Zijue mali za maselebu wa Bongo

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Thread hii ni maalum kwa mapicha na maelezo japo kwa muhtasari juu ya mali na miliki za maselebu wa bongo hasa wasanii wa muziki na filamu.

Tofauti na wenzetu wa nchi nyingine hata ndani ya Africa Mashiriki inaonekana wasanii wetu wana mafanikio finyu sana kiasi kuwa wengine wanaishia kuwa na fedha za kupiga pamba na kubadilishia mboga


Leo naanza na msanii maarufu na mwanadada gaidi ama Zay to the B...

Zay B: Nani anasema nimefulia?

ZAYBBBB.jpg


Yawezekana amefulia kimuziki lakini sio kimali...


Kutoka Bongo mwana Hip Hop wa kike aliyeleta mapinduzi katika game ya muziki wa kizazi kipya kwa upande wa wasichana, Zainabu Lipangile a.k.a Zay B (PICHANI JUU) mwishoni mwa wiki iliyopita alidondoka ndani ya safu hii na kupiga stori mbili tatu ikiwemo kutangaza baadhi ya aseti anazomiliki hivi sasa kama alivyofanya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Ndani ya safu hii Zay B alisema kwamba wapo baadhi ya watu, wakiwemo wasanii wenzie wamekuwa wakivumisha maneno mitaani kwamba hivi sasa amefulia baada ya kupotea kwenye game kwa muda mrefu kitu ambacho amekikanusha, ndiyo sababu iliyomfanya atangaze mali zake.

“Unajua watu wengine huwa wanakosa ishu za kuongea, mimi kutosikika siyo kwamba nimefulia, kuna ishu kibao nafanya zinazoniingizia kipato, kwanza muziki wa Bongo haulipi na umejaa majungu. Ningekuwa nimefulia ningeweza kujenga nyumba au kununua gari?” Alihoji Zay B huku akionesha picha za nyumba yake zilizokuwa kwenye simu.

Mwanadada huyo alisema kwamba mjengo huo ameushusha pande za Buyuni, Pugu nje kidogo ya Dar es Salaam huku akimiliki gari aina ya Toyota Premio. “Mbali na hayo pia nimesaini mkataba wa kufanya kazi ya muziki na Kampuni ya Butile Africa Group ya Afrika Kusini, watu wasifikiri nipo nipo tu, sijafulia kihiivyo,”.


Zay%2B2.jpg

Hili ni jumba la kifahari la mwanadada ZAY B

Zay%2BCar.jpg


Na huu ndio mchuma wake makini aina ya TOYOTA Premio
 
Lady Jay Dee naye hayupo nyuma ana miliki gari aina ya Landcruiser PRADO na jumba la kifahari kule Kimara.

Geto+la+JD.jpg

Nyumba ya Lady Jaydee kwa nje

DSC05978.JPG

Lady JayDee akiwa amepozi ndani kwake

jide8bc.jpg

Ray C, Lady JayDee na Masoud Kipanya enzi hizo, wadau wenye
mali za Ray C wekeni hapa hivi huyu mdada anamiliki nini?
 
Hayo majumba ya kifahari, ndiyo hayo yanaonekana hapo juu?!!! au macho yangu hayaoni!
 
Wamejitahidi bwana maana wengine heshima zaishia bar na kwa wenye nyumba wetu kodi ya pango inapoisha
 
iwe ya kifahari au ya kuishi, mimi nawapongeza kwa kweli, angalau wamepiga hatua ni maendeleo!!!
 
mkwere pia kuna siku ITV kwenye kipindi cha sanaa na wasanii walionesha nyumba yake.....

anastahili pongezi (samahani mimi si mtaalamu wa habari picha)
 
sasa hizo ni nyumba za kifahari, au ni nyumba za kujistiri na kuishi kawaida tu?!!!


ndio mana vidole havilingani, we unaona ya kujictiri mwenzio anaona ya kifahari....huyo zay b nae awe anafikiria mara 2 kabla ya kuongea.....
 
mkwere pia kuna siku ITV kwenye kipindi cha sanaa na wasanii walionesha nyumba yake.....

anastahili pongezi (samahani mimi si mtaalamu wa habari picha)


nilimuona mkweli ila sisemi neno mie ...
 
Hivi na mimi ni selebu ? kuna song langu moja limehit na kutoweka ghafla nadhani nastahiri kuwa celebrity wenu!!
 
Mbona ni vitu vya kawaida tu kwa mtu wa kawaida kumiliki - sio lazima uwe selebu ili uwe na kimeo (sorry Primeo)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom