Ziara Pwani Mchangani – Uchunguzi maalum

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130

Written by administrator // 20/05/2011 // Habari // 8 Comments

pwani-mchangani-500x272.jpg

Ally Saleh,
Leo nilikwenda Pwani Mcahangani kibinafsi kutizama hali ilivyo ikiwa ni karibu wiki mbili tokea tukio la kuchomwa moto vibanda vya biashara ambavyo vingi vilikuwa vikitumiwa na watu kutoka Tanzania Bara.
Kwa hakika sina haja ya kuutizama juu ya umiliki, au sababu za kuchomwa moto au nani na nani wameshtakiwa au ambao wanapata au wameelekezwa kupata fidia kwa kadhia hiyo.
Wala sina sababu ya kuhoji mantiki ya wana kijiji ya kuchukua hatua walizochukuwa, ikiwa ilikuwa ni siku moja tu kabla ya Serikali katika ngazi ya kwao kutekeleza amri ya kuvisafisha vibanda hivyo, kwa maana kwamba vyovyote vile maamuzi yalikuwa yameshafanywa kuviondoa.
Sitaki pia kuhoji mantiki ya uamuzi wao wala kupitia tena madai yao kuwa walikuwa wakikereka na vitendo vya uchafu wa ngono, ukahaba, uuazaji wa pombe na hata visa veyngine na hilo wakikazania ni kinyume na maadili yao kama Waislamu, Wazanzibari na wazawa wa eneo hilo.
Ila nimeona kuna mambo mengine makubwa zaidi ambayo ningeak kugawana na wenzangu katika kuwapa uzoefu nilioupata huko leo, baada ya kukaa kijijini kwa kiasi cha saa moja hivi.
  1. Kwanza ni kilio chao kuwa hawakutendewa haki na uongozi wa kitafia wa Zanzibar na hasa malalamiko yao yako wazi wazi kwa Balozi Seif Ali Idd, ambaye alifika kijijini hapo na kuwaona waathirika wa kuchomewa mambanda na moja kwa moja kaamini hadithi ya upande wao, upande mmoja tu wa shillingi.
  2. Wanasikitika zaidi kuwa si yeye Balozi Idd au maafisa wake hadi leo wiki mbili baada ya tukio hilo waliofika kijijini hapo kutaka kujua nini kimetokea hadi hali kufikia ilivyofikia na kwa hilo wanaona kuwa wametengwa wao kama Wazanzibari na wasio Wazanzibari wakipewa kipa umblee. Wameniambia niseme kuwa wanajiona kama “wanaharamu” kwa wanavyofaniwa.
  3. Tatu, ni masikitiko yao makubwa kuwa Mbunge wao Kheri Khatib na Mwakilishi wao Abdi Mossi tokea tukio hilo hawajafika kijijini hapo kwa ajili ya kukaa pamoja na wananchi kujadili suala hilo.
  4. Japo wanakiri kwamba walitoa kila mmoja wao shillingi 500,000 na kufanya millioni 1 kwa ajili ya kupewa wakili Abdulla Juma lakini wamesema wangetaraji kuwa Mbunge na Mwakilishi wangeshuka Jimboni kuja kuzungumza nao na chochote cha maamuzi kitokane na mchango wa wapiga kura wao.
  5. Wamemshukuru sana Diwani wa eneo lao ambaye wamekuwa nae kila wakati, bila ya kuogopa kuonekana yupo pamoja nao, na pengine anawaunga mkono, lakini hoja yao ni kuwa uamuzi ulikuwa ni wana kijiji na kila mwana kijiji yuko tayari kubeba dhamana na hakuna sababu ya Mbung au Muwakilishi kuogopa kukutana nao.
  6. Kwamba wamesikitishwa na chombo cha habari cha Serikali yaani Sauti ya Tanzania Zanzibar kuamua kutengeneza mazungumzo baada ya habari makhsusi kabisa kuwalaumu na kuwashutumu na hadi kusema kitendo kilichofanywa ni cha “kishenzi” ilhali wananchi hao hawapewi fursa ya kujibu – right to reply.
  7. Wamekosoa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilikuwa na vimekuwa vikiandika habari za tukio hilo bila kutaka kujua upande waona kwa hivyo kuupa nguvu upande mmoja wa tukio hilo na tayari kuhukumiwa kwa kitendo hicho.
  8. Walinionyesha katika kuthibitisha kuwa hawana chuki na watu kutoka Tanzania Bara maeneo mbali mbali ambayo Wabongo wamekuwa wakiendelea kukodi na kufanyia biashara na wengine wakikaa katika nyumba wanzo kodishwa na wazawa na wazawa wenyewe wakiwemo humo humo.
  9. Walionyesha wasi wasi wao kuwa familia za watu ambao wako ndani yaani watu saba hazijapata msaada wa kundi kubwa la watoto na wake zao, kwa njia bora zaidi, isipokuwa kuungwa mkono na wana kijiji kutokana na utamaduni wao wa kusaidiana.
  10. Kwa jumla kuna wake saba na watoto 28 wa umri mbali mbali na baadhi yao wakiwa na umri wa kwenda skuli.
  11. Kesi ya washtakiwa inakwenda tena Mahakamani Jumatatu na kuna uwezekano watuhumiwa wakarudishwa tena rumande na hii ikiashiria kuwa kunaweza kutokea matatizo ya kiutu kwa familia za watu hao walioko ndani.
 
hawana lolote na sababu zao hazina mashiko, kwani wao ndo binadamu zaidi kuliko wenzao, kwani hao wahanga wa tukio hilo hawana familia? jinsi walivojazana watu 40 vyumba viwili ndo utu huo? hakuna sababu yoyote ambayo wataieleza ili kuweza kujustify uhuni na ushenzi waliowafanyia wenzao! hawa watu ni wabaguzi,wana wivu, wamefilisika hekma na busara, wana udini uliokithiri kiasi kwamba wanabagua hata waislam wenzao kwa kuwa tu wametokea bara! nasema tena hawa jamaa ni wahuni na washenzi hawafai hata kusikilizwa maana hawajui hata utawala wa sheria! hizo sababu wanazotoa wanakijiji wakaziseme kama ushahidi mahakamani iwapo wanaamini ndipo haki itakapopatikana, hofu ya nini? utu na ubinadam wanaona kwa upande wao tu lakini upande wa pili hawaoni! hakuna kitendo kilichonikera kama hiki kilichofanywa na hawa washenzi, na hisia zangu zinapelekea kuhisi kwamba hata ngazi fulani ya uongozi ilitoa baraka zake kwa kitendo hicho kinachostahili laana zote kubwa, na iko siku moto utakapowaka huko kwao ndipo watakapoona m'bara ni rafiki zaidi kuliko mzenj mwenzake. Time will tell!
 
Uzushi mtupu huu wako.

Kwanini walale arubaini chumba kimoja, kwani wakilala humo vibandani?

Mbona wabara wako sehemu nyingi tu na hawajachomewa wala hawajabughudhiwa kwa namna yoyote ile?

Hao waliletwa baada ya moto ili kujenga ajenda ya kisiasa ili wapate kufifisha hisia za Wazanzibari kuhusu Muungano na ndio maana vyombo vya habari vinatumiwa kushupalia jambo hili.

Huna hoja ila chuki binafsi na wivu uliokithiri.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
Back
Top Bottom