Ziara ya Rais Kikwete Mkoani Tabora

USHIRIKISHWAJI WANANCHI KATIKA KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO
“Tusiwatenge, lakini tuendelee kuwalinda mpaka wimbi la sasa la kuwashambulia litakapopita kwa sababu hilo ni wingi tu la kupita tu. Hawa wajinga wakiona kuwa vidole na nywele za albino hazileti utajiri, wataacha tu,”amesema Rais.

Alikuwa akitoa maelekezo baada ya kuwa ameambiwa kuwa watoto albino katika wilaya hiyo wanasoma katika shule za walemavu wa kuona na kusikia katika wilaya hiyo.

“Tusiwatenge. Kwa sababu kwa kufanya hivyo, tutawatia hofu zaidi,” ameeleza Rais kabla ya kuambia kuwa wanafunzi hao wamewekwa katika shule hizo kwa sababu ya udhaifa wa kuona.
.[/SIZE][/FONT]

Rais wetu, mtu mwenye MADARAkA makubwa sana kikatiba (alisema yeye mwenyewe) katuambia kuwa TUSUBIRI wimbi la KUUWA MA-ALBINO liishe. Kama yanamshinda si abadili katiba na kumpa PM madaraka makubwa zaidi? PM ndiyo afe na wauwa ma-Albino. Wakati mwingine napata wasiwasi kama na yeye Muungwa huko Bagamoyo katika hizo Test Tube za waganga wake wa kiennyeji, haziingii ngozi za zeruzeru. To SAD. So the answer is JUST WAIT. Just wait my son. Just wait my daughter. Time is an answer.
 
USHIRIKISHWAJI WANANCHI KATIKA KUIBUA MIRADI YA MAENDELEO

Viongozi msikwepe wajibu wenu – Rais Kikwete


Na Mwandishi Maalum, Tabora

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa utaratibu wa kuwashirikisha wananchi katika kubuni na kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo usitumiwe na viongozi kama kisingizio cha wao kukwepa wajibu wao wa kuwa chachu ya maendeleo katika nafasi zao za uongozi nchini.

“Hii tabia ya viongozi kudai kuwa wananchi hawajaibua miradi sasa inatumiwa na sisi viongozi kukwepa majukumu yetu kama wakala wa mageuzi ya maisha ya wananchi nchini,” Rais Kikwete amewaambia viongozi wa Wilaya ya Tabora leo, Jumamosi, Oktoba 25, 2008.

Rais ametoa maelekezo hayo kwa viongozi wakati akipokea taarifa ya utendaji ya Wilaya ya Tabora katika siku ya tatu ya ziara yake ya siku nane katika Mkoa wa Tabora wakati alipowasili mjini Tabora akitokea wilaya za Sikonge na Urambo.


Ukifika Wilaya za Tabora na kuona Watu walivyochoka, ndipo utajua KIKWETE alikuwa akisema nini. Cha ajabu, hakuna DC au RC au Mbunge aliyepewa YELLOW CARD au Red card. Wapo wanapeta tu. Sijui Kikwete alijisikiaje kuwa huku Sikonge maana ukiona mji na watu unaamini kabisa kuwa hii ni kama ile miji iliyoandikwa kwenye Biblia kuwa "Yesu alipouna mji AKALIA".
Ukifika Tabora mjini ni Machozi tu kulenga lenga. Kama hakushtushwa basi jamaa kweli MWANA SIASA. Tabora utafikiri tulishiriki KUMUUWa Yesu na laana ya mababu zetu hadi leo tunayo sisi wajukuu zao.
Kibaya zaidi, CCM huku ndiyo imefika. Hata ufanyeje, uwaibie na kuwapiga viboko Wanyamwezi, bado CCM ni yao na wako too Proud na CCM yao. Kama ni usiku wa Mkesha, basi Tabora ndiyo kwanza tupo saa 23. Heri Wazenji wanaweza kudai Kuvunja Muungano, ila sisi bado hatujafikia kuliona hilo. Watanzania wa Mbeya, na Tarime wakiongozwa na Kilimanjaro, naona wao wako hatua kadhaa mbele. Hawa wanahitaji RC mkorofi wa kuchapa viboko Wajinga na Wavivu. Ka-Uarabu tunakapenda sisi Wanyamwezi!!!!
 
Back
Top Bottom