Ze Utamu Blogger

Status
Not open for further replies.
Wana JF huyu jamaa yuko wapi?amefikishwa mahakamani au yuko huru?
yuko kizuizini?

Ulipaswa kuuliza Chenge na Rostam haya mambo ya Ze Utamu hayana tija kwetu wasiwasi ni kwenu wakware. Akamatwe asikamatwe sioni athari yeyote kwa mlalahoi. Besides Mlalahoi kakwambieni vizuri tu, hakuna kesi kwa sababu mpaka kesho hawamfahamu mtu mwenyewe asa watashitaki ruhani?
 
Itakuwa mzee wake ameomba radhi...kijana amepotezwa ameambiwa asiguse blog tena!!kwa maandishi tena!!mambo yameisha!!atajitetea kuwa labda kila mtu alikuwa aanaweza post pic yake...ila yeye asingeweza kuweka picha ile ukijumlisha na msamaha wa mzee!!!kwisha
 
Malecela Peter Lusinde

Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza, kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo. Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.
 

Attachments

  • Ze Utamu blogger under arrest.pdf
    66.5 KB · Views: 119
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom