Zena wa TTCL Customer Service yake Hovyo - Soma haya majibu!

sasa hapo kiranga tatizo lilikuwa general hata yeye net alikuwa hana
m
na unajuaje kama hakulipeleka back office?
Na wakamjibu bado linashughulikiwa na mda kamili wa kuisha hawajajua?

Umesoma hiyo original post au una-theorize tu?
 
Customer care siyo jadi ya waTZ. Ndiyo maana hata kuna wachangiaji wasioweza kuona kosa la Zena.

Mimi juzi nilikuwa pale benki kubwa kabisa, niko counter nasubiri vi laki nane vyangu. Mdada anayenihudumia akasema hana noti za 10,000, hivyo atanipa elf tano tano. Nikamuambia naenda mbali na sina gari, hebu muombe mwenzako dirisha la pili naona ana noti nyingi za 10,000. Kumbe yule jirani anasikia nachosema, mara akaanza kuropoka "laki nane nazo pesa? kuna watu wanachukua millioni mia ndiyo iwe vilaki vinane". Nilichoka.
 
Au ni umaskini wa lugha yetu ya Kiswahili inafanya tusiweze ku-express kwa namna iliyo professional zaidi.

Juzi niliona kwenye gazeti la Guardian (tarehe 9 october), tangazo la kifo cha Kamishna Walid Juma. Lilikuwa limetolewa na idara ya PR ya TRA. Eti wanasema "We wish to inform...". Kwa namna yeyote ile ingepaswa isemwe kuwa "We regret to inform...", au "We are saddened to inform..."
 
Customer care siyo jadi ya waTZ. Ndiyo maana hata kuna wachangiaji wasioweza kuona kosa la Zena.

Mimi juzi nilikuwa pale benki kubwa kabisa, niko counter nasubiri vi laki nane vyangu. Mdada anayenihudumia akasema hana noti za 10,000, hivyo atanipa elf tano tano. Nikamuambia naenda mbali na sina gari, hebu muombe mwenzako dirisha la pili naona ana noti nyingi za 10,000. Kumbe yule jirani anasikia nachosema, mara akaanza kuropoka "laki nane nazo pesa? kuna watu wanachukua millioni mia ndiyo iwe vilaki vinane". Nilichoka.

Ishu ya Customer Care Tanzania ni janga la kitaifa....
 
tatizo lake huyo zena anafikiri kila mtu anataka kumtongoza hana lolote we asikuumize kichwa, labda tu kumripoti kwa wakubwa wake ili akafanyiwe training ya kazi hiyo...pole sana mkuu...tz bado tupo nyuma sana ktk suala la customer care...
Kumekua na malalamiko mengi kuhusu huduma mbaya kwa wateja hasa kutoka kwa mashirika ya Umma, na leo nimekutana na hili, ninafikiri kushare hizi experience na kama wahusika wanaona basi iwasadie kuchukua hatua.

Ninatumia huduma ya TTCL broadband kwa internet, ni huduma nzuri. leo mida ya saa 12 huduma ikakatika na mie nilikua na utitiri wa kazi, nikaamua kupiga simu huduma kwa wateja.

Nilipiga namba 100, haya yalikua maongezi yetu

Zena (Customer Service -TTCL): Hallow, nikusaidie nini
Mimi: Hallow, ninaitwa (nikataja jina), ninaongea na nani?

Zena (Customer Service -TTCL): Naitwa Zena, Nikusaidie nini?
Mimi: Asante Zena, ninaongea kutoka UmojaSwitch kijitonyama, toka nusu saa ilopita hatupati connection ya internet, kuna tatizo?

Zena (Customer Service -TTCL): Ndio, kuna shida kubwa kweli, hata sisi wenyewe hapa hatupati internet, lakini mafundi wanafanyia kazi
Mimi: Je, tuitegemee baada ya muda gani?

Zena (Customer Service -TTCL): hapana siwezi kusema, nimeshakwambia hata sisi wenyewe hatupati hiyo internet na mafundi wanafanyia kazi, unajua mimi sio injinia, kwa hiyo siwezi kusema itachukua muda gani
Mimi: sikia zena, sitegemei wewe uwe injinia, lakini nategemea wewe uwe taarifa, ndio maana nakuuliza, lakini asante.

zena akakata simu!.

Mytake:
Hapo kwenye red ndio tatizo.

Customer Service kazi yake (kwa kiasi kikubwa) ni kumpa mteja taarifa, nilitegemea kama kuna tatizo kubwa na wao wanajua nategemea zena awe angalau anajua itachukua muda gani kwa hilo tatizo kutatuliwa ili aweze kuwa-serve wateja.

sikua ninamuomba zena arudishe connection kwa wakati huo, ninaelewa kuna tatizo, ila ili niweze kujipanga ninaomba tu kujua the approximate time itayochukua kabla connection haijarejeshwa.
 
Hii ni mara ya kwanza kwangu kusikia customer care officer anamkatia simu mteja!

Ni ujeuri wa mwisho kabisa.

Inachodhihirisha ni kuwa huyo Zena ana tabia kama hizo za kijeuri hata nje ya ofisi na hapo anaziendeleza tu.

Ni aibu kwa jamii ya wastaarabu kuona alichokifanya Bi.Zena kuwa sahihi
 
Customer care siyo jadi ya waTZ. Ndiyo maana hata kuna wachangiaji wasioweza kuona kosa la Zena.

Mimi juzi nilikuwa pale benki kubwa kabisa, niko counter nasubiri vi laki nane vyangu. Mdada anayenihudumia akasema hana noti za 10,000, hivyo atanipa elf tano tano. Nikamuambia naenda mbali na sina gari, hebu muombe mwenzako dirisha la pili naona ana noti nyingi za 10,000. Kumbe yule jirani anasikia nachosema, mara akaanza kuropoka "laki nane nazo pesa? kuna watu wanachukua millioni mia ndiyo iwe vilaki vinane". Nilichoka.

Ulikua benki gani, itaje tu Stig, tena ukiweza ujitahidi kujua hata jina la huyo alokusemea hoyo ndio njia pekee ya kuwafanya watu wabadilike, wengine watakushambulia ndio, lakini si ndio gharama ya mabadiliko?
 
halafu inaelekea wasichana (hasa kuliko wanawake) wanaongoza kwa poor customer care, sijui kwa nini- uvivu, ushamba, ubishoo, inasikitisha anyway. sina maana hamna vijana/wanaume pia wanaojibu sivyo, ila ni nadra kukutana nao.
halafu ukikuta wasichana wenye majibu ya ovyo, mcheki akimuatend mwanamke mwenzie, utajuta, anaweza akakuangalia kwa kukushusha kuanzia chini hadi juu. tubadilike watanzania jamani, wakati umebadilika sana, mtu anaharibu kazi/biashara bila kujitambua.
 
Huyu dada ameshanikatia simu mara tatu..the first time she had me on hold for more than 13 minutes then hang-up, second time she just did it after I introduced myself and the third time she didnt even say the intro supposedly to be given she just picked it..said nothing and dropped it..I have nothing against her,people have bad days but if she is not in a good mood she should better stay off the phones which is very understandable.
 
Ni kweli tuna tatizo kubwa sana kwenye idara za customer care hapa tanzania. Lakini na sisi wateja kuna tuna matatizo makubwa sana. muda mwingine tunataka tunapokuwa na shida tupewe majibu au tuhudumiwe muda huohuo au hapohapo jambo ambalo ni gumu.

Huyu dada sioni kama alitumia kugha mbaya sana maana tayari alikwisha kukujibu kuwa hajui internet itarudishwa saa ngapi (kwa lugha nyingine hili jambo lilikuwa lipo nje ya uwezo wake wa kutoa maelezo kwa sababu ni suala la kiufundi)

Ni mtazamo wangu tu
 
zena unatuangu!! kitukama hukifaham mweleze mteja apige baada ya mda gn utakua na jibu sahihi, ukishindwa kujishusha na kuwa mnyenyekevu kwa mteja kama tulivyofundishwa unailetea cfa mbaya organization yk.
 
na bado Aye na Amu wanaita huu ni uzushi
402766_177324165738328_1992459943_n.jpg
 
Hiyo ni kawaida kwa watanzania. Pole sana.
Ni kww baadhi ya watu wanaotaka kuharibu kundi la wengi na isipokemewa tabia itaambukiza vizaz na vizazi ebu fikiria kama anaanza Trainee anafundishwa kazi na mtu wa aina hio (huduma mbovu ya "customer care")
 
Kumekua na malalamiko mengi kuhusu huduma mbaya kwa wateja hasa kutoka kwa mashirika ya Umma, na leo nimekutana na hili, ninafikiri kushare hizi experience na kama wahusika wanaona basi iwasadie kuchukua hatua.

Ninatumia huduma ya TTCL broadband kwa internet, ni huduma nzuri. leo mida ya saa 12 huduma ikakatika na mie nilikua na utitiri wa kazi, nikaamua kupiga simu huduma kwa wateja.

Nilipiga namba 100,
haya yalikua maongezi yetu

Zena (Customer Service -TTCL): Hallow, nikusaidie nini
Mimi: Hallow, ninaitwa (nikataja jina), ninaongea na nani?

Zena (Customer Service -TTCL): Naitwa Zena, Nikusaidie nini?
Mimi: Asante Zena, ninaongea kutoka UmojaSwitch kijitonyama, toka nusu saa ilopita hatupati connection ya internet, kuna tatizo?

Zena (Customer Service -TTCL): Ndio, kuna shida kubwa kweli, hata sisi wenyewe hapa hatupati internet, lakini mafundi wanafanyia kazi
Mimi: Je, tuitegemee baada ya muda gani?

Zena (Customer Service -TTCL): hapana siwezi kusema, nimeshakwambia hata sisi wenyewe hatupati hiyo internet na mafundi wanafanyia kazi, unajua mimi sio injinia, kwa hiyo siwezi kusema itachukua muda gani
Mimi: sikia zena, sitegemei wewe uwe injinia, lakini nategemea wewe uwe taarifa, ndio maana nakuuliza, lakini asante.

zena akakata simu!.

Mytake:
Hapo kwenye red ndio tatizo.

Customer Service kazi yake (kwa kiasi kikubwa) ni kumpa mteja taarifa, nilitegemea kama kuna tatizo kubwa na wao wanajua nategemea zena awe angalau anajua itachukua muda gani kwa hilo tatizo kutatuliwa ili aweze kuwa-serve wateja.

sikua ninamuomba zena arudishe connection kwa wakati huo, ninaelewa kuna tatizo, ila ili niweze kujipanga ninaomba tu kujua the approximate time itayochukua kabla connection haijarejeshwa.
Customer care wengi ni,majanga matupu,
Kuna mmoja yupo CRDB Dodoma,tawi mkabala na Nyerere sq,
Anakuhudumia wakati huo huo,anachart kwenye cm,ni lidada moja la hovyo sana
 
Back
Top Bottom