Zijue faida kabambe za kulala mtupu/uchi wakati wa usiku

Bennie 369

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
713
529
Zijue faida 11 za kulala uchi au mtupu nyakati za Usiku

UMEZOEA kulala na nguo nyepesi za kulalia? Au unahisi vizuri zaidi ukilala na nguo nzito laini za kulalia? Watu wengi hujifunika mashuka na wengine hujifunika mablenketi kabisa.Katika makala haya, utakufumbuliwa macho uanze kulala uchi/mtupu kwa kutumia hoja bora zilizochaguliwa kuelezea kwanini kulala uchi ni kuzuri kwako.Nguo za kulalia zina gharama kubwaNi kiasi gani cha fedha ambazo wewe hutumia kununua pea ya nguo za kulalia? Inaweza kuwa kati ya fedhaza kitanzania katiya shilingi 20, 000 na 40, 000 au zaidi.

Nimara ngapi huzifua hizo nguo? Sasa fikiria ni kiasi gani cha pesa na muda unachoweza kuokoa usipovaa nguo za kulalia.Hutengeneza uhusiano mzuri ukisaidiwa na kichocheo cha OxytocinNatasha Turner, daktari wa tiba asilia aliyeandika kwenye blogu ya HuffPost Canada, alifichua kwamba kulala karibu au mkiwa mmekumbatiana na mwenzi wako mkiwa uchi/watupu hufanya mwili kutoa kichocheo kiitwacho Oxytocin kinachofanya ujisikie vizuri. Hii inatokea pale kunapokuwa na mgusano wa ngozi kwa ngozi,hii inaweza kusaidia kuondoa msongo (Stress) na kushuka moyo (Depression).

Oxytocin pia inaweza kupunguza shinikizo la damu,kuimarisha tumbo na kupunguza uvimbe kwenye utumbo. Pia, utendaji wako wa tendo la ndoa pengine unaweza kuboreka.Hupelekea usingizi mwanana.Hivi unafahamu baadhi ya matatizo ya kukosa usingizi (Insomnia) yanaambatana kutokana na tatizo la mwili kudhibiti jotoridi? Taasisi ya Usingizi ya Los Angeles inaripoti kwamba hali hii haiathiri tu mzunguko wa usingizi ila pia hukuzuia kupata usingizi mnono. Kulala uchi/mtupu husaidia katika kurekebisha jotoridi la mwili (hivyo mwili hauchemki kupita kiasi, ni vibaya kuamka umelowana jasho.

Hukufanya ubaki kijanaKama tulivyoona hapo juu kuhusu kudhibiti jotoridi kama unahitaji usingizi mzuri, Natasha Turner anashauri kuweka mwili katika jotoridi chini ya 21?C ukiwa kitandani na njia nzuri kufantahivyo ni kulala uchi/mtupu. Hii huruhusu vichocheo vinavyozuia uzee na Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa kusinzia na kuamka kutenda kazi vizuri.

Utajihisi huru, Kulala kitandani kwako, bila kuvaa chochote inakufanya kujisikia huru.Huhamasisha vichocheo vya furaha (kuponya).Unapolala na nguo au kulala chini ya blanketi zito unazuia utokaji wa kichocheo cha ukuaji (Growth Hormone/HGH ). Hii ina maana hutoweza kupunguza mafuta ukiwa katika usingizi au hautofaidika na ukarabati wa usiku wa mifupa,ngozi na nyama za mwili wako.

Kulala uchi/mtupu pia huthibiti kiwango cha Cortisol,zinazo dhoofisha kinga ya mwili,kupandisha shinikizo la damu na lehemu (Cholestrol), kuvuruga mpangilio wa usingizi, kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuongeza hamu ya sukari.Inaimarisha kujipendaKama una matatizo ya kutokujiamini basi kulala uchi/mtupu kutakusaidia kujifunza kujipenda. Kwa kuanza, jizoeshe kulala bila nguo kila jioni. Baada ya muda utazoea pia baada ya muda unaweza kuwa umejifunza kuupenda muonekano wako bila nguo.Inatunza kiafyaviungo vya uzazi.Kina dada, mnafahamu mnaweza kupunguza matatizo ya mabukizi ya fangasi kwa kulala uchi/watupu?

Unaweza kupunguza kuzaliana kwa fangasi na uke wako utakushukuru kwa hilo. Vilevile wanaume wanaweza kufaidika kulala uchi/watupu kwa kuwa korodani zinakuwa katika jotoridi la kutosha na uzazi unaongezeka.Mzunguko wa damu unakuwa boraHakuna kitu kibaya kama lastiki inayozuia mzunguko wa damu. Ondoa nguo zenye lastiki na utajipata uko na furaha kwa mtiririko wa damu mzuri ndani mwili wako.

Kuwa na ngozi nzuriUnapokuwa uchi/mtupu ngozi yako inapata nafasi ya kupumua. Kama una chunusi au vipele mgongoni ni kitu cha thamani kuacha hewa ya Oxygen kufika kwenye maeneo hayo. Ngozi yako inastahili uhuru kidogo na utajisikia vizuri kwa kuiacha ngozi wazi.Kutokuwa mvivuFaida nyingine ya kulala uchi/mtupu ni kwamba mara baada ya kuamka unakuwa na ulazima wa kuvaa nguo kwa ajili ya siku hiyo mpya na sio kuamka na nguo zako za kulalia na kutoka nazo nje.
 
Aise wanadamu tunapishana sana akili, wengine wanawaza kupiga pesa ndefu kila siku lakini kumbe kuna wengine wanawaza mambo ya kulala uchi kama mbwa!!!

Labda wa Dar na Sudan. Hivi Arusha, Lushoto, Mbeya, Njombe, Makambako, Mafinga na maeneo baadhi ya Songea unawezaje kulala uchi?
 
Ulalaji wa kutovaa chochote ndio style yangu.ila sometimes naghairi ninapo sikia wizi wa majumbani nyakati za usiku umeingia mtaani kwetu(kwa sisi wa uswahilini).

Huwa nalala na bukta ili Iwe rahisi kukurupuka toka kitandani kwenda kuchungulia anaye chokora chokora sebuleni.
 
Mi sijawahi kulala uchi na haitatokea yaani sijui naonaje onaje, hizo faida wacha nizikose tu.usisahau kutaja na hasara
 
Ni raha unajisikiaga uhuru na hewa nyepesi,,,pia mashine inakua vizuriii bila kikwazo
 
Kama unalalala na mwenza wako sawa lakini kama peke yako si kitu kizuri linaweza likatokea tatizo ukazidiwa usiku dada zako au majirani wakavunja mlango wakajionea 'vitu vyako' unapolala hauna guarantee na Mungu kwamba kuwa kesho utaamka salama na pia usiku kuna viumbe wengine wabaya ambao wewe huwaoni wanaweza wakakugegeda
 
kama unalalala na mwenza wako sawa lakini kama peke yako si kitu kizuri linaweza likatokea tatizo ukazidiwa usiku dada zako au majirani wakavunja mlango wakajionea 'vitu vyako' unapolala hauna guarantee na Mungu kwamba kuwa kesho utaamka salama na pia usiku kuna viumbe wengine wabaya ambao wewe huwaoni wanaweza wakakugegeda


Ha ha ha ha hata ukiwa na nguo s wanajua hawaonekani wanakisevia tu
 
kama unalalala na mwenza wako sawa lakini kama peke yako si kitu kizuri linaweza likatokea tatizo ukazidiwa usiku dada zako au majirani wakavunja mlango wakajionea 'vitu vyako' unapolala hauna guarantee na Mungu kwamba kuwa kesho utaamka salama na pia usiku kuna viumbe wengine wabaya ambao wewe huwaoni wanaweza wakakugegeda
Hata majambazi wakivamia usiku nyumbani kwako..wakufume uchi???lazima wafumue marinda
 
kama unalalala na mwenza wako sawa lakini kama peke yako si kitu kizuri linaweza likatokea tatizo ukazidiwa usiku dada zako au majirani wakavunja mlango wakajionea 'vitu vyako' unapolala hauna guarantee na Mungu kwamba kuwa kesho utaamka salama na pia usiku kuna viumbe wengine wabaya ambao wewe huwaoni wanaweza wakakugegeda

Chalii angu mmoja aliwahi lewa Sana kiasi cha kushidwa kuja job. Sasa mie na bosi tukamfuatilia maana alikuwa na baadhi ya vifaa hitajika.

Tulipofika ilibidi nichungulie kwanza dirishani. Na alikuwa mtupu aibu yaani. Wa kibao akiwamo mama mwenye nyumba alikuwapo wakiwa na lengo la kuvunja mlango, ilibidi nitumie busara kuwaomba waondoke nibaki mwenyewe ili nivunje na kuyasitiri maungo yake.
 
Kwani huwezi kufikiri kupata hela huku upo uchi. wewe unatafuta hela au sent? Sisi wenye hela ndo tunaongoza kwa kulala uchi.
 
Aise wanadamu tunapishana sana akili, wengine wanawaza kupiga pesa ndefu kila siku lakini kumbe kuna wengine wanawaza mambo ya kulala uchi kama mbwa!!!
Labda wa Dar na Sudan. Hivi Arusha, Lushoto, Mbeya, Njombe, Makambako, Mafinga na maeneo baadhi ya Songea unawezaje kulala uchi?

How ironic?!

Kwani kuna sehemu amesema ni lazima??
 
Back
Top Bottom