Zijui Sifa kuu tatu za Kikwete

Another Scandal,hawa ndio waliolishwa yamini,It is a symbol of Al Fasad.Mungu atuepushie Mbali watu kama hawa.Kama ungejua utumbo unaofanyika usingesema haya.

KAMA INGEKUWA HAPA JF TUNATUMIA MAJINA YETU HALISI NINA UHAKIKA WENGI WASINGE INGIA HUMU KWANI HUENDA NI MAFISADI WAKUU. KAMA SIO WAO BASI BABA AU BABU ZAO NI MAFISADI.
 
Ahsanteni kwa michango yenu mizuri. U guys are very right. Kikwete angetaka heshima angejiheshimu yeye kwanza kabla ya sisi kumheshimu. Afterall kuyasema yale mtu anayoyafanya sidhani kama ni kutomheshimu kwani ndio wasifu wake Kikwete.

Kikwete amesahau kwamba hii nchi na hiyo nafasi ya urais amepewa na watanzania kwani amefanya hii nchi ya kikundi fulani kidogo ambacho kinaweza kufanya lolote juu ya rasilimali zetu na asiwepo wa kuwafanya lolote. Kikundi hichio ni cha yeye kikwete,el,rostam,kadamage,mramba,meghji na wengine. Ni ngumu kuamini kwamba mtu kama meghji,mramba na rostam bado wanapeta. Meghji na Mramba kwa kashfa ya EPA na rostam kwa kutajwa kwenye report ya CAG kwa kuliibia taifa bil 6 kupitia makampuni yake. Hakuna wa kuwachukulia hatua kwani kikwete ni mwenzao.

Na haya maigizo ya audit report ya E&Y ndio yanazidi kumdhalilisha jk bahati mbaya kwamba yy halioni hilo.Its fun kwamba report unayo badala ya kuchukua hatua kama rais unaunda tume nyingine kuchunguza uchunguzi kwa gharama ya wale wale walioibiwa bil 133. Huu utoto na upuuzi mpaka lini jamani?

Mbali kusema atawatangaza hadharani (rais anasema utumbo kama huu sijui ni nani wa kuchukua hatua) wezi wa miradi ya wananchi alishawahi kusema anawafahamu wala rushwa anawapa muda wajirekibishe-Huyu ni rais au msanii tu fulani wandugu??. So TAKUKURU wanachofanya ni kumpelekea majina then jk anawapa muda wajirekibishe mpaka lini na nini kitakuwa kimebaki no one knows. Hv hawa vibaka mtaani nani atawapa muda?

USHAURI WA BURE

'IPENDE NCHI YAKO KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE MWENYEWE NA USIICHUKIE NCHI YAKO KAMA UNAVYOJICHUKIA'
 
imetolewa mara ya mwisho: 01.02.2008 0123 EAT- MAJIRA
Kikwete atikisa mawaziri,wabunge

*Akerwa na waliojigeuza wafanyabishara
*Asema watu wanatilia shaka uadilifu wao

Na Hassan Abbas

RAIS Jakaya Kikwete ameweka bayana kuwa sasa viongozi wa kisiasa wa kada ya ubunge na uwaziri watalazimika kuchagua moja; siasa au biashara, msimamo unaoashiria bayana kurejea katika misingi ya Azimio la Arusha la mwaka 1967.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika hotuba yake ya kawaida ya kila kwa Taifa ambayo pia ni ya kwanza mwaka huu na ya pili tangu atimize miaka miwili ya uongozi, Desemba 21 mwaka jana.

Katika hotuba hiyo aliwaahidi Watanzania kuwa atasimamia maslahi ya Taifa katika kushughulikia suala la ufisadi mkubwa uliobainika kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akitoa msimamo wake huo kuhusu siasa na biashara katika Serikali yake, alisema tayari kuna ushahidi wa kuonesha migongano ya kimaslahi;
" Napenda kulizungumzia suala la viongozi wa siasa mawaziri na wabunge kuwa pia watu wanaojihusisha na shughuli za biashara moja kwa moja.

"Upo ushahidi wa kuwepo migongano ya maslahi kwa baadhi. Lakini, pia, hata pale ambapo hakuna dalili za wazi, hisia za kupata manufaa yanayotokana na nafasi zao hutawala. Matokeo ya yote hayo ni watu kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wa viongozi wetu
Jamani kweli kama KIKIWETE is serious then i believe Meghji,Mramba, Karamagi & co will do honourable thing na ku resign
 
'IPENDE NCHI YAKO KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE MWENYEWE NA USIICHUKIE NCHI YAKO KAMA UNAVYOJICHUKIA'
bado wajichanganya? nchi na kiongozi ni vitu viwili tofauti.hapa swala ni kiongozi ambaye alitoa ahadi kwa wananchi kabla hajachaguliwa...alisema atatetea walala hoi...give us any proof ya serikali yake kutetea masikini...wamachinga(self employed) wanafukuzwa hawana mahali...mafundi garage libya st wanaondolewa hawana pa kwenda....wapiga madebe wasitishwa hawapewi alternative kazi...na wakati huo kina Karamagi..Meghji yaani Kikwete cronies wana jifaidisha
 
Daily News On Saturday; Friday,February 01, 2008 @19:01
By Adam Lusekelo

THE prez, and AU chairman, Jack Mrisho, has told public rulers to chose to trade or become real politicians. They have chosen both. And there is nothing Jack can do – maybe fire them outright..

You see there is the selfishness which is inborn in mankind. We spend the rest of our lives trying to control that basic instinct. But most of us fail. So we succumb to greed.
You have money, so you also want to be an MP. But that is not enough. How about being a minister? Even that is not enough. You want to be a prime minister.

But that also is not enough. How about wanting to be the president? That is cool. But, believe me dear reader, even that is not enough. After president they even eye the post of the Almighty himself. They want to be God!

As the prez, you can't ask those psychological types to choose. They will want to be both – businessmen and politicians. One feeds on another. If you have a bus company you would also like to sit at the Bunge in Dodoma . There you can lobby for another hefty loan for 25 buses from the ministry of transport and whatever. You talk to the movers and shakers themselves.

If you want to sell power to Tanesco, you support things like fake dealers calling themselves Richmond . The deal sails through like a ship in calm waters. Dare I say that the rich guys are swarming to join the parliament to go and do business there - not to represent their constituents.

So it's me, me and me alone in their psyche. You cannot tell those guys to choose. You simply fire them. I know that the game could be tricky. Most politicians cum businessmen have actually bought their way to the political positions. Some have used their businesses to oil the wheels of os some political parties.

This really is Jack Mrisho's ball game. I also welcome the planned sweeping reforms to the existing leadership ethics legislation. But, believe me, those businessmen posing as politicians will never voluntarily choose between the two. The prez has just to bite and bullet and just kick them out.

But Mzee Ndesamburo, an MP, had something to say when he said: "You can't separate politics and business…in the past , such a thing was tried and it failed. If this law is eventually passed , I will hand over control of my business to my children and grandchildren…and continue with politics." he said.

That's great honesty by Mzee Ndesamburo. They all will do that and declare that they don't run any businesses. By the time the law is passed, those businesses will be owned by baby ‘directors' in nappies busy sucking their thumbs!
 
I gave him 12 months to put his act together. We all know the results after 24 months.
Tanzanians had so many hopes from his promises, but he is hopeless and don't know what to do as a leader. I hope this guy will not run again in 2010.
 
bado wajichanganya? nchi na kiongozi ni vitu viwili tofauti.hapa swala ni kiongozi ambaye alitoa ahadi kwa wananchi kabla hajachaguliwa...alisema atatetea walala hoi...give us any proof ya serikali yake kutetea masikini...wamachinga(self employed) wanafukuzwa hawana mahali...mafundi garage libya st wanaondolewa hawana pa kwenda....wapiga madebe wasitishwa hawapewi alternative kazi...na wakati huo kina Karamagi..Meghji yaani Kikwete cronies wana jifaidisha

Hoja zako dhaifu sana, hivi pale Libya ni mahali pa kutengenezea magari? you are kidding.
Wamachinga wametengewa maeneo, kweli au sio kweli?
Wanachotakiwa kufanya huko kwenye maeneo yao wajiimarishe kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kupiga hatua zaidi na hatimaye waweze kuwa na biashara za uhakika. Hakuna mtu au chama chochote kitakachokuleta pesa ndani ya mifuko yako. Kila mtu afanye kazi halali kwa kufuata taratibu hasa za mipamgo miji na kukuza mtaji wake. Ukifanya kinyume na hapo utakuwa unajipotezea wakati.

Wapiga debe = vibaka hawa wapigwe marufuku kabisa hiyo siyo kazi.
 
Wana JF nina wazo, ninaomba mlipitie na tulifanyie kazi kama inawezekana.
Kutokana na mtazamo wangu, wachangiaji wengi hapa kama sio wote ni wazalendo na wanauchungu na nchi yetu. Kwa sababu hiyo inawezekana kabisa kuna watanzania wengi sana wenye uchungu sana na nchi yetu, ila hawajajua waanzie wapi.
Ninaomba wana JF, kwa kutumia hii Blog yetu muhimu tuandae riport moja itakayoonyesha mambo yote yanayoendelea na yaliyofanyika hapo Tanzania, hadhari zake tuzieleze kwa undani kabisa, na tujaribu kuelezea nini kinakuja mbele yetu. Sasa basi baada ya kufanya hilo.
Kwa sababu watanzania wengi nadhani hawajajua hii blog, tutumie email forwarding service kuisambaza hiyo nakala yetu, ili isomwe na watanzania wengi, ili waelewe haya mambo ya hawa Mafisadi vizuri, Na kisha waelezwe ni wapi tunapambana na hawa jamaa ili watuunge mkono katika kazi hii ngumu ya kupambana na majizi na kulikomboa Taifa letu lililokuwa Tukufu enzi hizo.
Nadhani kwa kufanya hivi tutapaka wachangiaji wengi sana na kupata mambo mengine mengi yanayoendela na mwisho wa siku mapinduzi yatafikiwa kwa kupitia hapa hapa kwenye Keyboard tu
Naomba kuwakilisha wana JF

BADO NINA MASHAKA MAKUBWA NA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI.

UNAISHI WAPI?
 
Pundamilia07
Sijui unaishi katika dunia ipi? Hivi kama raisi akiwa anakumbatia wezi,wala rushwa na wazembe kuna haja ya kuendelea kumheshimu? Hivi unajua wakati wewe unaongea hapa hujui kuwa kuna asilimia kubwa tu ya watanzania wanateseka na kufa kwa kukosa huduma muhimu za kijamii? kama raisi wetu angelitumia mamlaka aliyopewa unafikiri Tanzania ingekuwa hapo? Hebu tu fikiria kashfa ya BOT inahusu wizi wa zaidi ya milion 100? hujaangalia Buzwagi na nyinginezo ambazo mimi na wewe hatuzijui? na haya yanatokea mbele ya huyo muheshimiwa je huu ni utu? je huyu mtu anapaswa kuheshimiwa bado?
Mimi naipenda sana nchi yangu na ninaamini kuwa watanzania hawapaswi kuishi maisha magumu namna hiyo huku wakuu wakiponda maraha kupindukia! halafu eti tukae hapa tukiimba wimbo wa kuwaheshimu ...no nasema noo.
 
Jazba, Chuki binafsi, husda na ukosefu wa hekima na busara vimetanda hapa JF.
Lakini kwa kifupi ni kuwa mama yako akishakwambia huyu ndiyo baba yako huna budi kumheshimu.

Kumkoma nyani mpaka giladi ndio hii Pundamilia, bravo!

By the way, mkuu Babah! karibu tena JF.
 
.......haya ngoja nijaribu kumjibu huyu Pundamilia

Jazba, Chuki binafsi, husda na ukosefu wa hekima na busara vimetanda hapa JF.

.......That can can be your own interpretation......call it whatever......ukweli unabaki kuwa ukweli Nchi yangu TANZANIA IKO NJIA PANDA.........moreover unatukosea adabu wengi wetu ambao tunaona mustakabali wa Taifa haueleweki, kwa kuona kuanzia IPTL, RADA (ambayo Rais huyo huyo aliwaomba watu wamsaidie kurudisha baadhi ya pesa zilizozidi/zilizoibiwa....very funny), RICHMOND, BUZWAGI, BoT, Pesa za wajasiriamali kutoka Japan, nk nk nk nk .....................haya yote mtu mwenye akili timamu huwezi kukaa kuimba "Kill me Softly"

Lakini kwa kifupi ni kuwa mama yako akishakwambia huyu ndiyo baba yako huna budi kumheshimu.

.......Agreed, na baba asipotimiza wajibu wake watoto wanakufa kwa maradhi, njaa na kukosa elimu, future iko wapi??.......what a father!!!!

As long as watanzania walimchagua Mh. Kikwete kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hamna budi kumheshimu kama RAIS.

......Only if akitekeleza yale yanayotakiwa kwa ajili ya manufaa ya taifa letu kwa ujumla wake

Kamwe sitakaa kimya kuona Rais wa nchi yangu anadhalilishwa kwani ni wajibu wangu kutetea taifa langu.

........Yes hakuna mtu anayependa Rais wa nchi yake akidhalilishwa..............but again.........kudhalilishwa kuna tofauti kubwa na kuambiwa ukweli........kama kuambiwa ukweli mtu ni kumdhalilisha.....then be it........kumbuka hapa some watu here are hyprocrite like you.......however ukiongea/ukileta sera mbovu JF wanachambua pumba na kuweka pembeni mchele........mchana kweupee

Nitailinda nchi yangu Tanzania na nitawaheshimu viongozi waliopewa dhamana na wananchi.

....Ohhh yes wote twailinda nchi yetu kwa kufichua maovu......na kuwaeleza ukweli viongozi pale wanapokosea.........viongozi wengi walioko madarakani........im sorry ni WABOVU, wametufikisha mahala ambapo, wapuuzi wanakuja na $5 na kuondoka na Billions.........na ndio maana hata JK anawaambia kuwa eti wachague uwaziri au Biashara.........however.....hapa JF tumeshaliona hilo kuwa ni CHANGA LA MACHO

Nitailinda nchi yangu na kuitetea wakati wote dhidi ya wadhalimu wachache.

......OOhh yeah wadhalimu ni wale wanoona unayeona uovu/hatari na kuunyamazia kimya.......may be you are among them!!!!

Nitajitahidi kujadiliana juu ya mustakabali wa nchi hii kwa uwazi bila ya kudharau mamlaka zote halali zilizowekwa kwa ridhaa ya wananchi
Ninaipenda nchi yangu na ninajivunia kuwa Mtanzania.

.......This is what we do at JF...wher we dare to talk openly bila unafiki

Mungu tuongeze hekima na busara watanzania

......Yes...tena wale wanaoona uovu na kuunyamazia

na uibariki nchi yetu na wananchi wake.

......Thanks and AMINA
 
Mungu tuongeze hekima na busara watanzania na uibariki nchi yetu na wananchi wake.

WEWE NDIO HUNA HEKIMA....WEWE UNAIPENDA TANZANIA KULIKO NANI HAPA??!!.............WAZALENDO NDIO SISI...TUNAIPENDA TANZANIA KULIKO TUNAVYOJIPENDA..YOYOTE ANAYEICHEZEA NA KUIFUJA AU KUIFISADI ..TUTAMSEMA..PIA ANAYELEA MAFISADI NAYE NI FISADI!!

NDIO TUNAIPENDA NCHI YETU PAMOJA NA KUWA HATUPATI MARUPURUPU...KUNA WANAYOIPENDA NCHI HII KWA AJILI WANAFAIDIKA NA SYSTEM..SISI TULIOWENGI HATUPATI MALIPO..MALIPO YETU YATAFSIRIWE KWA KUPELEKA HUDUMA BORA KWA WOTE ...NA KUPUNGUZA PENGO KUBWA LINALOKUWA KATI YA MASIKINI NA MATAJIRI......SASA KAMA HIYO NI UKOSEFU WA BUSARA...BASI HATUNA BUSARA!!!!
 
Ogah, Ogah,Ogah I bet you Nigerian blood from Agege.

I give you five for the truth.
 
Pundamilia07
Sijui unaishi katika dunia ipi?

Wembemkali, hivi kuna dunia ngapi? nifahamishe, nijuavyo mimi dunia ni moja.

Hivi kama raisi akiwa anakumbatia wezi,wala rushwa na wazembe kuna haja ya kuendelea kumheshimu?

Si kweli ninakanusha kauli yako, Rais hajakumbatia wezi, wala rushwa na wazembe.

Hivi unajua wakati wewe unaongea hapa hujui kuwa kuna asilimia kubwa tu ya watanzania wanateseka na kufa kwa kukosa huduma muhimu za kijamii?

Tafadhali lete data kamili kwa sababu si vema kukukatalia au kujadili zaidi bila ya data na source yake.

kama raisi wetu angelitumia mamlaka aliyopewa unafikiri Tanzania ingekuwa hapo?

Hujaeleka!!!

Hebu tu fikiria kashfa ya BOT inahusu wizi wa zaidi ya milion 100?

Nadhani hii habari ya BoT huifahamu vizuri zaidi ya kuwa labda shabiki tu, unajua kiasi gani hasa kinachoongelewa BoT?

hujaangalia Buzwagi na nyinginezo ambazo mimi na wewe hatuzijui? na haya yanatokea mbele ya huyo muheshimiwa je huu ni utu? je huyu mtu anapaswa kuheshimiwa bado?

Sijui fikra zako ziko wapi, lakini sidhani kama Rais huwa anakaa mahali kama mlangoni hivi kama bawabu na kuangalia kila kinachotoka na kuingia.
Wote tunajua hatua mbalimbali ambazo Mh Rais ameshazichukua dhidi ya masuala yote ambayo tumeyasikia.
Ameunda tume kushughulikia mikataba ya madini na kwa nia njema kabisa, akielewa hii ni nchi yetu sote ameshirikisha na viongozi toka katika vyama vingine vya kisiasa.
Jambo hili limo katika dhamira yake ya kuwashirikisha wanasiasa wa vyama vingine katika kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wa nchi yetu.
Juu ya sakata la BoT wote tunajua kuwa aliagiza mchakato ufanyike hadi ripoti imetolewa zaid ya hapo ameagiza ripoti ifanyiwe kazi ili hatua kadhaa zichukuliwe.
Kwangu mimi baada ya uchunguzi huo taarifa kwangu ni hatua gani zichukuliwe hali iliyojitokeza isijirudie tena na kuahakikisha kama kuna matatizo mengine yafanyiwe kazi kabla hayajaleta athari zaidi. Ikibidi pia kama kuna mapendekezo ya kubadilisha sheria basi muswaada utayarishwe kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Mimi naipenda sana nchi yangu na ninaamini kuwa watanzania hawapaswi kuishi maisha magumu namna hiyo huku wakuu wakiponda maraha kupindukia! halafu eti tukae hapa tukiimba wimbo wa kuwaheshimu ...no nasema noo.

Ninakubaliana kuwa watanzania hawapaswi kuishi maisha magumu, lakini ili usiishi maisha magumu inabidi ufanye kazi na uzalishe. Uchumi wa nchi yetu bado haujafikia uwezo wa kutoa ajira kwa kila mtu. Kinachotakiwa, tuondoe fikra mgando kwamba tujibweteke na tudai serikali itusaidie, hili haliwezekani, hata kule kwenye uchumi mkubwa kuliko wote duniani usipokuwa na bidii 'umeuwawa' na ndiyo maana hata ombaomba (homeless) wapo kibao.
Haikusaidii lolote kutokumuheshimu Rais halali wa nchi, be aggressive uponde maraha kwa jasho lako, hao wanaoponda maraha kwa pesa ambazo sio zao watashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na nina hakika hakuna ambaye ataonewa katika hili.
 
.......haya ngoja nijaribu kumjibu huyu Pundamilia

Jazba, Chuki binafsi, husda na ukosefu wa hekima na busara vimetanda hapa JF.

.......That can can be your own interpretation......call it whatever......ukweli unabaki kuwa ukweli Nchi yangu TANZANIA IKO NJIA PANDA.........moreover unatukosea adabu wengi wetu ambao tunaona mustakabali wa Taifa haueleweki, kwa kuona kuanzia IPTL, RADA (ambayo Rais huyo huyo aliwaomba watu wamsaidie kurudisha baadhi ya pesa zilizozidi/zilizoibiwa....very funny), RICHMOND, BUZWAGI, BoT, Pesa za wajasiriamali kutoka Japan, nk nk nk nk .....................haya yote mtu mwenye akili timamu huwezi kukaa kuimba "Kill me Softly"

HIVI MTU AKIWA NA MAWAZO MBADALA NA YA KWAKO ANAKUWA AMEKUKOSEA ADABU? HILI JIPYA, KUWA MVUMILIVU TAFADHALI111

Lakini kwa kifupi ni kuwa mama yako akishakwambia huyu ndiyo baba yako huna budi kumheshimu.

.......Agreed, na baba asipotimiza wajibu wake watoto wanakufa kwa maradhi, njaa na kukosa elimu, future iko wapi??.......what a father!!!!

BABA YAKO NI BABA YAKO TU KAMWE HUWEZI KUMBADILISHA KWA LOLOTE. SUBIRI 2010 UONGEE NA SANDUKU LA KURA, VINGINEVYO DEMOKRASIA ILISHACHUKUA NAFASI YAKE, WENGI WALICHAGUA RAIS ALIYEPO OFISINI KWA SASA. NI VEMA UKAJIPANGA KWA 2010 KAMA KWELI UNAMAANISHA UNAVYOONGEA LAKINI HATA HIVYO WENGI NDIYO WATAKAOAMUA NANI AONGOZE NCHI.

As long as watanzania walimchagua Mh. Kikwete kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hamna budi kumheshimu kama RAIS.

......Only if akitekeleza yale yanayotakiwa kwa ajili ya manufaa ya taifa letu kwa ujumla wake

KWAHIYO AKITELEZA KWA MTAZAMO WAKO ANATAKIWA ASIHESHIMIWE, HIVI MAMA YAKO 'AKITELEZA' HUTAMUHESHIMU?

Kamwe sitakaa kimya kuona Rais wa nchi yangu anadhalilishwa kwani ni wajibu wangu kutetea taifa langu.

........Yes hakuna mtu anayependa Rais wa nchi yake akidhalilishwa..............but again.........kudhalilishwa kuna tofauti kubwa na kuambiwa ukweli........kama kuambiwa ukweli mtu ni kumdhalilisha.....then be it........kumbuka hapa some watu here are hyprocrite like you.......however ukiongea/ukileta sera mbovu JF wanachambua pumba na kuweka pembeni mchele........mchana kweupee

JE, UNAWEZA KUTOFAUTISHA KATI YA KUDHALILISHA NA KUSEMA UKWELI KWA KUREJEA MTUNDIKO WA KWANZA ULIOBEBA MJADALA?

Nitailinda nchi yangu Tanzania na nitawaheshimu viongozi waliopewa dhamana na wananchi.

....Ohhh yes wote twailinda nchi yetu kwa kufichua maovu......na kuwaeleza ukweli viongozi pale wanapokosea.........viongozi wengi walioko madarakani........im sorry ni WABOVU, wametufikisha mahala ambapo, wapuuzi wanakuja na $5 na kuondoka na Billions.........na ndio maana hata JK anawaambia kuwa eti wachague uwaziri au Biashara.........however.....hapa JF tumeshaliona hilo kuwa ni CHANGA LA MACHO

SIDHANI KAMA VIONGOZI WENGI NI WABOVU KAMA UNAVYODAI, HUO NI MTAZAMO WAKO BINAFSI OTHERWISE TAARIFA RASMI ZILIZOTHIBITISHWA KUWA VIONGOZI WENGI NI WABOVU

Nitailinda nchi yangu na kuitetea wakati wote dhidi ya wadhalimu wachache.

......OOhh yeah wadhalimu ni wale wanoona unayeona uovu/hatari na kuunyamazia kimya.......may be you are among them!!!!

HATA WEWE AMBAYE HUHESHIMU MAMLAKA HALALI ZILIZOWEKWA NA WANANCHI WALIO WENGI NI DHALIMU, KWANI HUUESHIMU UAMUZI WA WATANZANIA WALIO WENGI.

Nitajitahidi kujadiliana juu ya mustakabali wa nchi hii kwa uwazi bila ya kudharau mamlaka zote halali zilizowekwa kwa ridhaa ya wananchi
Ninaipenda nchi yangu na ninajivunia kuwa Mtanzania.

.......This is what we do at JF...wher we dare to talk openly bila unafiki

SI KWELI

Mungu tuongeze hekima na busara watanzania

......Yes...tena wale wanaoona uovu na kuunyamazia

NINAONGEZEA ...NA WALE WASIOKUWA NA HESHIMA PIA

na uibariki nchi yetu na wananchi wake.

......Thanks and AMINA

NAKUSHUKURU KWA MCHANGO WAKO
 
WEWE NDIO HUNA HEKIMA....WEWE UNAIPENDA TANZANIA KULIKO NANI HAPA??!!.............WAZALENDO NDIO SISI...TUNAIPENDA TANZANIA KULIKO TUNAVYOJIPENDA..YOYOTE ANAYEICHEZEA NA KUIFUJA AU KUIFISADI ..TUTAMSEMA..PIA ANAYELEA MAFISADI NAYE NI FISADI!!

NDIO TUNAIPENDA NCHI YETU PAMOJA NA KUWA HATUPATI MARUPURUPU...KUNA WANAYOIPENDA NCHI HII KWA AJILI WANAFAIDIKA NA SYSTEM..SISI TULIOWENGI HATUPATI MALIPO..MALIPO YETU YATAFSIRIWE KWA KUPELEKA HUDUMA BORA KWA WOTE ...NA KUPUNGUZA PENGO KUBWA LINALOKUWA KATI YA MASIKINI NA MATAJIRI......SASA KAMA HIYO NI UKOSEFU WA BUSARA...BASI HATUNA BUSARA!!!!

I wish ungekuwa unayasikia uliyoyaandika, you are so funny. Well I reserve my comments.
 
BABAH, USAMEHEWE MAKOSA YAKO YOTE NA HATA YALE YA 'UTOTONI' KWANI HUJUI UTENDALO

SINA HAJA YA KUJUA UWEZO WAKO WA KUFIKIRI NA KUTENDA.

MH. JAKAYA KIKWETE NI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMBAYE AMECHAGULIWA NA KIHALALI KWA KURA ZA WANANCHI WENGI.

MOJA YA WAJIBU WANGU KAMA RAIA WA TANZANIA NI KUMHESHIMU RAIS KAMA TAASISI (HAIJALISHI HATA KAMA ANGEKUWA NI MTIKILA, MREMA AU MWINGINE YEYOTE).

FURSA INAYOPATIKANA KUPITIA JF KUTOA MAONI YAKO KWA UHURU HAIMAANISHI UNAWEZA KUPITILIZA KIASI CHA KUTOMHESHIMU RAIS WETU.

KUMBUKA DALILI ZA MTU AMBAYE HANA HESHIMA NI KUTOKUHESHIMU WENGINE.

Mambo ya kumheshimu JK sio sawa na amri ya kwanza kati kumi za MUNGU. Dharau ni matokeo ya matendo na tabia ya muhusika(hapa JK).Hata hivyo kilichofanyika hapa si dharau ila ni kuanika ukweli wa wasifu wake. Kinyesi ni Kinyesi tu we ukitaka kukiita ni makapi ya chakula kutoka katika tumbo la binadamu.hiyo ni juu yako ila usitake wote tuite hivyo.
Suala la heshima pia ni two way,sio one way.JK kama yeye hawaheshimu watu waliomchagua kwa kuwadharau,kuwaonyesha kiburi kuwa hawajui kinachoendelea basi hata hata yeye hana budi kutoeshimiwa.Heshima ya urais haiji automatically tu eti kwa kuwa wewe umepewa jina la urais. Heshima hiyo inakuja baada ya wewe kutekeleza majukumu halali yanayoendana na kofia hiyo.
Haiwezekani wewe kwa kuwa Rais,lakini ukawa mwizi, mzinzi au mlevi watu wasiseme huyu rais ni Mlevi,Mzinzi na Mwizi.
Kama unanidhamu ya woga kaa nayo wewe ila usitake pandikiza kwa wengine.
 
Back
Top Bottom