Askari hufahamiana vyeo vyao "seniority" kwa kuangalia vyeo vyao mabegani au ubavu wa mkono wa kushoto. Askari wa majeshi yote iwe ni TPS (Tanzania Prisons Services), TPF (Tanzania Police Force) au TPDF (Tanzania People's Defence Force) hupigiana salute kwa kuangalia nani ana cheo kikubwa na si nani anatoka jeshi gani.
Mfano; Wanapokutana Sajenti wa Magereza na Koplo wa Polisi, ni wajibu wa Koplo wa Polisi kumpigia salute Sajenti wa Magereza. Wanapokutana Kepteni wa Jeshi na ASP wa Polisi/Magereza ni wajibu wa Kepteni wa JWTZ kupiga salute kwa maafande hao wa Majeshi mengine waliomzidi vyeo.
Na ikumbukwe, vyeo vya majeshi ni internationalwise. Kepteni wa US Army atampigia salute Brigedia wa nchi ndogo na masikini Mauritania.
Ila utofauti unakuja katika vyeo vya IGP, CGP na CDF..IGP na CGP vyeo vyao ni sawa na Meja Jenerali. Kwa hiyo CDF ni mkubwa kwa IGP na CGP kwa kuwa CDF ni Jenerali
Mkuu hao hawapigiani salute ila unabana tu mikono na kusema "jambo afande".