Zilipendwa ananiomba ushauri, nimsaidieje?

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Wadau naomba mnisaidie kuchanga mawazo.

Zilipendwa wangu tuliyeachana miaka mitano iliyopita amenipigia simu anaomba ushauri.

Anasema mume wake amemtelekeza yeye na mtoto wake tangu alipokuwa na ujauzito wa miezi minne.Huyu shostito anafanya kazi kampuni moja ya simu na mumewe anafanya kazi serikalini.

Kisa cha mume kumkimbia ni kuwa mwanamke amekaidi kutekeleza matakwa yake. Mume anataka mkewe auze gari aliyonunua kabla hawajaoana na wahame toka kwenye nyumba wanayoishi mwenge iliyolipiwa na mke.Mume alihamia nyumbani kwa mkewe kabla hawajaoana, na mwanamke alinunua gari kabla hawajaoana, na jamaa hakuchangia hata senti moja.

Mwanamke kakataa kuuza gari ila amekubali kuhama nyumba kwa masharti kwamba iwe ni maeneo ya mwenge, sinza, kinondoni, ubungo ama mabibo. Mumewe anataka wahamie mbagala, kwamba ndipo anaweza kumudu kulipa kodi ya nyumba, hataki mkewe aongeze hata senti.Mume kuona mwanamke hatekelezi matakwa yake akaona isiwe tabu, kafunga virago amehamia mbagala.

Wadau mnisaidie, nimshaurije huyu shostito?
 
duuu, Inferiority Complex, jamaa anajishuku kuwa watu wanamuona kuwa kaolewa,
tatizo ni kuwa jamaa anajihisi kuwa watu walimuona huyo mama single na amepanga nyumba yake na ana gari lake mwenyewe, sasa kidume alipoingia kwenye nyuma akaonekana kana kwamba hana kitu alichokuja nacho zaidi ya vile vya mwana mama,

Ndoa zina mambo sana, kwa kweli hapo ushauri hauwezi kupatikana kwa maandishi humu, ushauri wa kweli unapatikana kwa kuongea nao hao wahusika ili uone kauli ya mama na kisha baba
 
Wakati mwingine sio lazima uwe na jibu la kumpa ndugu yangu, maana kuna ka mtego hapo! I hope you are a man enough to know what am saying!
 
Mme wa huyu dada ana matatizo
Kwani akikaa kwenye hiyo nyumba na akaendelea kulipa kodi ya nyumba yeye ni tatizo???
Na gari kwa nini iuzwe ???
Mambo mengine bwana ni hekima kidogo inahitajika
 
huyo mwanaume hajiamini,na zaidi sana anataka amtawale sana mwanamke kinachomshinda nyumba kapanga mwanamke na gari sio yake.lol.
ningekua mimi...nisingekubali kuuza gari, kwa misngi ipi? kwani halina kazi hapo? na kwa nini kuhamia mbali?
hmmm nahisi kuna upungufu wa elimu na kutokujiamini.
 
Jamani ndoa hizi Mungu atusaidie. Na wengine ndio tunataka kuingia.:msela:
 
duuu, Inferiority Complex, jamaa anajishuku kuwa watu wanamuona kuwa kaolewa,
tatizo ni kuwa jamaa anajihisi kuwa watu walimuona huyo mama single na amepanga nyumba yake na ana gari lake mwenyewe, sasa kidume alipoingia kwenye nyuma akaonekana kana kwamba hana kitu alichokuja nacho zaidi ya vile vya mwana mama,

Ndoa zina mambo sana, kwa kweli hapo ushauri hauwezi kupatikana kwa maandishi humu, ushauri wa kweli unapatikana kwa kuongea nao hao wahusika ili uone kauli ya mama na kisha baba

Kuongea nao wote wawili ndio kitu kigumu kidogo,
manake mumewe asije akahisi kwamba ninahuskia kumpa kiburi mkewe, kwanza nitaanzaje kuongea na mumewe kiongozi wangu.
 
Kuongea nao wote wawili ndio kitu kigumu kidogo,
manake mumewe asije akahisi kwamba ninahuskia kumpa kiburi mkewe, kwanza nitaanzaje kuongea na mumewe kiongozi wangu.

Mbon una presha sana na ndoa ya watu?unamtamani huyo dada tena nini,ushauri HAMIA KWAKE WEWE
 
Mme wa huyu dada ana matatizo
Kwani akikaa kwenye hiyo nyumba na akaendelea kulipa kodi ya nyumba yeye ni tatizo???
Na gari kwa nini iuzwe ???
Mambo mengine bwana ni hekima kidogo inahitajika

Mama wa kwanza,
bibie anasema mumewe anataka auze gari halafu wachangiane kununua gari nyingine.
Anataka wawe gari yao, sio gari ya mke wake. Haya ndo maajabu, hivi kumbe kwenye ndoa kila mtu anakuwa na chake?
 
Mbon una presha sana na ndoa ya watu?unamtamani huyo dada tena nini,ushauri HAMIA KWAKE WEWE

Punguza jazba kidogo kiongozi wangu,
sina pressure na ndoa yake, mimi nimeombwa ushauri, namimi nikaja kuwashirikisha hapa mnisaidie ushauri utakaomfaa.
Sasa nikihamia kwake kiongozi nitakuwa nimemsaidia?
 
Mwanaume alivyoumbwa, akihisi tu yupo chini ya mwanamke kwa chochote kile, kama hajajifunza maisha
Akaelewa vizuri ni kero kubwa kwa mwanamke.

Hata jambo dogo tu ukikosea au ukihoji anaona umemdharua yani ni very very iritative!

Daaa huyo dada bora awe na msimamo tu, ya nini kurudia umaskini wakati Mungu amembariki, manake anakoelekea lazima amwambie auze nyumba.

Asiuze gari wala nyumba asihame, halafu muone alivyo huyo eti ahamie mbagala haoni hata hiyo gharama ya nauli na muda. Alaaa dada usiukubali umaskini kirahisi rahisi. Achana nae huyo. Don't Spoil your Life into that Man.
 
Apime anapenda gari na nyumba, au mume...

Bado anampenda mumewe na anamhitaji. Hata kuuza gari lake ili wanunue jengine la wote kama anavyotaka bwana haoni shida.
Shida iko kuhamia mbagala. Anafanya kazi kwa shift, sasa akitoka shift ya usiku atafikaje mbagala peke yake? je akiporwa gari mmewe atamuelewa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom