Zingatia haya kuimprove speed ya computer yako

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Wadau tukizingatia mabo haya inawezekana kabisa computer zetu zikawa na spidi nzuri tu.Haijalishi PC yako ina RAM ya 64MB au 2GB

1.Computer yako ikiwa inaboot usiisumbue iache iboot kabisa mpaka imalize ndo ufungue application yoyote.

2.Refresh desktop ukishafunga application yoyote.
Hii inasaidia kutoa mafaili yasiyo na kazi katika RAM

3.Usiweke picha zenye size kubwa kama wallpaper yako
Hii izingatiwe sana na wale wenye RAM ndogo

4.Usijaze mashortcut mengi kwenye desktop
Kila shortcut inachukua kiasi fulani cha nafasi kwenye RAM

5.Empty recycle bin yako mara kwa mara
Hii ni kwasababu mafaili ya kwenye recycle bin yako kwenye Hard disk yako bado na yanachukua nafasi.

6.Futa temporary internet files mara kwa mara

7.Fanya DEFRAGMENTATION ya Hard disk yako mara kwa mara.
Hii itayapanga mafaili vizuri kwenye computer yako na kuifanya ifungue applications kwa haraka

8.Ifanyie partition hard drive yako.Parition ya pili ndo uinstall program kubwakubwa kama Photoshop
Hii ni kwasababu windows inatumia nafasi yote katika C: drive kama virtual memory ikiwa RAM ya computer
yako imejaa

9.Ukiinstall software mpya usiiruhusu iweke tray icon kwenye taksbar.Pia disable option ya program kuanza automatically ukiboot.

10.Hakikisha computer yako haipati vumbi na kama ikipata vumbi isafishe vizuri.
Vumbi linafanya feni za computer yako zijam na kuifanya computer iwe overheated hivyo kuipunguza CPU processing speed.

NB:RAM ndo mahali pa kufanyia kazi pa computer yako hivyo jitahidi kupaacha wazi kadri uwezavyo


RAI:Tusikeshe kutafuta source ya kilichoandikwa kwenye post,bali tuangalie post inasaidia au haisaidii
Shukrani za dhati zimwendee babu yangu Mkulutumbi(JF Senior Expert Member)
 
RAM ya computer iko wapi hasa: disc C, D,au?

RAM Random Access Memory ni chip ambayo inakuwa kwenye Motherboard ya Pc. Zipo aina nyingi za inbuilt RAM; katika electronics Mbalimbali. Hata simu, printer hata redio yako in RAM!!
 
Back
Top Bottom