fige
JF-Expert Member
- Jul 4, 2010
- 376
- 61
Wiki hii nzima magazetini na hapa kwetu jf pametawaliwa na minyukano mikubwa kati ya aidha wafuasi wa LW na wasio,au wana magamba na wengineo.
Kikubwa kilichoibua mjadala ni jinsi inavyosemekana mh. (ingawa hili neno silipendi) LW alivyowagalagaza magamba wakashindwa kumvua gamba mwenzao.Utetezi wenyewe ni jinsi yeye anavyodai kujaribu kushawishi kuwafukuza Richmond na kwamba Mkulu ndiye aliyemkwaza.
Nimetumia neno kujaribu kwa sababu kwa mtizamo wangu ushauri ule naweza kuuita geresha *****.Nasema hivyo kwa sababu kama alishauri mara moja hajatuonyesha kama aliendelea kusisitiza ushauri wake.
Pili ,inawezekana alikuwa anashauri jambo ambalo yeye mwenyewe haliamini na ndio maana lilikosa msisitizo.
Tatu, ni je baada ya kupuuzwa alichukua hatua gani ?Kama unaweza kupuuzwa katika jambo unaloamini kwa asilimia mia uko sahihi na usichukue hatua yeyote,je sisi wananchi tuendelee kukuamini ulikuwa na nia ya dhati ya kulisimamisha ?
Kwa mawazo yangu LW angejiuzulu kabla ya kuthumiwa kwa kutetea msimamo wake,nina hakika leo hii nchi nzima ingekuwa inampigia chapuo la uraisi hata kama ana mapungufu mengine makubwa.
Mnaomtetea LW pengine hamjaona alipodondokea mnataka kupatambua anapojaribu kusimamia.
Nawasilisha