Zembwela afunika kwenye Mkasi

Chilli

JF-Expert Member
Jul 17, 2011
1,655
743
Jana niliangalia kipindi cha mkasi kinachooneshwa EATV ambapo jana mgeni wao alikua Zembwela na host wake kama kawaida alikua Salama Jabir.
Kiukweli zembwela alifunika sana hasa katika uwezo wa kujibu maswali na kutoa hoja kwa umakini. Kiukweli huwezi fananisha ile interrview na nyingine za mastaa wa bongo ambao hata ukiangalia unaeza shindwa kumaliza kipindi kwa jinsi wanavyoboa.
Zembwela ana uwezo wa kutoa mifano ambayo mingi iko critical, na haboi kuangaliwa.
Japo kuna mapungufu flani lakini comparing with other Bongo super - stars, he is better.
 
... kwa kuwa nachukia watu wanao NATA, wanachanganya kingereza na kiswahili kwenye mahojiano ya kiswahili. nakuunga mkono, kwakuwa jamaa alikuwa anajibu kwa kiswahili bila kuchanganya changanya.

sikuhizi ma supersta hata wasio jua kingereza, utasikia.... actuale, becose, problem, ....

amefanya vizuri jamaa
 
Yap alifunika sana zembwela yupo fiti sana,jama ana msimamo si ulimsikia alivyosema kwamba basi zima lilmpeleka yeye mpaka sinza!
 
Ndo huyu aliyesajiliwa na simba duhh kweli Rage anajua kusajili vifaa
 
Kweli interview ilikuwa nzuri! Mtiririko wa maswali na majibu ulikuwa mzuri!
Zembwela hakuwa na mbwembwe za kiswangishi na mifano yake ilikuwa hai! Mfano maisha bora kwa kila mtanzania kwa maoni yake ni nikuwa na uwezo wa kutibiwa bila kujali umasikini wake nk
 
mi pia nilipenda ile interview. Kwanza anauelewa wa mambo mengine tofauti na usanii ambayo yanaafect maisha kiujumla. Tofauti na TID ambae alikua hajui chochote zaidi ya mziki na kutuachia nguo za ndani nje
 
alipresent hoja endelevu na champion wa matumaini mapya kwa vijana.
Usanii unahitaji ubunifu na kufanyia utafiti mambo mengi ya kijamii, uchumi na siasa.
ZEMBWELA kajipanga.
Salute bro

Jana niliangalia kipindi cha mkasi kinachooneshwa EATV ambapo jana mgeni wao alikua
Zembwela na host wake kama kawaida alikua Salama Jabir.
Kiukweli zembwela alifunika sana hasa katika uwezo wa kujibu maswali na kutoa hoja kwa umakini. Kiukweli huwezi fananisha ile interrview na nyingine za mastaa wa bongo ambao hata ukiangalia unaeza shindwa kumaliza kipindi kwa jinsi wanavyoboa.
Zembwela ana uwezo wa kutoa mifano ambayo mingi iko critical, na haboi kuangaliwa.
Japo kuna mapungufu flani lakini comparing with other Bongo super - stars, he is better.
 
Nakubaliana na wewe,
Zembwela toka tulipomchana hapa jf kuwa elimu ni ndogo
naona amepiga piga kitabu sana, hivyo kwa sasa mambo yake ni mswano kabisa,
hongera sana dogo zembwela.

Jana niliangalia kipindi cha mkasi kinachooneshwa EATV ambapo jana mgeni wao alikua Zembwela na host wake kama kawaida alikua Salama Jabir.
Kiukweli zembwela alifunika sana hasa katika uwezo wa kujibu maswali na kutoa hoja kwa umakini. Kiukweli huwezi fananisha ile interrview na nyingine za mastaa wa bongo ambao hata ukiangalia unaeza shindwa kumaliza kipindi kwa jinsi wanavyoboa.
Zembwela ana uwezo wa kutoa mifano ambayo mingi iko critical, na haboi kuangaliwa.
Japo kuna mapungufu flani lakini comparing with other Bongo super - stars, he is better.
 
Amenifanya nimkumbuke sana marehemu MAX ambaye hajatokea msanii wa mfano wake tena!
 
Jamani mimi naomba hapa tuelimishane kidogo, huwa nina hamu ya kuangalia hicho kipindi lakini nakosa timing, mara nyingi huwa naona wakiadvertise next guest, sasa mimi swali langu ni dogo tu, hicho kipindi kinahusu nini hasa na kinatoa Elimu gani kwa Watanzania? maana nilibahatika kumuona Ismail Aden Rage lakini mpaka kipindi kinaisha sikuelewa kitu zaidi ya kuona mtu anaoshwa miguu na kukwanguliwa kucha.
 
Back
Top Bottom