Zengwe la madaktari bingwa na serikali

Tumechaoka, kila kukicha ni issues za maslahi ya madaktari.... kwani wao tu ndio muhimu jamani??

Hawa wanataaluma wamegeuka wauaji, wanashabikia watu kufa. Wameshapoteza maisha ya wengi kwenye mgomo wao wa mwanzo lakini bado wana hamu ya kuondoa roho zingine. Wamenogewa kuua.

Laana iko juu yenu, kwa kutanguliza ulafi wenu wa pesa na kupigania kushibisha matumbo yenu ....kwa kutoa kafara roho za binaadam wenzenu.

usilolijua ni kama usiku wa kiza, mara zote utaishia kuchangia mambo kwa kuyaangalia juu juu tu bila kujua undani wake, kumbuka no research no right to speak and conclude on your own!!! mi napita tu!!!!
 
Ni wakati sasa wa kushirikisha na kushirikiana na taasisi/idara nyingine za serikali (siyo hao wanasiasa)na kuweka maazimio ya pamoja yatakayokuwa yana-favour kotekote kulingana na majukumu ya kila mtumishi kwa nafasi yake. Tunaona jinsi madaktari wanavyo pambana kudai haki zao za kimsingi, na madai yao si ya leo wala jana lkn bado muhafaka haupatikani:
tatizo ni nini!!!
-Madai yao si ya msingi??
-Serikali haina uwezo??
-Madaktari hawana umuhimu??
-Watumishi wengine wa umma mambo yao yako supa???
Obviuosly JIBU ni HAPANA.
Sasa kinachosubiliwa ni nini USHIRIKIANO WA PAMOJA UNAITAJIKA ili kuonyesha msisitizo ktk kile Madaktari wanachopigania miaka yote: nina Imani Serikali yetu uwezo inao na nia ya Serikali si kukumbatia na kulea MIGOMO bali ni kuhakikkisha Amani inakuwepo.
 
Hapo penye nyekundu mimi ndipo ninaposhangaa...kuna watu wengine wanalaumu maDaktari eti wanajifanya special, kivipi? Kinachodaiwa si uspecial, kinachodaiwa ni stahiki za Daktari kwa thamani ya fani yake. Kila fani ina jukumu la kuset thamani yake yenyewe...maDaktari hawawezi kuset thamani ya Nurse, Pharmacist, Engineer, Mwalimu au fani nyingine yeyote..kwa hiyo hawawezi kuwa na madai yanayocut across fani zote! Kila mtu ajitetee kivyake kama maDaktari wanavyokukuluka kivyao...hiyo siyo sababu ya kuwabeza eti kisa tu walifundishwa na walimu basi walimu ni bora zaidi mbona hawagomi! Kama kuna mtu au fani imeridhika na inachokipata, au wana njia mbadala ya kumudu maisha basi heri yao...sie wacho tugome tudai stahiki yetu halali! Kama kuna fani inayoona nayo inapunjwa kutokana na thamani waliyojitengea wademonstrate kivyao..si kubeza maDaktari. watu kama wangekuwa wana moyo wa kimageuzi, wangeona hii struggle ya maDaktari kama opportunity ya mageuzi ya kitaifa kwa kila kada..lakini wako kimyaa wanakalia kubeza maDaktari and call them all the st^pid names!
 
Well said Riwa...inasikitisha mara nyingine kuona watu wanavyowafikiria madaktari kama wasaliti au eti si wazalendo..inashangaza kuona watu wanavyoshindwa kuona kuwa madaktari lengo lao kimsingi ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa watanzania wote popote pale walipo....watu wanashindwa kutambua kuwa madaktari wakiboreshewa stahiki zao na pia mazingira yao ya utendaji kazi hakutakuwa tena na sababu ya daktari kukataa kwenda kufanya kazi vijijini, pia hakutakuwa tena na sababu ya daktari kuacha kituo cha kazi mapema na kwenda kuwahi kufanya kazi part time...haya yoote hayatatokea kama kilio cha madaktari kitasikilizwa na mwisho wa siku atakaefaidi kwa kupata huduma bora ni mtanzania.....sasa hivi madaktari wanakatishwa tamaa na serikali hii......moja ya athari itakayotokana na serikali kutowasikiliza madaktari ni pamoja na madaktari kuacha tiba na kuingia kwenye sekta ya research and development ndani na nje ya nchi....jambo ambalo serikali hawajalitambua bado....watasomesha madaktari lakini hawatawaona kwenye tiba....
Angalizo kwa serikali: Muda wa ubabishaji na siasa umeisha kwenye issue ya madaktari.....kinachotakiwa ni utekelezaji tu wa makubaliano....madaktari si watoto bali wanajua tatizo liko wapi.....ubabaishaji wa serikali hii utaimaliza TZ...
 
Kwanini ni serikali inahitaji kuwatambua kuwa ni maspecialist? je MAT wanawatambua?

Mzee Mwanakijiji, heshima kwako...(nimetanguliza heshima kwani pamoja na kuheshimu wanaJF wote, wewe una heshima ya ziada toka kwangu!)

Kuna kutambulika kwa namna tofauti, lakini ambazo nazirecall haraka haraka ni kutambulika academically, kwamba Daktari amehitimu level fulani ya kitaaluma mfano Masters, PhD etc...hilo ni jukumu la academic boards! Lakini pia kuna kutambulika kwa stahiki zako, kwamba umehitimu level fulani ya elimu/utaalamu basi daraja lako la kazi litapanda, na kutokana na hilo basi majukumu yako yanapanda na kuwa makubwa zaidi, na pia stahiki zako zinapanda (mshahara na marupurupu mengine)!

Tatizo la Wizara ya Afya katika sakata hili la maDaktari bingwa (specialists) ni kuwa...hawa mabingwa baada ya kuhitimu katika level ya Masters, wanatambulika kitaaluma na kupangiwa majukumu makubwa ya level ya specialist, lakini hawapandishwi daraja, kwani kwa kufanya hivyo stahiki zao nazo zitapanda. Sasa taasisi za kitaaluma zishafanya jukumu lao, lakini serikali haitaki kufanya jukumu lake la kuwapandisha madaraja na kuwalipa stahiki husika...na inachukua muda mrefu mabingwa wakifanya kazi kama mabingwa lakini mshahara na marupurupu ni wa Daktari 'general practitioner', na anapopandishwa hilo daraja, hawalipwi malimbikizo yao tangu walipoanza kazi kama mabingwa....huu ni uonevu na wizi!
 
Hapo penye nyekundu mimi ndipo ninaposhangaa...kuna watu wengine wanalaumu maDaktari eti wanajifanya special, kivipi? Kinachodaiwa si uspecial, kinachodaiwa ni stahiki za Daktari kwa thamani ya fani yake. Kila fani ina jukumu la kuset thamani yake yenyewe...maDaktari hawawezi kuset thamani ya Nurse, Pharmacist, Engineer, Mwalimu au fani nyingine yeyote..kwa hiyo hawawezi kuwa na madai yanayocut across fani zote! Kila mtu ajitetee kivyake kama maDaktari wanavyokukuluka kivyao...hiyo siyo sababu ya kuwabeza eti kisa tu walifundishwa na walimu basi walimu ni bora zaidi mbona hawagomi! Kama kuna mtu au fani imeridhika na inachokipata, au wana njia mbadala ya kumudu maisha basi heri yao...sie wacho tugome tudai stahiki yetu halali! Kama kuna fani inayoona nayo inapunjwa kutokana na thamani waliyojitengea wademonstrate kivyao..si kubeza maDaktari. watu kama wangekuwa wana moyo wa kimageuzi, wangeona hii struggle ya maDaktari kama opportunity ya mageuzi ya kitaifa kwa kila kada..lakini wako kimyaa wanakalia kubeza maDaktari and call them all the st^pid names!
ktk hili: bila kada nyingine Ku-Sympathize MaDaktari wataendelea kupigwa danadana, ukisema kila kada ipambane kivyake majibu hayatapatikana kwa uharaka zaidi ya kukimbizana tu, na ukumbuke kuwa mgomo ukiendelea anaye umia si Mwajiri(serikali) bali ni Mwananchi wa kawaida kabisa:
Haya endelea na yenu:
-MaEngineer
-Walimu,
-Wanasheria,
-Wahasibu,na
-Maafisa wa kada nyingine ktk ngazi za kiutawala nao watakuja kivyao bwana.
 
Nakubalina nawe PrN-Kazi 100/100 kwamba tunahitaji kada zote zije pamoja na kuraise issue moja tu...maslahi na maboresho ya mazingira yao ya kazi huko waliko ili kutoa huduma au uzalishaji kwa kiwango cha juu. Lakinin kama watu wengine hawataki kwa sababu tu wana njia m'badala ya kumudu maisha (angalia TRA, TANROADS, TICTS, Accountants, Banking industry etc), hawa wote wanagenerate hela kibiashara....hospitali ya Taifa muhimbili na hospitali nyingine (Bugando, KCMC, Mbeya referral, CCBRT, regional hospitals, district hospitals etc) zinatoa huduma tuu, hazigenerate hela...si kwamba haziwezi, zinaweza kwa kuwatoba gharama kubwa kwenye matibabu...sasa m'badala wa kumudu maisha ni kuchukua rushwa (hak'ya mungu hakuna kitu kibaya na kinachouma kwa Daktari kama kulazimika kuchukua au kuomba rushwa kwa toka kwa mgonjwa!). Au tutoe mimba? Tuibe dawa? Tusilale makwetu na familia zetu kila siku kwenda kulala zamu kwenye hospitali za waHindi? Tufanyaje nasi tumudu masiha bila kujali mshahara mdogo? Walimu, maNesi, maFamasia, wataalamu wa maabara ni wenzetu katika hili...wanasita kuungana nasi katika hili, hatuwezi kuwalazimisha...
 
Sio tu ni kazi ngumu jamani hii kazi ina torture physical and pyschological aspects za wahudumu wa afya

1. Pricks na zama hizi za HIV (Hata kama prophylaxis zipo)
2. Kuona mgonjwa anakufa kwa kukosa dawa au vifaa tiba na ujuzi unao
3. Sometimes unatoa pesa yako mfukoni kuokoa jahazi lisizame mgonjwa apate dawa
4. Imagine in a night shift unawitness binadamu wenzako say watatu wanakata roho....hapo hata ukirudi nyumbani asubuhi unakuwa psychologically disturbed sana tu
5. Mentioning just a few (ethics)

I once experienced and attended a patient with a "third degree tear" kijijini, ambulance haina mafuta.....Tazara hiyo ndo mpaka itoke Zambia na express ishapita zake....cutgut zikaisha usiku wa manane in a midst of the procedure I had kuendeshwa kwa bicycle na mume wa mzazi kufuata nyingine ili kumalizia kushona. Will neva forget that night.... halafu mtu ukaongeze ujuzi kweli usitambulike (kama kweli waraka umetoka)

Jamani mlio responsible please please hebu na mtende yaliyo muhimu ili kuwafanya wanaostahili kupata haki zao ili kuepuka kupoteza roho kama wakati wa mgomo wa kwanza...Chonde chonde

kinachomfanya mtu kuwa Dakitari bingwa ni kuhitimu masomo ya huo udakitari au kutambuliwa na serikali? mbona hawa jamaa wamezidi na mizengwe hilo nalo nila kujadiliana jamani ? kwa mfano mtu anahitimu shahada yake ya ualimu halafu serikali iseme huyo si mwalimu hadi hapo serikali itakapo mtambua hii kali kwa nn sasa wasiwe wanawatambua vibaraka wao ili wawe madakitari bindwa kama wanadhani ili uwe dakitari bingwa ni lazima utambuliwe na serikali. je kutambuliwa na serikalini kigezo cha mtu ili awe dakitari bingwa?
 
Hapo mkuu ni kama graduate wa Account na CPA holder vile...hope yu get it
 
kinachomfanya mtu kuwa Dakitari bingwa ni kuhitimu masomo ya huo udakitari au kutambuliwa na serikali? mbona hawa jamaa wamezidi na mizengwe hilo nalo nila kujadiliana jamani ? kwa mfano mtu anahitimu shahada yake ya ualimu halafu serikali iseme huyo si mwalimu hadi hapo serikali itakapo mtambua hii kali kwa nn sasa wasiwe wanawatambua vibaraka wao ili wawe madakitari bindwa kama wanadhani ili uwe dakitari bingwa ni lazima utambuliwe na serikali. je kutambuliwa na serikalini kigezo cha mtu ili awe dakitari bingwa?

NADHANI WEWE UMEKURUPUKA TU KUCHANGIA BILA KUANGALIA MICHANGO ILIYOPITA...HAPO CHINI NI UFAFANUZI KUJIBU HOJA YA MZEE MWANAKIJIJI AMBAYO INAFANANA NA YAKO KWENYE THREAD HII HII:

Kuna kutambulika kwa namna tofauti, lakini ambazo nazirecall haraka haraka ni kutambulika academically, kwamba Daktari amehitimu level fulani ya kitaaluma mfano Masters, PhD etc...hilo ni jukumu la academic boards! Lakini pia kuna kutambulika kwa stahiki zako, kwamba umehitimu level fulani ya elimu/utaalamu basi daraja lako la kazi litapanda, na kutokana na hilo basi majukumu yako yanapanda na kuwa makubwa zaidi, na pia stahiki zako zinapanda (mshahara na marupurupu mengine)!

Tatizo la Wizara ya Afya katika sakata hili la maDaktari bingwa (specialists) ni kuwa...hawa mabingwa baada ya kuhitimu katika level ya Masters, wanatambulika kitaaluma na kupangiwa majukumu makubwa ya level ya specialist, lakini hawapandishwi daraja, kwani kwa kufanya hivyo stahiki zao nazo zitapanda. Sasa taasisi za kitaaluma zishafanya jukumu lao, lakini serikali haitaki kufanya jukumu lake la kuwapandisha madaraja na kuwalipa stahiki husika...na inachukua muda mrefu mabingwa wakifanya kazi kama mabingwa lakini mshahara na marupurupu ni wa Daktari 'general practitioner', na anapopandishwa hilo daraja, hawalipwi malimbikizo yao tangu walipoanza kazi kama mabingwa....huu ni uonevu na wizi!
 
Itafika kipindi fani ya udaktari itakimbiwa ss sijui tunaenda mbele au tunarudi nyuma mi siielewi hii serikali isiyo sikivu
Hata sekta ya Ualimu walianza nayo hivyo hivyo mpaka sasa imefikia kudharaulika kiasi cha mtoto kutamani kuwa mwana Bongo fleva kuliko kutamani kuwa mwalimu. Huko ndiko udaktari nako wanakokuelekeza
 
Nakubalina nawe PrN-Kazi 100/100 kwamba tunahitaji kada zote zije pamoja na kuraise issue moja tu...maslahi na maboresho ya mazingira yao ya kazi huko waliko ili kutoa huduma au uzalishaji kwa kiwango cha juu. Lakinin kama watu wengine hawataki kwa sababu tu wana njia m'badala ya kumudu maisha (angalia TRA, TANROADS, TICTS, Accountants, Banking industry etc), hawa wote wanagenerate hela kibiashara....hospitali ya Taifa muhimbili na hospitali nyingine (Bugando, KCMC, Mbeya referral, CCBRT, regional hospitals, district hospitals etc) zinatoa huduma tuu, hazigenerate hela...si kwamba haziwezi, zinaweza kwa kuwatoba gharama kubwa kwenye matibabu...sasa m'badala wa kumudu maisha ni kuchukua rushwa (hak'ya mungu hakuna kitu kibaya na kinachouma kwa Daktari kama kulazimika kuchukua au kuomba rushwa kwa toka kwa mgonjwa!). Au tutoe mimba? Tuibe dawa? Tusilale makwetu na familia zetu kila siku kwenda kulala zamu kwenye hospitali za waHindi? Tufanyaje nasi tumudu masiha bila kujali mshahara mdogo? Walimu, maNesi, maFamasia, wataalamu wa maabara ni wenzetu katika hili...wanasita kuungana nasi katika hili, hatuwezi kuwalazimisha...

Mkuu pole sana hapo kwenye nyekundu maana hata wagonjwa inawaumiza sana maana mtu huna hili wala lile unapata ajali halafu unafika MOI unapata tu sindano ya maumivu na drip halafu wanakuangalia maana wanasema kunamsululu mrefu wa wanaofanyiwa operation pia vifaa ni vichache au hamna hivyo inabidi usubili hata siku mbili tatu ingawa umepata ajali ya kuvunjika miguu. Watu wanaamua kutoa rushwa ili wapate priority ya huduma hivyo kusababisha madaktari kukimbilia kuwapa huduma waliotoa rushwa na kuwaacha wengine ambao pengine ni mahututi zaidi.
 
kinachomfanya mtu kuwa Dakitari bingwa ni kuhitimu masomo ya huo udakitari au kutambuliwa na serikali? mbona hawa jamaa wamezidi na mizengwe hilo nalo nila kujadiliana jamani ? kwa mfano mtu anahitimu shahada yake ya ualimu halafu serikali iseme huyo si mwalimu hadi hapo serikali itakapo mtambua hii kali kwa nn sasa wasiwe wanawatambua vibaraka wao ili wawe madakitari bindwa kama wanadhani ili uwe dakitari bingwa ni lazima utambuliwe na serikali. je kutambuliwa na serikalini kigezo cha mtu ili awe dakitari bingwa?
Mkuu jaribu kuwa unapitia na kuelewa mada kabla ya kuchangia! Madaktari hawapiganii maslahi yao tu,wanapigania mazingira mazuri ya kazi pamoja na vifaa! Hawa wanapigania Watanzania wengi masikini ambao hawana uwezo wa kutibiwa katika hospitali binafsi,India na Ulaya.
 
Tumechaoka, kila kukicha ni issues za maslahi ya madaktari.... kwani wao tu ndio muhimu jamani??

Hawa wanataaluma wamegeuka wauaji, wanashabikia watu kufa. Wameshapoteza maisha ya wengi kwenye mgomo wao wa mwanzo lakini bado wana hamu ya kuondoa roho zingine. Wamenogewa kuua.

Laana iko juu yenu, kwa kutanguliza ulafi wenu wa pesa na kupigania kushibisha matumbo yenu ....kwa kutoa kafara roho za binaadam wenzenu.

....Muhimu wabunge, mawaziri, wakurugenzi, TRA na BOT.
 
Pale Utumishi watu wanafanya kazi kwa mazoea na uzandiki... hatuwezi kufika namna hii
 
Kama ndo hivyo nimebadili mawazo, niliikuwa na mpango wa kufanya masters ya internal medicine ili niwe specialist, but ngoja nipige kitu cha masters of science in clinical research niachane na mambo ya kushuhudia vifo vya watu kila siku kisa hamna dawa........
 
Msiulize kwa nini madaktari wanabadili fani na kuwa wanasiasa, wafanyabiashara, business managers na kadhalika. No satisfaction is available for healthworkers because they are not recognized as real nobelists, rather as much knows. Angalia mifano wanayotoa kila mara, hata Pinda juzi akiwa Muhimbili alisema kwamba watumishi wote wa umma ni sawa tu machoni pa serikali, na hivyo serikali haibagui, ati kuna wanasheria, walimu, engeneer nk. Waliokuwa wanamsikiliza wooote hawakumuelewa mpaka juzi walipogundua kwamba walirushiwa changa la macho.

Bahati mbaya madaktari wamezoezwa kuwa na huruma na upole maana wanakutana na watu walio katika hali mbaya kila wakati ambapo kibinadamu lazima huruma ije tu. Sasa kutoenda kuwaangalia usoni wagonjwa ndipo ujasiri wa kuiambia serikali hutokea. Madaktari hawagomi ila wanatumia mwanya huo kuiambia serikali yao kwamba nao wapo na wanaenda sokoni Kariakoo ambako hakuna bidhaa maalum kwa ajili yao kama jeshini kule.
 
jamani vipi kama jeshi nalo likagoma?kwa maana ya magereza,polisi na jeshi?niikiwa na maaana unakwenda oysterbay polisi kulalamika watu wanakuangalia, buguruni, changombe na vibaka wote mjini wanajua kuwa polisi wamegome itakuwaje?kwa maana hiyo basi kila kada ni muhimu kwa maisha ya kila siku na maisha magumu pande zote sio madaktari tu!
kama vipi vukeni mipaka mpaka hapo maslahi yatapoboreshwa
 
madaktari kama vipi acheni kazi jamani. Kama ni kufa kila mtu anakufa mara moja basiiiiiii. Nani aliwadanganya kuwa masomo magumu yanalipa sana? you have to work very hard! we need you and you all need our money. Hata kama hiyo kazi inafanana na kifo.........you must do it because you opted to do it otherwise acheni kazi mkafanye kazi zingine kama mnaweza!
 
Back
Top Bottom