ZEC Yakataa Kumuandikisha Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
ALIYEKUWA Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Jahazi Asilia, Mussa Abdallah Kitole, amekataliwa kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa madai kuwa hana kitambulisho cha Mzanzibari mkazi.

Tukio hilo lilitokea juzi katika Kituo cha Shule ya Gamba, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambako Kitole alikwenda kujiandikisha kama mpigakura.

Hata hivyo maafisa waandikishaji walimwambia kuwa hawezi kuandikishwa kwa sababu hana sifa.

Msimamizi wa Uandikishaji katika Wilaya ya Kaskazini Unguja A, Murshid Khamis, alisema Kitole hana kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi na kwa hiyo hawezi kuandikishwa.

"Sheria ni msumeno, hakuna aliyekuwa juu ya sheria," alisisitiza Khamis.

Kwa sasa Kitole ni Katibu Mkuu wa Jahazi, chama hicho ambacho kimejijengea ngome kubwa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Kassim Bakari Ali, alielezea kusikitishwa kwake na kwamba hizo ni njama za kukwamisha wapinzani wa kisiasa.

Alisema "Kitole ni mzaliwa halisi wa Zanzibar, kitendo cha kumkatalia kujiandikisha ni cha kumdhalilisha kiongozi huyo."

Hata hivyo alisema chama chake kimeamua kufanya mkutano mkubwa mwishoni mwa wiki hii kuelezea udhalilishwaji huo katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.


SOURCE: MWANANCHI.
 
Angalia huyu afisa wa tume mpuuzi anasema eti "...sheria msumeno..." basi ata handle haina?
 
Uchaguzi ujao nadhani CUF hawatakuwa Bungeni maana wamepaniwa sana . Si utani yaani jamaa badala ya kwenda Mahakamani anaenda kuitisha mkutano wa hadhara ndiyo utampa haki ?
 
Hapa ninaonekana kutoelewa vizuri; hivi kinachofanyika Zanzibar in kuandikisha wapiga kura ua kuboresha (update) daftari la kudumu la wapiga kura? Na sheria ya uchaguzi inasemaje?
 
Uchaguzi ujao nadhani CUF hawatakuwa Bungeni maana wamepaniwa sana . Si utani yaani jamaa badala ya kwenda Mahakamani anaenda kuitisha mkutano wa hadhara ndiyo utampa haki ?
Linyungu CUF hawana wasiwasi na ushindi,hilo mkae mkijua halina mbadala na CCM wanaelewa hivyo.
Kinachotokea hivi sasa ni mbinu za kisiasa ambazo zinaelekezwa kuikwamisha CCM na kusema kweli zinaelekea kufanikiwa.
CCM hawaiwezi CUF katika mbinu za kukampeni ndani ya nchi na kimataifa ,maana kwa ujuha walionao CCM huwa wanaingia kirahisi katika mitego ya CUF na hivyo wanazidi kuonekana kuwa ni wezi waliokubuhu.
Kwa hivyo hata raisi akitoka CCM anakuwa hana mvuto nje ya nchi na anaonekana kibaka tu.
 
Hapa ninaonekana kutoelewa vizuri; hivi kinachofanyika Zanzibar in kuandikisha wapiga kura ua kuboresha (update) daftari la kudumu la wapiga kura? Na sheria ya uchaguzi inasemaje?
Labda tujaribu kueleweshana kwa kuweka wazi ni kuwa ku-updates daftari kuna maana zaidi ya kuandikisha wapiga kura wapya, huy Bw.Kitole yumo katika daftari lililopita au la awali ambalo lilipoanza masharti ya kuwa na kitambulisho hayakuwapo au hata habari za vitambulisho ilikuwa haipo wakati huo. Pili, ni kuwa kuboresha daftari kuna nukta nyingi kama kuandikisha upya wale ambao wamebadili maeneo yao ya makaazi, mfano jimbo au shehia moja kwenda nyingine, kuondoa wale ambao wamepoteza sifa za kuwa wapiga kura mfano waliofariki n.k. Sasa inawezekana ikawa si kuwa Bw. Kitole anataka kuandikishwa kama mpiga kura mpya bali kwa kuboreshwa taarifa zake ambazo zimebadilika, hii ni kufuata sheria kabisa...sasa tume walitakiwa wawe na utaratibu wa kuhoji siyo kukurupuka kufukuza watu na huku wakijidai kuwa wanafuata sheria kumbe wanazivunja.
 
Cha kuangaliwa hapa ni sheria, kama sheria imesema ni wajibu kuonyesha hiko kitambulisho ili uandikishwe kwenye hio daftari, huyu Mheshimiwa alitakiwa afate sheria.
Haya mambo ya "hunijui mimi nani" ndio yanatuvuruga sometimes. Iwe Kikwete,Karume ama mlalahoi wote inatakiwa tufuate sheria. Hivi unadhani mfano Obama ama Bush anataka passport, anaweza kuomba bila ya cheti cha kuzaliwa kwa vile ni anajulikana?
Halafu sio kwenda mahakamani kulalamika eti mkutanoni? Kwa wanasiasa dizani hii (mgombea Urais?) no wonder tunazidi kudidimia.
 
Nina swali wakuu. Ni sifa zipi mtu anayo takiwa kuwa nayo kuandikishwa huko Zanzibar? Na je huyo mkuu alitimiza hizo sifa zote?
 
Katika hatua nyengine chama cha wananchi CUF, kimeilalamikia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa kuhamisha vituo vyote vya uandikishaji katika Jimbo la Mtambwe na kuvihamishia Shule ya Daya vituo Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkurugenzi wa Organizesheni na Uchaguzi wa chama hicho, Juma Said Sanani aliwaambia waandishi wa habari kwamba awali vituo vya uandikishaji vilikuwa vikitumika katika shule zilizokuwa karibu na jimbo hilo lakini hivi sasa ZEC imeamua kuvipeleka vituo hivyo umbali wa zaidi ya kilomita nane kwa lengo la kukidhoofisha chama chake na wananchi.
Amedai kwamba ZEC imefanya hivyo kwa makusudi ili kuwahangaisha wananchi wanaotaka kwenda kujiandikishwa washindwe kufika huko vituoni kwa kuwa hali ya uchumi wa kisiwani Pemba unafahamika ambapo wananchi wengi ni masikini na hawawezi kumudu kwenda masafa makubwa kwa miguu.
"ZEC kwa makusudi imehamisha vituo vyote vya jimbo la Mtambwe na kuvipeleka skuli ya Daya ambako ni zaidi ya kilomita nane bila taarifa wala kujali wazee wagonjwana asiojiweza lakini sisi tunajua kuwa huo ni mkakati maalumu wa kuidhoofisha CUF " amesema Afisa huyo.
Akizungumzia madai hayo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Salim Kassim Ali amesema madai hayo hayana msingi kwa kuwa ratiba ya uandikishaji ilitolewa tokea mwanzo na vyama vyote walipatiwa hivyo hakuna sababu za kulalamika kwa kuwa ZEC haijawahi kupokea malalamiko kutoka katika chama chochote cha siasa juu la umbali wa vituo hivyo.
"Ratiba tuliyoitoa ZEC tumewapa vyama vyote vya siasa na mpaka sasa hatujapokea malalamiko yoyote kutoka katika chama chochote cha siasa kwa maana hiyo basi ikiwa kuna chama kinalalamikia hilo basi waje kwetu kuleta hayo malalamiko yao na sio kuzungumza na vyombo vya habari" alisema Mkurugenzi huyo katika mahojiano yake na kituo kimoja cha radio nchini.
Mkurugenzi huyo alisema kuvipeleka vituo katika shule ya Daya ni kwa ajili ya usalama zaidi kutokana na vituo vingi vilivyopangwa huwa havina usalama wa kutosha kutokana na vitisho vya baadhi ya watu wenye nia mbaya na uandikishaji unaoendelea katika mikoa ya kaskazini Unguja na kaskazini Pemba.
"Sababu inayotolewa na ZEC ni kuogopa vitisho jambo ambalo sio kweli na ala halina mantiki kwa sababu ZEC imepewa ulinzi na vyombo vya dola sasa kama hio ndio sababu ya kuhamisha vituo huo ulinzi waliopewa unafanya kazi gani? Alihoji Sanani.
Mbali ya madai hayo CUF pia imesikitishwa na hatua ya ZEC kuzuwia vitambulisho vya waangalizi wa chama hicho katika majimbo ya Wete na Mtambwe kwa kisingizio cha kuwa waangalizi wa majimbo la Ole na Tumbe hawajarejesha vitambulisho hivyo jambo ambalo wamesema hali mahusiano.
Chama hicho pia kimedai kunyanyaswa kwa mawakala wao ambao wamekuwa wakikatazwa kuhoji jambo lolote katika vituo vya uandikishaji na maafisa wa ZEC jambo ambalo wamesema ni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi.
"ZEC imeamua kuwanyanyasa mawakala wetu wa CUF kwa maneno machafu na kuwanyima haki ya kuhoji na kuandika kitu chochote vituoni ili kuficha madudu yao wanaoyafanya" alisema Sanani katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi ZEC amesema hata taarifa ya suala hilo na hadi sasa hajapokea malalamiko yoyote kutoka kwa mawakala iwapo wananyanyaswa lakini iwapo suala hilo ni kweli basi ni kosa kwa maafisa wa ZEC kuwatolea maneno makali au kuwanyanyasa mawakala kwa kuwa wao wana haki ya kuhoji kwa mujibu wa sheria.
source:zanzibar yetu web blog.
 
Wakuu zangu,
Samahani kidogo kuhusiana na hii hoja..
Nchi nyingi za Ulaya zinafuata mfumo huu yaani ukiwa sii mkazi wa sehemu fulani (Zanzibar) huruhusiwi kujiandikisha wala kupiga kura hata kama umezaliwa hapo..Utapiga kura jimbo unaloishi na sio kurudi ulikozaliwa...

Sasa ikiwa kweli sheria hii imetumika Zanzibar na ndio mfumo ulokubalika sioni tatizo liko wapi.
Na binafsi nadhani sheria hii ni nzuri sana kwa Tanzania nzima yaani watu wataruhusiwa kujiandikisha kugombea na kupiga kura tu toka maeneo (majimbo) wanayoishi. leo hii unakuta mtu anaishi Dar ikifika Uchaguzi anakwenda kugombea Ukerewe na anapiga kura wakati sii mkazi wa pale. Akisha chaguliwa tu anarudi Dar anakoishi na kuwaacha wananchi wakijiuliza sababu gani mbunge huyo haonekani.
Hivyo kuna uzuri wa sheria hii na sidhani kama nchi za Ulaya wataweza kuelewa vizuri kinachodaiwa hapa ikiwa huyu Mussa Kitole sii mkazi wa Zanzibar lakini anataka kujiandikisha ktk daftari la kudumu la Zanzibar kwa sababu tu yeye ni mzawa... Hizi option za kuchagua mtu anataka kujiandikisha wapi ndizo zinaleta matatizo yote tunayoyapata ktk uchaguzi. Unamkuta mtu akiishi kata ya pili anakuja jiandikisha kata mbili au tatu kwa sababu hakuna utaratibu maalum kuzuia watu kupiga kura sehemu wasizoishi.

Wee kama ni mkazi wa Dar utapiga kura Dar tena kata yako na huwezi kugombea Ubunge jimbo jingine ambalo wee sii mkazi..hakuna njia bora ya kuzuia ukiukaji wa taratibu za upigaji kura zaidi ya hapo.. Kama upo nambieni!.. Mimi mkandara nikijiandikisha Ukerewe (nilikozaliwa) hiyo serikali itaweza vipi kufahamu ikiwa nitajiandikisha tena huko Mwanza (nakoishi) ambako naweza fika na kupiga kura kabla kituo hakijafungwa..

Kuchukulia swala la Mussa kama ni maonevu ni kujiongezea matatizo. Ikiwa yeye Mussa amekataliwa basi CUF wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa. na kama nakumbuka vizuri vurugu kubwa ya mwaka 2000 na 2005 ilitokana na watu kutoka sehemu nyingine kuja kupiga kura ktk kata ambayo wao sii wakazi. Watu hawa walitambuliwa kirahisi na ilifikia hata kugundua kuna watu kutoka bara waliingia Zanzibar na kupiga kura..

Hivyo akiruhusiwa Mussa Kitole itawapa sababu CCM kuandikisha watu kibao toka bara kwa sababu tu ni wazawa wa Zanzibar, watu ambao watapiga kura Bara na kisha kuingia Zanzibar.. Mnafikiri CCM mwaka 2005 walichelewesha uchaguzi wa Zanzibar kwa sababu gani?.. ilikuwa kuwawezesha wakazi wa dar kwenda Zanzibar kupiga kura wakati tayari watu hawa walisha piga kura zao Bara..
Binafsi naomba wakuu zangu mlitazame swala hili kwa umakini zaidi isije kuwa huyu Mussa Kitole anatumiwa kama chambo cha sheria hiyo kupitishwa ili CCM warudie tena mchezo wao wa mwaka 2005..
 
Last edited:
Vitu vingine vya ajabu sana maana kuna kama kweli SMZ wanataka kwenda na demokrasia ya kweli basi itakuwa vyema kama kweli wakiwa wakweli katika yote
 
kama sheria inasema lazima uwe na kitambulisho cha mkaazi huyo jamaa si akakichukue tu na kuandikisha?haiwezekani mtu akataka kuwaongoza watu afu yeye mwenyewe anakuwa wakwanza kuvunja sheria/taratibu za jamii aliyotarajia kuiongoza,kama hana hafai tu wala mjadala haupo,
 
Kwa zanzibar hilo si la kustaajabu. Alikataliwa mgombea urais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kule mtoni kisa yeye akitangaziwa kifo wanasema akiwa popote pale. Hivyo sheha wa shehia ya mtoni alimkataa sio mkazi wa mtoni.

Kuna mengi zanzibar. lakini tunamuomba Mungu ayaepushe.
 
Kwa zanzibar hilo si la kustaajabu. Alikataliwa mgombea urais wa zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kule mtoni kisa yeye akitangaziwa kifo wanasema akiwa popote pale. Hivyo sheha wa shehia ya mtoni alimkataa sio mkazi wa mtoni.

Kuna mengi zanzibar. lakini tunamuomba Mungu ayaepushe.
Ni baadhi ya vituko vya Zenj hivyo!
 
Ingefaa ZEC na NEC wafafanue ni nini kinaendelea.

Kwa maelezo yaliyotolewa mapema mwaka huu, NEC inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga kura Tanzania ambalo lilianza kuandikwa mwaka 2005. Wakati huo kila mpiga kura alipewa kadi yake na kama haijapotea, huyo mpiga kura anaweza kwenda nayo kituoni mwaka 2010 na akapiga kura. Kama amehama akaenda sehemu nyingine ya Tanzania, kitu anachotakiwa kufanya ni kwenda kituo kipya atakachopigia kura na kujiorodhesha hapo kabla ya siku ya kupiga kura. Akiwa Bara au Zanzibar ni vizuri haki hii iheshimiwe.

Kuboresha Daftari la Kudumu pia ni kuandikisha wapiga kura wapya ambao mwaka wa 1005 hawakuwa na umri wa kujiandikisha (miaka 18) au walikuwa nje ya nchi na kushindwa kujiandikisha.

Kuboresha Daftari pia kunaweza ni kutokana na Mpiga Kura kupoteza kadi yake aliyopata mwaka wa 2005.

Kwa maoni yangu, vurugu hizi za Zanzibar za kutaka mpiga kura awe ni mtu aliyeishi mfululizo Zanzibar kwa miaka mitatu, zinatokana na juhudi wa kuzuia Wazanzibari fulani washindwe kupiga kura, ili chama fulani kishinde au kishindwe. Siku moja hata Makamu wa Rais Shein anaweza kuzuiwa kupiga kura eti kwa vile kwa miaka 10 amekuwa anaishi Dar es Salaam au Dodoma, na sio Pemba! Huku kumzuia hata mwananchi aliyekuwa na sifa za kugombea Urais mwaka 2005, asijiandikishe kunatia aibu. Hata ndugu yake Rais Karume anayeishi Roma sasa kama Balozi wetu anaweza kuzuiwa kujiandikisha kuwa mpiga kura 2010!

Mimi nashauri CUF badala ya kuandamana, waende Mahakama Kuu ya Katiba na watake tamko la Mahakama kwamba Sheria ya Kupiga Kura iwe ni moja kwa Zanzibar na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tuachane na hizi juhudi zisizokuwa na kichwa wala mkia, za kubagua wananchi kutokana na hisia zetu kwamba wanaweza kutupinga kisiasa.
 
Sheria za uchaguzi wa Zanzibar zinasenma ili uandikishwe kuwa mpiga kura ni lazima uwe Mzanzibari Mkaazi katika jimbo unalojiandikisha. Ukijadili tafadhali zingatia hilo. Huu ni utawala wa sheria Bwana!!!. Usiwakandie ZEC tu. Hata hao uliowasema0- kama hawana Zan Id hawatoandikishwa katika uchaguzi wa 2010.
 
Sasa huu ni upumbavu kupita maelezo. Kama huyu jamaa aliwahi kugombea ngazi ya urais huko Zanzibar halafu leo unasema hana sifa za kuandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Assume kama angeshinda katika huo uchaguzi, then ZEC wangesemaje? Sasa ilikuwaje jamaa akagombea katika ngazi hiyo kama hana sifa za kuandikishwa kwenye hilo daftari? Kusema hivyo ina maana una haki ya kupigiwa kura na si kupiga kura. Mmh hapo ndo watu wanasema kuwa Tanzania kuna demokrasia. Kweli hiyo ndiyo demokrasia halisi (UNAWEZA KUPIGIWA KURA LAKINI HUWEZI KUPIGA KURA). Hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika, kanuni ya 6(ii), haya ya 17 kipengele cha cha 65, sentensi ya 20 kutoka mwisho.
 
Back
Top Bottom