Zijue hatari na changamoto za daraja la Kigamboni kabla hujalitumia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
NJIA ZA DARAJA LA KIGAMBONI0011.jpg
kigamboni brj.jpg
kigambn nnn.jpg
View attachment 342355
kigamboni brj.jpg
kigambn nnn.jpg

Enyi wapenda maendeleo humu JF;

Nimeona niwashirikishe machache juu ya Daraja pendwa, daraja kubwa la kigamboni linalounganisha kigamboni na kurasini.

AINA ZA BARABARA

Daraja hili lina njia tatu kwenda kigamboni na njia tatu kurudi kurasini.

MATUMIZI YA BARABARA UENDAPO KIGAMBONI

Endapo unatokea mjini, kuna barabara mbili zinazoweza kukufikisha na kukuvusha kwenda kigamboni, moja ni ile ya mataa ya uhasibu(TAZARA), ambayo ili uweze kufika, unapaswa uelekee kusini (barabara ya bandarini) ambapo kwa mbele njia zinaongezeka na kuwa nine, njia mbili kushoto zinanyoosha kwenda bandari hadi SHIMO LA UDONGO, na njia mbili kulia kwa pamoja kama m30 mbele zinagawanyika tena na moja kushoto inanyosha tena bandarini kuungana na zile mbili za mwanzo, halafu moja kulia ndiyo inayoenda Kigamboni na kuungana na inayo U-TURN kurudi kigamboni, njia hizi hukupeleka moja kwa moja hadi kigamboni.

Note: Hakikisha unabana upande wa kulia halafu nenda polepole ukiwa unaingia kwenye hizo flyover kwani kuna makutano na watumiaji wengine watokao Kigamboni kwenda bandarini (shimo la udongo) au zinazo U-TURN, waweza jikuta unagongana na gari zitokazo Kigamboni zinazo U-turn kurudi Kigamboni au kwenda bandarini (shimo la udongo) bila kutegemea.

UTOKEAPO BANDARI AU SHIMO LA UDONGO

Hakikisha unakaa upande wa kushoto,hii itakuleta moja kwa moja hadi darajani, utokeapo bandarini njia hii pia waweza kaa upande wa kulia ili ikupeleke hadi uhasibu (TAZARA) maana inaumgana na itokayo kigamboni kwenda TAZARA (tizama mchoro hapo kwenye picha)
CHECK POINT


Mwisho wa daraja kuna check point ambapo utafata maelekezo kutokana na chombo gani unatumia na wapi upite. Soma vibao ie, BUS, CAR n.k

BAADA YA CHECKPOINT

Safari inaendelea njia tatu kwenda ambapo hadi mwisho kuna barabara ya vumbi, itakupasa uingie barabara ya vumbi iliyo kulia kwako ili ikupeleke moja kwa moja hadi kuungana na lami itokayo feri kwenda Kibada kupitia kisiwani (shortcut ya Kibada)

UTOKAPO KIGAMBONI

Kama wewe unatoka Kigamboni, njoo moja kwa moja hadi check point, na baada ya hapo daraja linaanzia, utatembea na hizo njia tatu, hadi unapokaribia daraja la njia ya reli iliyopita juu (soma maelekezo ya vibao kwa juu relini yamebandikwa) M100 kabla kama ulikuwa kushoto hama, kaa katikati na uzame njia ya chini ili ukaibukie/ikupeleke moja kwa moja hadi Uhasibu mataa(TAZARA/UBUNGO) au kama unataka kupita bandarini Shimo la udongo, hapo ya kupasa ukae kushoto na ukubali kubana hukohuko kushoto itakuzungusha kupinda kulia kuelekea bandarini au shimo la udongo ama ku U-TURN kurudi Kigamboni.

Note: Hakikisha unaingia polepole kwani eneo hilo ndipo gari zitokazo uhasibu mataa (TAZARA/UBUNGO) zinapoingilia kwenda Kigamboni.

WATEMBEA KWA MIGUU

Kwa watembea kwa miguu kuna njia maalumu pembezoni mwa barabara zenye kingo kila upande kwa usalama wako, hupaswi kuruka na kuingia njia ya magari ni hatari kwako.

HUDUMA NA OFFICE ZILIZOPO

Upatwapo na tatizo lolote, ni vyema ukawasiliana na watoa huduma pale darajani, upande wa Kigamboni ndiko ziliko office, kuna office ya ZIMA MOTO, KITUO CHA POLICE, ZAHANATI- FIRST AID, Ofisi za NSSF na ukumbi wa mikutano,MZANI n.k.

CHANGAMOTO

Utumiapo daraja hili chukua tahadhari kwani utakutana na wengine wasiyoijua njia.

a. Ni vyema kwenda taratibu hususani unapokaribia kuingia (yaani sehemu inayounganisha U-turn ya kurudi Kigamboni na ile itokayo Uhasibu/TAZARA (ufikapo sehemu hiyo kuwa makini sana vinginevyo utageuka kafara). Nashauri sehemu hii serikali iweke taa maalum za kuongozea au tuta kwa watokao Kigamboni kwenda bandari na wanao u-turn wasimame ili wasigongane na watokao Uhasibu/TAZARA na kuingia moja kwa moja darajani.

b. Unapotokea Kigamboni pindi unavuka daraja la reli na kugundua umekosea njia ukabana kushoto, yaani kama lengo lako ni kwenda Uhasibu/TAZARA , ya kupasa uka U-turn urudi tena kigamboni ukaanze upya, ili ukae katikati kulia na si kushoto.

Note; Kuhama ghafla toka kushoto kwenda kulia ufikapo eneo hili kunaweza kusababisha bonge la ajali kwa kugongwa au kumwingilia aliye kwenye channel yake.

c. Pindi unapovuka kwenda Kigamboni VIJIBWENI CENTER Hakuna barabara inayowapeleka vijibweni center, wanalazimika kwenda moja kwa moja hadi mwisho wa lami na ku u-turn kurudi ili kuelekea vijibweni center.

NASHAURI, barabara moja kulia (KARIBU NA TRANSFOMA YA UMEME) baada ya tuta unapotoka kwenye check point, waweke taa itobolewe kulia kuingia vijibweni center ambayo kwani ni barabara mhimu sana kwasababu huko mbele inaenda hadi Kibada, baada ya kupita yard ya mama ANNA MKAPA inaenda kuungana na barabara nyingine itokayo kisiwani HOSPITALI YA JIJI/makaburini kwenda hadi Kibada kupitia shule ya Mizimbini secondary

d. Kwa watembea kwa miguu daraja ni lefu takribani mita 600, kwa mida ya usiku si salama kutokana na wakabaji wanaoweza kutumia pikipiki kukukaba na kukimbia, nashauri serikali waweke walinzi dolia, kila mita 100, kila upande, achilia mbali kituo cha police kilichopo, hii itasaidia kuimalisha ulinzi wa raia na miundombinu iliyopo.
NB; kuna changamoto nyingine ya watu wanaopotosha umma juu ya FLYOVER, ili kujua usahihi wa fly over kujengwa vile bonyeza link hapa (Mnaokosoa ujenzi wa fly-over za daraja la Kigamboni mnayajua haya?)


EPUKA KUWA KAFARA WA DARAJA LA KIGAMBONI, ENDESHA KWA USALAMA….

Endapo umepotea na kuhitaji msaada wa kuelekezwa nami waweza kunitumia ujumbe mfupi PM nitakuelekeza. Unaruhusiwa pia kuboresha hii thread ili kutoa maelekezo sahihi kwa wadau wengine.

Imeandaliwa na mpenda maendeleo Dmkali

AHSANTE
 
Asante kwa maelezo.
Pia ukiwa unatoka Kigamboni pale daraja la treni, kwa siku hizi za mwanzo kumbuka kusoma na kufuata maelezo na kuepuka mazoea. Mfano, ukienda kimazoea, kama unatokea kigamboni, kwamba ukichukua mchepuko wa kushoto kuwa utaelekea uhasibu imekula kwako. Jamaa yangu jana kapita kwa kukariri, anatoka kigamboni sasa pale daraja la treni kwa juu hakufuata maelezo, akapita mchepuko wa kushoto sababu ndo muelekeo wa uhasibu, matokeo yake akarudi bandarini na ilimbidi aende tena kigamboni hadi mwisho wa lami na arudi ili afike tena kwenye junction, kuelekea bandarini unachukua mchepuko wa kushoto na uhasibu unachukua mchepuko wa kulia.
 
Mtoa mada, Kidongo Chekundu unamaanisha Shimo la Udongo, au? Nadhani unakusudia Shimo la Udongo...

Halafu hapo uliposema unapotoka mjini, kuna ile ya "Mataa ya Uhasibu, ambayo ili uweze kufika, unapaswa uelekee kusini (barabara ya bandarini)...."

Kwa mgeni wa eneo husika hawezi kufahamu ni barabara ipi inaelekea bandarini; nadhani ingekuwa wepesi zaidi ungesema kama unatoka mjini, "ukifika Mataa ya Uhasibu chukua Left turn."

Na kwa nyongeza ungeongeza "kama unatoka TAZARA, ukifika Mataa ya Uhasibu nyoosha moja kwa moja... kisha ujumuishe na hayo maelezo ya ukitoka mjini ukafika Mataa ya Uhasibu...

Ni ushauri tu!
 
sasa mimi kwetu huku mwanza nanilii... huku sengerema au huku kishapu ya shinyanga sasa mimi kigamboni nikafanye nini kwa mfano?? au nije kupiga picha??
 
Back
Top Bottom