Zilipendwa ananiomba ushauri, nimsaidieje?

Kwa ushauri wangu usimshauri chochote, piga kimya, inawezekana anakutega huyo.

inawezekana ananitega, lakini pia inawezekana hanitegi.
Mumewe keshahamia mbagala zaidi ya mwaka sasa.
Jamaa inaonekana amedhamiria mke lazima afanye atakavyo yeye.
 
Jamani ndoa hizi Mungu atusaidie. Na wengine ndio tunataka kuingia.:msela:

Usiogope kuingia,
Muhimu zaidi ni kumfahamu vizuri mtu unayekusudia kuishi naye.
Lakini kama unataka kuoa/kuolewa kwa kufuata mkumbo,ama unatamani sherehe ya harusi usithubutu.
 
Anaatakiwa tu ende mbagala kwa mumewe na gari lake akifika huko yeye kama mwanamke atajua namna ya kuongea na mumewe. sidhani kama mume atamfukuza.
 
Usiogope kuingia,
Muhimu zaidi ni kumfahamu vizuri mtu unayekusudia kuishi naye.
Lakini kama unataka kuoa/kuolewa kwa kufuata mkumbo,ama unatamani sherehe ya harusi usithubutu.

Lakini mkuu watu pia huwa wanabadilika, unaweza ukawa confident kwa kipindi hicho kuwa 'huyu ndio wangu wa kufa na kuzikana' ila kibao kinapokuja kubadilika unaweza kutamani kifo kuliko kuishi.

Anyway, ninamuomba Mungu katika hili anisaidie na aniongoze......maana kwa akili zangu za kibinadamu sidhani kama nitaweza.
 
Apime anapenda gari na nyumba, au mume...

Mkuu ukisema hivyo utakuwa hujamtendea haki huyo dada. Si huyo kaka alimuoa akiwa na gari yake, kwa nini sasa amwambie aliuze na ni kwamba hiyo gari wanaihitaji. Mwanaume yuko na inferiority complex ambayo ukweli haiwezi kutibiwa kwa huyo dada kuhamia mbagala au kuuza gari.

Poor me.......i thought love suppose to be unconditional........(sijui naishi kwa dunia gani)
 
Sasa mtu ameondoka mwaka sasa, dada bado anataka ushauri? mwanaume gani huyo hata akili kidogo tu ya kuwaza hana? mtu anafanya kazi posta umpeleke kuishi mbagala si bora hiyo nyumba ingekua yao wamejenga ila ya kupanga mbali kote huko. Wanawake wengine kupenda gani uko? au ndio unaogopa kwamba watu watakucheka huna mume? aghrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr mi ningemchunia tu kama ananipenda atakaa chini tuelewane kama akikataa basi hakupangwa kuwa wangu.
 
Well said kbd mtu anakua ana masharti + makero + magubu huyo dada akienda mbagala siku nyingine ataambiwa wahamie chanika, akiuza gari siku nyingine ataambiwa auze hata hereni zake watu wa hivyo hawabadilikagi kila siku atakua anaanzisha jipya nakwambia. Ila ndio hivyo mapenzi bwana ni kitu cha ajabu sana mi nakushauri mwita huyo dada usimshauri chochote muache mwenyewe aamue anataka nini, wapenzi unaweza kumshauri vizuri lakini akikutana na mwenzie anapuuza na anaweza hata kukutaja fulani kanishauri hivi.
 
Usiogope kuingia,
Muhimu zaidi ni kumfahamu vizuri mtu unayekusudia kuishi naye.
Lakini kama unataka kuoa/kuolewa kwa kufuata mkumbo,ama unatamani sherehe ya harusi usithubutu.

Mwita Maranya umeongea point,cha muhimu kweli ni kufahamiana vizuri na huyo unaetegemea kuishi nae.
 
Lakini mkuu watu pia huwa wanabadilika, unaweza ukawa confident kwa kipindi hicho kuwa 'huyu ndio wangu wa kufa na kuzikana' ila kibao kinapokuja kubadilika unaweza kutamani kifo kuliko kuishi.

Anyway, ninamuomba Mungu katika hili anisaidie na aniongoze......maana kwa akili zangu za kibinadamu sidhani kama nitaweza.

Ni kweli wakati mwingine watu hubadilika, lakini kama ulimuomba Mungu na akakupatia huyo mwenzio hata akibadilika si kiasi cha kukukimbia ama kukupa masharti magumu yasiyokuwa na manufaa kwa familia yenu.
 
Mtalaka hatongozwi mzee. Huyo ndo vile kakukumbuka. Ushauri kitu gani bwana.....mi sio tatizo hapo.
 
Sasa mtu ameondoka mwaka sasa, dada bado anataka ushauri? mwanaume gani huyo hata akili kidogo tu ya kuwaza hana? mtu anafanya kazi posta umpeleke kuishi mbagala si bora hiyo nyumba ingekua yao wamejenga ila ya kupanga mbali kote huko. Wanawake wengine kupenda gani uko? au ndio unaogopa kwamba watu watakucheka huna mume? aghrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr mi ningemchunia tu kama ananipenda atakaa chini tuelewane kama akikataa basi hakupangwa kuwa wangu.

Maty,
ndoa si nyepesi kiasi hicho ndugu yangu, tena wamefunga ndoa kanisani, si kwamba walichukuana kienyeji.
Pamoja na kukaa mbali na mumewe mwaka mzima lakini anahitaji kuinusuru ndoa yake.
Kumbuka tayari wana mtoto, na mtoto anahitaji malezi na mapenzi ya wazazi wote wawili.
 
[/B]

Well said kbd mtu anakua ana masharti + makero + magubu huyo dada akienda mbagala siku nyingine ataambiwa wahamie chanika, akiuza gari siku nyingine ataambiwa auze hata hereni zake watu wa hivyo hawabadilikagi kila siku atakua anaanzisha jipya nakwambia. Ila ndio hivyo mapenzi bwana ni kitu cha ajabu sana mi nakushauri mwita huyo dada usimshauri chochote muache mwenyewe aamue anataka nini, wapenzi unaweza kumshauri vizuri lakini akikutana na mwenzie anapuuza na anaweza hata kukutaja fulani kanishauri hivi.

Ahsante kwa ushauri wako.
 
Amwache aende mbagala, na hataki gari, akapande dirishani kivyake...

Mama kama unampenda sana mfuate kama vipi mpotezee!
 
Maty,
Haya maneno ya signature yako yanaweza kuwa na ujumbe mzito kwa huyu shostito, au we unasemaje?

"If you love something, set it free. If it comes back, it was, and always will be yours. If it never returns, it was never yours to begin with"
 
Mme wa huyu dada ana matatizo
Kwani akikaa kwenye hiyo nyumba na akaendelea kulipa kodi ya nyumba yeye ni tatizo???
Na gari kwa nini iuzwe ???
Mambo mengine bwana ni hekima kidogo inahitajika
umeongeza masuali tu, hujatoa solushen mheshimiwa mke wa rais
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom