Zitto afikishwa Mahakamani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe jana alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kigoma akikabiliwa na shitaka la kumtoa kwa nguvu mtuhumiwa mmoja aliyekuwa chini ya ulinzi halali wa polisi.

Katika kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2010 iliyosomwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Emmanuel Mrangu, Zitto anadaiwa kufanya hivyo huku akijua anatenda kosa kinyume cha sheria
Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi, Amoni Mimata aliieleza mahakama kuwa Zitto alitenda kosa hilo Oktoba 27 mwaka huu, majira ya saa 5:00 asubuhi kwenye kituo cha polisi cha Mahembe kilicho Wilaya ya Kigoma.

Inadaiwa kuwa akiwa katika kituo hicho, Zitto alimtorosha Peter Kibwega, ambaye ni mwanachama wa Chadema aliyekamatwa kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuhatarisha kuvunjika kwa amani.

Kwa mujibu wa mashitaka hayo, Zitto anadaiwa kufanya kosa hilo kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 115 kifungu kidogo cha kwanza cha kifungu kidogo C na kifungu cha 35.

Mwendesha mashtaka huyo alisema kuwa Peter Kibwega, aliyekuwa akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya uvujivu wa amani wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, alikamatwa na jeshi hilo na kuanza kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo
Alidai kuwa wakati mtuhumiwa huyo akihojiwa, Zitto alifika kituoni na kumchukua kwa nguvu licha ya jitihada za polisi waliokuwepo zamu kuzuia jaribio hilo bila mafanikio.

Hata hivyo, Zitto amekanusha kufanya kosa hilo na mahakama imempa dhamana baada ya kukidhi masharti.
 
And so ...??

Wa-Tanzania wangapi walifikishwa mahakamani kwa siku ya hapo jana?? Ndugu mleta hoja usitafsiri kama ni shambulio kwako ila tu ni kwama huyu ndugu ni too much kwenye publicity na asijue gharama za kupenda misifa.

Pole yake anyway!!!
 
Back
Top Bottom