Zilizokuwa Dawa za CCM, Ndizo Sumu Zinazoiua CCM!

English Learner

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
355
355
Iwapo unaumwa, njia pekee ili upate kupona lazima upate matibabu. Na kwa wale wa imani za kileo matibabu yao ni kwa njia ya uponywaji. Lakini pia, wakati mwingine si mpaka uumwe. Unaweza kutumia dawa ili kujikinga na maradhi kabla hata hayajakufika. Kinga ni bora kuliko tiba, na pia ni vema kuswali kabla hujaswaliwa!

Naamu! CCM inayoongoza Serikali isiyokuwa na dini, nayo toka kale inazo dawa na sindazo zake za kinga na matibabu. Miongoni mwa dawa na sindano hizo ni UMOJA wa Kitaifa, UADILIFU wa Viongozi, CHEO kama DHAMANA, na UONGOZI Bora wa Watu Kujiletea Maendeleo yao Wenyewe. Vifuko vya dawa hizi, vingi vilijumuhiswa na kufanywa kifurushi kimoja cha dawa iitwayo AZIMIO la Arusha.

Taifa chini ya CCM lilipougua ukabila na udini, viongozi wa CCM walifanya utabibu haraka wakitumia dawa iitwayo UMOJA wa Kitaifa, rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma punde tu ulipoibuka, wale wote waliobainika mara moja walidungwa sindano ya UADILIFU. Na mwenendo wa Serikali katika kupambana na maadui (Ujinga, Umaskini, na Maradhi) wa Taifa ilikuwa si kutembeza bakuli la kuomba misaada toka Ulaya na Amerika bali kuwatumia VIONGOZI Bora kuwaunganisha wananchi katika kuchangia vipawa, ujuzi, na mali katika kujiletea maendeleo yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao. Na hii ndiyo ilikuwa dhana kuu ya UJAMAA na KUJITEGEMEA.

Lakini la ajabu, leo hii, CCM ndiyo kinara wa kuchua dawa ya kubomoa UMOJA wa Kitaifa kwa kuendekeza Udini na Ukabila. Tumelishuhudia hili wakati wa Uchaguzi Mkuu na limejirudia tena katika Chaguzi Ndogo za Igunga na Arumeru. Tumeona jinsi CCM ya leo inavyoshangilia wasio-WAADILIFU kuwadunga sindano za mauti Wanaopinga RUSHWA na UBADHILIFU wa Mali za Umma. Na kubwa zaidi sote tu mashahidi, kwa CCM ya leo Cheo si DHAMANA bali BIDHAA inayonunuliwa na Matajiri ili wafanikishe mambo yao kupitia migongo ya Wapiga kura.

CCM imefanikiwa kwa muda kugeuza matumizi ya dawa zake bila kudhurika. Habari njema ni kwamba, dawa zote sasa zimefikia ukomo wa matumizi na zimegeuka sumu tena kali. Kwa sasa, UMOJA unaanzishwa na Wananchi wenyewe kuikabili CCM. Wananchi hawakubali tena kugawanywa katika makundi ya kidini wala kikabila ili CCM ipenye kuwatawala tena. Wananchi wanawataka na wanawajua watu waadilifu. Na wanapojitokeza wanaogawa RUSHWA, wananchi wanaipokea na kuila lakini haibatilishi maamuzi yao yaliyo sahihi moyoni. Au wanaitumia hiyo pesa ya RUSHWA kumchangia mtu muadilifu wampendaye ili afikie hatma ya kuwa kiongozi wao. Hili limethibitika katika Uchaguzi Mkuu na limejirudia tena hivi karibuni huko Arumeru Mashariki. Kiongozi ambaye Wananchi wanamhitaji ni yule atakaye waongoza katika kutetea HAKI zao na kuwaunganisha KUJILETEA maendeleo. Kitendo alichokifanya Kilema mmoja huko Mwanza, cha kutoa Kuku wake wa Pasaka anadishwe katika Harambee ya kuchangia madawati iliyoongozwa na Mbunge Wenje ili naye achangie watoto kupata mazingira mazuri ya kusomea ni fundisho tosha kwa CCM na watoa RUSHWA.

Ili CCM ipone na dhahama ya sumu inayoendelea kuenea mwilini mwake, lazima kwanza itapishwe na kukamuliwa sumu zote (Ubaguzi, Rushwa, Ubadhilifu, Viongozi Uchwara/wafanyabiashara, n.k) na kisha ianze upya matumizi ya dawa zake za awali (UMOJA, UADILIFU, UONGOZI BORA, CHEO kama DHAMANA). Ni makosa ya makadirio ya kisiasa kwa CCM kufikiria jinsi itakavyobaki madarakani hapo 2015. Hili jambo haliwezekani bila matumizi makubwa yaliyopitiliza ya dola yatakaambatana na umwagaji wa damu isiyo na hatia. Kadirio sahihi kwa CCM ni kufikiri nini itakuwa “Fall-Back Position” hapo 2015 na nini kiandaliwe ili baada ya hapo warudi tena madarakani ndani ya miaka mitano (5). Ni rahisi kwa CCM kurudi ndani ya muda mfupi namna hii kwa sababu, pamoja na maandalizi yanayoendelea kwenye vyama vya upinzani kushika dola, bado ni yatima wa mipango na rasilimali watu makini wa kutekeleza na kukidhi matumaini ya Wananchi ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano (5). Vyama vya Upinzani vimefanya na vinaendelea kufanya makosa makubwa sana kwa kuacha wananchi kuweka matumaini makubwa kupitiliza juu ya nini watakifanya wakiingia madarakani. Wamewaaminisha wanancnhi kwamba kile walichoshindwa CCM kwa miaka 54 (hapo 2015) wao watakifanikisha ndani ya miaka mitano! Kwa kosa hili, wategemee kuchukiwa haraka sana na kupingwa na wananchi hao hao watakaokuwa wamewapa ushindi. Ebu nisitoke ndani ya mada maana hii tayari ni mada nyingine kabisa.

Nakutakia tafakuri njema.
 
well said, but at the end I don't think if you are right (my interpretation and analysis), but see, we have given ccm and its leaders about 50 years to rule this country instead of LEADING people to reach their EXPECTATIONS AND their dreams. Throughout all these 50 years we have seen our country going backward instead of going forward. Refer the number of industries we had in 1980s and the number of industries we have now, refer the number of unemployed people in 1980s and now days. Then see how poverty rate have increased, inflation, quality of education, number of failure students, poor health services and so many problems. All these show that we are Moving backwards instead of forward...

Really we need changes...these changes can only be brought about by changing the ruling party. Even though we can do this, but we don't have to EXPECT dramatic changes to be brought by new party which will replace CCM. Changes can not be brought within 5 years. In normal circumstances, its impossible to build all the foundations of our nations which have been destructed by CCM within 5 years. So we have to give time the new party so that we can experience the difference....
THANK YOU...M4C FOREVER....KEEP ON KILLING CCM AND ALL ITS MEMBER.....GOD BLESS US.

TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED.....YES WE CAN.....GOD BLESS CDM..AND AL OF US...
 
STK ONE,
Thank you for your insightful contribution. What I'm sure of is that change is inevitable. And what I'm guessing is the magnitude and time within which that changes are expected to be vividly realized. However, that change expected under fortcoming regime are unknowingly miscalculated or deliberately hyped. Lets wait and see.
 
[MENTION]Kadakabikile[/MENTION]
This is a good stuff for you

I wrote it in Swahili, easily to comprehend!

Iwapo unaumwa, njia pekee ili upate kupona lazima upate matibabu. Na kwa wale wa imani za kileo matibabu yao ni kwa njia ya uponywaji. Lakini pia, wakati mwingine si mpaka uumwe. Unaweza kutumia dawa ili kujikinga na maradhi kabla hata hayajakufika. Kinga ni bora kuliko tiba, na pia ni vema kuswali kabla hujaswaliwa!

Naamu! CCM inayoongoza Serikali isiyokuwa na dini, nayo toka kale inazo dawa na sindazo zake za kinga na matibabu. Miongoni mwa dawa na sindano hizo ni UMOJA wa Kitaifa, UADILIFU wa Viongozi, CHEO kama DHAMANA, na UONGOZI Bora wa Watu Kujiletea Maendeleo yao Wenyewe. Vifuko vya dawa hizi, vingi vilijumuhiswa na kufanywa kifurushi kimoja cha dawa iitwayo AZIMIO la Arusha.

Taifa chini ya CCM lilipougua ukabila na udini, viongozi wa CCM walifanya utabibu haraka wakitumia dawa iitwayo UMOJA wa Kitaifa, rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma punde tu ulipoibuka, wale wote waliobainika mara moja walidungwa sindano ya UADILIFU. Na mwenendo wa Serikali katika kupambana na maadui (Ujinga, Umaskini, na Maradhi) wa Taifa ilikuwa si kutembeza bakuli la kuomba misaada toka Ulaya na Amerika bali kuwatumia VIONGOZI Bora kuwaunganisha wananchi katika kuchangia vipawa, ujuzi, na mali katika kujiletea maendeleo yao kwa kutumia rasilimali za nchi yao. Na hii ndiyo ilikuwa dhana kuu ya UJAMAA na KUJITEGEMEA.

Lakini la ajabu, leo hii, CCM ndiyo kinara wa kuchua dawa ya kubomoa UMOJA wa Kitaifa kwa kuendekeza Udini na Ukabila. Tumelishuhudia hili wakati wa Uchaguzi Mkuu na limejirudia tena katika Chaguzi Ndogo za Igunga na Arumeru. Tumeona jinsi CCM ya leo inavyoshangilia wasio-WAADILIFU kuwadunga sindano za mauti Wanaopinga RUSHWA na UBADHILIFU wa Mali za Umma. Na kubwa zaidi sote tu mashahidi, kwa CCM ya leo Cheo si DHAMANA bali BIDHAA inayonunuliwa na Matajiri ili wafanikishe mambo yao kupitia migongo ya Wapiga kura.

CCM imefanikiwa kwa muda kugeuza matumizi ya dawa zake bila kudhurika. Habari njema ni kwamba, dawa zote sasa zimefikia ukomo wa matumizi na zimegeuka sumu tena kali. Kwa sasa, UMOJA unaanzishwa na Wananchi wenyewe kuikabili CCM. Wananchi hawakubali tena kugawanywa katika makundi ya kidini wala kikabila ili CCM ipenye kuwatawala tena. Wananchi wanawataka na wanawajua watu waadilifu. Na wanapojitokeza wanaogawa RUSHWA, wananchi wanaipokea na kuila lakini haibatilishi maamuzi yao yaliyo sahihi moyoni. Au wanaitumia hiyo pesa ya RUSHWA kumchangia mtu muadilifu wampendaye ili afikie hatma ya kuwa kiongozi wao. Hili limethibitika katika Uchaguzi Mkuu na limejirudia tena hivi karibuni huko Arumeru Mashariki. Kiongozi ambaye Wananchi wanamhitaji ni yule atakaye waongoza katika kutetea HAKI zao na kuwaunganisha KUJILETEA maendeleo. Kitendo alichokifanya Kilema mmoja huko Mwanza, cha kutoa Kuku wake wa Pasaka anadishwe katika Harambee ya kuchangia madawati iliyoongozwa na Mbunge Wenje ili naye achangie watoto kupata mazingira mazuri ya kusomea ni fundisho tosha kwa CCM na watoa RUSHWA.

Ili CCM ipone na dhahama ya sumu inayoendelea kuenea mwilini mwake, lazima kwanza itapishwe na kukamuliwa sumu zote (Ubaguzi, Rushwa, Ubadhilifu, Viongozi Uchwara/wafanyabiashara, n.k) na kisha ianze upya matumizi ya dawa zake za awali (UMOJA, UADILIFU, UONGOZI BORA, CHEO kama DHAMANA). Ni makosa ya makadirio ya kisiasa kwa CCM kufikiria jinsi itakavyobaki madarakani hapo 2015. Hili jambo haliwezekani bila matumizi makubwa yaliyopitiliza ya dola yatakaambatana na umwagaji wa damu isiyo na hatia. Kadirio sahihi kwa CCM ni kufikiri nini itakuwa "Fall-Back Position" hapo 2015 na nini kiandaliwe ili baada ya hapo warudi tena madarakani ndani ya miaka mitano (5). Ni rahisi kwa CCM kurudi ndani ya muda mfupi namna hii kwa sababu, pamoja na maandalizi yanayoendelea kwenye vyama vya upinzani kushika dola, bado ni yatima wa mipango na rasilimali watu makini wa kutekeleza na kukidhi matumaini ya Wananchi ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano (5). Vyama vya Upinzani vimefanya na vinaendelea kufanya makosa makubwa sana kwa kuacha wananchi kuweka matumaini makubwa kupitiliza juu ya nini watakifanya wakiingia madarakani. Wamewaaminisha wanancnhi kwamba kile walichoshindwa CCM kwa miaka 54 (hapo 2015) wao watakifanikisha ndani ya miaka mitano! Kwa kosa hili, wategemee kuchukiwa haraka sana na kupingwa na wananchi hao hao watakaokuwa wamewapa ushindi. Ebu nisitoke ndani ya mada maana hii tayari ni mada nyingine kabisa.

Nakutakia tafakuri njema.
 
ukitaka kufanya biashara ya vitabu unaweza kuwa milionea ukitumia mifumo ya ccm. Ina mafunzo mengi na vituko vya kusisimua vya kukaa kwenye simulizi.
 
Ni kweli kabisa CCM ilikiuka utamaduni iliwojiwekea yenyewe ya kuwa na viongozi WAADILIFU kama POUL SIOZIGWA na kuruhusu kubakwa na viongozi matapeli kama akina ADEN RAGE ambao background zao hawana hata chembe za sifa za uongozi
 
Salaam Wanabodi!

Huyu mtu aliingia madarakani mwaka 2005 huku akituhakikishia maisha bora kwa kila mtanzania na kusema kwamba kuchekacheka kwake kuna msimamo katika mambo ya msingi!

Jakaya Mrisho Kikwete alibeba matumaini ya watanzania maskini tena mafukara wa kutupwa akiwaahidi ahadi mbalimbali za Uongo mpaka kufikia kupata zaidi ya 80% kura zote zilizopigwa na kuwaacha mbali wapinzani wake! Ingawa mwaka 2010 zilishuka sana na kuna tetesi kwamba alishindwa uchaguzi!

Kinachonifanya nikate tamaa na rais wangu Jakaya M.Kikwete ni kushindwa kudhibiti vitu vifuatavyo.

(a).Deni la Taifa:
Ndugu rais wangu JK umeshindwa kudhibiti deni hili mpaka sasa tunaambiwa linafikia trilion 20,hivi una uhakika na uhalali wa deni hilo? Mbona uko kimya? Tulikopa ili kufanya nini? Tunapewa majibu mepesi kwamba ni umeme wa gesi na maji!hivi kweli umeme na maji ndio trilioni 20? Jamani rais Kikwete unatupeleka wapi nchi hii?

(b)Mfumuko wa bei
kwa uzoefu nilionao sijawahi kuona mfumuko wa bei wala kusikia kwa kiwango kilichofikiwa na serikali ya awamu ya nne ya rais Jakaya Kikwete tangu uhuru,mfumuko wa bei unatisha sana ndugu Rais kikwete watu wanalalamika sana na hasa vijana na akina mama.

(C).Udhibiti wa Rushwa.
Hivi sasa kwenye ofisi za serikali na hasa jeshi la polisi Rushwa imekuwa ni kitu cha kawaida sana! Ukienda kupata huduma bila rushwa bila rushwa kwanza mtoa huduma anakushangaa wewe vipi kwani hujui utaratibu wa ofisi? Kwa hapo unatuambiaje watanzania!

(d)Ufisadi wa Elimu wa baadhi ya mawaziri!
Mawaziri kiboko na wa ajabu wametokea kipindi hiki kama vile Mulugo(Amim)kununua cheti cha mtu na bado akapata uwaziri je kuna ajenda gani hapo? Ni fadhila au ni ukada?
(e)Mauaji ya raia wasio na hatia!
Rais uko kimya kabisa hatujui umekusudia nini katika nchi yetu au una malengo gani kwani umekuwa ukihudhuria misiba ya wasanii tu!

(F)Malumbano ya kidini.
Kulizungumzia hili inatakiwa kuwa na moyo mgumu sana,malumbano haya yameanza na kukua kwa kasi awamu hii ya nne,Je nchi inaelekea wapi?

Inanikatisha tamaa sana ninapowaza mambo hayo,je wewe mwana Jf una maoni gani? hii ni kwa mustakabali wa Nchi yetu.karibuni.!
 
Watetezi wa Serikali ya JK, watadai Rais ni msikivu, watadai Rais ni muumini wa demokrasia na utawala bora!
Mimi nasema, hatujapata kuwa na Serikali dhaifu kama hii tangu Uhuru, ingawa imeingia madarakani wakati kodi inakusanywa zaidi, hazina ikiwa imenona zaidi.
Ni awamu ambayo sheria haziheshimiwi, WaTz hawaviamini vyombo vya dola, na ufisadi umeota mizizi zaidi, uongozi na kuteuliwa uongozi kunaitwa "kuula".
Nathubutu kusema kuwa iwapo tutapata Serikali kama hii 2015 hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Hiyo ndiyo sirikali ya Jakaya Kikwete chaguo la Mungu kuwaudhi watanzania ili wajikomboe. Kuna kipindi kila shari huwa na neema na kila neema huwa na shari. Ni suala la waathirika kutathmini na kujitathmini na kuamua the way forward. Tusimlaumu Kikwete bali tutumie udhaifu wake kujikomboa na kuikomboa nchi yetu. Mbona nchi nyingine wameweza? Nani alituroga tuishie kulalamika badala ya kufanya kweli?
Watetezi wa Serikali ya JK, watadai Rais ni msikivu, watadai Rais ni muumini wa demokrasia na utawala bora!
Mimi nasema, hatujapata kuwa na Serikali dhaifu kama hii tangu Uhuru, ingawa imeingia madarakani wakati kodi inakusanywa zaidi, hazina ikiwa imenona zaidi.
Ni awamu ambayo sheria haziheshimiwi, WaTz hawaviamini vyombo vya dola, na ufisadi umeota mizizi zaidi, uongozi na kuteuliwa uongozi kunaitwa "kuula".
Nathubutu kusema kuwa iwapo tutapata Serikali kama hii 2015 hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Serikali inayoendekez propaganda na kutake advantage ya ujinga wa Watanzania siku wakijanjaruka nchi hii haitatawalika.

Deni la taifa linaongezeka kwa kasi kama speed ya ndege ya Fastjet kutoka Dia - Kia na wananchi bado tunachekelea.
 
Hiyo ndiyo sirikali ya Jakaya Kikwete... Kuna kipindi kila shari huwa na neema na kila neema huwa na shari. Ni suala la waathirika kutathmini na kujitathmini na kuamua the way forward. Tusimlaumu Kikwete bali tutumie udhaifu wake kujikomboa na kuikomboa nchi yetu. Mbona nchi nyingine wameweza? Nani alituroga tuishie kulalamika badala ya kufanya kweli?

Maandamano ya Mtwara, ni ujumbe kuwa hata wale waliodhaniwa kuwa vilaza wameshajua udhaifu wa serikali hii.
 
Serikali inayoendekez propaganda na kutake advantage ya ujinga wa Watanzania siku wakijanjaruka nchi hii haitatawalika.

Deni la taifa linaongezeka kwa kasi kama speed ya ndege ya Fastjet kutoka Dia - Kia na wananchi bado tunachekelea.

Si umeona watu wa Mtwara juzi? Ni ishara mbaya.
Serikali inayowaza kututawala kutumia hata hila za propaganda za kutugawa kidini na kikabila.
 
Ukweli uko waz, hatuna haja ya kujadili sana, na tusitegemee kitu kipya kwa miaka hii iliyobaki..! Ila tusichoke kupiga kelele, mana tukinyamaza nchi ndo itauzwa kabisa.!
 
aliposema Mnyika wengi hamkuelewa, afadhali wewe umeokoka leo. hii serikali ni dhaifu
 
Back
Top Bottom