Zitto afanya mkutano wa hadhara mjini Katesh wilayani Hanang'

Status
Not open for further replies.

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
791
Mh. ZZK akiwa amefuatana na Mh. Rose Kamili, Mbassa, Kasulumbay na viongozi wengine wa Chadema Wilaya na kata.

Mkutano ulikuwa ufanyikie viwanja vya shule ya msingi lakini walinyimwa na baadaye ukafanyikia viwanja vya mnadani ambavyo viko nje kidogo ya mji wa Katesh ila watu walikuwa wengi na Katibu wa Mary Nagu alihudhuria.

Mkutano ulikuwa wa dharura na ulikuwa wa dk 45 tu. Kadi za Chadema ziligawanywa.

Nitajaribu kuwawekea picha japo natumia simu.
 
Jitahidi kutuwekea picha,huo uwanja naufahamu sana siyo mbali na mjini maana ni km 500m nje ya mji kuelekea singida!viva cdm!kanyaga twendeeeeeeeee
 
Mh. ZZK akiwa amefuatana na Mh. Rose Kamili, Mbassa, Kasulumbay na viongozi wengine wa Chadema Wilaya na kata.

Mkutano ulikuwa ufanyikie viwanja vya shule ya msingi lakini walinyimwa na baadaye ukafanyikia viwanja vya mnadani ambavyo viko nje kidogo ya mji wa Katesh ila watu walikuwa wengi na Katibu wa Mary Nagu alihudhuria.

Mkutano ulikuwa wa dharura na ulikuwa wa dk 45 tu. Kadi za Chadema ziligawanywa.

Nitajaribu kuwawekea picha japo natumia simu.
Mkuu Naytsory, kwanza asante kwa taarifa. Naomba ufafanuzi kidogo, aliyefanya mkutano ni ZZK au Rose Kamili?!. Nombeni tuache ushabiki uliopitiliza!, headline inasema ZZK afanya mkutano Katesh!, inside story unamtaja Kamili ambaye base yake ni Katesh!.

Kwa maoni yangu mkutano ni wa Rose Kamili, ZZK atakuwa alikaribishwa kuuhutubia!.
Naunga mkono utoaji wa taarifa zozote humu jf, ila natatizwa sana na taarifa zenye "ill motives behind"!.
 
Amezungumzia ugawaji wa mashamba ya NAFCO na matumizi ya yale majengo, masuala ya ufisadi na kutetea haki za watanzania wasio na kitu. Lakini pia kasema vita vya watanzania vitakuwa kati ya walionacho na wasionacho.
 
Huo mkutano utakuwa hauna kabali cha chama kwanini uwe na dharura?

rose kamili na zzk wote ni majeruhi wa chadema
 
Zitto ndiyo aliyehutubia ila hao wengine niliowataja amefuatana nao. Na hawakupata nafasi ya kuhutubia.
 
Zitto na kundi lake wanatoka kivyao kuelekea urais 2015. Namtakia maandalizi mema ila njia siyo tambarare...
 
Huo mkutano utakuwa hauna kabali cha chama kwanini uwe na dharura?

rose kamili na zzk wote ni majeruhi wa chadema

Mkuu sijakusoma, wewe ndo unayetoa vibali vya mikutano ya CDM????? Mbona tunaanza kutafunana sisi kwa sisi wakuu???? nijuavyo mimi, mpaka dakika hii Zitto akisimama popote, credit zinaenda kwa CDM, na si kwa chama kingine, kwa sababu hajahama chama, sasa wewe mshawasha wa nini????
 
Alitumia nafasi hiyo kutangaza nia ya kugombea Urais? Na vipi alimtangaza mgombea mwenza wake?
 
Mkuu Naytsory, kwanza asante kwa taarifa. Naomba ufafanuzi kidogo, aliyefanya mkutano ni ZZK au Rose Kamili?!. Nombeni tuache ushabiki uliopitiliza!, headline inasema ZZK afanya mkutano Katesh!, inside story unamtaja Kamili ambaye base yake ni Katesh!.

Kwa maoni yangu mkutano ni wa Rose Kamili, ZZK atakuwa alikaribishwa kuuhutubia!.
Naunga mkono utoaji wa taarifa zozote humu jf, ila natatizwa sana na taarifa zenye "ill motives behind"!.

Unamind nini sasa? wewe ulikuwepo hapo? kwani zzk anakatazwa kufanya mkutano kwenye eneo la mwingine? Harafu wewe na Zitto ni ndugu au kibaraka wake tu?? Likizungumzwa jambo la zitto unakurupuka shume weee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom