Zito: Jamii Ya Wezi na Wala Rushwa Uzaa Viongozi Wezi na Wala Rushwa!!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Jamii Ya Wezi na Wala Rushwa Uzaa Viongozi Wezi na Wala Rushwa!!Hiyo ni Kauri ya Zito akiongea na Mtangazaji Zembwela na Michael Baruti wa Kipindi cha Super Mix East Africa Radio.Alikuwa akijibu maswali ya Watangazaji hao wakiongelea mada mbalimbali juu ya jamii.Zitto Anasema watanzania wanaishi double ikiwemo kama hili la kuishi kwa uchafu anasema Watanzania ni wachafu na imedhihirka hivyo wakati wa mafuriko.

Watangazaji hao wamemuuliza swali hili Kwa uchafu huo kwamba hivyo Taifa hili limefika hapa kwa kuwa Wananchi wake wanaishi double life na hivyo kufanya mambo ambayo yamelifikisha Taifa hapa tulipo. Yeye Zitto anasema Taifa hili limefika hapa kutokana na kuwa na viongozi wanaotaka Yale Wananchi wanayotaka kusikia na sio yale Wananchi wasiotaka kusikia.

Pia aliulizwa na Watangazaji hawa Zembwela na Michael Baruti ushiriki wake wakati wa Kamati ya Madini ya Repoti ya Madini. Zitto anasema Mikataba yote ya Madini haina kipengele chochote chenye kuonyesha kuwa mikataba ya madini ni ya siri, hivyo hakuna Mkataba wa Madini wa siri hapa Tanzania.

Ameulizwa Swali na Michael Baruti kuwa Wanachi wa eneo husika la uchimbaji wa madini chukulia mfano mgodi huko kijitonyama wanachi wake wanafaidika vipi na mgodi husika kuwepo kwenye eneo hilo kwa watu wake. Zitto amejibu akasema Tanzania kimfumo ni Nchi ambayo ni Unitary
[A unitary country or organization is one in which two or more areas or groups have joined together, have the same aims, and are controlled by a single government.].Hivyo kwa mfumo huo Taifa ukusanya fedha au mapato yake toka maeneo mbalimbali na kisha kuweka ndani ya kapu moja la pamoja [Basket Fund] hivyo kwa mfumo huo inakuwa ngumu kwa mapato yanayopatikana toka kwenye migodi hiyo kubaki eneo husika.Hivyo anasema kuwa mfumo huo wa kukusanya fedha kidogo unapaswa kuangaliwa upya ili kuleta faida kwa eneo husika. Akasema chukulia mfano Wilaya Kahama ina migodi miliwili ya Bulyangulu na Tulawaka ambako kwa kila mgodi unabakiza kwa sasa dola laki mbili yani kwa ujumla dola laki nne,lakini anasema kama tukisema kahama ipate asilimia 20% ya mapato ya mgodi basi inaweza kupata dola millioni tatu.

Alipoulizwa Makapuni ya kigeni kubadilisha Majina kwa Makampuni ya kigeni Zitto alijibu kwa kusema ukwepaji mkubwa unafanywa na off shore yani makampuni ya kigeni yanatoka kwao yakiwa yamesajiliwa uko Nje ya Taifa letu Tanzania, lakini yanaingia Nchini na kuomba lesini ya kufanya biashara yakiwa na umilki wake huko nje.Hivyo mataifa yenye nafasi kubwa ya kutoa Tax heaven kama Uholanzi ambako kampuni kama Celtel Africa mmilki wa iliyokuwa Celtel Tanzania ilifunguliwa Uholanzi hivyo ilipouzwa Celtel Africa Nchini Uholanzi hivyo moja kwa moja Celtel Tanzania Inauzwa ikiwa ndani ya hiyo kampuni hivyo kupelekea maamuzi ya aliyenunua Celtel Africa uko Uholanzi kuwa na umilki wa uamuzi wa kuamua juu ya Celtel Tanzania.

Zitto pia kajadili kuhusu maswala Swali la Twiga Kusafirishwa Swalla repoti za kamati za Bunge.

Zitto anaomba sana Wanchi wahakikishe Accountabiliy na akaongeza Answer for Accountability

Maungumzo hayo yanendele sasa hivi Radio East Africa.
 
Natamani kungekuwa na gharika na kimbuga kama vya enzi za mitume na kuwapoteza watu wote wenye Upako wa Rushwa katika Tanzania. Ndani lindi la umasikini uliokithiri, waroho hawa bado wana wanawabana maskini wanaokesha kujikwamua na laana hii ya umaskini.
 
Ok, so (in between the Lines) Zitto anajaribu kujenga hoja ya kujustify wala rushwa, kutokana na theory yake ya jamii ya wala rushwa huzaa wala rushwa? naiona theory hiyo kuwa misguided sawasawa na statement wazitumiazo teenagers wakati wa kushawishiana kufanya ngono prematurely outside the wedlock, wenyewe husema 'everybody is doing it why should'nt I and You??, statements kama hizi zisingenishangaza kama zingetolewa na jamii ya magamba, lakini zinatia shock zikitolewa na mtu aliyetafuta kuwa kiongozi wa opposition camp!? yaelekea point aliyotaka kuwasilisha ni kuwa tusiwashutumu wala rushwa after all watu wengi wanakula rushwa, what a pathetic, wicked and reprehensible statement from an otherwise peoples representatives? Hivi hakuna jinsi yoyote ya kumfukuza zitto Chadema mapema iwezekanavyo ili akipenda ajiunge na magamba wenzake?
 
haa,haa,haa,Zitto ni Kichwa kajadili vitu kwa kina na kwa undani..Acha chuki binafsi..Zitto tuliokusikiliza tumekubali uwezo wako ni wa hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom