Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

Mkuu huwezi kuunderestimate power ya hizi organizations.
Mfano:
Rais wa Marekani Franklin D. Roosevelt, Waziri mkuu wa UK Winston Churchill na General Stalin wa urusi walikutana kwa siri IRAN kujadili jinsi watakavyomshughulikia Hitler katika WW2. Ni KGB waliogundua mtego wa spy wa wanazi waliokuwa wamefurika mji huo Tehran kuwaangamiza hasa rais wa US na Churchill. Kwa uoga Rais wa Marekani aliforce kwenda kujificha ubalozi wa Urusi ili awe na maximum usalama. Maana Walikamatwa maspy 400 wa hitler na KGB hapo mjini.
Ikumbukwe kama hawa wawili US na hasa Uk hakukua na mtu yoyote sio mfalme wala Waziri mkuu aliyekuwa na gut za kumbishia Hitler hata kutangaza pambano hadi walioenda nyumbani kwa Churchill (political reject) aje na baadae akaachiwa nchi awe PM. Yeye ndie hadi kesho Uk anaheshimika kuliko mtu yoyote. kama Isngekuwa KGB WW2 ingekuwa ni stori nyingine.
Sawa nime kupata vyema mkuu..
 
Sawa nime kupata vyema mkuu..
Yap isingekuwa Juhudi ya Kachero Gevork Vartanian na kikosichake cha KGB,
WaNAZI wangeandika upya historia ya dunia. Maana WW2 bila combination ya Flanklin D. Roosevelt, Winston LAmeck Spenser Churchill na General Joseph Stallin hakuna dunia nzima ambaye angemsogelea hitler na ujerumani dunia nzima enzi hizo.
 
Kama ilivyo CIA, KGB (imekuwa FSB kuanzia 1995)shirika la kijasusi la USSR sasa URUSI limewahi kuhusika katika operation hatari sana maeneo mbalimbali Duniani. Kilele cha operation hizo ilikuwa kipindi cha vita baridi. Taarifa nyingi zilijulika pale jasusi la KGB Vasili Mitrokhin lilipotorokea uingereza na Mafaili yenye siri nyingi maana alikuwa ni mtunza kumbukumbu wa shirika hizo.

1:MASHAMBULIO KWA MIUNDOMBINU YA MAREKANI
Hungry-Horse-Dam.png

kUANZIA 1957 Hadi 72 KGB walianza kupiga picha miundombinu ya marekani kwa siri. Mitambo ya umeme,Mafuta chochote kile ambacho kingeleta athari za kudumu kwa mmarekani kilipigwa picha.Mipango yote ilikuwa ni kuahakikisha ikitokea vita, wanapiga shambulio moja amerika hasa new york inakoswa umeme, na kuanza kushambuliwa na russia mtaa kwa mtaa.

2: MIKAKATI HATARI YA KUOKOA MATEKA RAIA WA URUSI.

Hostage-Retribution.jpg

Mwaka 74 walinda kikosi maalumu kiitwacho ALPHA GROUP. KBG waliunda kikosi hiki kutekeleza mission za siri sana na Za kikatili kupita kiasi ili kuwaokoa mateka wao. Mfano ni huu wa LEBANON.
Magaidi waliwateka wanadiplomasia wanne wa kirusi siria. Lengo ni kuizuia russia isiiunge mkono siria.Baada ya maridhiano kufeli na magaidi kuonyesha wamemuua mmoja wa mateka, ndipo kikosi hiki kikaingilia kati, waliperereza na kujua kundi hilo ni hesbula. Wakamteka ndugu wa karibu na kiongozi mkuu wa hesbula. wakawa wanamkata vipande vidogo vidogo vya mwili wakivituma kwa kiongozi huyo vikiambatana na ujumbe.Baadae walimuua na wakamtumia kiongozi huyo ujumbe kuwa wanajua pote walipo ndugu na familia yake na kinachofuata ni kuwafanya wote kama huyo ndugu yao akiwemo na yeye aliyedhani hajulikani. Haraka sana magaidi waliwaachia hao mateka bila masharti yoyote.

3:KUTUMIA WANAWAKE WAREMBO KUREKODI VIDEO ZA NGONO ZA VIONGOZI
Blackmail-Stewardess.jpg

KGB ilijumuisha wanawake warembo waliowaita "SWALLOWS", USSR walikuwa na mpango wa kutawala dunia, Mshirika wao Indonesia alipopata nguvu walipata hofu atawaasi na kujikita na uislamu. Raisi wa nchi hiyo SURKANO ndio alikuwa kikwazo. Baada ya kumfuatilia waligundua anaudhaifu mkubwa katika NGONO. Walipanga SwALLOWS wa kutosha hotelini alipofikia na kwenye ndege kama wahudumu. Bila kujua wakamrekodi akiwa anafanya mapenzi na wadada hao kwa mpigo. Walipomtishia na kumtumia hizo clip ili awe mpole aendelee kuwaunga mkono, majibu yakawa tofauti maana hakushtushwa na aliomba wamtumie nyingine zaidi maana zile zilikuwa ni chache. Jaribio likafeli.

4:KBG HACKERS (WADUKUZI WA KIMTANDAO) WALITEMBELEA ZAIDI YA COMPUTER 400 ZA WANAJESHI WA MAREKANI
Old-Computer.jpg

mwAKA 80 Walikuwa wanatafuta jinsi ya kuPATA siri za jeshi la marekani. Walimuajiri jamaa anayeitwa Markus Hess mtaalamu aliyebobea katika anga hizo. Shughuli nzima ilifanyikia UJERUMANi ambapo aliweza kuACCESS computer zaidi ya mianne za jeshi la US. Akifanikiwa kubashiri PASSWORD za computer muhimu kabisa PENTAGON na kupata taarifa za siri za wanajeshi lukuki.
Hadi pale mtaalamu wa US Cliford stoll siku moja katika pitapita zake akaona vitu asivyovielewa kwenye system yao. ilimchukua miezi 10 kujua nini kilikuwa kinaendelea na huyo jamaa aligundua ana SUPPERACCESS ya Deffensive system ikiwemo mitambo ya nyuklia marekani. Hadi alipowekewa mtego wa kimtandao na kunaswa huko hannover ujerumani. alikuwa anawauzia KBG hizo siri.

5:OPERATION RYAN
Spying-on-the-US.jpg

Miaka ya 80, ulizuka uvumi kuwa US wanajiandaa kuilipua russia muda wowote na makombora ya NYUKLIA. Ndio KGB na urusi wakaja na hii operation ambayo ni kubwa kuwahi kutokea.
Walipanga kuweka satelite zitakazopiga picha vituo vya kijeshi marekani nzima kila sekunde kuona kama kuna kombola linakuja,Pia kumonitor matumizi ya RADA amerika yote ili kuangalia uwezekano wa shambulio. Pia kuwachunguza raia na wanajeshi wa marekani wote wanapoondoka US, PIa kuiweka NATO chini ya uachunguzi wa hali ya juu. Walijaribu kuingilia mawasiliano ya simu yote nchini marekani na ulaya yote. Waliweka mtandao wa MAKACHERO duniani ambao wako tayari muda wote kushambulia wakiona urusi inavamiwa na marekani. Operation hii ya mabilioni ilihairishwa miaka mitatu baadae.

6:KUNUNUA BENKI ZA WAMAREKANI
6-us-bancorp.jpg

KBG hawakupanga kutumia mashushu wao kujua siri za selikali ya malekani, Badala yake walitumia BENKI.Wlipanga kununua BENKI TATU huko Northern California. Hawakukurupuka walijua benk hizi zilitumika na makampuni yaliyokuwa yanatengeneza TECHNOLOGY za jeshi la US, Wakaona kumiliki hizo benki watapata taarifa za siri za nini wanafanya jeshini kwa maana ya teknolojia.CIA walishtukia huu mchakato baada ya kugundua Mnunuzi kutoka Singapole aliingiziwa pesa kutoka RUSSIA.

7:OPERATION PANDORA
Watts-Riots.png

Waliendelea kuiandama marekani maana ndio alikuwa adui yao namba moja. Safari hii KBG wanapanga machafuko ndani ya US. Unakumbuka miaka ya 60 kulikuwa na vuguvugu la watu kupinga ubaguzi, kwa KGB hii ilikuwa ni fursa. Waliandaa vipeperushi NEW YORK na majarida feki yaliyoonyesha watu weusi wanawavamia wenye asili ya WAYAHUDI na kuwaibia vitu. Majarida haya yalionyesha kuwa walalamikaji ni kundi la waisrael JEWISH DEFENCE LEAGUE ambao kwa FBI walihesabiwa kama magaidi. Kisha wakayasmbaza kwa watu weusi waliokuwa wanamiliki silaa na mapolisi/wanajeshi weusi uchochezi huu wajiandae na mashambulizi ya wayahudi. Kuzidi kuchochea KGB walipanga kukilipua chuo kilichojaa wanafunzi weusi tu. Baada ya kulipuka chuo watume ujumbe kwa vyama vyote vya watu weusi kuwa ni WAYAHUDI ndio wanahusika.

8:SAKAFU YA KUSIKILIZIA
Hotel-Viru.png

KBG walikuwa wako vizuri sana ktk kuweka vinasa sauti kusikiliza mazungumzo katika maofisi na majengo mengi. Yaani waliwahi kuweka vinasa sauti katika hoteli maarufu kwa zaidi ya miaka 20 bia kujulikana. Mfano nchini ESTONIA jengo lenye ghorofa 22 lililokuwa linafikiwa na wafanya biashara wakubwa duniani, kulikuwa na floor ya 23 ya siri iliyokaliwa na KGB kwa muda wa miaka 20 hadi USSR ilipoanguka mwaka 1991. Mtoto mdogo aliyempa barozi wa Marekani Russia zawadi ambayo ilipachikwa kinasa sauti chenye uwezo wa hali ya juu. Kwa miaka saba KGB walikuwa wanasikiliza mawasiliano yote hadi kilipo gunduliwa ka bahati mbaya na mfanyakazi wa radio wa UK alipokosea mawimbi na kusikia mazungumzo asiyoyaelewa.

9:KUFADHILI UGAIDI
Terrorists.jpg

Jasusi la KGB Aleksandr Sakharovsky anajinasibu kuwa "Utekaji wa ndege ni UVUMBUZI WAKE".
Waliungana na YASSER Alafat na kumsaidia kuchukua madalaka ya PARESTINA. Walitengeneza magaidi wa kutosha na wapigania uhuru ili kuwadhoofisha maaduia wao. Mfano mwaka 69 tu ndege zaidi ya 82 zilitekwa sehemu mbalimbali duniani na hawa jamaa. Walichochea vita huko IRELAND kwa kuwasambazia Bunduki,bastola, mabomu wanajeshi kitu kilicholeta machafuko makubwa. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza mataifa mengi yenye kuunga mkono ukomunisti.

DUNIA INA MAMBO MENGI,
HII NI TAASISI MOJA TU LAKINI UKISOMA KUHUSU CIA(US), MOSSAD(UZAYUNI), MI6(UK), ISI (PAKISTANI),BND(ujerumani), RAW(INDIA), DGSE (UFARANSA),ASIS(AUSTRALIA) NA MSS(CHINA) UTAJUA GHARAMA YA KUILINDA NA KUITANGAZA NCHI KATIKATI YA MAADUI BILA VITA.
No 1. That is called strategic war ( strategic bombing )
Kupiga picha ni hatua ya mwanzo kabisa ambayo kijeshi huitwa reconnaissance, kwa lugha rahisi ni survey. Hatua hii hulenga kataka kujua nguvu ya adui. Mara baada ya picha izo kupatikana, hufanyiwa uchambuzi na kupewa uzito au kipaumbele ya maeneo muhimu ya kushambuliwa punde tu, taifa husika litakapoingia vitani na taifa hasimu

Hii hulenga kupiga au shambulia maeneo ambayo yanampa adui nguvu za kupambana kivita. Lengo ni kumdhoofisha adui kwa kushambulia haya maeneo. Mfano, kambi kubwa za jeshi zenue hifadhi ya silaha kubwa / nzito, sehemu zenye hifadhi ya mafuta, sehemu zenye shehena kubwa za chakula.

Hii njia ilitumika sana na marekani na washirika wake kwenye vita ya pili ya dunia dhidi ya ujerumani 1940's

Pia marekani walitumia njia hii kumdhoofisha sadam hussein na jeshi lake kwenye vita ya 1991 kwa kushambulia madaraja ili majeshi yashindwe kupata supplies / provisions kama silaha, chakula na madawa. Pia majeshi yashindwe Ku retreat ya kishindwa na yashindwe kupata askari wa ziada pale wanapozidiwa na adui kwenye uwanja wa kivita.

Wakipiga visima vya mafuta, wanadhoofisha uwezo wa adui kua na nguvu za kupigana vita kwa kumfanya ashindwe kutumia silaha zake. Unakuta jeshi lina Vifaru au ndege za kivita nyingi lakini linashindwa kuvitumia kutokana na kukosa mafuta nk. Mfano, mwaka 1943 ujerumani wanagundua ndege yao ( first jet fighter aircraft ) The ME264, wanashindwa kushinda vita ya anga kwasababu visima vyake vya mafuta Romania, vilivyokua vinazalisha 60% ya mafuta yote yaliyotumika ujerumani vilikua tayari vimeteketezwa na wamarekani na washirika wake.
 
Kama ilivyo CIA, KGB (imekuwa FSB kuanzia 1995)shirika la kijasusi la USSR sasa URUSI limewahi kuhusika katika operation hatari sana maeneo mbalimbali Duniani. Kilele cha operation hizo ilikuwa kipindi cha vita baridi. Taarifa nyingi zilijulika pale jasusi la KGB Vasili Mitrokhin lilipotorokea uingereza na Mafaili yenye siri nyingi maana alikuwa ni mtunza kumbukumbu wa shirika hizo.

1:MASHAMBULIO KWA MIUNDOMBINU YA MAREKANI
Hungry-Horse-Dam.png

kUANZIA 1957 Hadi 72 KGB walianza kupiga picha miundombinu ya marekani kwa siri. Mitambo ya umeme,Mafuta chochote kile ambacho kingeleta athari za kudumu kwa mmarekani kilipigwa picha.Mipango yote ilikuwa ni kuahakikisha ikitokea vita, wanapiga shambulio moja amerika hasa new york inakoswa umeme, na kuanza kushambuliwa na russia mtaa kwa mtaa.

2: MIKAKATI HATARI YA KUOKOA MATEKA RAIA WA URUSI.

Hostage-Retribution.jpg

Mwaka 74 walinda kikosi maalumu kiitwacho ALPHA GROUP. KBG waliunda kikosi hiki kutekeleza mission za siri sana na Za kikatili kupita kiasi ili kuwaokoa mateka wao. Mfano ni huu wa LEBANON.
Magaidi waliwateka wanadiplomasia wanne wa kirusi siria. Lengo ni kuizuia russia isiiunge mkono siria.Baada ya maridhiano kufeli na magaidi kuonyesha wamemuua mmoja wa mateka, ndipo kikosi hiki kikaingilia kati, waliperereza na kujua kundi hilo ni hesbula. Wakamteka ndugu wa karibu na kiongozi mkuu wa hesbula. wakawa wanamkata vipande vidogo vidogo vya mwili wakivituma kwa kiongozi huyo vikiambatana na ujumbe.Baadae walimuua na wakamtumia kiongozi huyo ujumbe kuwa wanajua pote walipo ndugu na familia yake na kinachofuata ni kuwafanya wote kama huyo ndugu yao akiwemo na yeye aliyedhani hajulikani. Haraka sana magaidi waliwaachia hao mateka bila masharti yoyote.

3:KUTUMIA WANAWAKE WAREMBO KUREKODI VIDEO ZA NGONO ZA VIONGOZI
Blackmail-Stewardess.jpg

KGB ilijumuisha wanawake warembo waliowaita "SWALLOWS", USSR walikuwa na mpango wa kutawala dunia, Mshirika wao Indonesia alipopata nguvu walipata hofu atawaasi na kujikita na uislamu. Raisi wa nchi hiyo SURKANO ndio alikuwa kikwazo. Baada ya kumfuatilia waligundua anaudhaifu mkubwa katika NGONO. Walipanga SwALLOWS wa kutosha hotelini alipofikia na kwenye ndege kama wahudumu. Bila kujua wakamrekodi akiwa anafanya mapenzi na wadada hao kwa mpigo. Walipomtishia na kumtumia hizo clip ili awe mpole aendelee kuwaunga mkono, majibu yakawa tofauti maana hakushtushwa na aliomba wamtumie nyingine zaidi maana zile zilikuwa ni chache. Jaribio likafeli.

4:KBG HACKERS (WADUKUZI WA KIMTANDAO) WALITEMBELEA ZAIDI YA COMPUTER 400 ZA WANAJESHI WA MAREKANI
Old-Computer.jpg

mwAKA 80 Walikuwa wanatafuta jinsi ya kuPATA siri za jeshi la marekani. Walimuajiri jamaa anayeitwa Markus Hess mtaalamu aliyebobea katika anga hizo. Shughuli nzima ilifanyikia UJERUMANi ambapo aliweza kuACCESS computer zaidi ya mianne za jeshi la US. Akifanikiwa kubashiri PASSWORD za computer muhimu kabisa PENTAGON na kupata taarifa za siri za wanajeshi lukuki.
Hadi pale mtaalamu wa US Cliford stoll siku moja katika pitapita zake akaona vitu asivyovielewa kwenye system yao. ilimchukua miezi 10 kujua nini kilikuwa kinaendelea na huyo jamaa aligundua ana SUPPERACCESS ya Deffensive system ikiwemo mitambo ya nyuklia marekani. Hadi alipowekewa mtego wa kimtandao na kunaswa huko hannover ujerumani. alikuwa anawauzia KBG hizo siri.

5:OPERATION RYAN
Spying-on-the-US.jpg

Miaka ya 80, ulizuka uvumi kuwa US wanajiandaa kuilipua russia muda wowote na makombora ya NYUKLIA. Ndio KGB na urusi wakaja na hii operation ambayo ni kubwa kuwahi kutokea.
Walipanga kuweka satelite zitakazopiga picha vituo vya kijeshi marekani nzima kila sekunde kuona kama kuna kombola linakuja,Pia kumonitor matumizi ya RADA amerika yote ili kuangalia uwezekano wa shambulio. Pia kuwachunguza raia na wanajeshi wa marekani wote wanapoondoka US, PIa kuiweka NATO chini ya uachunguzi wa hali ya juu. Walijaribu kuingilia mawasiliano ya simu yote nchini marekani na ulaya yote. Waliweka mtandao wa MAKACHERO duniani ambao wako tayari muda wote kushambulia wakiona urusi inavamiwa na marekani. Operation hii ya mabilioni ilihairishwa miaka mitatu baadae.

6:KUNUNUA BENKI ZA WAMAREKANI
6-us-bancorp.jpg

KBG hawakupanga kutumia mashushu wao kujua siri za selikali ya malekani, Badala yake walitumia BENKI.Wlipanga kununua BENKI TATU huko Northern California. Hawakukurupuka walijua benk hizi zilitumika na makampuni yaliyokuwa yanatengeneza TECHNOLOGY za jeshi la US, Wakaona kumiliki hizo benki watapata taarifa za siri za nini wanafanya jeshini kwa maana ya teknolojia.CIA walishtukia huu mchakato baada ya kugundua Mnunuzi kutoka Singapole aliingiziwa pesa kutoka RUSSIA.

7:OPERATION PANDORA
Watts-Riots.png

Waliendelea kuiandama marekani maana ndio alikuwa adui yao namba moja. Safari hii KBG wanapanga machafuko ndani ya US. Unakumbuka miaka ya 60 kulikuwa na vuguvugu la watu kupinga ubaguzi, kwa KGB hii ilikuwa ni fursa. Waliandaa vipeperushi NEW YORK na majarida feki yaliyoonyesha watu weusi wanawavamia wenye asili ya WAYAHUDI na kuwaibia vitu. Majarida haya yalionyesha kuwa walalamikaji ni kundi la waisrael JEWISH DEFENCE LEAGUE ambao kwa FBI walihesabiwa kama magaidi. Kisha wakayasmbaza kwa watu weusi waliokuwa wanamiliki silaa na mapolisi/wanajeshi weusi uchochezi huu wajiandae na mashambulizi ya wayahudi. Kuzidi kuchochea KGB walipanga kukilipua chuo kilichojaa wanafunzi weusi tu. Baada ya kulipuka chuo watume ujumbe kwa vyama vyote vya watu weusi kuwa ni WAYAHUDI ndio wanahusika.

8:SAKAFU YA KUSIKILIZIA
Hotel-Viru.png

KBG walikuwa wako vizuri sana ktk kuweka vinasa sauti kusikiliza mazungumzo katika maofisi na majengo mengi. Yaani waliwahi kuweka vinasa sauti katika hoteli maarufu kwa zaidi ya miaka 20 bia kujulikana. Mfano nchini ESTONIA jengo lenye ghorofa 22 lililokuwa linafikiwa na wafanya biashara wakubwa duniani, kulikuwa na floor ya 23 ya siri iliyokaliwa na KGB kwa muda wa miaka 20 hadi USSR ilipoanguka mwaka 1991. Mtoto mdogo aliyempa barozi wa Marekani Russia zawadi ambayo ilipachikwa kinasa sauti chenye uwezo wa hali ya juu. Kwa miaka saba KGB walikuwa wanasikiliza mawasiliano yote hadi kilipo gunduliwa ka bahati mbaya na mfanyakazi wa radio wa UK alipokosea mawimbi na kusikia mazungumzo asiyoyaelewa.

9:KUFADHILI UGAIDI
Terrorists.jpg

Jasusi la KGB Aleksandr Sakharovsky anajinasibu kuwa "Utekaji wa ndege ni UVUMBUZI WAKE".
Waliungana na YASSER Alafat na kumsaidia kuchukua madalaka ya PARESTINA. Walitengeneza magaidi wa kutosha na wapigania uhuru ili kuwadhoofisha maaduia wao. Mfano mwaka 69 tu ndege zaidi ya 82 zilitekwa sehemu mbalimbali duniani na hawa jamaa. Walichochea vita huko IRELAND kwa kuwasambazia Bunduki,bastola, mabomu wanajeshi kitu kilicholeta machafuko makubwa. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza mataifa mengi yenye kuunga mkono ukomunisti.

DUNIA INA MAMBO MENGI,
HII NI TAASISI MOJA TU LAKINI UKISOMA KUHUSU CIA(US), MOSSAD(UZAYUNI), MI6(UK), ISI (PAKISTANI),BND(ujerumani), RAW(INDIA), DGSE (UFARANSA),ASIS(AUSTRALIA) NA MSS(CHINA) UTAJUA GHARAMA YA KUILINDA NA KUITANGAZA NCHI KATIKATI YA MAADUI BILA VITA.
No 3. Blackmail tactics or manipulations

Hii njia hulenga kumtumia mtu kufanya vile utakavyo kwa kumtishia kua utatoa siri zake ambazo aidha ni matukio ambayo mhusika kajihusisha nayo ambayo yapo kinyume na sheria au kinyume na maadili. Ukisisitiza kua aidha , siri izo zikitoka zinaweza fanya apelekwe mahakamani, apate aibu, ajihudhuru kutoka kwenye nafasi yake ya uongozi au kuharibu mahusiano yake na familia, ndugu na watu wengine wa karibu yake.

Mfano wa siri izo ni
- Matukio ya rushwa
- " ". ya ushoga
- ". " ya matumizi mabaya ya madaraka
- ". ". ya ufisadi
Nk

Ingawa hii njia haina ufanisi mzuri, kama ilivyoelezwa hapo juu
 
Nilipenda Mission ya iliyofanywa na Mossad ya ku defect( Mig -21) kwenda Israel izi egence ni balaa
 
na wapo kila sehemu, Mfano Mshambuliaji wa Alsenal Andre Arshavin alifurushwa england baada ya kujulikana ni JASUSI wa Russia kwa jina la (RED FOX). Kuna kipindi inasemekana alijifanya yuko injury ili abaki london anakusanya taarifa. Na inasemekana alitumiwa wadau wengine watatu in case mission imekamilika wamtoroshe. Ili kuwapoteza wasimfuatilie uliandaliwa uvumi kuwa anatakiwa kujiunga na madrid
...aseee hii MPYA ..jamaa alikua yuko KIKAZI zaidi
 
Walistruggle sana Warusi ila mwisho wa siku wakashindwa na ndo maana ilikufa
 
CIA na KGB ni sawa na TISS hapa lakini wa kwetu wapo busy kwenye ile misitu ya pale maeneo pande wakikarabati kucha

Kuna mambo mengi yanafanyika mpka ww sahii vidole vyako vipo salama unatype hayo unayo sema hata siyo mission na sidhani kam yanakuwa documented ktk idara
 
Wengine wanaandika watakachojisikia hawajui vijana wanapata shida gan hadi wao wanaburudika sasa na kuongea watakacho
 
CIA na KGB ni sawa na TISS hapa lakini wa kwetu wapo busy kwenye ile misitu ya pale maeneo pande wakikarabati kucha
military intelligence itakuwa bora zaidi Ila tiss nao watakuwa vizuri hao wanaojitapa mitaani ukute ni mainformer tu.
Mimi naamini tuko salama kwa sababu kuna watu wachache wapo kazini kuwezesha.
Kwa nchi yetu tunaishi kwa siri sio misifa.
 
kuna ile mission CIAwaliifanya kule sudani kama sikosei, jamaa walichapwa kama watoto

Sio unaongelea mission ya Somalia ya Jeshi la Marekani wakachapwa sana?. Hii walikuja kusaidia na Grup Gerak Khas (GGK) kikosi maalumu cha Malyasia kumuokoa rubani aliyetekwa. Inasemekana GGK ndio wana training ngumu kabisa katika special forces
 
Watu wanadhani amani inatokea tu yenyewe, hawajui kuwa kuna mengi yasiyoonyeshwa kwenye taarifa ya habari au magazeti ambayo yanailinda hiyo amani.

Watu wanapenda kuona kiatu bila kujali nguvu iliyotumika na material zilizotumika ili kiatu kiwe kama kilivyo. Tuna-overlook sana vitu kiasi kwamba hatutaki kufahamu tena uhalisia wa jambo tunachotaka ni matokeo tu.
Watu wanatakiwa watambue matokeo yanayoonekana leo ni muendelezo wa matukio yasiyoonekana yaliyofanywa kwa kiwango fulani ili kuleta matokeo haya.
 
Mada kama hizi nazipenda sanaa,napozisomaaa hua naenjoy mbayaa.ile zetu za kibongo wanazibana sana
 
Back
Top Bottom