Ziara za Kikwete hazina Tija kwa Taifa

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
34
Namuomba Rais Jakaya Kikwete asitishe mara moja ziara anazofanya kwenye wizara mbalimbali kwa sababu hazina tija kwa Taifa na zinasababisha hasara kubwa na kupoteza muda wa kazi mwingi kwa wafanyakazi wa wizara anazokuwa anatembelea.

Siku nzima ya jana wafanyakazi wote wa Wizara ya Nishati na Madini hawakufanya chochote wakimsubiri rais aje na alipokuja hakuna kilichofanyika wakisubiri aondoke. Alipoondoka ilikuwa ni mijadala ( unajua watanzania kwa ushabiki wao) jinsi Waziri alivojikanyaga, mikwara ya rais, dowans nk.! fikiria manhours zilizopotea kwa rais kuja wizarani ambako hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia wala kutoka baada ya mkulu kuja.

Kama Kikwete anafikiri ni muhimu kukutana na watendaji wa wizara, anatakiwa awe anawaita ikulu na kuwapa kibano huko huko kuliko kuja ku disrupt kazi zetu za kila siku, vinginevyo inaonekana anatembelea kuja kuuza sura kama afanyavyo anapokwenda huko ughaibuni. Fikiria umati mkubwa uliokaa pale nje ya wizara ukisubiri kumuona, fikiria matatizo aliyosababisha kwa kuzuia magari kupita mtaa wa samora jana, na misongamano aliyoisababisha mjini!
 
hahahahah mkuu sijui nani atakusikiliza?? wazo zuri sana!
 
Mimi naziona ziara hizi kama mwendelezo wa tatizo kubwa ambalo tangu mwanzo wa utawala wake, limekuwa likiathiri utendaji kazi huko serikalini; nalo ni kupindisha kanuni za utawala. Mojawapo ya kanuni muimu kwenye utawala ni kwamba mtu anapashwa awajibike kwenye mamlaka moja tu (unity of command). Kulingana na kanuni hiyo rais hapashwi kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na watumishi wa mawizara kwasababu hawawajibiki kwake. Hivyo kitendo cha kutaka kuwa na mawasiliano na watumishi hao ya moja kwa moja kinawavunja nguvu wasaidizi wao wakuu. Kwa yeyote aliyefuatilia sakata la Dowans atakuwa amebaini chanzo cha sakata hilo ni kwa waziri mkuu na wizara mama ya TANESCO kujichukulia madaraka ya bodi ya shirika hilo. Ni hivi jana tu nimeambiwa ya kwamba hivi sasa Tanroad hairuhusiwi kuingia mkataba wowote wa ujenzi wa barabara mpaka kwanza uidhinishwe na serikali. Mambo yale yale; tangu lini serikali ikawa na umakini kwenye masuala ya mikataba! Lakini vile vile ikiwa serikali inajiingiza moja kwa moja kwenye mambo ya utendaji nani atakayefanya kazi ya usimamizi?
 
naamini baadae ziara hizi zitazaa wajukuu "semina elekezi"huko ngurdoto ama movenpick au kempisiky...2005-2015 drama play in Tanzania
 
naamini baadae ziara hizi zitazaa wajukuu "semina elekezi"huko ngurdoto ama movenpick au kempisiky...2005-2015 drama play in Tanzania
 
Back
Top Bottom