Ziara za Lowassa na coverage anazopewa, ni utetezi?

Dr. Slaa Vs EL 2015 for president patachimbika. Kwanza ndani ya CCM kwenye mchakato wenyewe ni kuwa kutakuwapo na mpambano mkali sana huku akina Membe, Sumaye, Magufuli, Prof. Mwandosya nk wakitaka nafasi.

Wakishampitisha EL, anakutana na Dr Slaa (Its my hope atagombea), Dr. wanachuana vikali huku kashfa za hapa na pale zikitawala, na EL kwa sasa anasafisha jina kwa kupewa coverage kubwa kwa mujibu wa taarifa za kikao kilichopita, jamaa alitaka kumlipua JK kuwa alijiuzuru kulinda heshima ya serikali. Na JK hawezi kumfanya kitu, hata hii kitu ya katiba anatamani kuona kuna mabadiliko makubwa ya katiba, lakini anajikuta kwenye pressure kubwa kutoka ndani ya kundi la CCM linaongozwa na EL.
 
Wiki hii nzima magazetini na hapa kwetu jf pametawaliwa na minyukano mikubwa kati ya aidha wafuasi wa LW na wasio,au wana magamba na wengineo.

Kikubwa kilichoibua mjadala ni jinsi inavyosemekana mh. (ingawa hili neno silipendi) LW alivyowagalagaza magamba wakashindwa kumvua gamba mwenzao.Utetezi wenyewe ni jinsi yeye anavyodai kujaribu kushawishi kuwafukuza Richmond na kwamba Mkulu ndiye aliyemkwaza.

Nimetumia neno kujaribu kwa sababu kwa mtizamo wangu ushauri ule naweza kuuita geresha *****.Nasema hivyo kwa sababu kama alishauri mara moja hajatuonyesha kama aliendelea kusisitiza ushauri wake.
Pili ,inawezekana alikuwa anashauri jambo ambalo yeye mwenyewe haliamini na ndio maana lilikosa msisitizo.

Tatu, ni je baada ya kupuuzwa alichukua hatua gani ?Kama unaweza kupuuzwa katika jambo unaloamini kwa asilimia mia uko sahihi na usichukue hatua yeyote,je sisi wananchi tuendelee kukuamini ulikuwa na nia ya dhati ya kulisimamisha ?

Kwa mawazo yangu LW angejiuzulu kabla ya kuthumiwa kwa kutetea msimamo wake,nina hakika leo hii nchi nzima ingekuwa inampigia chapuo la uraisi hata kama ana mapungufu mengine makubwa.

Mnaomtetea LW pengine hamjaona alipodondokea mnataka kupatambua anapojaribu kusimamia.
Nawasilisha
Ndugu ulivyosema ni sawa na kweli kabisa tatizo EL kawalisha watu kasumba(kuwarubuni kwa vijisenti)kiasi kwamba sasa watu wamekuwa mazezeta hawasikii wala hawaambiwi ,nafikiri watu wangejiulize kwanini mtu kama huna tatizo uhangaike kupita makanisani na kujifanya unachangia harambee ,hapo zamani mbona alikuwa hafanyi hivyo?na hizo hela anazomwaga kwenye hayo makanisa kazipata wapi,pia kwenye vyombo vya habari ni vivyo hivyo,kwenye UVCCM ndio usiseme,je kweli hapo kuna nia njema.Hata hapa JF kawajaza wapambe wake kibao na usishangae kusoma comments za hovyo kutoka kwa hao wapambe.Hata hivyo tunasahau kuwa ukweli na uongo ni sawa na maji na mafuta,asilani havitapatana
 
Mkuu aliyoyakwepa wakati ule kwa kutochukua hatua ndilo anguko lake

Kweli hilo ni anguko tosha kwa EL, lakini cha ajabu anataka/anashawishi kuwa madhambi kama hayo alikuwa nayo hata yeye JK wakati wa kinyang'anyiro cha kumtafuta Rais ndani ya CCM ambayo yalipelekwa na Paul Sozigwa lakini hayakuangaliwa mpaka akafanikiwa kuupata Ufalme huu alionao, hivyo ndivyo anavyotaka na yeye afunikiwe kombe ili mwanaharamu apite, baada ya kutoa siri hiyo ndipo Mkapa akajua sasa kikao kitanuka (wengine tulikuwa hatujui kwanini mzee Sozigwa alitupwa ghafla toka ndani ya system..kwa hilo tumshukuru EL kutufumbua) harakaharaka hoja ikafungwa Mwenyekiti DrJMK,Rais JMK,DrJK, Amiri Jeshi mkuu JK, hoja hii iliachwa bila muafaka na naamini itarudi kwa kuanzia hapo walipoiachia...

HISTORY LIVES AND IF DIES IT NEVER DECAY
 
Ndugu ulivyosema ni sawa na kweli kabisa tatizo EL kawalisha watu kasumba(kuwarubuni kwa vijisenti)kiasi kwamba sasa watu wamekuwa mazezeta hawasikii wala hawaambiwi ,nafikiri watu wangejiulize kwanini mtu kama huna tatizo uhangaike kupita makanisani na kujifanya unachangia harambee ,hapo zamani mbona alikuwa hafanyi hivyo?na hizo hela anazomwaga kwenye hayo makanisa kazipata wapi,pia kwenye vyombo vya habari ni vivyo hivyo,kwenye UVCCM ndio usiseme,je kweli hapo kuna nia njema.Hata hapa JF kawajaza wapambe wake kibao na usishangae kusoma comments za hovyo kutoka kwa hao wapambe.Hata hivyo tunasahau kuwa ukweli na uongo ni sawa na maji na mafuta,asilani havitapatana

Sitta leo yuko st Thereza Arusha akimwaga pesa na king maker mpya Mr Mengi, mbona hakiwaaumi kinawauma cha Eddo?
 
Back
Top Bottom