa kichwa bila kukaribishwa na kuelekezwa. Msaliti huyu akijulikana; ni heri asingezaliwa!

Ni lazima kuamka sasa na kusimama imara kulilinda na kulitetea taifa letu. Watu wachache, hata kama wana nguvu za fedha hawawezi kuliyumbisha taifa letu.

Tusiwakubalie, tukatae na kupambana nao. Makala hii ni wito wangu kwa Watanzania kuwa macho na kutambua kwamba hali imekuwa mbaya zaidi; kama mafisadi wamefanikiwa kujipenyeza kwenye taasisi za dini, tumeingiliwa! ni lazima kutafuta dawa vinginevyo tunateketea.

Niupongeze mkutano mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa msimamo wao wa kumpigia kura ya imani Askofu Alex Malasusa.

Kura asilimia 96.6 alizozipata Askofu Dk. Malasusa, si zake peke yake bali za heshima ya kanisa na taasisi zote za kidini hapa Tanzania. Nawapongeza wajumbe wa mkutano huu kuu kwa kuzikubali fedha za fisadi na kuzitafuna lakini wakabaki na msimamo wenye heshima na uliotukuka.

Wangefanya kinyume; historia ya kanisa na taasisi za kidini hapa Tanzania zingeandika historia mpya; historia ya kuongozwa na kutawaliwa na nguvu za "giza". Likifanyika kosa la kuruhusu "shetani" huyu kuingiza ushawishi wa fedha kwenye uongozi wa kanisa, ndo utakuwa mwisho amani na utulivu katika taasisi za kidini.

Taasisi za kidini zikivurugika, amani na utulivu itapotea kabisa kutoka katika maisha ya kila siku ya Mtanzania.

Ingawa watu hawa waliotaka kulivuruga Kanisa la KKKT wamebatizwa jina la "Mafisadi", mimi ningependa kusema kwamba kwa kitendo chao cha kutaka kuingilia hata uongozi wa kanisa watu hawa si mafisadi tu bali "Majambazi".

Hawa ni hatari kwa taifa letu, na kama tusipoamka wataendelea kutuyumbisha na kutuchanganya kama walivyojaribu kufanya ndani ya kanisa la KKKT.

Wengine wanasema, hawa si kundi la watu bali mtu mmoja au wawili. Mwenye nguvu zaidi anajulikana kama "King Maker". Wanasema huyu ndiye anayewapitisha wabunge, mameya hata na Rais wa nchi anatengenezwa na yeye.

Mtu huyu aliuvuruga umoja wa Vijana wa CCM, aliuvuruga pia umoja wa wanawake Tanzania na inasemekana mtu huyu ndiye anayeivuruga CHADEMA na ataendelea kuivuruga hadi atakapohakikisha viongozi wa CHADEMA ni wale wanaompigia magoti na kumtumikia.

Mtu huyu amevuruga vyombo vya habari karibu vyote na kuhakikisha kila chombo cha habari kina mtu wake anayelipwa donge nono ili kuhakikisha agenda zake zinapita bila matatizo.

Bila kupita kwake ni vigumu kusonga mbele. Huyu mtu ana mbinu na watu wengi amewaweka mfukoni mwake. Habari za kuaminika ni kwamba hata na spika wa bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, alichaguliwa kwa maelekezo ya huyu bwana "King Maker".

Wanaofuatilia mambo wanasema, "King" huyu alisafiri hadi nyumbani kwa Spika na kujaribu kumshawishi akubali kusimama na kupambana na Spika aliyekuwa akimaliza muda wake wa uspika.

Ushawishi wake kwenye mchakato wa kumtafuta Spika, haukuwa na lengo kama lile tunalolisikia leo hii la kuwapatia wanawake nafsi za juu katika taifa letu, bali ni ushawishi wa kutaka kuhakikisha kila nafasi ya juu katika taifa letu inakamatwa na mtu mwenye uwezo wa kupiga magoti na kumsujudia huyu "Kinger maker".

Kama uchaguzi wa Spika Mwanamke, ungekwenda sambamba na wazo zuri la kuwapatia wanawake nafasi za juu katika uongozi wa taifa letu, basi mwaka huu tungeshuhudia; Makamu wa Rais Mwanamke, Waziri Mkuu Mwanamke, Mkuu wa Majeshi Mwanamke. Kwa vile hili hatulioni, ndo tunatambua janja ya hawa " Majambazi" ambao bila aibu wala woga wanataka kujipenyeza kanisani!

Haishangazi ni kwa nini Askofu Dk. Alex Malasusa, alilengwa na fisadi huyu na maswahiba wake. Msimamo wa Askofu, unajulikana wazi.

Amekuwa mstari wa mbele kupigia kelele "Ufisadi", wakati wa uchaguzi mkuu alijitokeza na "Kauli mbiu" ya chagua mtu, usichague chama. Ni wazi hii ni Kuli mbiu isiyowapendeza wakubwa.

Lakini yeye kama Nabii, alikuwa akitimiza wajibu wake na kawaida Nabii, hapendwi! Nabii, akipendwa na kushangiliwa anakuwa hafanyi kazi yake!

Historia inatwambia kwamba Manabii waliuawa, walifukuzwa na walibezwa na jamii. Na Nabii wa kweli ni yule asiyeogopa kufa, asiyeogopa kutukanwa wala kufukuzwa.

Hali inayojitokeza sasa hivi katika taifa. Wakati demokrasia inachezewa; fedha inakuwa na nguvu ya kuwaweka watu madarakani; fedha inatumika kuwachaguliwa watu mwakilishi wao.

Serikali inanyanyasa haki ya wapiga kura kama ilivyotokea kule Karagwe na majimbo mengine ambako ushindi ulilazimishwa hata kwa kura moja na sehemu nyingine kwa mtutu wa bunduki ni lazima viongozi wetu wa dini kusimama imara na kufanya kazi yao ya unabii.

Viongozi wetu wa dini wasiogope kutukanwa, wasiogope kufukuzwa na wasiogope kufa. Wawe tayari kuutetea ukweli kufikia kiasi cha kuhatarisha maisha yao.

Mtu anakufa mara moja katika maisha yake; hata ukiogopa kufa leo, utakufa kesho au kesho kutwa na ukweli ni kwamba hakuna mtu atakayeishi milele. Atakayekuua leo, naye atakufa kesho.

Hivyo ni bora viongozi wetu wajitokeze kufanya kazi yao ya unabii hata kama mbele yao kifo kitakuwa kikiwakaribisha. Hiyo ndo njia ya manabii wote waliotutangulia.

Huyu aliyetaka kuuvuruga uchaguzi wa KKKT, anajulikana. Itashangaza sana kama viongozi wengine wa dini hawatasimama na Askofu Dk.Alex Malasusa, kumlaani na kupambana na "Jambazi" huyu hadi ashindwe kwa Jina la Yesu na kwa jina la Mitume wote waliotumwa na Mungu, kuwasha moyo wa haki, amani, upendo na wema hapa duniani.

Source: Tumeingiliwa, tusimame imara kulinda usalama wetu
 
Hivi hata kama Zitto alipigiwa na Rostam nae Zitto akawa anakata simu bila ya kuongea chochote sie tutajuaje?

We will never know........ lakini am sure kuna some call duration ambayo itaonekana..... Nadhani hapa issue sio kama waliongea issue ni waliongea nini and taliking by itself does not matter ila if there some other questionable things happening..... Then defenetly there something wrong somewhere.......
 
Hii ndo kazi ya wale nusu ya usalama Wa taifa wanao ripoti kwa Slaa ambao walishindwa kumjuza Slaa namna ya kuzuwia kuibiwa kura?

Hebu tufumbe macho tufikiri simu ya Slaa itatoka na majina ya watu gani anaowasiliana nao?

Mwanahalisi linajua fika kuwa inachofanya ni uchonganishi lakini ni wazi kuna kitu kinapikwa na CDM(since gazette limefungamana na chama)

Nionavyo "'akufukuzae hakwambii toka"
G'

the whole cdm game is well choreographed, unfortunately zitto may not be cleanest and freeman is not intelligent
 
Hivi hata kama Zitto alipigiwa na Rostam nae Zitto akawa anakata simu bila ya kuongea chochote sie tutajuaje?

Teacher...hapa kuna maswali mengi sana na hakuna mwenye majibu zaidi ya Zitto mwenyewe na RA. Labda watakuja mbele ya public wakanushe ili twende kwenye hatua nyingine. Ila hata yale mawasiliano na boss wa TISS hayatolewa maelezo. Ukweli kuwa kiongozi mkuu wa chama kikukuu cha upinzani anawasiliana na mtu wa aina ya RA hata kama hawakuongea kitu chochote lazima imfanye mtu yeyote makini kukuna kichwa. Hata hivyo tunatakiwa kuwachukulia kuwa hawakuwa wanapanga kitu chochote kibaya (jinai) hadi hapo tutakapokuwa na taarifa rasmi. Au wewe unaonaje?
 
Zitto hajwahi kumiliki Hammer........ilikuwa ni ya Kaka yake........Gari pekee la gharama ambalo Zitto amewahi kununua halizidi shilingi milioni 30 ....Huyo Anthony Komu mwenyewe ......Zitto alimpa PRADO bure bila ya kutoa senti........

Zitto hana kaka yake na yy ni first born kwao. Mbona wajichanganya? Tupe evidence.....Mara unaonesha ZT hana pesa mara unaonesha ana pesa hadi kumnunulia mtu prado....mara.....mara...yaani hueleweki mkuu.........
 
zitto at first he did made me believe in siasa...but as time goes...ninashawishika kuamini kuwa zitto is a political prostitute!
 
Wewe utasutwa. fuatilia mambo kwanza kabla ya kuropoka. Zitto hajwahi kumiliki Hammer. Hammer aliyokuwa nayo ilikuwa ni ya Kaka yake ambaye ni mfanyabiashara wa magari iliuzwa mika minne iliyopita. Gari pekee la gharama ambalo Zitto amewahi kununua halizidi shilingi milioni 30 na yote ni second hand tena second hand za hapa Tanzania. Zitto alipopewa fedha zake za ubunge mwanzoni aislimia kuwa alisurrender kwa Mbowe kama kumpunguzia mzigo wa michango yake katika kampeni kumbe fedha alizokuwa Mbowe anadai ni zake ni za kutoka kwa Rostam...zaidi ya milioni 100.

Lakini pia kumbuka Zitto sio mbunge wa vikao vya bunge tu. Anatumia sana eleimu yake kama consultant na hivyo kujipatia mapato zaidi ambayo yote huishia katika matumizi ya kibunge na chama. Zitto miaka yote hii amekuwa akijitolea kusaidia chama ama viongozi wenzake bila ya kuomba kulipwa kama wafanyavyo viongozi wenzake.

Huyo Anthony Komu mwenyewe ambaye ndio mpika majungu gatika gazeti lake la Mwanahalisi lilioanzishwa kwa msaada mkubwa wa Zitto, Zitto alimpa PRADO bure bila ya kutoa senti....

By the way acha ushamba, hivi unajua thamani ya used hammer? Its less than 25,000USD na kama Zitto angetaka kumiliki he could afford just kwa kutumia mkopo wa lazima wa magari wanaopewa wabunge....

Najiuliza kwa nini mwana CCM awe mtetezi wa Zitto....hayo tu!
BTW: Zitto ni mwanachama hapa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom