Zikwepeni bidhaa bandia asema Mufuruki

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
WATANZANIA wametakiwa kuzikwepa bidhaa bandia zilizozagaa nchini, ili kuisaidia serikali katika jitihada zake za kupambana na uingizaji wa bidhaa hizo. Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Biashara Nchini, Ali Mufuruki.

Alisema ili kuisaidia serikali katika mapambano yake dhidi ya bidhaa bandia, wananchi wanapaswa kuzikataa kwa kuacha kuzinunua. "Kama wananchi watazikataa bidhaa hizo kwa kuacha kuzinunua ni wazi kwamba hazitaingizwa nchini kwa kuwa zitakosa soko," alisema Mufuruki, alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka la Woolworth lililopo Mikocheni.

Nionavyo mimi jukumu la kuzuia bidhaa feki zisizagae nchini ni la Serikali kwani ndo inayomiliki dola. Kudhibiti bidhaa feki ni rahisi sana kama serikali ikiamua. Kwanza entry points za bidhaa zote hizi zipo chini ya serikali, Pili sheria ziwekwe vizuri/zisimamiwe ipasavyo badala ya maafisa wenye dhamana kula rushwa, tatu badala ya viongozi wetu kwenda Marekani kucheza na akina 50 Cent, waende ulaya kujifunza mfumo waliotumia nchi za wenzetu walioendelea kudhibiti bidhaa feki. Naomba msitubugudhi katika hili tunalipa kodi ya kutosha kuhudumiwa na Serikali. Umeme mshindwe, Maji mshindwe, ufisadi muushindwe, jamani hadi kudhibiti bidhaa feki nayo mshindwe?????
 
Back
Top Bottom