MKWEPA KODI
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 28,707
- 71,003
- Thread starter
- #141
Tume haina mamlaka hayo, hayo ni mamlaka ya Mahakama baada ya kupelekewa malalamiko na kuyasikiliza na kuyatolea maamuzi kwa hakiInawezekana imeenda shule, lakini suala la msingi linabakia palepale. Je Tamko la Jecha kufuta uchaguzi ni halali kikatiba na kisheria?
Kama si halali, hii yote inayofuata, kutangaza marudio ya uchaguzi ni kuzidi kuongeza tatizo.
Tatizo zaidi lipo hapa.
Je ZEC (au Jecha) ina mamlaka kisheria ya kufuta au kutengua matokeo ya uchaguzi? Matokeo ambayo ZEC na wasimamizi wa uchaguzi majimboni walishayatangaza, kuyabandika kutani na kuwakabidhi washindi(wateule) vyeti vya ushindi?
Link ZEC: Sheria ya Uchaguzi Zanzibar inaruhusu mtu kujitoa, si chama