newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,378
549
external-content.duckduckg.jpg


Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.
Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.


MICHANGO YA BAADHI YA WADAU
UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!
(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)

Kuna usemi flani unatumiwa na watu wengi sana. unasema; "kazi ndio msingi wa maendeleo ya mtu yeyote" . Hata mimi nakubaliana na usemi huu kwani ni kweli kabisa kazi ndio msingi wa hatua yoyote ya maendeleo ya mtu yeyote chini ya msingi mkuu ambao ni Mungu.

Kinyume chake, asiyefanya kazi (ya kuajiriwa/kujiajiri) basi atabaki kuwa maskini na mtu wa shida ya kipato, mahusiano mabaya na wanadamu wenzako, kuwa tegemezi nk. Kwa kuwa tunatamani sana kutoka katika kongwa hili la umasikini wa kipato na hali mbaya ya maisha, tunalazimika kufanya jukumu letu kuu la kumuomba sana Mungu ili atuwezeshe kujua na kufahamu mbinu mbalimbali kisha kujifunza na kufahamu kwa makini tena kwa njia rahisi mno za kututoa katika hali hii ya umaskini uliokithiri.

Ikumbukwe kwamba, kujifunza kwa msisimko tu bila ya kuyaingiza mambo hayo uliyojifunza katika mazoezi na vitendo vya makusudi maishani mwetu ni wazi kwamba hayatatusaidia, bali yatabaki vichwani mwetu kama hadithi tu za alfulelaulela na maisha ya kubahatisha maarufu kama akadabraakadabra. Hivyo tumuombe sana Mungu wetu ili mafundisho haya yaweze kubadili maisha yetu kwa uchumi bora na endelevu ili tuweze kupata kipato na kurudishia Mungu zaka na sadaka badala ya kukaa kulalamika kuwa hatuna cha mkurudishia muumba wetu YEHOVA.

Kama ilivyo chunvi ya dunia, ufugaji pia huhitaji upendo, uvumilivu, karama, utu na maombi ya dhati ambayo yatazaa namna nzuri ya kuipenda kwa dhati ya moyo wako kazi hii ya ufugaji. Vinginevyo utabakia kuwa mtu wa kujaribu na kuishia kushindwa kila mara. Kama ilivyo kanuni ya maendeleo yoyote yale, ufugaji wa kuku pia huhitaji; Ubunifu, utundu wa akili, kujaribu bila kukata tamaa, kugundua, kujifunza, kufanyia kazi mawazo yaa wengine, kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo kazi yako, kujishughulisha nk. Hata ukifundishwa darasani huwezi kufundishwa vyote na mwalimu wako, vingine itakubidi utafute mahali pengine kwa ubunifu mkubwa, ugunduzi na mambo mengine mengi ili ufanikishe lengo la kupata elimu bora ya kile unachokitaka. Hii huhusisha akili yako vema katika kujifunza kutoka kwa watu au vitu vingine nk. Lakini mafanikio zaidi yatapatikana pale utakapokuwa katika utendaji zaidi.

UFUGAJI WA KUKU WATANO (5) WA KIENYEJI UPATE KUKU MIA MBILI (200) KWA MIEZI SITA (6) TU!
(Kuku 200 x 5,000 = 1,000,000)

Unaweza ukaniona kama mimi ni kichaa na ninaye ota ndoto za mchana ambazo hazina mafanikio wala tija maana nadharia hii inaweza isiwaingie vizuri watu vichwani mwao. Watu wengi wamekuwa wakisema na kushauri hata kushauriwa hata na wale wasiofaa. Ninaamini wengi wetu hawapendi kuamini kile wanachoambiwa hadi pale watakapoona kwa macho yao ndipo waamini (akina Tomaso).

Sikia nikuambie! kama huamini haraka kitu chochote hebu usimkatishe tamaa yule aliyekwambia habari hizo za kukatisha tamaa, badala yake jaribu kupeleleza na kufuatatilia hatua kwa hatua tena kwa makini maelezo uliyopewa, kisha yaweke katika utendaji (tenda/fanya) kwa ufanisi kisha subiri matokeo. Baada ya kupata matokeo sasa unaweza kwenda mbele kidogo ukauliza/kusoma/kujifunza zaidi ili kuona kama kuna mahali umekosea au hukuzingatia kanuni na maelekezo uliyopewa.

Baada ya kupata maelezo ya ziada hebu rudia kufanya tena kwa kuboresha kupitia maelekezo ya awali na hayo mapya uliyopata yote kwa pamoja ili upime matokeo yake. Hapo sasa utakuwa upo kwenye haki ya kuamini au kutoamini kwamba jambo hilo ni kweli au siyo kweli na siyo kutaa tu kwa ubishi usiokuwa na maana yeyote. Kwa kufanya hivi hakika utapiga hatua mbele katika kuboresha maisha yako ya sasa na ya baadae. Ila ukifanikiwa usije ukamkufuru Mungu aliyekuwezesha.

Hebu anza na kuku Watano (5) tu Majike wenye Rika/Umri mmoja (au wanaokaribiana). Watunze vizuri kwa kuwapatia chakula kilicho na mchanganyiko kamili wa viini lishe vinavyotakiwa katika mwili wa kuku, yaani; wanga, protini, calcium, chumvichumvi, madini joto nk (kama nilivyoeleza hapa chini). Wawekee na Jogoo mmoja mzuri wa kienyeji/kizungu/chotara (kama nilivyoeleza hapa chini juu ya uchaguzi wa majogoo).

Wanapoanza kutaga watayarishie mahali pazuri/Kiota kizuri cha kutagia na kuatamia kwa kuwajengea viota ndani ya banda. Hakikisha mahali hapo hapavuji wala hapapati unyevunyevu wala joto kali sana. Hakikisha mahali hapo pana usalama wa kutosha (mahali wanyama hatari kama vicheche, pakashume, nyoka nk hawawezi kufika).

Kuku wakiendelea kutaga na sasa ukaona wanakaribia kuatamia,Anza kuchagua aina ya mayai unayotaka kuku wako walalie. Hii inamaanisha kuwa; ukichagua mayai makubwamakubwa hayo yanakuwa na vifaranga majogoo na mayai madogomadogo mara nyingi huwa ni ya vifaranga majike. Acha kuwawekea mayai ya mviringo kama mpira!

Hakikisha kuku wote wanasubiriana ili walalie/waatamie kwa pamoja.

Weka mayai 12 hadi 15 kwa kila kiota cha kuku 1 kulingana na umbo la kuku wako. Kuku anaweza kutaga hadi mayai 30 kwa kila msimu wa kutaga unapofika. Unaweza kutumia mayai machache kati ya 30 kwa kumuatamishia kuku wako huku mayai mengine yakisubiri awamu ya pili ya kuatamiwa.Kwa mfano ukiwawekea kuku wako hao watano, Kuku 5 x Mayai 12 = Mayai 60.

Kwa kawaida kuku huatamia/hulalia mayai kwa siku 19 hadi 21/24 tu hadi anapototoa vifaranga. Hakikisha unawawekea kuku walioatamia chakula chenye viini lishe vya kutosha na maji mengi karibu na viota vyao ili wakitoka kwenye viota vyao wale chakula mara moja na kunywa maji kisha warudi haraka kwenye mayai yao. Hii itasaidia kuangua mayai yote 12/15 bila kuharibu yai hata moja. Au hata yakiharikbika basi hayataharibika mengi kama ukiacha kuwawekea chakula waende kufukuzana na panzi na vyakula majalalani huko nje na kuchelewa kurudi kwenye mayai yao.

Wakati ukisubiria siku hizo 21/24 anza kujenga kibanda kidogo ndani ya banda kubwa ulilojenga awali au jikoni au andaa boksi kubwa na gumu kwaajili ya kutunzia vifaranga watakaoanguliwa ndani ya siku 21/24 zijazo.

Baada ya kuku hao 5 kuangua vifaranga wako 60 hapo ndipo kazi kubwa ya kulea vifaranga inapoanza. Elewa kuwa ili upate mafanikio haraka hakikisha kuwa kazi ya kulea vifaranga inakuwa yako na siyo ya kuku! Kwanza, Unatakiwa kuondoa na kuchoma moto/kufukia mabaki yote ya mayai na kuboresha usafi wa banda lote ili kuepusha magonjwa kama vile kuharisha, viroboto, papasi nk. Hapo unaweza kuwatoa vifaranga wako wote 60 mmojammoja kadri wanavyoanguliwa hadi kufikia kifaranga wa mwisho, yaani Yule wa 60 na kuwaweka katika kibanda kidogo/boksi ulichokijenga na kuwawekea mayai mengine mama zao (yale 15/18 kati ya 30 uliyoyabakiza) ili waatamie tena kwa siku 21 hadi 24 zingine. Unapotoa kifaranga kutoka kwa kuku aliyeatamia humfanya kuku Yule ashindwe kutoka kwenye mayai maana hana mtoto wa kulea.

Akimaliza kuangua mayai yote na ukamuwekea mengine ni rahisi kwake kuendelea kuatamia maana atasubiri kupata vifaranga na ndipo atajikuta amelalia kwa siku 21 zingine bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo utakuwa tayari umejipatia vifaranga/kuku zaidi ya 100 ndani ya wiki 7 tu! Sasa Unatakiwa kuwajali sana kuku hawa wanaolalia kwa mara ya pili kwa kuwapa chakula cha kutosha, maji, majani ya makongwe, mchicha, mchunga nk ili wapate vitamini na madini mengine muhimu kwa afya zao. Fanya hivyo hata watakapokuwa wametotoa na ukawanyang'anya vifaranga. Hii itawasaidia ili wasinyonyoke sana manyoya maana kuku wengi hunyonyoka manyoya wanapoatamia. Kwa kufanya hivi, kuku wako watakaa kwa wiki 2 hadi 3 bila vifaranga na kisha wataanza kutaga tena na kuatamia kama mwanzo.

Vifaranga wako hakikisha unawatengenezea chumba chao kido ndani ya banda kubwa/jikoni, kisha wawekee chanzo chochote cha joto kama vile; taa ya chemli/jiko la mkaa/vizinga vya moto nk ili wasiathiriwe na baridi hasa wakati wa usiku. Umakini mkubwa sana unatakiwa hapa! Hakikisha unakuwa makini wakati wa usiku ili kuongeza na kupunguza joto ndani ya kibanda cha vifaranga maana wakati huu maranyingi joto hupungua na ubaridi huongezeka na hivyo unaweza kuua vifaranga wako.

NAMNA YA KULEA VIFARANGA
Katika ulezi wa vifaranga kama kuku utawanyang'anya vifaranga vyao utatakiwa kuwajengea banda dogo (ndani ya banda kubwa/uzio) ili uwawekee chanzo cha joto kama taa/jiko la mkaa (kama ni sehemu/majira ya baridi). Kama utatumia jiko la mkaa unatakiwa kuacha kwanza hadi mkaa mweusi uwake wote ndipo uweke bandani maana mkaa ukitoa moshi unaweza kuathiri vifaranga vyako. Angalia namna ya kuweka jiko lako la mkaa juu kidogo ili vifaranga wasiungue. Hakikisha taa yako haitoi moshi sana na haivujishi mafuta. Pia uwe na akiba ya mafuta ya taa ya kutosha. Usiweke mafuta mengi kwenye taa maana inaweza kulipuka ikakuletea hasara. Vifaranga wasizidi 50 kwa boksi 1. Hakikisha umewasha taa/jiko lako ndani ya boksi saa tatu au zaidi kabla ya kuwaweka vifaranga ili chumba/boksi lipate joto kabla ya vifaranga kuwasili. Njia hizi zinahitaji uangalifu wa hali ya juu sana kwani kuhatarisha/kuua vifaranga ni kuhatarisha maendeleo yako. Kama utaamua kutumia umeme pia ni vizuri zaidi maana inapunguza hatari zaidi.

Kwa hiyoa njia zote tatu unaweza kutumia jedwali lifuatalo ili kuweza kumeneji joto la kibanda cha vifaranga;
UMRI WA KKUKU/VIFARANGAJOTO NDANI YA BOX/KIBANDA CHA KULELEA VIFARANGAJOTO NDANI YA CHUMBA/BANDA
Wiki 133-35oc30-32oc
Wiki 230-33oc27-29oc
Wiki 327-31c24-26oc
Wiki 424-29oc21-23oc
Wiki 526-27oc22-23oc
Baada ya wiki ya 4/5 pasua box/watoe kwenye banda la kulelea ili walelewe kwa joto la kawaida la banda/chumba.
Kwa kawaida joto hupimwa kwa kipimajoto (thermometer), lakini kama huna kipimo hiki, njia rahisi ni kuwaangalia kulingana na tabia zifuatazo; Kama vifaranga wamejikusanya sehemu moja basi joto ni kidogo bandani mwao, au kama wanaenda mbali na chanzo cha joto huku wanatanua mabawa yao na wakihema harakaharaka basi joto ni kali/limezidi kiwango. Pale watakapo tawanyika vizuri ndani ya boksi/kibanda cha kulelea huku wanakula na kunywa maji vizuri basi joto ni la wasta na ndilo linalofaa. Kama unatumia njia ya Boksi, basi unatikiwa kulipanua kulingana na ukuaji na mahitaji ya vifaranga vyako.

Vifaranga wako wape chakula cha vifaranga cha kutosha, maji safi na salama, majani mabichi ambayo hufungwa kwa kuning'inizwa kwa kamba,na CHANJO za minyoo nk ili wapate vitamin, madini na protini itakiwayo na kuzuia tabia ya kudonoana ili wakue vizuri.

Hakikisha kuwa chumba chao ni kisafi na hakina unyevunyevu wakati wote. Unyevunyevu husababisha ugonjwa wa baridi na hufanya vifaranga wajikunyate na kutetemeka na wanaweza kufa ghafla!

Inashauriwa kuwa siyo salama kufuga aina nyingine ya ndege kama vile njiwa, bata, bata mzinga nk kwa kuwachanganya na kuku maana kila aina ya ndege wanamagonjwa yao. Hivyo kuwachanganya kutakufanya ushindwe namna ya kuwatibu wanapopatwa na ugonjwa. Pia chawa wa njiwa huleta ugonjwa wa Ndui hasa kuku wanapoangua vifaranga wao. Hapa ugonjwa unaweza kufyeka vifaranga wako wote 60/100 kama utafuata ushauri wangu!

Baada ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuwanyang'anya vifaranga kuku wako wataanza tena kutaga mayai. Wakiatamia wote 5 Kama utaimarisha huduma kwao na kwa vifaranga/kuku wale 100 tayari utakuwa una kuku 105 au zaidi. Kuku wale 5 wa mwanzo wakiatamia tena kwa siku 21 hadi 48 (kama utafuata mfumo ule wa mwanzo wa kuaatamishia mara 2) utajipatia vifaranga wengine 100 tena na hivyo kuwa na kuku zaidi ya 200 ndani ya miezi 5/6 tu! Ukiwahudumia vifaranga wale wa mwanzo 100 vizuri kwa miezi 3 na nusu nao wataanza kutaga kama mama zao.

Kwahiyo, Chukulia walalie majike 5 wa mwanzo na majike 50 waliopatikana baada ya uzao wa kwanza kwa miezi ile 3 ya mwanzo utakuwa na mitetea 55. Wote wakiatamia na watoe vifaranga 10 kila mmoja kwa siku zilezile 21 hadi 46, tayari utakuwa na vifaranga 550! Sasa jumlisha na wale 150 waliobakia kati ya kuku 200 na wote wakakua vizuri utapata kuku na vifaranga zaidi ya 700! Jumlisha na 550 watakaototolewa na mama zao wale 5 wa kwanza na wale 50 wa uzao wa 1 na 2 kwa mara ya 2 si tayari utakuwa na kuku zaidi ya 1,200 ndani ya miezi 6 hadi 8 tu? Hivyo utajikuta unao kuku zaidi ya 1,000!

Kati ya kuku 1,000 ukisema utoe kuku 800 wa kuuza na ukiwauza kwa bei ya Tsh. 4,000 kwa kila kuku 1 tayari utakuwa na Jumla ya Tsh. 3,200,000/= ambazo unaweza kufanya mtaji wa mambo mengine au kuboresha mradi wako zaidi. Unafikiri hapo hujaanza kufikia lengo la kuku 1 akuletee shilingi Milioni 1? Ukiendelea hivi inamaana kuku 1 atakuzalishia zaidi ya hapo.

BANDA LA KUKU
Unatakiwa kuwa na banda bora la kufugia kuku ambalo litaweza kutunza kuku ili wasiweze kupatwa na madhara mbalimbali kama vile; kuliwa/kujeruhiwa na wanyama wakali, kuchukuliwa na wezi nk. Lakini banda bora pia litawasaidia kuku kuhimili mabadiliko mbalimbali ya hali ya hewa yanayoweza kujitokeza.

Sehemu ambayo inafaa kwa ujenzi wa banda bora ni ile ambayo inaweza kufikika kwa urahisi, iwe na mwanga wa kutosha, isiwe na upepo mkali na isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.

Banda ni vema likawa la ukuta/mbao/mabanzi.matete/mianzi imara ili lishikilie paa vizuri lisianguke. Kuta hizi zaweza kujengwa kwa matofali ya saruji/matope/kuchomwa/mabanzi/mbao nk. Katika kuezeka waweza kutumia mabati/vigae/nyasi. Banda ni vema likawa kubwa kulingana na kiasi cha kuku na umri walionao. Kitu cha kuzingatia ni kwamba banda liwe na hewa ya kutosha.

Kuku wanaofugwa ndani ni vema wakatengenezewa uzio mpana (angalau Mita 8x10) ili wapate mahali wanapoweza kuota jua, kupumzikia/kupunga hewa na kufanya mazoezi (wawekee kamba/bembea/ngazi ndani ya banda). Hakikisha kuwa banda ni imara na hawatoki nje ya banda na kwenda mbali ili uweze kuwawekea chakula cha kutosha na maji na hata wale wanaotaga/kuatamia wapate chakula na kurudi haraka.

Banda likiwa kubwa na bora litapunguza magonjwa kwani litakuwa na hewa ya kutosha ambayo itasaidia kupunguza joto na unyevunyevu usio wa lazima bandani mwako. Hii itasaidia uingizaji oksijeni ya kutosha na kupunguza hewa chafu zenye madhara kwa kuku. Pia litasaidia namna ya kufanya usafi kwa urahisi na kupunguza vumbi ambalo linaweza kusababisha kikohozi kwa kuku wako. Ni vema banda lisipungue Mita 3 kwenda juu.
Mambo muhimu ndani ya Banda.
  1. Sakafu nzuri (iliyotengenezwa kwa saruji/udongo ili isituamishe maji. Isiwe na nyufa ili iweze kusafishwa kwa urahisi.
  2. Hakikisha kuwa banda linakuwa na Viota (vitagio) vizuri kwaajili ya kutagia. Viota viwe na urefu wa Sentimita 30 na upana sentimita 30 na kina sentimita 35. Sehemu ya mbele izibwe kwa sentimita 10 tu chini. Sehemu zote hizo zizibwe kwa ubao. Kama kuku wako ni wakubwa unaweza kuongeza upana, urefu na kina kiasi cha kutosha mfano, Upana na Urefu 35cm, kina 55cm nk. Hakikisha kiota/kitagio kinakuwa na giza kiasi maana kuku hupenda kutaga mahala pa giza kidogo/palipojificha. Giza litasaidia kuku asiweze kula mayai au asiweze kudonoana na kuku wengine. Kiota pia kinatakiwa kiwe mahali ambapo ni rahisi kwa kuku kuingia na kutoka, pia iwe ni rahisi kusafisa.
Ndani ya kiota kuwekwe majani makavu/maranda ya mbao laini na kinyunyize dawa ya unga ya kuzuia viroboto/utitiri kabla ya kuweka nyasi.

AIDHA, ni vizuri sana kuwawekea kuku wanaoatamia mayai wakati wa usiku maana ukimuwekea wakati wa mchana anaweza kuyaacha.

Kuku anayetarajiwa kuatamia ni vema akachunguzwa kama anao utitiri/viroboto/chawa kwenye manyoya yake. Wadudu hawa humkosesha raha kuku anayeatamia na wengi huacha mayai na kukimbia/wasitulie kwenye viota vyao. Hali inapelekea kuanguliwa kwa vifaranga wachache. Unaweza kumuona mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi.
  1. Banda liwe na vichanja maana kuku hupenda kulala juu ya vichanja maana nao ni ndege.
  2. Vyombo safi na vizuri kwaajili ya chakula na maji.
  3. Walazie majani makavu/maranda ya mbao/makapi ya mazao sakafuni kwa banda zima.
UCHAGUZI NA UHIFADHI WA MAYAI
Mayai huharibika kwa urahisi sana yasipo tayarishwa na kutunzwa vizuri kwa uangalifu. Matayarisho huanzia bandani hadi ndani kwa kufanya yafuatayo;
  • Hakikisha viota vyote ni safi wakati wote.
  • Chakula kiwe ni cha kuimarisha gamba la yai na vyakula vingine.
  • Vyombo vya kukusanyia mayai viewe safi na imara.
  • Kusanya mayai mara2 hadi 3 kwa siku ili kuepuka mayai kuvunjwa/kuliwa/kuchafuka kwa mayai mengi na kupoa haraka.
  • Ondoa mayai yaliyo na nyufa na maganda yasiyo imara.
  • Safisha mayai mara baada ya kukusanya na kabla ya kuweka kwenye chombo cha kuhifadhia saa 12-24. Mayai yanaweza kuoshwa kwa maji ya uvuguvugu (nyuzijoto 35oc) na kusugua taratibu kwa mkono ili kuondoa uchafu (kama upo). Lakini unashauriwa kusugua kwa mkono bila maji ili kusafisha maana maji hupunguza ubora wa yai na maranyingi yai huharibika haraka.
  • Weka katika vyombo visafi kwa kuelekeza sehemu ya yai iliyo pana iwe juu na sehemu nyembamba iwe chini, beba kwa uangalifu.
  • Hifadhi mayai katika sehemu ya baridi nyuzijoto10 hadi 16 za sentigredi.
  • Mayai yapangwe kwa daraja kwa kufuata ukubwa na rangi ili kuvutia wateja na kuongeza bei. Pia unaweza kuweka kwa kufuata muda unapoyaokota kutoka bandani. Weka lebo yenye tarehe ili usichanganye wakati wa kuwaatamishia kuku wako/kuuza.
Kuchagua mayai ya kuatamishia kuku kwaajili ya kuangua vifaranga.
Mayai yanayofaa kwa kuatamiwa na kuanguliwa ni vema yawe na ukubwa wa wastani, yasiwe na ufa/nyufa, yasiwe ya mviringo kama mpira, yasiwe na uchafu wowote juu ya gamba lake, yasiwe yametengwa kwa zaidi ya wiki 1 (siku 7).

NJIA MBALIMBALI ZA UFUGAJI WA KUKU
Kuna njia kuu mbili za ufugaji wa kuku.
  1. Ufugaji Huria
Aina hii ya ufugaji, kuku huachiwa huru wajitafutie chakula na maji wao wenyewe. Utaratibu huu hutumika zaidi kufugia kuku wa kienyeji ambapo mfugaji hupata hasara na pengine hupata faida kidogo maana kuku hukosa uangalizi na hawapewi chakula cha ziada.
Faida.
  • Haina gharama kubwa za ufugaji.
  • Kuku hupata mazoezi ya kutosha.
Hasara.
  • Huharibu mazingira maana hula nafaka, mazao nk.
  • Ni rahisi kuambukizwa na kusambaza magonjwa.
  • Ni rahisi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa, watu na wanyama wakali kama paka, vicheche, mwewe, kipanga, nyoka nk.
  • Ni rahisi kutaga mayai porini/vichakani na hivyo mayai/kuku mwenyewe kupotea.
  • Ukuaji wake ni hafifu/uliodhorota.
  • Kuna uwezekano wa kuhamia nyumba nyingine/kwa jirani kwa urahisi.
  1. Ufugaji wa ndani ya Uzio/Banda.
Hufanyika katika sehemu iliyozungushiwa uzio/ndani ya uzio maalum ambapo kunakuwa kuna utaratibu wa kuku kupewa chakula na maji kwa urahisi. Ndani ya uzio huwekwa banda zuri, bora na imara ambalo huruhusu kuku kuingia na kutoka wanapopumzika/kulala/kutaga mayai. Ufugaji huu hutumika zaidi kwa kuku wa kigeni na kuku chotara na hata wa kienyeji pia.
Faida.
  • Gharama ya ufugaji wake ni kubwa.
  • Faida yake ni kubwa hasa ukufuga kibiashara.
  • Ni rahisi kuelewa kiwango cha utagaji na utotoaji wa kuku wako.
  • Ni rahisi kufahamu kuku wazuri wa kuatamiashia mayai na kulea kwa faida ya haraka.
  • Siyo rahisi kuku kuathiriwa na wezi/wanyama/vicheche/mwewe/hali mbaya ya hewa.
  • Siyo rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali kutoka nje.
  • Ni rahisi kutibu na kujua maendeleo ya kuku wako kwa urahisi.
  • Wanakuwa na usalama wa uhakika.
  • Faida zake ni nyingi kuliko ufugaji huria.
Hasara
  • Gharama za mwanzo za ujenzi wa banda, uzio na vifaa vya chakula na maji ni kubwa kiasi. Hivyo zinahitaji mtaji.
  • Njia hii inahitaji eneo kubwa na huru.
  • Ni rahisi kuambukizana ugonjwa kama itatokea.
  • Ufugaji huu unahitaji utaalam na umakini wa kutosha
UCHAGUZI WA KUKU.
Chagua kuku wenye sifa zifuatazo;
  • Wenye kukua haraka,
  • Wenye uwezo wa kustahimili magonjwa,
  • Wanaotaga mayai mengi,
  • Wawe na uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi na kuwalea (jike/mtetea).
Ni vema sana kutumia majogoo chotara au majogoo wa kienyeji wale wakubwa, warefu, wenye kucha fupi. Chagua wenye maumbile mazuri, uzito wa wastani na wawe wenye rangi za kuvutia kisha uwachanganye na majike/mitetea yenye umbo zuri, uzito mzuri na rangi nzuri ili kupata kuku chotara wanaokua haraka na wenye uzito mzuri kwaajili ya biashara nk. Kama huna kuku wenye sifa hizo basi ni bora sana ukanunua kutoka mahali pengine.
Wakati wa kuatamia ni vema kuku mmoja apewe/awekewe mayai 12 hadi 15 kwenye kiota chake mwenyewe na siyo kuwachanganya kama wakati wa kutaga maayai. Kama wametotoa kuku 2 au zaidi kwa wakati mmoja ni vema aangaliwe kuku mwenye uwezo wa kulea vifaranga ili aachiwe vifaranga vyote (kama utashindwa kuwatengenezea boksi/kibanda cha vifaranga kama nilivyoshauri hapo juu) na kuku wengine watengwe na vifaranga ili waanze kulishwa vizuri na kuchanganywa na majogoo, hapa wataanza kutaga baada ya wiki 2 hivi.
MUHIMU: Ni vema sana kutofautisha makundi ya kuku kulingana na umri wao ili kupunguza kuku kudonoana/kuumizana.

NAMNA BORA YAKULISHA NA KUNYWESHA KUKU.
  1. MAJI.
Maji ni muhimu sana kwa kuku wawapo bandani. Wape maji ya kutosha kila wakati unapoona yanapungua/kuisha ili waendelee kuyeyusha chakula wanachokula Nna kupunguza joto mwilini. Kuku 1 anaweza kunywa hadi robo lita ya maji kwa siku. Kwa hiyo utawawekea kulingana na wingi wao. Pata chombo kizuri ili uwaning'inizie juu kidogo kutoka usawa wa ardhi. Hii itasaidia kupunguza uchafuzi wa maji na magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya maji.

ZINGATIA= hakikisha kuwa maji ni safi na salama.
  1. CHAKULA.
Ni vema kutafuta vifaa vizuri kwaajili ya kuwawekea chakula. Tafuta vyombo ambavyo utaweza kuning'iniza/tundika juu kidogo kutoka chini kulingana na umri wa kuku.

Hii itasadia sana kupunguza uwezekano wa kutosambaa kwa magonjwa hasa yale yanayoenezwa kupitia viatu tunvyo vaa tunapoingia bandani. Pia itasaidi sana kupunguza chakula kinacho mwagika chini wakati kuku wanapokula.

Kwa mfugaji yeyote wa kuku anapaswa kuelewa kuwa chakula cha kuku ni ghali. Hivyo ni vema kufuata taratibu vizuri katika ulishaji na kutengeneza/kununua vyombo ambavyo kuku hataweza kumwaga chakula. Kumbuka kwamba kama vyombo siyo vizuri basi vitamwaga chakula kingi na hivyo kukuletea hasara.

Ili kuweza kupata mazao mazuri yenye faida, ni vema ununue chakula cha kuku madukani au utengeneze wewe mwenyewe kama nitakavyoeleza hapa chini ili uwape kuku wako chakula chenye viini lishe vyote muhimu kwa kuzingatia umri wa kuku ulionao. Kwa vifaranga, unaweza kuwawekea chakula chini kwenye magazeti/mifuniko ya ndoo/sahani. Baada ya siku 10 unaweza kuwawekea kwenye chombo maalum.

Namna ya kuandaa chakula cha kuku.
Vyakula vya kuku vinapaswa kuwa na aina/viini lishe muhimu kama vile Protini, Wanga, madini na Vitamini.
Vyakula hivyo vimegawanyika kama ifuatavyo;
  • Vyakula vya kujenga mwili ni; Jamii ya kunde,samaki, dagaa,mashudu ya ufuta/alizeti/pamba,
  • Vyakula vya kulinda mwili ili usipatwe na maradhi ni; Mafuta ya samaki na majani mabichi kama vile; kabichi, mchicha,majani ya mpapai na nyasi mbichi.
  • Vyakula vinavyojenga mwili/mifupa ni kama vile; Aina za madini, chokaa, chumvi na mifupa iliyosagwa.
  • Vyakula vilivyotajwa vinaweza kumkuza vizuri kuku hadi uuzwaji/kuliwa kwake. Surghum Larrymeal huzuia kudonoana, huboresha kiini cha yai na kuongeza mayai. Changanya kg 1 kwa kg 50 za pumba.
Ukosefu wa madini kama fosforasi na kalsiam husababisha matege, vidole kukunjamana, kufyatuka kwa misuli ya magoti, kuwa kilema na kupofuka macho kwa kuku.

Mfugaji wa kuku anaweza kununua vyakula hivi kwenye maduka ya pembejeo za kilimo/mifugo. Na kama huwezi unaweza kujitengenezea wewe mwenyewe kwa kukusanya mahitaji muhimu ya viinilishe kama ifuatavyo hapa chini;



Aina ya chakulaKiwango cha uchanganyaji (%)
VyakulaVifaranga
(Kgs)
Kuku wa Nyama
(Kgs)
Kuku wa Mayai
(Kgs)
Mahindi707070
Ulezi204040
Mtama203030
Mpunga407070
Ngano54040
Pumba za Mahindi102020
Pumba za Mpunga102020
Pumba za Matama102020
Pumba za Ngano51515
Mashudu ya Nazi103040
Mashudu ya Pamba51010
Mashudu ya Alizeti102020
Mashudu ya Ufuta10105
Damu iliyokaushwa555
Mifupa iliyosagwa557.5
Dagaa1055
Lucina555
Chokaa555
Chumvi0.50.50.5
Soya102020
Sorghum Larry Meal111


NB. Kabla ya kufanya kazi hii unaweza ukamuona mtaalam wa mifugo kwa ushauri zaidi kama utaona ni muhimu.

Mfano wa namna ya kuandaa kilo 100 za chakula cha kuku.
  1. Mfano wa chakula cha vifaranga kuanzia umri wa siku 1-wiki 4.

VYAKULAKIASI(Kilogram) KG
Mahindi30kg
Pumba za Mahindi20kg
Soya18kg
Mashudu ya Alizeti20kg
Dagaa5kg
Mifupa iliyosagwa4kg
Chumvi0.5kg
Vitamini2.0kg
Jumla 100

  1. Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia Wiki 4-8

VYAKULAKIASI(Kg)
Mahindi45kg
Pumba za Mahindi20kg
Mashudu ya Pamba5.0kg
Soya20kg
Dagaa2.5kg
Mifupa iliyosagwa5.0kg
Chumvi0.5kg
Vitamini/Damu kavu2.0kg
Jumla 100[/TD] MAGONJWA YA KUKU. Kuku huweza kushambuliwa na magonjwa mengi ambayo mara nyingi husababisha hasara kubwa kwa mfugaji. Hasara hizo ni kama vile; gharama za matibabu, upungufu wa mayai, kudumaa kwa kuku, na vifo. Magonjwa ya kuku yamekuwa ni tishio na hukatisha tamaa sana watu wanaofuga kuku. Magonjwa mengi husababishwa na Bakteria, Virusi, Vimelea, Minyoo, Viroboto, Chawa, Utitiri, Lishe duni au Uchafu. Lakini sauala hili limegundulika kuwa mara nyingi makosa ni ya wafugaji wenyewe kwani maranyingi hupuuzia suala la umuhimu wa kuwaona wataalam wa mifugo (ndege) na baadhi wanapobahatika kuwaona wataalam, basi hupuuzia ushauri wa wataalam hao. Baadhi ya magonjwa hayo na njia rahisi ya kuyatibu ni kama ifuatavyo (nimejitahidi kutafsiri kidogo,lakini maneno mengine ni ya kiingereza ambayo sikupata tafsiri yake kwa urahisi); MAGONJWA YA NDEGE WANAOFUGWA MAJUMBANI (HASA KUKU)
������������
JINA LA ASILIDALILIKISABABISHO
(PRESUMPTIVE DIAGNOSIS)
DALILI KUU
(CLINICAL SIGNS)
MATIBABU RAHISI LAKINI MUHIMU NA HARAKA TENA KWA GHARAMA NAFUU
Kideri/
Mdondo (Newcastle Disease)
Kusinzia,
kuhara, kushusha mabawa chini, kukosa hamu ya kula nk
Newcastle VirusKuku kuharisha kinyesi cha kijani/cheupe km chokaa na njano, kukohoa, kuhema kwa shida, kutokwa na mate mdomoni,kizunguzungu, kishiwa na maji, kukosa hamu ya kula,kushusha mabawa chini,kuku kufa hadi 90%.
  1. Pilipili kichaa na majivu
  2. Katani/Alovera
  3. Kitaalam tumia chanjo ya NEWCASTLE.
  4. Usafi wa banda &vyombo vote.
  5. Usafi wa mazingira na kuchoma moto mizoga yote.
  6. Usiruhusu watu kiungia ovyo bandani/usiingize kuku asiyechanjwa.
  7. Fuata ushauri wa daktari
Ndui (Fowl Pox)Vipele kwenye upanga (Nodules) na sehemu zisizo na manyoya.Fowl poxVipele kwenye upanga,masikio.miguu na sehemu zisizo na manyoya.Kuku hufa hasa wale wadogo.
  • Kuku wapewe chanjo, vitamin na antibayotiki (kiua vijasumu).
  • Uasfi wa banda na mazingira viimarishwe.
Mafua ya kuku/ Kuvimba machoSwollen eyes/ FluBakteriaKuvimba uso na macho,kamasi hutiririka kutoka puani na mdomoni,hukohoa,huhema kwa shida na kukoroma, utando mweupe/njano kwenye macho),upofu,nkBoresha Usafi wa banda na mazingira yake, kuku wagonjwa watengwe na ikibidi wachinjwe.
Muone mtaalam wa mifugo ili upate chanjo.
Ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa.Chronic Respiratory infection.Infections bronchitis laringotracheitis/Chicken Influenza (Bakteria)Kuku hupata Mafua, kushindwa kupumua,hutokwa na makamasi,vifaranga hudumaa,utagaji hupungua na viungo vya mifupa huvimba.Boresha usafi, hakikisha kuna hewa ya kutosha.
Muone mtaalam akupe antibayotiki huponya/kwa ushauri zaidiTenganisha kuku wenye ugonjwa.
Gumboro/Kuhara chokaaWhitish diarrhoeaFowl typhoidVifaranga kuharisha kinyesi cheupe, kupungua uzito,hushindwa kuhema,manyoya husimama,hutetemeka na hatimaye hufa.Chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku 1.
Zingatia usafi wa banda, vyombo vya maji na chakula.
Tumia mkaa.
Hakuna tiba ya kitaalam
Viroboto/ Utitiri/Fleas/mitesEctoparasitesFleas around the eyes, Restlessness (Kutulia kwa muda mrefu bila kuchangamka)Tumia kuweka majivu bandani. Kitaalam tumia dawa yenye unga kama poda.
PapasiSoft ticksSoft ticksSores on skin(Vidonda kwenye ngozi), Paralysis(ku, AnaemiaTumia kuweka majivu bandani. Kitaalam tumia dawa yenye unga kama poda.
kunyonyoka manyoyaMinyoo/bacteriaKunyonyoka manyoya na kubaki mtupu. Shingo kurudi nyuma, kushindwa kula vizuri.Tumia kinysi cha n'ombe. Kitaalam tumia Vitamin B12 na Egg Plus Fomula.
Kuhara choo cheupeWhite Bacillary DiarrhoeZaidi ni kwa vifaranga kabla ya wiki 4 kuhara mharo mweupe.Tumia mkaa, Alovera.
Kitaalam tumia OTC+
Homa ya matumboBloody diarrhea/
Typhoid
CoccidiosisUgonjwa huu huambukizwa kupitia maji/mayai/kinyesi/kudonoana na mazingira machafu. Kuku huharisha mharo wa kijani, vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu,manyoya kusimama.Tumia mkaa, Alovera.
Vitunguu swaumu robo kilo ikitolewa maganda,ikatwangwa na kuchanganywa na maji lita 1,chuja na kuwapa maji yake kwa wiki 1.
Ondoa kuku wenye ugonjwa na usitumie mayai yenye ugonjwa kuanguliwa vifaranga.
Kitaalam tumia Furazolidone.
Muone mtaalam
Kuvimba miguuSwollen legsScaly legsScales on legs(mikato miguuni), lameness.Tumia Alovera
Muone mtaalam
Kipindupindu cha kukuFowl CholeraBacteriaMharo wa njano, husinzia na kulegea,hulala kichwa kikining'inia kwenye mabawa,manyoya husimama,hushindwa kuhema na hatimaye hufa.Imarisha usafi wa banda,vyombo na mazingira yake.
Kitaalam unaweza kutumia dawa aina ya Salfa/muone daktari.
Mayai kuvunjika tumboni
Sleepy, on PM broken eggs with foul smellMuone mtaalam kwa ushauri.
Broken eggs in abdomen[/TD] Egg peritonitis
Kwa kutumia dawa za asili nilizosema hapo juu;
  1. Pilipili kichaa 50, twanga, changanya na majivu kikombe cha chai 1, weka maji Lita 1 wape kuku.
  2. Katani/alovera. Ipondeponde, iloweke kwenye maji usiku kucha, wape wanywe.
  3. Mkaa. Kama kuku wako wanaharisha,Chukua kiasi cha mkaa, kitwange, changanya kwenye chakula, wape, hawataharisha tena. Mama E.G.White katika kitabu chake cha Uponyaji wa Mungu Uk.64 ameeleza juu ya Tiba ya Mkaa. Jaribu uone mafanikio yake kwa kuku anyeharisha kawaida na siyo kideri.
  4. Kinyesi cha Ng'ombe. Kausha kinyesi cha ng'ombe, kisage na kisha changanya na chakula cha kuku. Hii inasaidia sana kwa kuku wanaonyonyoka manyoya.
MINYOO. Hawa ni wadudu wanaoleta madhara kwa kuku na wanyama wengine pia. Kuku hupata minyoo kwa kula vyakula vyenye wadudu/vimelea vya wadudu hao. Dalili. Kuku Hudumaa, manyoya huwa hafifu, hupungua damu na uzito, utagaji wa mayai hupungua, minyoo huweza kuonekana kwenye kinyesi. Namna ya kuzuia minyoo.
  • Safisha banda mara kwa mara (ukiweza tumia dawa za kuua wadudu)
  • Badilisha matandazo mara kwa mara.
  • Safisha vyombo vya chakula na maji mara 2/3 kwa siku.
  • Tenganisha kuku wakubwa na wadogo.
  • Wape kuku dawa za kuzuia minyoo kila baada ya miezi 3.
  • Muone mtaalam kwa ushauri zaidi.
MAGONJWA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA/VIINI LISHE. Iwapo kuku watapewa chakula chenye viini lishe kidogo/kisicho na viini lishe muhimu kama vile; Protini, Wanga, Madini na Vitamini wanaweza kupata madhara yafuatayo;
  • Kudumaa,
  • Kupungua uzito,
  • Kupungukiwa na damu,
  • Mifupa kupinda/kuvimba/kutokuwa imara,
  • Utagaji wa mayai hupungua na uangaji wake pia huwa hafifu,
  • Ganda la yai huwa laini,
  • Manyoya huwa machache na laini,
  • Kujikunja kwa shingo/miguu na vidole,
  • Kuwa na majimengi mazito chini ya ngozi ya kifuani,
  • Kupata magonjwa mara kwa mara,
  • Hali hii inaweza kusababisha Kuku kufa.
Namna ya kuzuia.
  1. Kuku wapewe chakula chenye mchanganyiko wa viinilishe vyote muhimu kama vile Vitamini, madini na Chokaa kufuatana na umri/aina na mahitaji yake.
  2. Wapewe majani mabichi kama mchicha, kabichi na majani ya mapapai.
  3. Wapewe mchanganyiko wa vitamin na madini kama chokaa na chumvi kwa kiwango maalum maana ikizidi pia yaweza kuathiri kuku.
MUHIMU. Ili liziua magonjwa ya kuku na kupata faida kubwa kwa kufuga kuku, ni muhimu sana mtu anayehudumia kuku bandani aweze kutambua haraka dalili za magonjwa ya kuku kama nilivyoeleza hapo juu ikiwa ni pamoja na kuzingatia usafi wa banda. Ni lazima ajue tabia ya kuku ya kila siku. Kuku mgonjwa unaweza kumtambua kwa kuangalia yafuatayo;
  1. Tabia ya kuku.
  2. Kinyesi cha kuku (mabadiliko ya kinyesi).
  3. Ulaji wa chakula na unywaji wa maji kama umepungua.
  4. Utagaji wa mayai na uimara wa mayai kama vimepungua.
  5. Kuku kutochangamka.
  6. Vifo ni dalili ya mwisho.
Kama utaona kuna kuku mgonjwa bandani basi mtenge na wenzie kama unavyowafanyia vifaranga. Ili uweze kuwahudumia peke yao. Wengine ambao hawajaonesha dalili wapewe dawa ya kinga haraka iwezekanavyo kupitia ushauri wa mtaalam wa mifugo aliye karibu. Chanjo na matibabu yoyote yafuate ushauri wa mtaalam/mtengenezaji wa dawa husika bila kupuuzia ili upate mafanikio. Hii itakuwezesha kupunguza/kuponya magonjwa na kupunguza gharama za matibabu na vifo. Hakikisha kuwa chanjo/tiba zinatoka kwa mtaalam anayejua kutunza chanjo/dawa kwenye ubaridi unaotakiwa kulingana na maagizo ya mtengenezaji. ANGALIZO Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha magonjwa au kupunguza uzalishaji hivyo kuleta hasara zisizo za lazima kwa mfugaji.;
  1. Kufuga kuku wengi kwenye eneo dogo.
  2. Chumba/banda lisilo na hewa na mwanga wa kutosha.
  3. Banda kuwa chafu.
  4. Vyombo vichache/visivyotesheleza kwaajili ya chakula na maji.
  5. Vyombo vichafu vya maji na chakula.
  6. Chakula kisicho na viini lishe vya kutosha/kichache.
  7. Kubadili ladha ya chakula.
  8. Kuchelewa kudhibiti magonjwa ya kuku.
  9. Kuchanja/kutibu kuku bila utaratibu/ushauri wa kitaalam.
  10. Kutishia kuku wakati wa kuingia bandani/kuwashika/kuwasumbuasumbua.
  11. Mabadiliko ya hali ya hewa.
  12. Kufuga kiholela bila kuwachambua.
MWISHO
  • Chagua njia bora na rahisi inayokufaa kulingana na eneo ulilopo na mahitaji yako pia. Angalia njia itakayokupa faida kwa gharama ndogo.
  • Chagua kuku wenye uwezo wa kukua haraka, wanaostahimili magonjwa, wanaotaga mayai mengi, wanaoweza kuangua vifaranga wengi na kuwalea.
  • Chagua jogoo aliye na uzito mzuri na mwenye kucha fupi.
  • Uwiano wa jogoo kwa majike iwe ni jogoo 1 kwa majike/mitetea 10.
  • Kuku anayetazamiwa kuatamia mayai anatakiwa asiwe na chawa/viroboto/utitiri.
  • Kuku ambaye hakidhi sifa za kuwa kuku bora anayefaa kuwa kwenye kundi inafaa aondolewe ili asilishwe kwa hasara awapo bandani.
Waafrika tulio wengi hatuna utamaduni wa kutunza kumbukumbu. Ni vizuri basi uanze kutunza kumbukumbu za mwenendo wa kazi zako za ufugaji wa kuku. Hii itakurahishia sana kujua faida, hasara na hata kujua namna bora ya kuboresha ufugaji wako. Kwa mfano;
  1. Kumbukumbu za uzalishaji mayai zitakuwezesha kujua kiasi cha mayai yanayotagwa kwa siku. Idadi ikiwa chini ya 60% utagaji huo siyo mzuri hivyo utatafuta sababu ya tatizo nk. Utagaji unatakiwa uwe 70% hadi 95%.
  2. Kumbukumbu ya vifo itakusaidia kujua hatari itakayokujia. Mfano vifo vikizidi 1% inaashiria tatizo la ugonjwa. Hivyo uchunguzi ni lazima ufanyike ili kutatua tatizo.
  3. Kumbukumbu za mapato na matumizi pia zitakusaidia kujua faida na hasara nk. Hapa utajua ni ghara kiasi gani ulitumia kufuga na faida kiasi gani umepata baada ya mauzo ya mayai/kuku husika.
MAKADIRIO YA CHINI YA MTAJI WA KUANZIA| UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI
Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao. Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!

Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasa kuwa makini zaidi.

Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 .

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu mwanajamvi, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana.

Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo.

==============

MAELEZO ZAIDI: UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

UTANGULIZI

Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nimeamua kuuleta kwenu wana JF ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo.

A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI?
1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.

B. FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka

Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku

C:MAPUNGUFU
Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.

D: KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna maelezo ya kusisimua sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku. Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka.

Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.
Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

(i) KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

(ii) CHING'WEKWE
Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo. Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.

(iii)UMBO LA KATI
Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.

(iv) SINGAMAGAZI
Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.

(iiv) MBEYA
Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49

(iiiv)PEMBA
Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42

(xi) UNGUJA.
Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.


SEHEMU YA PILI
1. MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
A. MFUMO HURIA
Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

FAIDA.
Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

HASARA
Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.

B.MFUMO NUSU HURIA
Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

FAIDA
Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.

C. MFUMO WA NDANI
Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

FAIDA
Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

HASARA
Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
1. Matandiko yageuzwe kila siku
2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.

UTATUZI WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
Mambo ya kuzingatia:
Mabanda bora - Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Sifa za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi
Kuwa makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi bora.

UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano.

Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha ya fuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo

Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.

Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao. Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.

Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja. Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.

Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

UTEKELEZAJI WAKE
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga. Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.

Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja.
Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

MUHIMU
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

TAMBUA VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.

JIFUNZE MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
Zoezi hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
Taz.

Hesabu ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu.
Mpaka mwisho wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya vifaranga 2520.

Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo ili ufundishwe zaidi kuhusu mbinu hiyo ya kuzalisha kuku wengi.

ULEAJI WA VIFARANGA
NJIA YA KUBUNI
NJIA YA ASILI
Njia zote mbili zinafahamika kama huzifahamu tafadhali fuatilia kwa mtaalamu aliye karibu nawe.

MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.
A. MAGONJWA.
Ugonjwa hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi (Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata vijijini.

Pamoja na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini
Ndui ya kuku(Fowl pox)
Mafua ya kuku(Infectious coryza)
Homa ya matumbo (Cocciodiosis)
Minyoo na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.

DALILI ZA KUKU MGONJWA.
Huzubaa
Hali chakula/maji vizuri
Hujitenga na wenzake
Hujikunyata au kuinama
Hutetemeka
Hutembea kwa shida
Utagaji wa mayai hupungua au hukoma kabisa

MAGONJWA YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
Yako mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.

ATHARI ZA MAGONJWA.
Hili liko wazi
Maelezo haya ya magonjwa ni mengi hivyo tuwe wafuatiliaji kwa wataalam.

MATIBABU
KIDERI - Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.

KUMBUKA
Mdondo au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
Mdondo ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine huzunguka na huzungusha vichwa.
Mdondo unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3

NDUI YA KUKU
HOMA YA MATUMBO (Fowly typhoid)
MAFUA YA KUKU(Infectious coryzya)
KUHARISHA DAMU(Coccidiosis)
Minyoo na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k

Kwa magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini watatusaidia.

TIBA ZA ASILI
Kuna madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.

BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.
MWAROBAINI - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
ALOEVERA - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana zaidi namna ya kuandaa dawa hii.

Hapa nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na kukinga kuku. Mwarobaini, Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge, Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili kichaa.

NAWASHUKURU PIA NAOMBA MWENYE MCHANGO ZAIDI AENDELEE KUONGEZEA TUSIWE WACHOYO WA MAARIFA KIDOGO GAWANA NA MWENZIO
UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI
SEHEMU YA KWANZA

UTANGULIZI
Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Nimeamua kuuleta kwenu wana JF ili kwa mtu mwenye malengo ya kufanikiwa kupitia ufugaji wa kuku ajue mlolongo mzima na changamoto ambazo atakabiliana nazo.

A. KWA NINI KUKU WA KIENYEJI?
1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdonde, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza.
2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula ardhini.
3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k
4. Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE)
5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja na sifa hizi ni muhimu muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha.

B. FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI.
Faida ni nyingi na zinafahamika lakini nitaeleza zile ambazo kwa wengine huenda zikawa ni ngeni kwao.
- Mayai huweza kutumika kwa tiba. (Pata maelezo jinsi yai la kuku wa kienyeji linavyoweza kutumika kwa tiba kutoka kwa wataalam wa tiba mbadala)
- Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele (shampoo)
- Manyoya yake yanaweza kutumika kama mapambo.
Fuga kuku upate faida kwa kuzingatia:
Chanjo ya mdondo kila baada ya miezi mitatu na chanjo ya ndui mara mbili kwa mwaka
Zuia viroboto, utitiri na minyoo.
Chagua mayai bora kwa ajili ya kuatamiza
Panga kuuza kuku kwa makundi uongeze kipato
Kula mayai na kuku kadri uzalishaji unavyoongezeka.
Kipato unachokipata utenge pia na kiasi kwa ajili ya uendelezaji wa kuku

C: MAPUNGUFU
Yako mapungufu mengi yanayofahamika lakini hapa naomba niweke lile la muhimu zaidi. MAGONJWA kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku kutokana na kutokuzingatia kuchanja kuku kwa wakati.

D: KABILA ZA KUKU WA KIENYEJI
Kuna maelezo ya kusisimua sana kuhusu makabila ya kuku wa kienyeji, hata hivyo kuna ugumu kidogo kuweza kuyachanganua makabila hayo kutokana na muingiliano mkubwa wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Hata hivyo kuku hawa wana tofauti za kimaumbile zinazosaidia kwa kiasi fulani kutambua uwepo wa baadhi ya makabila ya kuku.

Kabila hizi pia zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na eneo kuku wanakotoka. Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kwa maumbile yao Mfano:
a. Kishingo - kuku wasio na manyoya shingoni
b. Njachama au Nungunungu - Hawa ni wale wenye manyoya yaliyosimama.
c. Kibwenzi - Ni wale wenye manyoya mengi kichwani.
d. Kibutu- Hawa hawana manyoya mkiani
Mwingiliano wa vizazi unaweza ukasababisha kuku kuwa na aina ya maumbile mchanganyiko. Mfano kuku aina ya kuchi anaweza kuwa na alama ya kishingo, Njachama, Kibwenzi au Kibutu.

Hivyo kabila za kuku zifuatazo zinaweza kutambuliwa kama ndiyo kabila za kuku wa kienyeji kulingana na maumbile yao na maeneo wanakotoka.

(i) KUCHI
Ni kuku warefu kwa umbo na wenye kusimama mgongo ukiwa wima. Wana manyoya machache mwilinini na hasa kifuani, vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa Kg. 2.5 na mitetea kg 1.5 mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gm 45. Kuku hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

(ii) CHING'WEKWE
Kuku hawa ambao jina lao ni gumu kidogo kwa mtu asiyekuwa na meno kulitamka wana sifa zifuatazo.
Majogoo wana wastani wa kg 1.6, Mitetea wastani kg 1.2, mayai wastani wa gm 37. Kuku hawa wenye umbo dogo hupatikana zaidi maeneo ya CHAKWALE mkoani Morogoro na pia sehemu za umasaini. Kuku hawa hutaga mayai mengi sana kuliko aina nyingine ya kuku wa kienyeji waliopo Tanzania, kwa hiyo wanafaa sana kwa biashara ya mayai.

(iii)UMBO LA KATI
Majogoo wana uzito wa wastani wa kg. 1.9, Mitetea kg. 1.1, Kuku hawa ndio hasa wanaoitwa wa kienyeji(wa kawaida) Wana rangi tofauti. Utafiti umeonyesha kuwa kuku hawa hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa mdondo (Castle desease)
Muhimu - Mfugaji akifanya uchaguzi kutoka kwenye aina hii ya kuku na kutoa matunzo mazuri kwa hao kuku waliochaguliwa, Hakika anaweza kupata kuku walio bora na wenye uzito wa kutosha pia kutaga mayai mengi na makubwa.

(iv) SINGAMAGAZI
Ni aina ya kuku wakubwa wa kienyeji wanaopatikana zaidi TABORA, kuku hawa wana utambulisho maalum kutokana na rangi zao. Majogoo huwa na rangi ya moto na mitetea huwa na rangi ya nyuki. Uzito - Majogoo uzito wa wastani wa kg 2.9, mitetea wastani wa kilo 2 mayai gramu 56.

(iiv) MBEYA
Kuku hawa wanapatikana Ileje mkoani mbeya. Asili hasa ya kuku hawa ni kutoka nchi ya jirani ya Malawi na si wa kienyeji asilia bali wana damu ya kuku wa Kizungu "Black Australop". Majogoo Kg 3 mitetea kg 2 mayai gram 49

(iiiv) PEMBA
Hupatikana zaidi Pemba. Majogoo Kg.1.5 Mitetea Kg 1 mayai wastani gm 42

(xi) UNGUJA.
Majogoo Kg 1.6,mitetea kg 1.2 mayai gm 42. Kuku hawa wa Unguja na Pemba wanashabihiana sana na Kuchi isipokuwa hawa ni wadogo.

SEHEMU YA PILI
1. MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI.
A. MFUMO HURIA

Katika mfumo huu kuku huachiwa wakitembea toka asubuhi wakijitafutia chakula na maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si nzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

FAIDA.
Mfumo huu una faida za gharama ndogo za uendeshaji kiujumla.

HASARA
Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, kuibiwa mitaani n.k
Kuku huweza kutaga popote na kusababisha upotevu mkubwa wa mayai.
Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa
Utagaji unakuwa si nzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Uwekaji kumbukumbu si nzuri.
Ni vigumu kugundua kuku wagonjwa hivyo kusababisha ugumu katika utoaji wa tiba.

UTUMIAJI NZURI WA MFUMO HUU
Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote hali ya hewa inapokuwa si nzuri.
Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
Kuku waandaliwe kwa viota vya kutagia.
Kuku 100 ni vizuri wakitumia eneo la ardhi la ekari 1.

B.MFUMO NUSU HURIA
Huu ni mfumo ambao kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa uzio/ wigo. Mfumo huu ni ghari kiasi ukilinganisha na mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji faida haraka sana.

FAIDA
Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria, utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na mfumo huria, Ni rahisi kutibu magonjwa ya mlipuka kama mdondo (Newcastle desease), Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo sana ukilinganisha na mfumo huria.

C. MFUMO WA NDANI
Kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani. Mfumo huu kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao(randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwa katwa.

FAIDA
Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia, uangalizi mzuri na rahisi wa kuku, Joto litokanalo na matandiko lina uwezo wa kuua vimelea vya maradhi, kuku wanakingwa na hali ya hewa mbaya na maadui wengine.

HASARA
Uwezekano wa kuku kudonoana ni mkubw na pia Gharama za ujenzi wa mabanda

UTUMIAJI MZURI WA MFUMO HUU.
1. Matandiko yageuzwe kila siku
2. Kila mara matandiko yawe makavu kwa kuwa na madirisha yanayopitisha hewa ya kutosha, ambayo yatatoa unyevunyevu hewa chafu ikiwemo ammonia.
4. Mita mraba moja hutosha kuku 5 hadi 8.

UTATUZI WA KUKABILIANA NA VIKWAZO KATIKA UFUGAJI.
Mambo ya kuzingatia:

Mabanda bora -
Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.
Sifa za banda bora (Waone wataalam wa mifugo)
Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi
Kuwa makini na aina ya mitetea na majogoo unatakiwa kuchagua ili kuwa na kizazi bora.

UTAGAJI WA MAYAI
Kwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano.

Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji anashauriwa kuondoa kila yai linalozidi hayo matatu kila siku linapotagwa na kuliweka alama ya tarehe au namba kwa kutumia penseli ili kumfanya kuku aendelee kutaga kwa lengo la kufikisha mayai 15 mpaka 20. Mayai yanayoondolewa yawekwe kwenye chombo kikavu kinachopitisha hewa ni vizuri pia kuweka mchanga ndani ya chombo hicho.

Hakikisha yafuatayo.
Sehemu iliyochongoka iwe chini na pana iwe juu.
Hifadhi sehemu yenye hewa ya kutosha na isiyohifadhi joto
Mayai yasikae kwenye hifadhi hiyo zaidi ya wiki mbili toka siku ya kuanza kutagwa.

UATAMIAJI WA MAYAI NA UANGUAJI WA VIFARANGA
Uatamiaji na uanguaji wa kubuni - Mfumo huu hutumia mashine za kutotoleshea vifaranga (Incubators) hutumika kuangua mayai mengi kati ya 50 hadi 500 kwa wakati mmoja Mashine zinazotumika kutotoleshea vifaranga wa kisasa zinaweza kutumika pia kutotoleshea wa kienyeji.
Uatamiaji na uanguaji wa asili

KUCHAGUA MAYAI YA KUANGUA.
Hili nalo ni muhimu kuzingatia. Ni vizuri kuchagua mayai ya kuatamia ili mayai yasiyofaa yaweze kuuzwa au kutumiwa nyumbani kwa chakula. Mayai ya kuatamia yawe na sifa zifuatazo
Yasiwe na uchafu yawe masafi
Yasiwe na nyufa
Yatokane na kuku aliyepandwa na jogoo
Yasiwe madogo wala makubwa bali yawe na ukubwa wa wastani kulingana na umbile la kuku.
Yasiwe mviringo kama mpira pia yasiwe na ncha kali sana.
Yasiwe yamekaa muda mrefu zaidi ya wiki mbili toka yalipotagwa
Yasiwe yaliyohifadhiwa kwenye sehemu yenye joto.

KUMTAYARISHA KUKU WA KUATAMIA
Pamoja na matayarisho hayo zingatia kumuwekea mayai yasiyozidi 15 pia ni vizuri yasipungue 12. Kuku wanaotazamiwa kuatamia ni lazima wachunguzwe kwa makini kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba hawana chawa, utitiri n.k. Kuwepo kwa wadudu hao huwafanya kuku wakose raha na kutotulia kwenye viota vyao.

Hali hii husababisha kuanguliwa kwa Vifaranga wachache.
Sasa unatakiwa kufanya yafuatayo:-
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu ndani ya kiota
Pia mnyunyuzie dawa kuku anayetarajia kuatamia
Weka mayai kwenye kiota huku mikono yako ikiwa imepakwa jivu ili kuepuka kuwa na harufu kwani kuku anaweza kuyasusa.

Ni vizuri kuifanya kazi hii ya kumuandaa kuku anayetaka kuatamia wakati wa usiku. Pia ifahamike kuwa kwa kawaida kuku huatamia mayai yake siku 21.

PIA JIFUNZE MBINU ZA KUATAMIA MAYAI MENGI KWA NJIA ZA ASILI
Iwapo una kuku wengi wanaotaga kwa wakati mmoja ni vema ukawafanya wakaatamia na kutotoa pamoja. Unachotakiwa kufanya ni kuchagua mayai ya kuatamia ukianzia na yai la mwisho kutaga.

Unaweza kuwaandaa kuku wako zaidi ya mmoja ili waanze kuatamia kwa pamoja na kupata vifaranga vingi kwa mara moja kuku wa kwanza anapoanza kuatamia. Mwekee mayai viza au ya kuku wa kisasa kwani kuku huatamia hadi mayai yanapoanguliwa hivyo ukimuwekea mayai yasiyo na mbegu atakaa hapo muda mrefu hadi vifaranga watoke.

UTEKELEZAJI WAKE
Kuku anapotaga kila siku weka alama ya namba au tarehe kulinganisha na siku anayotaga. Yanapofika mayai matatu yaondoe na muwekee mayai viza au ya kisasa huku ukiendelea kuweka alama mayai yanayotagwa kila siku.

Mara kuku anapoanza kuatamia muongezee mayai ya uongo yafikie 8 hadi 10
Fanya hivyo kwa kila kuku anayetaga hadi utakapoweza kupata idadi itakayoweza kukupatia vifaranga wengi kwa wakati mmoja. Wawekee kuku wote mayai siku moja kwa kuondoa mayai ya uongo na kuwawekea mayai ya ukweli wakati wa usiku.

MUHIMU
Mayai ya kuatamia yasishikwe kwa mkono ulio wazi na wala yasipate harufu za mafuta ya taa, manukato n.k.

JIFUNZE PIA KUTAMBUA MAYAI YALIYO NA MBEGU NA YALE YASUYO NA MBEGU.
Mfugaji anaweza kutambua mayai yaliyo na mbegu na yale yasiyo na mbegu siku ya saba baada ya kuanza kuatamia iwapo atapima mayai kwa kutumia box lililotengenezwa maalum pamoja na tochi yenye mwanga mkali ndani ya chumba chenye kiza. Hii itamuwezesha mfugaji ayatumie mayai yasiyo na mbegu kwa chakula cha familia au kuyauza.

TAMBUA VYAKULA NA UZALISHAJI WA KUKU - Sitalielezea hili naomba ufuatilie mwenyewe.

JIFUNZE MBINU ZA KUZALISHA KUKU WENGI KWA MUDA MFUPI
Zoezi hili linawezekana iwapo uleaji wa vifaranga kwa njia ya kubuni utatumika. Kuku mmoja anaweza kutotoa zaidi ya mara saba kwa mwaka.
Taz.
Hesabu ya uzalishaji wa kuku wengi kwa mwaka kwa kutumia mtetea mmoja tu.
Mpaka mwisho wa mwaka unaweza kuwa na idadi ya vifaranga 252 kwa kadirio la vifaranga 8 kila mzao. Hivyo kama una kuku 10 wanaotunzwa vizuri utakuwa umezalisha jumla ya vifaranga 2520.

Fuatilia kwa wataalamu wa mifugo ili ufundishwe zaidi kuhusu mbinu hiyo ya kuzalisha kuku wengi.

ULEAJI WA VIFARANGA
NJIA YA KUBUNI
NJIA YA ASILI
Njia zote mbili zinafahamika kama huzifahamu tafadhali fuatilia kwa mtaalamu aliye karibu nawe.


MAGONJWA NA WADUDU WANAOSHAMBULIA KUKU WA KIENYEJI NA JINSI YA KUKINGA.
A. MAGONJWA.
Ugonjwa hatari - Mdondo/ Kideri (Newcastle desease) Hapo nyuma dawa ya kukinga ugonjwa huu ilikuwepo lakini ilikuwa inahitaji kuhifadhiwa kwenye hali ya ubaridi (Friji) Hali hiyo ilisababisha iwe ngumu kutumika vijijini kwa dawa hiyo. Hivi sasa kumepatikana chanjoa ambayo inastahimili joto ambayo inaweza kutumika hata vijijini.

Pamoja na mdondo yapo pia magonjwa yanayoshambulia kuku hapa nchini

Ndui ya kuku(Fowl pox)
Mafua ya kuku(Infectious coryza)
Homa ya matumbo (Cocciodiosis)
Minyoo na wadudu kama viroboto, chawa, utitiri na kupe wa kuku.

DALILI ZA KUKU MGONJWA.
Huzubaa
Hali chakula/maji vizuri
Hujitenga na wenzake
Hujikunyata au kuinama
Hutetemeka
Hutembea kwa shida
Utagaji wa mayai hupungua au hukoma kabisa

MAGONJWA YA KUKU HUSABABISHWA NA NINI?
Yako mambo mengi yanayosababisha lakini matunzo hafifu pia huchangia.

ATHARI ZA MAGONJWA.
Hili liko wazi
Maelezo haya ya magonjwa ni mengi hivyo tuwe wafuatiliaji kwa wataalam.

MATIBABU
KIDERI - Sifahamu tiba ya kitaalam ya ugonjwa huu kama kuna ambaye anafahamu tunaomba atufahamishe lakini ziko dawa za asili na za kitaalam ambazo zinafaa zaidi kwa chanjo.
Ugonjwa huu unaweza kuukinga kwa kuwapa kuku chanjo ya Mdondo. Pia usichanganye kuku wako na kuku ambao huna taarifa zao za chanjo.

KUMBUKA
Mdondo au kideri ni ugonjwa tishio ambao huweza kuua kuku wote
Mdondo ukitokea vifo huwa vingi pia kuku hupumua kwa taabu, hupooza na wengine huzunguka na huzungusha vichwa.
Mdondo unaweza kuzuilika kwa chanjo kila baada ya miezi 3

NDUI YA KUKU
HOMA YA MATUMBO (Fowly typhoid)
MAFUA YA KUKU(Infectious coryzya)
KUHARISHA DAMU(Coccidiosis)
Minyoo na wadudu wanaoshambulia kuku kama viroboto n.k

Kwa magonjwa na wadudu tuliowataja hapo juu please wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe Kwani siwezi kueleza kila kitu hapa wataalamu tunao naamini watatusaidia.

TIBA ZA ASILI
Kuna madawa ya asili ambayo hutokana na mimea ambayo hukinga kuku.

BAADHI YA MIMEA INAYOTIBU NA KUKINGA MARADHI YA KUKU.
MWAROBAINI - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda
ALOEVERA - Typhoid, kuhara, kideri, kifua na vidonda,ngozi na Cholera. Tutaelekezana zaidi namna ya kuandaa dawa hii.

Hapa nataka niorodheshe baadhi ya madawa ya asili ambayo yanasaidia kutibu na kukinga kuku.
Mwarobaini, Aloevera, Mtakalang'onyo(Euphorbia),Mbarika, mlonge, Ndulele/dungurusi/tura/ndura, Majani ya mpapai, Mwembe, Minyaa na Pilipili kichaa.

NAWASHUKURU PIA NAOMBA MWENYE MCHANGO ZAIDI AENDELEE KUONGEZEA TUSIWE WACHOYO WA MAARIFA
ZINGATIA LISHE BORA YA KUKU
Ili kuku wawe na afya nzuri, ukuaji nzuri na kutoa mazao mengi na bora wanahitaji vyakula aina ya Wanga, protini, madini, vitamin na maji.

KUMBUKA
-Ukosefu wa vitamini A hujitokeza baada ya kiangazi kirefu
-Macho ya kuku huharibika
-Ugonjwa unakuwa mgumu kutibika dalili za wazi zikionekana
-Husababisha vifo hasa kwa kuku wanaokua.
-WAPE MAJANI MABICHI WAKATI WA KIANGAZI
-VITAMINI ZA KUKU ZA MADUKANI HUFAA KWA KINGA YA KUKU WENGI

MCHANGANYIKO WA VYAKULA WENYE ASILI ZIFUATAZO UNAFAA KWA KULISHA KUKU.
1.Mizizi - Mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi n.k
2.Nafaka- Mahindi, mtama, mpunga, ulezi, pumba za nafaka n.k
3.Mboga- Jamii mbali mbali ya majani kama vile kunde,mboga za majani, nyanya, kisamvu n.k
4.Matunda- mapapai, maembe n.k
5.Mbegu za mafuta- karanga , ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, machicha ya nazi n.k
6.Wadudu mbalimbali.
7.Maji

Vyakula nilivyotaja hapo juu hupatikana kwa wingi zaidi wakati wa mvua na mavuno, mara baada ya kipindi hicho kunakuwepo na upungufu mkubwa sana ambao unachangia ukuaji taratibu na utagaji hafifu.

Utafiti unaonyesha kuwa kiasi cha chakula wanachojitafutia wenyewe huwa hakiwatoshi. Inakadiriwa kuwa wakati wa mavuno kuku anaweza kuku anaweza kujitafutia asilimia 50 - 70 ya chakula na wakati wa kiangazi asilimia 30- 50 tu ya mahitaji yake ya chakula. Kwa kawaida kuku wa kienyeji hutumia zaidi ya 90% ya masaa ya siku katika umbali wa mita 110 hadi 175 ili kujitafutia chakula, kuku aliyepevuka anayefugwa huria anahitaji gramu 80 za chakula cha ziada kwa siku.

Hivyo ili kuku waweze kuzalisha wafikie uwezo wao ni muhimu wapewe chakula cha ziada. Chakula cha ziada mara nyingi hutokana na vyakula vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira aliyopo mfugaji. Nakuomba ufuatilie zaidi kwa mtaalamu wa mifugo aliye karibu nawe ili upate mbinu zaidi za namna ya kuandaa chakula cha kuku.

Kuhusu kuku wa kisasa sina uzoefu nao.
KUKU WA KIENYEJI NI 'HOT CAKE'
Mkuu wazo zuri sana, kuhusu soko wala usiwe na wasiwasi hawa kuku wa kienyeji ni hot cake. Nakushauri tu ili uongeze production jaribu kutafuta machine ya kuangulia mayai - then anza kununua mayai aina ya kongoni ( kuku weusi wanapatikana sana Songea) weka kwenye machine yako, after 21 days vifaranga vinaanguliwa. vitunze vizuri na vipe chanjo ili visije pata maradhi yanayoepukika.

Unaweza kuwa unapata vifaranga 200 kila baada ya siku 21 kutokana na ukubwa wa machine, by doing that lazima ufikie malengo yako ya kuku 1000 ndani ya mwaka mmoja.

Ndani ya miezi sita ya project yako pia utaanza kupata mayai ambayo utaweka kwenye machine ya yanayobaki utayauza - tray moja ni sh. 9,000 hadi 12,000.

Mafanikio mema mkubwa. - Kuhusu machine ya kuangulia mayai jaribu kufika pale VETA section ya Umeme Mdogo. (Electronics), Kuna siku ulini PM, ila sikuwa arround - nitakujibu.
AINA ZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
Chakula wanachokula kuku wa kisasa ni hicho hicho cha kienyeji
kwani kuna pumba, mahindi, mashudu ya alizeti, dagaa nk
kwahiyo hatakuwa wakisasa ila watakua vizuri kwa wakati tofauti na wale wanaijitafutia chakula kwani saa ingine wanaweza wasipate virutubisho vyote hasa kwa maeneo ya mjini.

Labda nikufafanulie kidogo.

Kuna ufugaji kuku wa kienyeji wa aina 3
  1. ufugaji huru
Ufugaji huu ni ule wakuacha kuku ajitafutie chakula mwenyewe. Yaani unamfungulia asbh anarudi jioni. Pia huu unaweza kuufanya uwe kisasa kidogo kwa kujaribu kuwaongezea chakula cha ziada (kwa dizaini ya kuwatupia).
Sio wa gharama sana kwani kuku anajitafutia chakula, ila unahitaji kuwa naeneo kubwa.
Ni hatari kwani wezi, wanyama wakali wanaweza kuwashambulia kuku.
Mayai yanaweza kutagiwa porini na usijue yalipo.
Kuku anaweza kuambukizwa magonjwa na ndege wengine au kuku kutoka kwa majirani.

2. ufugaji nusu huru
Ufugaji huu. ni banda ndani ya uzio yaani unawapa chakula na maji kama kawaida lakini hawatoki nje ya uzio. Unakuwa umewatengenezea eneo la kuchezea na kukumbizana.
nao unahitaji eneo kubwa kidogo, kuku wanakua salama dhidi ya wezi na wanyama wakali kwa kiasi fulani.
Utahitji kuwatafutia chakula kwa zaidi ya 50%.

3. ufugaji wa ndani
huu ni wagharama zaidi. kwani kuku huitaji kutafutiwa chakula kwa 100%.
ila kuku huwa salama dhidi ya magonjwa wezi na wanyama wakali.
Tatizo kubwa nivigumu kudhibiti ugonjwa uingiapo banda kwa hiyo inakupasa uhakikishe magonjwa hayafiki.
jingi ne tabia mbaya kama ya kula mayai na kudonyoana inaweza kusambaa kwa haraka.

Kwa hiyo ni methods tu za ufugaji hazibadilishi kuku wa kienyeji kuwa wakisasa.
MAGONJWA, TIBA NA LISHE BORA YA KUKU WA KIENYEJI

Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.Lengo la makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi
zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na
hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi
kwa kufuga kuku:

1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya
kuku.

SEHEMU YA I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI
ZINAZOENDELEA

NAFASI YA MIFUGO

Licha ya kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika nchi za
hari (tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo. Idadi ya wanyama wanaofugwa
huongezeka sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo huzidi.
Idadi kubwa ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya bidii
kuzalisha chakula na mapato kutoka kwa shamba.

Ufugaji wa ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba ili
kupanda mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya vyakula
na sehemu ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo fedha.

Katika nchi za hari ufugaji wa kienyeji hautahitaji kazi nyingi, kazi hii hufanywa na akina mama na
watoto. Kwa kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani hutekelezwa na mama. Vyakula vya
kuku vyaweza kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka jikoni
na 4) Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekwe, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k). Mfumo
wa kufuga kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na kuimarisha hali
ya kiuchumi na chakula bora kwa jamii.

Ni muhimu sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula bora
na kuongeza mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida yake
huzaana tu kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya wanafunzi,
malipo ya hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya kijamii
(kwa mfano kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili wadudu,
kwekwe na kuimarisha rutuba kutokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba mifugo ni
muhimu sana kwa mkulima yeyote yule.

UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji wa
kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi.
Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku wa
nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji.

Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi
za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai. Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine, utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa yanayostawi.

"Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa
majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300
kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na
kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.

Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni
rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa
zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida.
Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango
kidogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI
Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili.
Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.

· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu

Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.
Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:

Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.

Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku
akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la
kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga
walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne
wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.

Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu
nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze
kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.

Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka
iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo
cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje
huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi
nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.

Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo,
huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa
nafaka.

Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku
wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:

Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.

TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya
magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko
kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu
huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida
ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa
na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.

Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata
katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa
muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani
aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye
mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.

Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni
piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1
kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au
dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu

Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri
husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii
hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.

Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa
mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku
150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa
chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.

Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha
kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.

Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya
kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa
wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.

Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha
kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana
na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati
mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili
vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
..................................//...............................
KWA UFUPI (SUMMARY)
Kabila za Kuku
Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano
1. Kuchi
  • Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
  • Wana manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
  • Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo 1.8
  • Mayai gram 45
2. Ching'wekwe (Umbo dogo)
  • Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
  • Majogoo kilo 1.6
  • Mitetea kilo 1.2
  • Yai gram 37
  • kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.
3. Umbo la Kati


  • Majogoo kilo 1.9
  • Mitetea kilo 1.1
  • Mayai gramu 43
  • Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)
4. Singamagazi
  • Hupatikana zaidi Tabora
  • Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
  • Majogoo kilo 2.9
  • Mitetea kilo 2
  • Mayai gramu 56
5. Mbeya
  • Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
  • Mjogoo kilo 3
  • Mitetea kilo 2
  • Mayai gramu 49
  • Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine
6. Pemba
  • Maumbo ya wastani na miili myembamba
  • majogoo kilo 1.5
  • mitetea kilo 1
  • mayai gramu 42
7. Unguja
  • Hawatofautiani sana na wa Pemba
  • Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
  • Majogoo kilo 1.6
  • Mitetea kilo 1.2
  • Mayai gramu 42
SIFA WA KUKU WA KIENYEJI
  1. Wastahimilivu wa Magonjwa
  2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula
  3. Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
  4. Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
  5. Nyama yake ina ladha nzuri
KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA
  1. Wajengewe nyumba bora
  2. Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
  3. Malezi bora ya vifaranga
  4. Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.
NYUMBA BORA
Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe
  • Linafikika kwa urahisi
  • Limeinuka juu pasituame maji
  • Pasiwe na pepo zinazovuma
Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku
  • Paa imara lisilovuja
  • Kuta zisiwe na nyufa
  • Sakafu isiwe na nyufa
  • Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
  • Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
  • Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba
Mambo muhimu ndani ya nyumba
  • Chaga za kulalia kuku
  • Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
  • Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)
UATAMIAJI WA MAYAI
Kuna njia 2
  • Njia ya kubuni (incubators)
  • Asili
Kumuandaa kuku anayeatamia
  • Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
  • Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
  • Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
  • Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
  • Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa
ULEAJI WA VIFARANGA
Kuna njia mbili
  • Njia ya kubuni
  • Njia ya asili
Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga;

Njia ya KUBUNI
Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.

KULISHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe
  • Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
  • Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
  • Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
  • Matunda-Mapapai, maembe, n.k
  • Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
  • Unga wa dagaa
  • Maji
KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU
  • Pumba.............kilo20
  • Mashudu ya Pamba n.k...kilo 3
  • Dagaa iliyosagwa.........kilo 1
  • Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa........kilo 2
  • Unga wa Mifupa ..........kilo 0.25
  • Chokaa ya mifugo ........kilo 0.25
  • Chumvi........................gramu 30
  • Vichanganyio/Premix...gramu 25
KUPANDISHA
  • Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
  • Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
  • Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
  • Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
  • Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8
MAGONJWA YA KUKU
1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili
  • Kuhalisha choo cha kijani na njano
  • Kukohoa na kupumua kwa shida
  • Kupinda shingo kwa nyuma
  • Kuficha kichwa katikati ya miguu
  • Kukosa hamu ya kula na kunywa
  • Idadi kubwa ya vifo hadi 90%
Kinga
  • Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
  • Epuka kuingiza kuku wageni
  • Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
  • Zingatia usafi wa mazingira
NDUIYA KUKU/ FOWL POX
Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili
  • Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
  • Kukosa hamu ya kula
  • Vifo vingi
Kinga
  • Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
  • Epuka kuingiza kuku wageni
  • Zingatia usafi wa mazingira
HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID
  • Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
  • Kuku hukosa hamu ya kula
  • Kuku hukonda
  • Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
  • Kinyeshi hushikamana na manyoya
Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga
  • Usafi
  • Fukia mizoga
  • Usiingize kuku wageni
  • Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6
MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa
Dalili
  • Kuvimba uso
  • Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
  • Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
  • Hukosa hamu ya kula
  • Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya
Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili
  • Kuharisha damu
  • Manyoya husimama
  • Hulala na kukosa hamu ya kula
MINYOO
Dalili

  • Kunya minyoo
  • Hukosa hamu ya kula
  • Hukonda au kudumaa
  • Wakati mwingine hukohoa
Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili
  • Kujikuna na kujikung'uta
  • Manyoya kuwa hafifu
  • Rangi ya upanga kuwa hafifu
  • Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga
Kuzuia
  • Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
  • Fagia banda mara mbili kwa wiki
  • Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
  • Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
  • Nyunyiza dawa kwenye viota
  • Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
  • Fuata kanuni za chanjo
  • Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima
UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili
  • Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
  • Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
  • Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
  • Huwa na manyoya dhaifu

FORMULA 100Kgs ZA CHAKULA CHA KUKU
  1. Mahindi yaliyoparazwa 25Kgs.
  2. Pumba za Mahindi 25Kgs.
  3. Dagaa/Uduvi 10Kgs.
  4. Unga wa Mifupa/Bionemeal 5Kgs.
  5. Chokaa/Limestone 5Kgs.
  6. Mashudu ya Alizeti 5kgs.
  7. Mashudu ya Pamba 10kgs.
  8. Ngando ndogondogo 5kgs.
  9. Machicha ya ngano/Wheat Brand 10kgs.
NI MRADI MZURI SANA. FUATA USHAURI HUU

Huo ni mradi mzuri sana. Kwani kuku wa kienyeji ni wazuri sana kama utawafuga zero grazing. Ni vizuri uanze na kuku sita kwa maana Jogoo mmoja na matembe watano.

Tengeneza kibanda kizuri sana na uweke sehemu nzuri ya stara kwani kuku hawezi kutaga sehemu yenye vurugu. Kuku wa kienyeji kama utawatunza vizuri wanataka mayai 15 mpaka 18. Na kama atatamia vizuri basi utapata vifaranga 15 na wakitunzwa vizuri utapata kuku 13 au 12. Na akifikisha wiki mbili tu vifaranga hivyo unatakiwa kuvitenganisha na mama yao. waweke sehemu maalum na kuna vyombo vya kutunzia vifaranga vya kienyei huko Tanzania bara.

Vile vile jua kwa mwaka kuku anataga mara tano. Na kama kila kuku akipata vifaranga 12 kila mzao kwa mwaka atatoa vifaranga 60. Na kwa kuku watano utapata kuku 300 kwa mwaka.

Chakula cha kuku hawa ni Pumba za mahindi unawachanganyia na vumbi la dagaa. Debe moja la Pumba unachanganya na vumbi la dagaa kilo moja au moja na nusu.

Kumbuka vile vile kuku wanakula sana majani. Usiache kuwapa majani na maji safi ya kunywa. make sure maji unayabadilisha kila siku asubuhi na kuosha vyombo vyao vya chakula ma maji.

Ili kuku wanenepe na kuwa wazito ni vizuri japo mara mbili au tatu pita feri ukawachukulie utumbo wa samaki unaotupwa. Hii inawanenepesha sana. Vile vile kuku wa kienyeji hawana magonjwa mengi kama wa kizungu. Mti wa ayovela ni mzuri sana kuwakinga na magonjwa. make sure that atlest mara mbili au tatu unatwanga majani ya mti wa Ayovela na kisha unawachanganyia katika maji ya kunywa kuku zako.

Kuna mengi sana lakin kama una suala niulize nitakujuza. Kwani mimi niliwafuga sana na nilifikisha mpaka kuku 3500.

Lakin faida ya kuku wa kienyeji ni kuwa bei yake ni kubwa kuliko kuku wa kawaida. Mayai yake bei kubwa kuliko kuku wa kizungu lakin pia hata mayai ya yasiyo anguliwa (mayai viza)vile vile wananunua waganga wa kienyeji.

faida ni nyingi sana.

UZOEFU WA MDAU
Safari yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10 kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10 unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu sana! Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!

Safari ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia. Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja! Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapajoto la kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!

Ili utotoreshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia incubator, tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga kwa pamoja hufikia wakati mayai huishatumboni unakuta wamelala kwenye viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15.

Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120. Kwa kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya. Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!

Kuku akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine wanambinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tega, au Box kubwa au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA.

Hawa kuku wakitoka JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia. Pia kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai lililotagwa siku hiyo! Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo. Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi! Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto la Mama bure!

Ndugu zangu wana JF naendelea kuelezea utotoleshaji bado sijamaliza hebu niwarushie hii kwanza maana nimeona nimechelewesha kuwakilisha na nimewaudhi, poleni, mwenzenu nilikuwa nahangaika kufukia tanuru la mkaa nimekuta limefunguka! Si mnajua maisha jamani!
 
Mkuu newmzalendo, ukienda kwenye thread za zamani kwenye hili jukwaa la business unaweza kupata ushauri/maoni/uzoefu ambao ulitolewa na wapendwa wanaJF.

Sorry, sina ujuzi wa kuweka link hapa moja kwa moja. Labda wengine wasaidie. Nakumbuka Pearl (kama sikosei) alikuwa ana mradi wa kuuza kuku wa kienyeji, kama alivyoeleza kwenye thread moja hapa jamvini.

Nakutakia kila la heri katika mradi wako huo.
 
Last edited by a moderator:
Hutakosa wateja tena ukitegemea ni kuku wa kienyeji,,,mie nnafanya biashara iyo ila sio Dar.

Nilianza kutafuta wafanyabiashara asa masokoni ili nipate angalizo na soko la jumla au rejareja,pia mahotelini unaweza pitia nk nk. Unajua biashara hii kweli ujue tu kujieleza na ukidhi haja ya wateja kwa uzuri,me ilinsaidia hasa ya masokoni na mnaingia mkataba kabisa.

Pia ukiwa na plani ya biashara (sijui niitaje business plan/profile??) ambayo umeiandika unaweza onyesha wateja asa big customers nk haaa si haba.

Keep it up ndugu
 
Mzalendo unachekesha eh! Hivi ulishawahi kufuga tena ? Maana watu hawaanzagi hivyo! Siku zote watu wanaanza na Majike! maana utaazima mbegu hata kwa jirani lakini wewe umeanza na jogoo!

Anyway Mwanzo mgumu sasa wewe fuga soko no kubwa sana tu. Kwa kuanzia unapeleka tu madukani watanunua. maana hayo mayai ya kienyeji yanatafutwa sana!
 
Mzalendo unachekesha eh! Hivi ulishawahi kufuga tena ? Maana watu hawaanzagi hivyo!!!!!!!! Siku zote watu wanaanza na Majike! maana utaazima mbegu hata kwa jirani lakini wewe umeanza na jogoo! Anyway Mwanzo mgumu sasa wewe fuga soko no kubwa sana tu. Kwa kuanzia unapeleka tu madukani watanunua. maana hayo mayai ya kienyeji yanatafutwa sana!

Comment yako imenifanya ni -smile
 
Mzalendo unachekesha eh! Hivi ulishawahi kufuga tena ? Maana watu hawaanzagi hivyo!!!!!!!! Siku zote watu wanaanza na Majike! maana utaazima mbegu hata kwa jirani lakini wewe umeanza na jogoo! Anyway Mwanzo mgumu sasa wewe fuga soko no kubwa sana tu. Kwa kuanzia unapeleka tu madukani watanunua. maana hayo mayai ya kienyeji yanatafutwa sana!

Hii kali kweli, mimi nilishajua jamaa ana majike tayari kumbe ana majogoo!
 
Mzalendo unachekesha eh! Hivi ulishawahi kufuga tena ? Maana watu hawaanzagi hivyo!!!!!!!! Siku zote watu wanaanza na Majike! maana utaazima mbegu hata kwa jirani lakini wewe umeanza na jogoo! Anyway Mwanzo mgumu sasa wewe fuga soko no kubwa sana tu. Kwa kuanzia unapeleka tu madukani watanunua. maana hayo mayai ya kienyeji yanatafutwa sana!

Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

Photo-0107.jpg
 
Mzalendo unachekesha eh! Hivi ulishawahi kufuga tena? Maana watu hawaanzagi hivyo!!!!!!!! Siku zote watu wanaanza na Majike! maana utaazima mbegu hata kwa jirani lakini wewe umeanza na jogoo!

Anyway Mwanzo mgumu sasa wewe fuga soko no kubwa sana tu. Kwa kuanzia unapeleka tu madukani watanunua. maana hayo mayai ya kienyeji yanatafutwa sana!

Mkuu ushauri mzuri natumaini atauzingatia, ila nimecheka sanaaaaa
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

Duh! nimeipenda sana hii mzee. hata mimi nimevutiwa nayo please kama inawezekano send it even to me. Maana " We normally learn good from the ways of people than from people themselves". Please do it maana nipo katika mchakato huo huo, japo siko Dar.
 
Duh! nimeipenda sana hii mzee. hata mimi nimevutiwa nayo please kama inawezekano send it even to me. Maana " We normally learn good from the ways of people than from people themselves". Please do it maana nipo katika mchakato huo huo, japo siko Dar.

Cheki hiyo imeisha leo - nimefunga mahesabu yangu ya mwezi huu.
 

Attachments

  • Layers Mesh Production - May 2010.xls
    15.5 KB · Views: 4,792
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

View attachment 10528

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

Mkuu hebu tuma hiyo database. So impressed by your set up.
 
Cheki hiyo imeisha leo - nimefunga mahesabu yangu ya mwezi huu.
Asante kwa kutufungua macho, na ninashukuru kwa mchango wako.

Kuna tatizo la mahesabu kidogo. Jumla ya gharama ni 1,590,277 na siyo 1,490,277 na kufanya faida kuwa 1,702,523. Kwa kuwa unatumia Msexcel

nakushauri utumie formulas badala ya kutype figures zote:

Column ya mapato( e3)andika =b3*d3 press enter, jibu litakuja pale. Then click kwenye E3 then kwenye right hand lower corner itakuja alama ya msalaba (+), press your left side mouse usiachie na vuta kwenda chini. Fomula itakuwacopied hadi chini yaani E4 itakuwa =b4*d4 nk. Kuweka jumla mwishoni click kwenye cell unayotaka jibu liwe e34 halafu nenda juu kwenye tool bar click

∑ basi jibu la jumla ya namba hizo itakuja,kwanza itajionyesha kwa kuhighlight, au andika =sum(e3:e33) press enter. Fanya hivyo hivyo kwa upande wa gharama, utapata jibu sahihi. Na profit ni =e34-f34. Hii inapunguza makosa madogo madogo ya kimahesabu

Pili tungefurahi zaidi kama ungetueleza una kuku wangapi? na sikuelewa eggies!

Thanks again
 

Attachments

  • Elnino layers p&l for May 2010.xls
    16.5 KB · Views: 2,340
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom