Zijue MISSION 09 za KBG (FSB sasa) ambazo kama baadhi zingefanikiwa Dunia ingekuwa tofauti na leo

stori yote imeishia kufa kwa soviet,na baada ya hapo hakuna lunaloendelea sababu nafikiri wamekubali kushindwa hawa warusi.
 
Mkuu MSEZA MKULU ,
Shirika la KGB lilivunjwa na kuwa SVR na FSB mara baada ya kuanguka kwa jumuiya ya nchi za kisovieti mwaka 1991 na siyo mwaka 1995.

Haya nianze kukosoa kwenye vinasa sauti hapo.
Hivi unajua mnamo mwaka 1970 C.I.A walichimba shimo refu chini ya Ubalozi wa Soviet Marekani kwa dhumuni la kufanya udukuzi?

Hilo la ugaidi.
Mbona C.I.A na MOSSAD nao ni magwiji wa kutengeneza magaidi?
Unayakumbuka haya makundi;

  1. Khmer Rouge la Cambodia?
  2. Contras or FDN wa Nicaragua?
  3. The Mujaheddin au Al-Qaeda la Afghanistani?
  4. Hawa ISIS je?
....kweli, dunia ina mambo!
 
Kuna uzi mmoja hapa niliuliza swali sikupata jibu.Ni hivi hawa wapelelezi iwe wa ndani kama FBI au wa nje kama CIA wanapomfuatilia mtu ambaye kaikimbia nchi yake mathalani from Russia to USA na ukizingatia ukubwa wa nchi na miji mingi sana wanawezaje kum-track mtu hadi wampate alipo?Wakati hapa jf ukinitajia jina tu na kunimbia unaishi Dar sitoweza kukupata asilani,hawa wanawezaje kumtafuta mtu katika eneo kibwa kabisa la utafutaji.
 
Kuna uzi mmoja hapa niliuliza swali sikupata jibu.Ni hivi hawa wapelelezi iwe wa ndani kama FBI au wa nje kama CIA wanapomfuatilia mtu ambaye kaikimbia nchi yake mathalani from Russia to USA na ukizingatia ukubwa wa nchi na miji mingi sana wanawezaje kum-track mtu hadi wampate alipo?Wakati hapa jf ukinitajia jina tu na kunimbia unaishi Dar sitoweza kukupata asilani,hawa wanawezaje kumtafuta mtu katika eneo kibwa kabisa la utafutaji.
mkuu hili lianzishie thread lijadiliwe kwa mapana.
Ila hata wewe inawezekana kukupata hata ukiwa DSM pande gani. Technology haidanganyi.
Mfano KGB walikuwa wanamsaka kwa muda mrefu sana mdau mmoja huko yugoslavia. Kuna siku akajichanganya akampigia simu rafiki yake ambaye wote walikuwa under surveillance 24/7. wakatrack location. KBG wakapanga chumba cha jirani wanamfuatilia wanapishana nae hadi takribani miezi 10 akidhani hajulikani. siku ilipofika alikamatwa rahisi kabisa.

Katika maficho yote ya wanaosakwa na hawa CIA,MOSSAD,Mi6,ISI huwa kuna kosa wanafanya linalogharimu ujifichi wao.
JIHAD JOHN pamoja na kuwa katikati ya ngome ya ISIS alikuwa chini ya msako mkali wa M15,FBI na Scotland Yard kutafuta Identity yake, Siku anatoka kwenye jengo la jirani huko kitovuni kbs kwa ISIS al-Raqqah aingie kwenye gari yake anakutana na bomb na kugeuzwa majivu.
Mfano Bin laden kosa dogo tu la mfuasi wake akajulikana na kuwekwa under surveilance zaidi ya miezi kumi. Fuatilia Ci programs pia utaona mengi. Njia salama dunia hii ni kuamua kuwa muaminifu na kufuata utaratibu. Huwezi kuchomoka ukijifanya mjanja sio Bongo wala duniani kote.
 
Bora hao wanajitangaza bar Mbona hao FBI wanavaa kabisa vizibao vyao wala haihitaji mtu kwenda kusikiliza,japo kuna wasiovaa pia kama wale wa TISS nao wasio jitangaza.
Tafuta tofauti ya CIA na FBI, ujue,fbi wanavaa utambulisho na akija kwenye operation lazima ajitambulishe na avae uniform. Lakin CIA Ni vigumu kumjua na havai kitambulisho au uniform yeyote. TISS ni kama CIA ila kosa lao wanajiweka kama FBI unajulikana
 
stori yote imeishia kufa kwa soviet,na baada ya hapo hakuna lunaloendelea sababu nafikiri wamekubali kushindwa hawa warusi.
wew ndo unasema yameish ila waulize wenzako.mwaka 2006
stori yote imeishia kufa kwa soviet,na baada ya hapo hakuna lunaloendelea sababu nafikiri wamekubali kushindwa hawa warusi.
wew ndo unasema yameish ila waulize wenzako.mwaka 2006 aliyekuw msaliti wa KGB bwana Alexander Litvinenko aliyekimbilia nchini uingereza aliwekew sumu iliyokuj kuonekan baada ya wiki 3,kuj kufatilia kumb jamaa alikutan na jasusi wa FSB kweny hotel, aliwekew sumu kweny chai ambayo ndo ilipelekea kuw mwish wa maish yake
stori yote imeishia kufa kwa soviet,na baada ya hapo hakuna lunaloendelea sababu nafikiri wamekubali kushindwa hawa warusi.
 
hizi nchi zikikutak unaondok tu mapem maan wameajir watu weng san weny mafunzo na mbin za kutosh,FSB wameajir watu 300,000 idadi ambayo hat jesh letu zima alifikii hichi kitengo.sasa unategemea wasiwrz kukupat kweli
na wapo kila sehemu, Mfano Mshambuliaji wa Alsenal Andre Arshavin alifurushwa england baada ya kujulikana ni JASUSI wa Russia kwa jina la (RED FOX). Kuna kipindi inasemekana alijifanya yuko injury ili abaki london anakusanya taarifa. Na inasemekana alitumiwa wadau wengine watatu in case mission imekamilika wamtoroshe. Ili kuwapoteza wasimfuatilie uliandaliwa uvumi kuwa anatakiwa kujiunga na madrid
 
Kama ilivyo CIA, KGB (imekuwa FSB kuanzia 1995)shirika la kijasusi la USSR sasa URUSI limewahi kuhusika katika operation hatari sana maeneo mbalimbali Duniani. Kilele cha operation hizo ilikuwa kipindi cha vita baridi. Taarifa nyingi zilijulika pale jasusi la KGB Vasili Mitrokhin lilipotorokea uingereza na Mafaili yenye siri nyingi maana alikuwa ni mtunza kumbukumbu wa shirika hizo.

1:MASHAMBULIO KWA MIUNDOMBINU YA MAREKANI
Hungry-Horse-Dam.png

kUANZIA 1957 Hadi 72 KGB walianza kupiga picha miundombinu ya marekani kwa siri. Mitambo ya umeme,Mafuta chochote kile ambacho kingeleta athari za kudumu kwa mmarekani kilipigwa picha.Mipango yote ilikuwa ni kuahakikisha ikitokea vita, wanapiga shambulio moja amerika hasa new york inakoswa umeme, na kuanza kushambuliwa na russia mtaa kwa mtaa.

2: MIKAKATI HATARI YA KUOKOA MATEKA RAIA WA URUSI.

Hostage-Retribution.jpg

Mwaka 74 walinda kikosi maalumu kiitwacho ALPHA GROUP. KBG waliunda kikosi hiki kutekeleza mission za siri sana na Za kikatili kupita kiasi ili kuwaokoa mateka wao. Mfano ni huu wa LEBANON.
Magaidi waliwateka wanadiplomasia wanne wa kirusi siria. Lengo ni kuizuia russia isiiunge mkono siria.Baada ya maridhiano kufeli na magaidi kuonyesha wamemuua mmoja wa mateka, ndipo kikosi hiki kikaingilia kati, waliperereza na kujua kundi hilo ni hesbula. Wakamteka ndugu wa karibu na kiongozi mkuu wa hesbula. wakawa wanamkata vipande vidogo vidogo vya mwili wakivituma kwa kiongozi huyo vikiambatana na ujumbe.Baadae walimuua na wakamtumia kiongozi huyo ujumbe kuwa wanajua pote walipo ndugu na familia yake na kinachofuata ni kuwafanya wote kama huyo ndugu yao akiwemo na yeye aliyedhani hajulikani. Haraka sana magaidi waliwaachia hao mateka bila masharti yoyote.

3:KUTUMIA WANAWAKE WAREMBO KUREKODI VIDEO ZA NGONO ZA VIONGOZI
Blackmail-Stewardess.jpg

KGB ilijumuisha wanawake warembo waliowaita "SWALLOWS", USSR walikuwa na mpango wa kutawala dunia, Mshirika wao Indonesia alipopata nguvu walipata hofu atawaasi na kujikita na uislamu. Raisi wa nchi hiyo SURKANO ndio alikuwa kikwazo. Baada ya kumfuatilia waligundua anaudhaifu mkubwa katika NGONO. Walipanga SwALLOWS wa kutosha hotelini alipofikia na kwenye ndege kama wahudumu. Bila kujua wakamrekodi akiwa anafanya mapenzi na wadada hao kwa mpigo. Walipomtishia na kumtumia hizo clip ili awe mpole aendelee kuwaunga mkono, majibu yakawa tofauti maana hakushtushwa na aliomba wamtumie nyingine zaidi maana zile zilikuwa ni chache. Jaribio likafeli.

4:KBG HACKERS (WADUKUZI WA KIMTANDAO) WALITEMBELEA ZAIDI YA COMPUTER 400 ZA WANAJESHI WA MAREKANI
Old-Computer.jpg

mwAKA 80 Walikuwa wanatafuta jinsi ya kuPATA siri za jeshi la marekani. Walimuajiri jamaa anayeitwa Markus Hess mtaalamu aliyebobea katika anga hizo. Shughuli nzima ilifanyikia UJERUMANi ambapo aliweza kuACCESS computer zaidi ya mianne za jeshi la US. Akifanikiwa kubashiri PASSWORD za computer muhimu kabisa PENTAGON na kupata taarifa za siri za wanajeshi lukuki.
Hadi pale mtaalamu wa US Cliford stoll siku moja katika pitapita zake akaona vitu asivyovielewa kwenye system yao. ilimchukua miezi 10 kujua nini kilikuwa kinaendelea na huyo jamaa aligundua ana SUPPERACCESS ya Deffensive system ikiwemo mitambo ya nyuklia marekani. Hadi alipowekewa mtego wa kimtandao na kunaswa huko hannover ujerumani. alikuwa anawauzia KBG hizo siri.

5:OPERATION RYAN
Spying-on-the-US.jpg

Miaka ya 80, ulizuka uvumi kuwa US wanajiandaa kuilipua russia muda wowote na makombora ya NYUKLIA. Ndio KGB na urusi wakaja na hii operation ambayo ni kubwa kuwahi kutokea.
Walipanga kuweka satelite zitakazopiga picha vituo vya kijeshi marekani nzima kila sekunde kuona kama kuna kombola linakuja,Pia kumonitor matumizi ya RADA amerika yote ili kuangalia uwezekano wa shambulio. Pia kuwachunguza raia na wanajeshi wa marekani wote wanapoondoka US, PIa kuiweka NATO chini ya uachunguzi wa hali ya juu. Walijaribu kuingilia mawasiliano ya simu yote nchini marekani na ulaya yote. Waliweka mtandao wa MAKACHERO duniani ambao wako tayari muda wote kushambulia wakiona urusi inavamiwa na marekani. Operation hii ya mabilioni ilihairishwa miaka mitatu baadae.

6:KUNUNUA BENKI ZA WAMAREKANI
6-us-bancorp.jpg

KBG hawakupanga kutumia mashushu wao kujua siri za selikali ya malekani, Badala yake walitumia BENKI.Wlipanga kununua BENKI TATU huko Northern California. Hawakukurupuka walijua benk hizi zilitumika na makampuni yaliyokuwa yanatengeneza TECHNOLOGY za jeshi la US, Wakaona kumiliki hizo benki watapata taarifa za siri za nini wanafanya jeshini kwa maana ya teknolojia.CIA walishtukia huu mchakato baada ya kugundua Mnunuzi kutoka Singapole aliingiziwa pesa kutoka RUSSIA.

7:OPERATION PANDORA
Watts-Riots.png

Waliendelea kuiandama marekani maana ndio alikuwa adui yao namba moja. Safari hii KBG wanapanga machafuko ndani ya US. Unakumbuka miaka ya 60 kulikuwa na vuguvugu la watu kupinga ubaguzi, kwa KGB hii ilikuwa ni fursa. Waliandaa vipeperushi NEW YORK na majarida feki yaliyoonyesha watu weusi wanawavamia wenye asili ya WAYAHUDI na kuwaibia vitu. Majarida haya yalionyesha kuwa walalamikaji ni kundi la waisrael JEWISH DEFENCE LEAGUE ambao kwa FBI walihesabiwa kama magaidi. Kisha wakayasmbaza kwa watu weusi waliokuwa wanamiliki silaa na mapolisi/wanajeshi weusi uchochezi huu wajiandae na mashambulizi ya wayahudi. Kuzidi kuchochea KGB walipanga kukilipua chuo kilichojaa wanafunzi weusi tu. Baada ya kulipuka chuo watume ujumbe kwa vyama vyote vya watu weusi kuwa ni WAYAHUDI ndio wanahusika.

8:SAKAFU YA KUSIKILIZIA
Hotel-Viru.png

KBG walikuwa wako vizuri sana ktk kuweka vinasa sauti kusikiliza mazungumzo katika maofisi na majengo mengi. Yaani waliwahi kuweka vinasa sauti katika hoteli maarufu kwa zaidi ya miaka 20 bia kujulikana. Mfano nchini ESTONIA jengo lenye ghorofa 22 lililokuwa linafikiwa na wafanya biashara wakubwa duniani, kulikuwa na floor ya 23 ya siri iliyokaliwa na KGB kwa muda wa miaka 20 hadi USSR ilipoanguka mwaka 1991. Mtoto mdogo aliyempa barozi wa Marekani Russia zawadi ambayo ilipachikwa kinasa sauti chenye uwezo wa hali ya juu. Kwa miaka saba KGB walikuwa wanasikiliza mawasiliano yote hadi kilipo gunduliwa ka bahati mbaya na mfanyakazi wa radio wa UK alipokosea mawimbi na kusikia mazungumzo asiyoyaelewa.

9:KUFADHILI UGAIDI
Terrorists.jpg

Jasusi la KGB Aleksandr Sakharovsky anajinasibu kuwa "Utekaji wa ndege ni UVUMBUZI WAKE".
Waliungana na YASSER Alafat na kumsaidia kuchukua madalaka ya PARESTINA. Walitengeneza magaidi wa kutosha na wapigania uhuru ili kuwadhoofisha maaduia wao. Mfano mwaka 69 tu ndege zaidi ya 82 zilitekwa sehemu mbalimbali duniani na hawa jamaa. Walichochea vita huko IRELAND kwa kuwasambazia Bunduki,bastola, mabomu wanajeshi kitu kilicholeta machafuko makubwa. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza mataifa mengi yenye kuunga mkono ukomunisti.


DUNIA INA MAMBO MENGI,
HII NI TAASISI MOJA TU LAKINI UKISOMA KUHUSU CIA(US), MOSSAD(UZAYUNI), MI6(UK), ISI (PAKISTANI),BND(ujerumani), RAW(INDIA), DGSE (UFARANSA),ASIS(AUSTRALIA) NA MSS(CHINA) UTAJUA GHARAMA YA KUILINDA NA KUITANGAZA NCHI KATIKATI YA MAADUI BILA VITA.
ni hatari
 
Back
Top Bottom