ZIARA: Mawaziri na manaibu wote..waenda mikoani kuisafisha serikali

wamezomewa tena leo kule songea,kazi ipo naamini kuwa mwisho wa kuzomea ni watu kuamua kuwahukumu mafisadi hawa wenyewe kwani ni vibaka hawa,
 
wamezomewa tena leo kule songea,kazi ipo naamini kuwa mwisho wa kuzomea ni watu kuamua kuwahukumu mafisadi hawa wenyewe kwani ni vibaka hawa,


Haki sawa hebu tupe hizo nyepesi kwa undani zaidi yaliyo jiri huko Songea! Hii inatia moyo sana..
 
Wananchi wamekwisha gundua kwamba corrupt government ya JK haiwezi kuwapa maisha bora na nyota njema imeshachomoza mapambano yameanza na mafisadi wanatetema kwa kukurupuka.
 
Alamu za nyakati:

1. JK alizuiwa kuingia Buzwagi kwenye mgodi na WTZ ambao hawapendezwi na serikali yake katika mikataba mibovu.

2. EL ameshindwa kujibu swala la mtoto wa shule ya sekondari.

3. EL kukimbia mkutano wa hadhara kwenye mgodi mkubwa wa Geita.

4. Ngeleja (naibu waziri wa madini) Azomewa jimboni kwake Sengerema

5. Ngeleja azomewa Geita

6. Mbeya mawaziri wazomewa bila huruma

7. ......................................

8. ......................................


The litany continues, guess what's next?........... I wonder!
 
MAISHA BORA ILIKUWA CAMPAGNE LADDER..MAANA NASHANGAA SASA HIVII KILA WAZIRI ANAKAZANA KUWAAMBIA WANANCHI KWA KEJELI KUWA ..MAISHA BORA HAYASHUKI TOKA MBINGUNI KAMA MANA"ref lowassa..mwanza.batilda burian tabora et al...

mimi nabaki kujiuliza kama walijua maisha bora hayaji kama mvua..wangetuambia tangu wakati wa kampeni..ili watu wajue..i think the proper campagne slogan ingekuwa"" MAISHA BORA YANALETWA NA KAZI" yes hata nyerere alisema "uhuru na kazi" kwa usemi huu wa mwalimu wananchi walikuwa wavumilivu wakijua uhuru haikuwa sababu yoyote ya kupata raha..bali kazi ndio msingi wa maendeleo... angekuwa kikwete angesema "uhuru na maisha bora"
 
Waona Wizara zetu zinaongezewa mamilioni tuu kila siku

World Bank approves US$40m for Tanzania’s Performance Results and
Accountability Project

WASHINGTON, DC, October 2, 2007 The World Bank Board of Executive Directors on September 27, approved an International Development Association (IDA)credit* of US$40 million for the Government of Tanzania's Performance Results and Accountability Project (PRAP).

The PRAP, whose theme is Demanding results and accountability,
will aim at enhancing the capacity, performance and accountability of government ministries, departments and agencies in the use of public resources and service delivery. The project will ensure timely and effective implementation of strategic and priority programs, which will contribute to the achievement of the National Strategy for Growth and Reduction of Poverty (MKUKUTA) goals.

We in the World Bank are pleased to be associated with the
Government of Tanzania’s efforts to improve the performance of the public service.
http://web.worldbank.org/external/projects/main?pagePK=64283627&piPK=73230&theSi
 
Hamjanijibu swali langu kuwa hizo ziara zipo ktk priorities za serikali tangu awali?? na ni bajeti au kasma ipi inatumika kugharimia hizo ziara za kuupaka uongo rangi??

Tena kwa kuwa majibu ya serikali yapo ktk vipande vipande basi nadhani serikali ipo ktk state ya vipande vipande... Mafisadi lazima wastaafishwe na sheria ichukue sura yake...

...wakuu nilikuwa mbaaaali na network kwa kitambo sasa lakini nitatengemaa hivi karibuni..
 
Alamu za nyakati:

1. JK alizuiwa kuingia Buzwagi kwenye mgodi na WTZ ambao hawapendezwi na serikali yake katika mikataba mibovu.

2. EL ameshindwa kujibu swala la mtoto wa shule ya sekondari.

3. EL kukimbia mkutano wa hadhara kwenye mgodi mkubwa wa Geita.

4. Ngeleja (naibu waziri wa madini) Azomewa jimboni kwake Sengerema

5. Ngeleja azomewa Geita

6. Mbeya mawaziri wazomewa bila huruma

7. ......................................

8. ......................................


The litany continues guess what next?........... I wonder!

Next itakuwa jamaa kugundua kwamba wananchi wamechoka na usanii wao na ujumbe wao haukubaliki hivyo inabidi wabadili mwelekeo, lakini sidhani kama wana uwezo wowote wa kubadili mwelekeo.

Ukiwa kama kiongozi wa nchi na timu yako halafu kila unapojaribu kuongea na wale unawaongoza na wao wanakuzomea inabidi ukubali something is very wrong somewhere and you have to be ready to change the tune that will be acceptable to your countrymen and women. Tulisema ni silaha ya mnyonge lakini inaelekea kupamba moto katika kila kona ya Tanzania very soon jamaa watayakimbia majukwaa maana wanajua watazomewa tu.
 
Wananchi waiponda ziara ya mawaziri

* Wasema inaongeza mzigo kwa walipakodi
* Tathmini yaonyesha zaidi ya Sh100m kuteketea

Chanzo: Mwananchi

WANANCHI kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wameiponda na kuipinga ziara ya mawaziri kuwa haina cha ziada zaidi ya kuongeza gharama kwa serikali.

Ziara hiyo ambayo imekuwa ni ya machungu kwa baadhi ya mawaziri baada ya wananchi kuwazomea na kuwataka kushughulikia matatizo ya wananchi na siyo kufanya ziara ya kuelezea matumizi ya bajeti.

Wengi wa wananchi waliotoa maoni yao, wamelalamikia matatizo yanayowakabili ambayo wanadai serikali imeshindwa kuyatatua.

Pia wamelalamikia gharama ambazo mawaziri wanazitumia kuwa fedha hizo za mizunguko yao zingeweza kuwasaidia wananchi badala ya kusubiri misaada kutoka kwa nchi wahisani au kwa watu binafsi.

Habari zilizopatikana kutoka serikalini zinaeleza kuwa karibu mawaziri wote na manaibu wao 60 wapo mikoani wakiwa wameambatana na wasaidizi wao, maafisa habari na madereva na baadhi ya waandishi wa habari, wote wanaofikia 118 kutoka katika wizara 29 wanalipwa posho na serikali kwa kipindi cha siku 10.

Ukiondoa posho za mawaziri ambazo ni za viwango maalum, maafisa wengine walioambatana nao wanalipwa kati ya Sh45,000 na 55,000 kwa siku, lakini katika baadhi ya maeneo wanakuta halmashauri za wilaya, ofisi za wakuu wa wilaya na mikoa zimeshalipia gharama za malazi.

Mbali na posho hizo, baadhi ya mawaziri na wasaidizi wao, wamelipiwa usafiri wa ndege kwenda na kurudi katika mikoa husika, ile ya mbali nauli ni zaidi ya Sh400,000 kwa tiketi ya ndege kwenda na kurudi Dar es Salaam.

Gharama nyingine ni mafuta ya magari ambayo wanatumia mawaziri hao. Gharama inategemea umbali wa safari ambayo ataifanya waziri.

Chanzo chetu kutoka serikalini kimesema ukijumlisha gharama hizo ambazo zimetolewa kwa kila wizara kujitegemea, si ajabu zikazidi Sh100 milioni.

Juma Salum kutoka Temeke jijini Dar es Salaam alisema, "Kwa kweli hii ziara ya mawaziri na lengo lao inasikitisha. Katika hospitali ya Temeke wagonjwa wodi ya kinamama wanalala zaidi ya mmoja kitandani, na wengine wanalala sakafuni. Hata Binti Mfalme wa Ubeligiji amejionea mwenyewe.

"Sina hakika vipaumbele vya serikali hii viko katika mpangilio gani, lakini huenda gharama ya waziri mmoja katika kuzunguka huko mikoani inatosha kununua vitanda zaidi ya kumi, ili kupunguza adha ambayo wagonjwa wanapata katika hospitali hii na nyingine hapa nchini".

Kwa upande wake Gideon Swalle wa Mafinga, Iringa alisema katika barua pepe, "...hapa serikali na CCM wamepigwa bao la kisigino na mawaziri. Ziara hii inatumiwa na hawa mawaziri ambao ni makada wa CCM kukamilisha kampeni zao za kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM katika uchaguzi mkuu mwezi huu".


Alisema wengi wa mawaziri wanaozunguka nchini hivi sasa ni makada wa CCM wanagombea nafasi katika NEC ambao wanatumia fursa hiyo kujinadi mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kote wanakopita ili wawachague.

Naye Alisa John mkazi wa Karatu, Arusha alisema hajafurahishwa na ziara hizo kwani amejaribu kuhudhuria na kuwasikiliza baadhi ya mawaziri ambao wanaeleza mikakati mizuri bila kueleza ni lini itatekelezwa.

"Wanaongelea yale mazuri tu, lakini hawatumii nafasi hiyo kutueleza masuala ya mikataba na mambo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT)...wananchi tunaumia wao wanafanya ziara ya kueleza bajeti? Ladha ya bajeti tunatakiwa kuiona kwa matendo kwa kupunguza bei ya mafuta na si kwa kutumia mafedha na maposho mengi pasipo suluhisho," alisema John.

Msomaji mwingine wa Mwananchi, Kakuru Mtembezi kutoka Tanga yeye aliuliza swali, "Hiyo misafara ya mawaziri huko mikoani ni gharama ya nani? Je wanapewa posho au hawapewi na mafuta wanayoyaunguza ni ya nani?

Alisema kama gharama hizo ni kutokana na kodi za wananchi, fedha hizo zinapotea bure maana yeye haoni chochote wanachofanya kumuondolea Mtanzania umasikini alionao.

Mwingine aliyezungumzia ziara hiyo ni Nancy Athuman mkazi wa Kisarawe, Pwani alisema yeye anaona viongozi hawa wanaelekea pabaya sasa, kampeni za kuwaelezea wananchi habari ya bajeti hazifai na badala yake wangeeleza wananchi nini kifanyike ili waweze kuishi maisha bora waliyoahidiwa.

"Wafanye kazi ionekane kwa kila mtu na si kuzitumia tena kodi za wananchi kuzunguka mikoani. Hizo fedha wazitumie kujenga shule kwa wanafunzi wa Kisarawe ambao wanakaa chini ya miti kwa kukosa madarasa na viti vya kukalia? Hivi Rais hana washauri?" anahoji Athuman.

Aliongeza kuwa mwananchi hahitaji kuelezwa kama bajeti ni nzuri au la, anatakiwa aone mabadiliko katika eneo alipo; barabara nzuri, shule nzuri, kituo cha afya au zahanati nzuri.

"Usijekuta gharama za ziara ya mawaziri zingetosha kununua vyandarua kadhaa kwa ajili ya kuwakinga watoto wadogo na malaria," anasema.
 
Gharama zote ni zaidi ya sh billioni 2,naona hiyo million 100 ni kiasi kidogo,hakitatosha kwa siku 10.
 
mh, huyu mshauri wa serikali sijui nimwitaje1
sisiem wanacheza mpira wa hatari, na ninaamini mwisho wa mechi (2010) either ngoma itakuwa droo au wakishinda refa ujue kawabeba.

Haiwezekani jinsi wananchi wanavyolalamika wao waibuke na ziara ya nchi nzima, wacha wajionee wenyewe ugumu wa maisha na chuki waliyonayo wananchi kwa kuwazomea, labda watajifunza kitu bunge lijalo.

Aluta kontinua.....
 
Nakumbuka wakati wa kipindi cha bunge kilichopita asilimia kubwa ya wabunge walikuwa wanatoa malalamishi na kusema wangeomba mawaziri waende wakasikilize vilio vya wananchi wenyewe ili wajue uchungu na wakati wa bajeti wajue kwanini Rombo na Sio Namtumbo etc... au kwa nini shule na sio afya kwenye vipa umbele...

Nakumbuka maswali kama hili au la aina hii yalikuwa mengi sana kutoka kwa wabunge wa majimbo!

"Mheshimiwa spika, Je waziri atakubaliana nami aje mwenyewe auone na kuwajibu wananchi kero zao mwenyewe maana mimi sina cha kuwaeleza tena? na mimi nitamngoja na kumuandalia malazi kule kijijini kwetu?"

Sasa Mawaziri hao,,, issue tena,,, nadhani ni kwa kuwa wameenda wakati Mh. Zitto, Mrema, Mbowe etc. kwenda huko,,, kama isingekuwa hivyo nadhani ingekuwa serikali inasikiliza na Wabunge wangewapongeza...

Ndio siasa za TZ!

Kwa maoni yangu ziara zimekuwa za mafanikio, maana upinzani waliopata wakikaa kwenye baraza la mawaziri au kwenye vikao vyao vya ndani watajua nini maana ya kuhitaji kuwa makini zaidi na jamii ya kitanzania inabadilika kwa kasi kubwa na tekohama ya mtandao inavyobadilika...

Hayo ndio maoni yangu!
 
Kiltime , mbona sasa hatuoni wanapo eleza hiyo bajeti kwa ufundi ila wana hangaika kuwataka Watanzania kuachana na habari za Slaa na Zitto ama majina haya 2 yalikuwa muhimu katika bajeti yetu ?Au ndiyo source ya ubaya wa bajeti ?
 
naona muungwana ameingia dar..kapokewa na mamia ya wana ccm chini ya kamati ya ,maandalizi ya mapokezi ikiongozwa na kandoro...watu wamechukuliwa vingunguti ,na maeneo mengine wamepewa elfu tano tano na fulana ...usanii ni pale walipokuwa wanahojiwa baadhi ya watu wa hapa dar..mwingine anasema katoka iringa kuja kumlaki jk,na jamaa mmoja msanii anayeshinda hapo steers ..tunamjua anasema katoka tanga special kuja kumlaki jk...kwa nini tunadanganyana???
 
Nakumbuka wakati wa kipindi cha bunge kilichopita asilimia kubwa ya wabunge walikuwa wanatoa malalamishi na kusema wangeomba mawaziri waende wakasikilize vilio vya wananchi wenyewe ili wajue uchungu na wakati wa bajeti wajue kwanini Rombo na Sio Namtumbo etc... au kwa nini shule na sio afya kwenye vipa umbele...

Nakumbuka maswali kama hili au la aina hii yalikuwa mengi sana kutoka kwa wabunge wa majimbo!

"Mheshimiwa spika, Je waziri atakubaliana nami aje mwenyewe auone na kuwajibu wananchi kero zao mwenyewe maana mimi sina cha kuwaeleza tena? na mimi nitamngoja na kumuandalia malazi kule kijijini kwetu?"

Sasa Mawaziri hao,,, issue tena,,, nadhani ni kwa kuwa wameenda wakati Mh. Zitto, Mrema, Mbowe etc. kwenda huko,,, kama isingekuwa hivyo nadhani ingekuwa serikali inasikiliza na Wabunge wangewapongeza...

Ndio siasa za TZ!

Kwa maoni yangu ziara zimekuwa za mafanikio, maana upinzani waliopata wakikaa kwenye baraza la mawaziri au kwenye vikao vyao vya ndani watajua nini maana ya kuhitaji kuwa makini zaidi na jamii ya kitanzania inabadilika kwa kasi kubwa na tekohama ya mtandao inavyobadilika...

Hayo ndio maoni yangu!



Strong points!
 
Back
Top Bottom