Zijue dalili za magonjwa ya Hofu (anxiety disorders)

Nov 3, 2014
38
10
Je, unajua kua mshtuko au Hofu iliyopitiliza ni ugonjwa na kua unatibika? Watu wenye tatizo hili huwa hofu kubwa wakati mwingine bila sababu; huhisi kama wanashindwa kufikiri vizuri; Wanashindwa ku concentrate kwenye kazi zao au masomo au mahusiano.

Hofu hii inaambatana na dalili za kimwili kama;

· Mapigo ya moyo kwenda kasi (racing heart beat),
· Kizunguzungu ( dizziness)
· Kukakamaa misuli (muscle tension),
· Kufa ganzi (numbness)
· Maumivu ya tumbo (stomach pain)
· Kutokwa jasho (sweating)
· Kutetemeka (shaking) na
· Kushindwa kuhema (shortness of breath).
· Kichefuchefu (nausea) N.k
· Ndoto za kutisha (nightmares)
· Kumbukumbu za matukio yanayoumiza hisia kama vile yanajirudia (flashbacks)

Hizi ni baadhi tu ya dalili za magonjwa ya hofu (anxiety disorders) ambayo ni pamoja na Panic; PTSD; GAD; Phobia n.k
Kikubwa ni kua magonjwa haya yanawasumbua watu wengi bila kujua kua yanatibika na matibabu yake hutolewa bure katika hospitali za serikali.
 
Mkuu nahisi nina hilo tatzo.
Sasa nkienda kwa dokta ntamwambia naumwa ugonjwa gan?
Au nimwambie tu kwa kifupi nina hofu?
 
Je, unajua kua mshtuko au Hofu iliyopitiliza ni ugonjwa na kua unatibika? Watu wenye tatizo hili huwa hofu kubwa wakati mwingine bila sababu; huhisi kama wanashindwa kufikiri vizuri; Wanshindwa ku concentrate kwenye kazi zao au masomo au mahusiano, Hofu hii inaambatana na dalili za kimwili kama
· Mapigo ya moyo kwenda kasi (racing heart beat),
· Kizunguzungu ( dizziness)
· Kukakamaa misuli (muscle tension),
· Kufa ganzi (numbness)
· Maumivu ya tumbo (stomach pain)
· Kutokwa jasho (sweating)
· Kutetemeka (shaking) na
· Kushindwa kuhema (shortness of breath).
· Kichefuchefu (nausea) N.k
· Ndoto za kutisha (nightmares)
· Kumbukumbu za matukio yanayoumiza hisia kama vile yanajirudia (flashbacks)
Hizi ni baadhi tu ya dalili za magonjwa ya hofu (anxiety disorders) ambayo ni pamoja na Panic; PTSD; GAD; Phobia n.k
Kikubwa ni kua magonjwa haya yanawasumbua watu wengi bila kujua kua yanatibika na matibabu yake hutolewa bure katika hospitali za serikali
Mkuu hilo tatzo hata mm linanisumbua hasahasa phobia tiba yake ipoje?
 
kwa mwenye tatizo la phobia hapo juu napenda kwanza kukupa pole na pili maelezo kuhusu Social Phobia (angalia post nitakayoituma muda mfupi ujao) tatizo hili pia linaitwa social anxiety. matibabu ni kati ya Dawa au psychotherapy ambapo matibabu hutolewa bure katika hospital ya taifa muhimbili na pia katika baadhi ya private hospitals. kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata matibabu na kujua zaidi dalili za magonjwa mengine ya kisailolojia tufuate instagram psychological_support_tz au like faceboock page yetu @ psychological support and mental health awareness[h=2][/h]
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nahisi nina hilo tatzo.
Sasa nkienda kwa dokta ntamwambia naumwa ugonjwa gan?
Au nimwambie tu kwa kifupi nina hofu?

inabidi umwambie dalili zote unazozipata kama zilivyo hapo juu na hata kama kuna nyinginezo. kila mtu yupo tofauti hivyo sio lazima zote zifanane. kama una baadhi tu ya dalili pia inawezekana ikawa una mild to modarate anxiety. tatizo baadhi ya madaktari wetu (except for psychiatrists) ni rahisi sana kumis diagnose anxiety hivyo suala la kumwambia una hofu ni muhimu sana. pia kwa kua wataalam wa suala hili ni Clinical psychologist kuliko medical doctors. ningekushauri kama unaweza umtafute msaikolojia tiba. (sio counsellors wala psycologist wengine bali CLINICAL PSYCHOLOGIST) Wanapatikana muhimbili na baadhi ya private hospitals kama agakhan
 
Na presha inaanza mapemaaaa hasa ishu ya kazi interview, jumlisha cjui nn tutapona kweli. Mapigo yanaenda ovyo ovyooo
 
Back
Top Bottom