Zena wa TTCL Customer Service yake Hovyo - Soma haya majibu!

Kazi kweli kweli hata wasomi hamjui maana ya Internet au kirefu chake huyo Zena Mbaga yeye anahold hizo Wavuti? Keshasema hata TTCL hawapati Internet mlitaka akailete wapi? Ingekwa Broadband sawa nijukumu lake hata km ni Voda, tigo, airtel hupati Internet sio kazi ya customer care eti Provider wangu mbona hanirushii fb, yahoo, google jf nk
Hebu hamia BlackBerry km utampata hata Mama yake Customer care

Ukwaju, Soma kabla ya kupost!
 
This country bwana! Ngoja wanaojua "how to care customers" waingie katika soko! Ni rahisi sana kupoteza wateja 10 kwa mpigo kuliko kumpata mteja mmoja.!
 
Zena (Customer Service -TTCL): hapana siwezi kusema, nimeshakwambia hata sisi wenyewe hatupati hiyo internet na mafundi wanafanyia kazi, unajua mimi sio injinia, kwa hiyo siwezi kusema itachukua muda gani
Mimi: sikia zena, sitegemei wewe uwe injinia, lakini nategemea wewe uwe taarifa, ndio maana nakuuliza, lakini asante.

Zena akakata simu!.

Zena Zena Zena wewe ni mwanamke hodari, ntakutafuta nikupe ela ya soda. That is an extremely perfect answer na wala mtoa mada huwezi hata siku moja kumlaumu eti Zena amekujibu vibaya.Kwa taarifa yako mimi nafanya kazi ya IT and from mya heart I really really heart someone to breath on my neck when I am doing a technical job which need my concetration kwa hiyo hata mtu akija akaniuliza eti brother please just give me a time frame when do you think this job will be done. Mimi nachomjibu ni kwamba I am doing a technical job and I can not promise kwamba I will be through kwa muda gani maana naweza nikasema dakika 10 kumbe ikaja ikawa saa nzima ndo nikazidisha matatizo na matusi kwa wateja. Kwa hiyo the simplest answer is am working on it and once it is done I will let you know. Kwa hiyo hata Zena dada yangu huenda amekutana na IT kama mimi ndo maana akakujibu jibu kama hilo maana yeye sio technician. WELL DONE ZENA


...Kama injinia wetu wa IT anashindwa hata kutofautisha tu maneno ya Heart na Hate, kwa nini tusiwe na akina Zena wengi tu na Watetezi wao Kibao???
 
Hiyo ni kawaida kwa watanzania. Pole sana.
...Pole mkuu nadhani hapo tatizo sio Zena nadhani aliyemuajiri atakuwa amechangia kumfanya Zena awe hivyo alivyo...mbona TTCL yenyewe inapoteza mvuto kila kukicha? nadhani wamefika mwisho wa upeo wao wa kufikiri hawana kitu kipya though it is a state owned entity lakini linaelekea kupata degedege na cjui kama litatibiwa...wamechoka mbaya hao!!
 
...Kama injinia wetu wa IT anashindwa hata kutofautisha tu maneno ya Heart na Hate, kwa nini tusiwe na akina Zena wengi tu na Watetezi wao Kibao???

Umeona eeh! unajua mtu akifungua mdomo tu ndio unamjua ni mtu wa aina gani.
 
mbona sio ttcl peke yake we nenda hata benk ze2 au kwenye ofc za hii mitandao ya cmu esp 0713 utachoka majibu yao

Acha hao ambao huonani hao, usiombe ukutane na hawa wahudumu wa M-Pesa ama Tigo pesa. Wana majibu ya kunya halafu wanajiona wao ndio wanajua kila kitu.
Kuna mmoja kidogo nimlambe makofi juzi pale Stand kuu Arusha.
 
Hivi nyie mnacheza na ucustomercare eee
kiukweli tusiwalaumu hawa watu ile kazi ni balaa simu zinapishana sekunde 3 kuingia na ni automatic ikikatika moja inaingia nyingine
u can imagine wewe ni mtu gani unaongea tu nonstop tena unatatua matatizo ya watu
hata wao wanapata maudhi kama yenu ninatawapa mifano
1. kuna wale wanaopiga kukutukana tu ukipokea tu mtu anakushushia matusi mpaka unaogopa
2.kuna wengine wanapiga simu hawajui kiswahili wala english wanaongea kilugha
3.bado wale wa kukutongoza
4. wale ndugu zetu wasukuma anasafirisha ng'ombe kuja dar anakupigia kukuomba namba ya simu eti "dada nipe namba yako nikifika dar nikupigiyage tuwage wote"
5.kuna wale ambao kupiga ucustomer care na ukipokea ni furaha kwao kama kaokota Tanzanite lo ushamba ulioje eti "dada nafurahi sana kuongea na wewe" na anakubusu kabisa huyo hana tatizo lolote au hana hata comment yoyote ya kusema yeye kapiga ajifurahishe na akuchumu tu
6.na kuna wale wateja wengine ambao hajui hata namba moja inaandikwaje halafu anataka umsaidie ajue kutuma ujumbe
neno ujumbe(sms) hajui hata maana yake na hajui inakuwaje
7.kuna yule anayekuambia dada naomba unitumie vocha au hela maana nyie mnazo nyingi
mimi nimepiga hiyo kazi to be honest niliiacha mwenyewe na sitegemei kufanya ucustomercare tena nimekoma
dada zena nikupe ujanja TTCL mpo wengi mtu akipiga kama huyo unaona anataka exactly answer na wewe hujielewi mwambie piga baada ya nusu
ha ha akipiga tena inakuwa haiingii kwako msala wa another customer care representative
hivi mtoa mada hujawahi kukutana na ile wanakuhold kwa simu zaidi ya nusu saa?
Ila kuna wateja wengine kuwahudumia hadi raha unafurahije kama wewe mtoa mada ningefurahi kukuhudumia maana ni muelewa sema tu zena labda alikuwa kachoka
na wewe mtoa mada next tyme ukiona hujaridhika na jibu kata simu piga tena atapokea mwingine muelezee tatizo atakuhudumia sitegemei wote wawili watakosa majibu ya kukupa ukaridhika
ila kuja kuanika hapa mhh ni mbaya zena akikosa chakula cha familia utajisikiaje?nina imani hiyo kitu ukijua itakuumiza sana moyo kama una utu kidogo wa ubinadamu itakuuma kiukweli sijaona sababu ya kumuanika hapa hajakukosea kihivyo labda kama una sababu zingine
nawakilisha
......
 
Mkuu anaitwa Zena Mmbaga. Ana " URAFIKI" na wakubwa pale Extelecoms. Mimi namfahamu sijashangazwa na bandiko lako

na wewe mtoa mada next tyme ukiona hujaridhika na jibu kata simu piga tena atapokea mwingine muelezee tatizo atakuhudumia sitegemei wote wawili watakosa majibu ya kukupa ukaridhika
ila kuja kuanika hapa mhh ni mbaya zena akikosa chakula cha familia utajisikiaje?nina imani hiyo kitu ukijua itakuumiza sana moyo kama una utu kidogo wa ubinadamu itakuuma kiukweli sijaona sababu ya kumuanika hapa hajakukosea kihivyo labda kama una sababu zingine
nawakilisha
......

Sikia Amu,

Moja, mie simfahamu Zena (in person, mbali na kuongea nae tu kwa simu nilipopiga customer service), siwezi kuwa na sababu nyingine yeyote, nimelisema hili hata hapo mwanzo. Nimequote post ya mchangiaji mwingine, Janatu Firdaus (hata yeye hatufahamiani), yeye anadai kumfahamu Zena, anasema kwa namna anavomfahamu ashangai kuona bandiko langu, akataja na jina lake la pili ambalo mie wala sikua nalijua


Pili, Kwamba Zena anaweza kupoteza kazi, hilo halikua lengo langu, lengu langu ni Zena, Aye na wenzao wajirekebishe

Tatu, presha za kazi, ugumu wa kazi na vitu vyote hivo ulivosema havi-justify huduma mbovu kwa mteja, kimsingi hakuna sababu hata moja ya cso kutoa huma mbaya kwa mteja. I am a person who never accept mediocrity, ndio maana watu kama Zena na Aye wakikutana na mie lazima watapa taabu tu
 
Sasa naomba nikuulize mpaka hapo unahisi labda Zena na Aye wamepata tabu gani?
Na wewe kuja kuwaanika huku imesaidia nini?
Unajua sijapatakitu bado
 
Sasa naomba nikuulize mpaka hapo unahisi labda Zena na Aye wamepata tabu gani?
Na wewe kuja kuwaanika huku imesaidia nini?
Unajua sijapatakitu bado

Suala hapa ni namna wanapaswa kuboresha na kujua mbinu za kuongea na wateja hasa kwa nafasi zao za u customer care. Nafasi za akina Zena mahali popote huwa ni muhimu katika yote mawili, kuvuta na kufukuza wateja na hakuna manager makini ambaye anamvumilia mfanyakazi anayesababisha shirika ama taasisi yake iharibu PR.:photo:
 
[
embu muulize bana naona kashupalia kweli hii ishu utafkiri sjui analipwa badala ya kufanya mambo yake
 
Suala hapa ni namna wanapaswa kuboresha na kujua mbinu za kuongea na wateja hasa kwa nafasi zao za u customer care. Nafasi za akina Zena mahali popote huwa ni muhimu katika yote mawili, kuvuta na kufukuza wateja na hakuna manager makini ambaye anamvumilia mfanyakazi anayesababisha shirika ama taasisi yake iharibu PR.:photo:

ur really a GT hilo ndo muhimu kuongelea jinsi ya kuboresha huduma hiyo
siyo kumchambua mtu mmoja mmoja
 
Sasa naomba nikuulize mpaka hapo unahisi labda Zena na Aye wamepata tabu gani?
Na wewe kuja kuwaanika huku imesaidia nini?
Unajua sijapatakitu bado

Swali:
Sasa naomba nikuulize mpaka hapo unahisi labda Zena na Aye wamepata tabu gani?
Jibu
Kama wangekua wana-report kwangu, na hivi ndio wanahudumia wateja, for sure wangekua wamejiingiza matatani, lakini kwa sababu wao wako TTCL na mie niko kwingine, sina uwezo wa kuwaadabisha.

Swali

Na wewe kuja kuwaanika huku imesaidia nini?
Jibu
much better customer service kwangu na kwa watanzania wenzangu, kwa sababu ninaamini Zena na Aye watajirekebisha.
 
Suala hapa ni namna wanapaswa kuboresha na kujua mbinu za kuongea na wateja hasa kwa nafasi zao za u customer care. Nafasi za akina Zena mahali popote huwa ni muhimu katika yote mawili, kuvuta na kufukuza wateja na hakuna manager makini ambaye anamvumilia mfanyakazi anayesababisha shirika ama taasisi yake iharibu PR.:photo:

ur really a GT hilo ndo muhimu kuongelea jinsi ya kuboresha huduma hiyo
siyo kumchambua mtu mmoja mmoja


Straight on the face ndio njia sahihi ya kumsaidia mtu, kila siku tunakemea rushwa na trafic bado wanaendelea kukwapua, why? msg yetu is just too general, hebu tuanze ku-pinpoint, akiomba askari A akiomba rushwa tuseme Askari A anaomba rushwa, inabidi ajirekebishe.

you got it all wrong amu, ukisoma unaona majadala wa nini cha kufanyika, hakuna mjana wa Zena mrefu au mfupi, mweupe au maji ya kunde hapana, maada hapa ni Huduma yake kwa wateja sio nzuri na nini afanye (au tunategemea afanye) ili aboreshe huduma kwa wateja
 
kumekua na malalamiko mengi kuhusu huduma mbaya kwa wateja hasa kutoka kwa mashirika ya umma, na leo nimekutana na hili, ninafikiri kushare hizi experience na kama wahusika wanaona basi iwasadie kuchukua hatua.

Ninatumia huduma ya ttcl broadband kwa internet, ni huduma nzuri. Leo mida ya saa 12 huduma ikakatika na mie nilikua na utitiri wa kazi, nikaamua kupiga simu huduma kwa wateja.


nilipiga namba 100, haya yalikua maongezi yetu


zena (customer service -ttcl): Hallow, nikusaidie nini
mimi: Hallow, ninaitwa (nikataja jina), ninaongea na nani?

zena (customer service -ttcl): Naitwa zena, nikusaidie nini?
mimi: Asante zena, ninaongea kutoka umojaswitch kijitonyama, toka nusu saa ilopita hatupati connection ya internet, kuna tatizo?

zena (customer service -ttcl): Ndio, kuna shida kubwa kweli, hata sisi wenyewe hapa hatupati internet, lakini mafundi wanafanyia kazi
mimi: Je, tuitegemee baada ya muda gani?

zena (customer service -ttcl): hapana siwezi kusema, nimeshakwambia hata sisi wenyewe hatupati hiyo internet na mafundi wanafanyia kazi, unajua mimi sio injinia, kwa hiyo siwezi kusema itachukua muda gani
mimi: Sikia zena, sitegemei wewe uwe injinia, lakini nategemea wewe uwe taarifa, ndio maana nakuuliza, lakini asante.

zena akakata simu!.

mytake:
hapo kwenye red ndio tatizo.

Customer service kazi yake (kwa kiasi kikubwa) ni kumpa mteja taarifa, nilitegemea kama kuna tatizo kubwa na wao wanajua nategemea zena awe angalau anajua itachukua muda gani kwa hilo tatizo kutatuliwa ili aweze kuwa-serve wateja.

Sikua ninamuomba zena arudishe connection kwa wakati huo, ninaelewa kuna tatizo, ila ili niweze kujipanga ninaomba tu kujua the approximate time itayochukua kabla connection haijarejeshwa.

kuna mdada wa hubert kairuki naye ni noma, aliniboa sana na majibu yake
 
unamlaumu zena bure. Keshasema hata wao wana tatizo la network na hawajui tatizo litaisha muda gani, na kasema mafundi wanashughulikia. Ulitaka akutabirie kuwa liitaisha baada ya nusu saa? Then huo muda uishe halafu hola kisha uanze tena matusi? Kuna watu wanapenda kudanganywa na kubembelezwa bila sababu za msingi, mleta mada akiwa mmoja wao. Tuache gubu. Kwani tunajua ni presha gani ilikuwa nyuma ya zena? Tena kajibu vizuri kweli, ila mleta mada alipotaka kulazimisha majibu ndio akakatiwa simu. Let us be smart
 
hii inanikumbusha kipindi fulani niliwahi kutukanwa na mteja lakini baadae aliomba radhi. Nilikuwa na repair machine yake nikamwambia hatua ya kwanza nifanya ila ina bidi uiache machine hadi kesho niweze kuangalia kwa sababu tatizo hili huenda limesababishwa na lingine na troubleshooting kugundua hilo lilosababisha naomba utulie uiache machine akawa anang'ang'ana nimwambie kesho saa ngapi nika mwambia nitampigia simu. Kesho akaja asubuhi eti hata kama bado sijaona tatizo la pili kwakuwa inafanya kazi nimpe wakati kwa kawaida ukiiangalia inafanyakazi lakini kwa fundi unaona bado kuna matatizo technical manager akaamuru nimpe mteja ijapukuwa niligoma lkn wakampa kwa sababu cc aliahidi mteja aje kesho saa nne. baada ya siku mbili ikarudishwa na tatizo lile lile
 
ndugu zangu kama uko kwenye first stage of troubleshooting ni ngumu sana kujua matengenezo yatachukua muda gani. Kwa hili zena alikuwa sahihi kwa kuusema ukweli kuliko kudanganya
 
Back
Top Bottom