Ziara za Lowassa na coverage anazopewa, ni utetezi?

Jamaa nadhani anakitu cha ziada ambacho nadhani wanaccm hawana....mda huu pia kipindi anaendesha Paschal Mayala, jamaaa anaendelea kuuza sura!
 
na mara zote amepewa sifa ya kuwa msemakweli, tofauti na serikari iliyopo madarakani.
Na Paschal anasema siku moja atakuja na ukweli kuhusu richmond,
Tusubiri, tuone.
 
Your a great thinker mkuu..hizi ndizo threads zinazotakiwa kuletwa hapa JF watu wafikirie na kuweka kwenye wazi nini maana ya haya yote.Nimekuwa natazama sana siku za karibuni,jamaa anafanya ziara za kufa mtu,jana alikuwa Monduli tena ndani kabisa,nikashangaa leo namuona Dar pale sabasaba...halafu kitu kinachonisumbua sijui kama nipo ok!! HIVI LOWASA NI WAZIRI MSTAAFU au WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU..Maana kwasasa vituo vingi vya habari vinamtamka kama waziri mkuu mstaafu kitu ambacho sidhani kama ni sawa.Tukirudi kwenye mada,huyu jamaa anajua anachofanya,hili si jambo la kawaida na hebu tujiulize..
  1. Kwanini kipindi hiki?
  2. Kwanini bungeni hasemi na anakuwa msemaji sana akiwa uraiani kwasasa kuliko kipindi chochote?
  3. Kwanini kila sehemu ambapo anahisi kutakuwa na mkusanyiko wa watu au coverage ya vyombo vya habari lazima atie timu?
Kwahili tutambue moja ni maandalizi ya uchaguzi wa NEC 2012 na maandalizi ya kuutaka uraisi 2015 ambao hataupata hata kwa dawa..hata kama atashinda kwa T.B Joshua miaka yote iliyobaki kabla ya uchaguzi wa 2015...

Mkuu kila kitu kinahitaji maandalizi.
 
poleni msiosoma alama za Nyakati.
Huyu jamaa ndiye Rais ajae 2015 kama hujui naomba ulijue hili.
sehemu anazoenda nyingi ni kufnya tathimini ya namna anavyokubalika kwa raia.

kuwasilisha
 
Heeeeh Rais sio DR. Slaa tena amegeuka Lowasa?Mbona mnatuchanganya ama ndio mbinu za kupoteza lengo ushindi uwe mwepesi 2015.
 
Sielewi cheo cha sasa cha Edward Lowasa.
Kila taarifa ya habari TBC, lazima aonekane. Je yeye ni mbunge tu wa Monduli au ana cheo kingine kinachompa nguvu ya hizo ziara.
Je yeye ndiye remote controller ya mtawala wa juu wa nchi?
Sielewi inakuwaje mtu ambaye si mwenyekiti wa chama wala kiongozi wa serikari apewe kipaumbele katika habari za kila siku?

Ni Waziri mkuu mstaafu, na mpokea kijiti cha uenyekiti 2012 mtarajiwa wa Chama cha Magamba na pia yeye ndiye ataimbiwa kale ka wimbo ka TIOT 2015 "Tazama kumekucha, Tazama kumekucha, Jogoooo limewika Chimwagaaaaaa! kada wa ......."
 
Sielewi cheo cha sasa cha Edward Lowasa.
Kila taarifa ya habari TBC, lazima aonekane. Je yeye ni mbunge tu wa Monduli au ana cheo kingine kinachompa nguvu ya hizo ziara.
Je yeye ndiye remote controller ya mtawala wa juu wa nchi?
Sielewi inakuwaje mtu ambaye si mwenyekiti wa chama wala kiongozi wa serikari apewe kipaumbele katika habari za kila siku?

unajua hawa jamaa wa tbc ni wa ajabu sana sijuhi kwa sababu wengi waliletwa na el,wapo tayari kutompa coverage bosi wao wa sasa lakini wakampa el ya kufa mtu mfano wakati jk anatoa kamisheni kwa wanajeshi kule chuo cha tma monduli jumamosi ya novemba 26,2011 tbc hawakutumia kabisa hiyo habari nilikuja kuiona itv asubuhi baada ya kuangalia taarifa ya habari lakini nilifuatilia taarifa zote za tbc lakini sikuiona.juzi naangali naona wanamtoa el kwa kina haikiwa huko huko monduli sijuhi hilo seriklika na chombo chake kama wanaliona
 
Kuna unapana wa jambo hilo tofauti na unavyofikiri wewe ki juu juu. Hilo lilikuwa jambo zito ambalo lilibeba kashfa iliyokuwa inamuhusu rais pia. Kukurupuka kama unayotaka wewe kungesababisha mtafaruku mkubwa na mgongano wa kuiutawala. Alichofanya EL ni kutumia busara ya hali ya juu kunusuru hali. Kumbuka alitaka kuvunja mkataba wa RICHMOND, Akampigia simu raisi kutaka ushauri. Akaambiwa asubiri rais anashauriana na makatibu wa wizara. Ungekuwa wewe ungefanya nini. Aliwajibika katika hali ya kuepusha pepo mchafu katika serikali yake.

huo ni upande wa el bado hatjasikia pande wa jk,si ajabu jibu la alimpigia simu kwa ujanja ili kupata go ahead na alivyoipata akaitumia barabara jamani hivi jamaa mnamfhamu alivyokuwa smart ama mnamsikia ? muulizeni mzee malecela na magari ya kwanza kabisa ya wabunge ndipo mtajuta kumfahamu el,mnakumbuka mafuriko ya lushoto ndipo mtajuta kumfahamu el msiyemfahamu ndiyo mnakurupuka,aliyekuwa waziri msabaha anaushahidi tena wa maandishi wa memo kutoka kwa el,jk alipigwa mtego wa simu alivoingia king jamaa katumia chance
 
Kila jambo lina wakati wake! Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Tusubiri mwisho wa siku tutaja kufahamu kila kitu
 
Your a great thinker mkuu..hizi ndizo threads zinazotakiwa kuletwa hapa JF watu wafikirie na kuweka kwenye wazi nini maana ya haya yote.Nimekuwa natazama sana siku za karibuni,jamaa anafanya ziara za kufa mtu,jana alikuwa Monduli tena ndani kabisa,nikashangaa leo namuona Dar pale sabasaba...halafu kitu kinachonisumbua sijui kama nipo ok!! HIVI LOWASA NI WAZIRI MSTAAFU au WAZIRI MKUU ALIYEJIUZULU..Maana kwasasa vituo vingi vya habari vinamtamka kama waziri mkuu mstaafu kitu ambacho sidhani kama ni sawa.Tukirudi kwenye mada,huyu jamaa anajua anachofanya,hili si jambo la kawaida na hebu tujiulize..
  1. Kwanini kipindi hiki?
  2. Kwanini bungeni hasemi na anakuwa msemaji sana akiwa uraiani kwasasa kuliko kipindi chochote?
  3. Kwanini kila sehemu ambapo anahisi kutakuwa na mkusanyiko wa watu au coverage ya vyombo vya habari lazima atie timu?
Kwahili tutambue moja ni maandalizi ya uchaguzi wa NEC 2012 na maandalizi ya kuutaka uraisi 2015 ambao hataupata hata kwa dawa..hata kama atashinda kwa T.B Joshua miaka yote iliyobaki kabla ya uchaguzi wa 2015...
Akiwa kimya mnasema akiongea mnasema kweli binadamu haridhiki.
 
Hizo ni moja wapo ya mbinu alizopewa na washauri wake wa mambo ya kisociallogia. Aweze kujifamiliarize na jamii ya kitanzania iliyomtenga tokea mwaka 2008, kufuatia sakata la kampuni feki ya Richmond.

Jambo moja lililowazi, ni kwamba ni rahisi sana kufua na kutakatisha nguo iliyomwagikiwa na tindikali kuliko jina lilochafuka.
 
Mwenye Kiingereza kizito ni David Cameron ndio mwenye Lugha yake. una la zaidi?

achana na ndimu changa hizo

siku hizi JF ni mavuno forum, vitoto vinalipwa kuja kujamba humu na kuchafua hali ya hewa ilimradi watu waache kujadili hoja waishie kijadili viroja vya hawa wapewa token wakati wakuu wenyewe wamelala na kukoroma
 
Lowassa ni:

...Mbunge
...Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
...Waziri Mkuu Mstaafu.
...Mjumbe wa CC na NEC CCM.
...Mtanzania mwenye kuitakia mema nchi yake.

Hivyo, anastahili kupewa coverage ya kutosha na TBC.

Lowassa ni Waziri mkuu wa zamani aliyejiuzuru, siyo waziri mkuu mstaafu kwa vile bado anafanya kazi za kisiasa kama mbunge wa Monduli. Kustaafu kunaashiria kuwa kuachana kabisa na kazi na kuanza kula pensheni. Huwei kustaafu kutoka kwenye cheo cha kuteuliwa ambacho unaweza kuteliwa kukichukua tena; vile vile huwezi kustaafu kwa kulazimishwa. Kwa vile uwaziri mkuu ni cheo cha kisiasa tena cha kuteuliwa, Lowasa hawezi kustaafu uwaziri mkuu na kubaki kuwa mbunge wa monduli kwa vile anaweza kuteuliwa tena. Vile vile akigombea ubunge na kushindwa, bado hataitwa waziri mkuu mstaafu kwa vile hakuacha kwa hiari.

Tanzania tuna wastaafu wachache sana wa kisiasa, ila hatujui. Nyerere ndiye rais pekee aliyestaafu kulingana ka katiba iliyokuwapo wakati wake; Mwinyi na Mkapa hawakustaafu, bali walimaliza muda wao. Kwa mawaziri wakuu, wastaafu ni Nyerere, Kawawa, Salim, Sumaye na Msuya tu; wengine wote ama walicha siasa kwa kushindwa ubunge au kwa kutokuteliwa tena. Sokoine siyo mstaafu kwa vile alifariki wakati akiwa bado yuko kazini.
 
Hapo ameanza kazi. Ulimsikia mayala alivyosema kuwa sasa ni wazi yeye hakuwa na kosa alilinda heshima ya serikali.
 
Sielewi cheo cha sasa cha Edward Lowasa.
Kila taarifa ya habari TBC, lazima aonekane. Je yeye ni mbunge tu wa Monduli au ana cheo kingine kinachompa nguvu ya hizo ziara.
Je yeye ndiye remote controller ya mtawala wa juu wa nchi?
Sielewi inakuwaje mtu ambaye si mwenyekiti wa chama wala kiongozi wa serikari apewe kipaumbele katika habari za kila siku?
Ni Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na usalama kama sikosei,pia ni gamba gumu sana ambalo kubanduka "haliwezekaniki"
 
Back
Top Bottom