Ze Utamu Blog: Ni aibu kubwa mno kwa taifa!

Status
Not open for further replies.
kama unaangalia zamani kidogo UTAMU wakati inaanzishwa kulikuwa na mtu anaitwa Abdalah Issah sasa huyu abdalah issa ambaye ni mfanyakazi wa Shigongo ana habari nyingi na za ndani zaidi kuhusu THEUTAMU historia inaonyesha hivyo na hata rudepichaz anavyojibu email za watu IP ADDRESS yake ni ya globalpublishes hapo bamaga ni kitu kirahisi tu
 
Sasa huyu Erick shigongo si mlokole type!Kwa kweli inavyoonyesha hii The Utamu imeumiza wengi sana!na haya magazeti yake yako mbioni kufa otherwise abadilike!
 
Hata hivyo pongezi kwa alie weza muangusha,invisible ur great wizard in this
kula tano mtu wangu saaaaaaaaaaaaaafi sana.

Tumehangaika wengi macomputer wizard kumleta offline lakini alkua anatuzidi ujanja



we frahi tu...na wewe ulikuwamo kati ya wahanga wachafuliwa?
Nakuona umefrahia kweli kweli....lakini si wengine tutamiss kujua data za mafisadi wa ngono na kukwepa cycle ya kujinafasi....maana wengine cycle huwa kubwa na ya kutisha unaweza kuona mnazunguka kwenu wote indirect.
 

Mkuu Invisible,

Mkuu Invisible mie nina mawazo tofauti sana kuhusu hili.
Ni vema kutofautiana mkuu... Ndo discussion yenyewe!

Ndiyo ilikuwa inawachafua ila kwa kiasi flani iliweza kueleza bayana yaliyo muhimu,hasa wale wenye tabia ya uzinzi ,ilisaidia watu kuwafahamu watu hao jinsi walivyo.Ye s ilisaidia kupunguza maambukizo ya ukimwi sababu watu walipata tahadhari kuhsu hili.
Kuna mengine nakubaliana naye jamaa, tatizo ni kuwa kuna vitu vingine alishindwa kuvi-manage. Yani kuna ukweli katika baadhi ya kashfa alizokuwa akiibua, kweli kabisaa, tena imesaidia watu kuwajua watu flani... Binafsi tatizo langu ni kwenye uwekaji picha huku zikiambatana na matusi, angekuwa detective mzuri kama angesajili tovuti, aweke fomu ya watu kujisajili kabla ya kuanza ku-comment ili wanachama wake wanapochangia wachangie kwa heshima kidogo. Matusi yalizidi mkuu!

Yani kazi yake ingekuwa na heshima kubwa na wengi wangenyooshwa kwa kuwa na tovuti au blog ambayo mtu anapojisajili anatambua anafanya hivyo kwa hiari yake, hapo analindwa na COPA laws!
Suala la kurekodi e-mail za watu nina mashaka nalo sana kwa kuwa nafahamu structure ya blog ilivyo.inachukua path tu na mwenye uwezo wa kujua ni nani huwa ana post picha inafahamika na administrator wa google na tena anajua kwa kutumia IP address.si rahisi kumfahamu owner wa blog kama akidanganya.what google stores is the Path only..Hivi nchi hii ambayo haina hata Data Protection Act kwanini tunapenda kuwatisha sana watanzania???this shit happen hata kipindi kile Jf inafungwa kwa sababu ya kijinga sana 'uhalifu wa kimtandao'?sheria ya wapi?
Emails labda hujaelewa ni kivipi... Ni kuwa mhusika anafahamika tu, clearly kabisaa! Na barua pepe yake nahisi akibanwa anaweza ku-reveal waliokuwa wakimtumia barua pepe (labda watumie fake mail accounts kutuma picha husika) na hilo ndilo nililolenga kuwahadharisha ambao walikuwa wanaendelea kusukuma picha huko, watambue barua pepe hiyo imekuwa chini ya uangalizi tangu Julai mwaka huu.

tusiwatishe watanzani kuwa kuwa uwezo wa kuwakamata wachangiaji labda kama mwenye blog awataje mwenyewe.
Niwahakikishie watanzania kuwa wasitishike na masuala ya online, ila unapoona kuna kitu si fair basi unaposhiriki ujue kuwa unafanya vile kwa ridhaa yako mwenyewe! Huyu labda awe nunda asimtaje mtu na ahakikishe anafanya kufuta kila kitu kwenye barua pepe yake!

I know why imefungwa na nina uhakika kaifunga mwenyewe kwa kupewa kitu kidogo sababu ilimgusa flani mwenye maslahi huko.
Hapana, si kwa hiari yake mwenyewe... Sina maelezo zaidi juu ya hili :)

Sikuwahi kuchangia huko ila kila weekeend nilikuwa nikipita katika blog hiyo kujua ni upuuzi gani unaendelea katika nchi yangu.Yes kuna mengine aliharibu ila alisaidai madada zetu kuwajua mabazazi.
Binafsi sikuwahi kwenda kule hadi ilipoanzishwa hii topic nikajua watanzania wameguswa pabaya! Kumbuka, huyu aliwahi kuwa kwenye server yangu pia, alipozidisha mambo zake nikaona hapana, nikamwacha aende penye uhuru zaidi! Kazi ilikuwa nzuri, tena sana mkuu... Naamini dada zetu waliweza kuwajua mabazazi kama unavyosema hapo juu, si dada zetu tu, hata kaka zetu naamini... Tatizo lake ni moja "Uhuru wa commenting..." Ulizidi. Too much of anything is harmful bro!

Hakuna tofauti kati ya Jf na The utamu,The utamu wanajadili mafisadi wa ngono,siye tunajdili mafisadi wa wizi wa mali zetu.tofauti ni kwamba kule watu wako huru zaidi
Hata JF watu wako huru, watu wamewajadili wengi humu kutokana na tabia zao chafu, kuna watu wa BoT wamejadiliwa humu, commenting ya hapa inakuwa na heshima kwakuwa mtu anapoandika anatambua wazi kuwa amejisajili kwa hiari yake na anabeba jukumu la kulinda nickname aliyojisajili nayo! Inawezekana matusi yaliyokuwa yanaonekana kule yakawamo yangu, yako, ya GT na ya hata Mwanakijiji etc... Ni kwakuwa tulikuwa hatuna ID maalumu ya kuandikia!

Admin wa Utamu,kama wakifungulia Kesi naomba unitafute nikusaidie sababu wewe hauna kosa
Naamini anakusoma, kesi hana, akiwa nayo hata mimi naweza kumsaidia...!
 
Am supporting u,mwana badala ya kukaa vibarazani sas wanasutana ktk website.Hivi hakuna wadau wanao shughulika na website ili ikiwezekana ifungiwe.
 
Hata kama UTAMU ni tatizo,lakini tatizo kubwa ni visitors wa blog hiyo.Let's be honest:ni watu wangapi waliokuwa wanaitembelea blog hiyo ilhali kabla haijafunguka kuna warning kuhusu contents zake?Binafsi naona tofauti pekee kati ya UTAMU na magazeti yetu mengi ya udaku huko nyumbani ni ownership.Kwamba wamiliki wa magazeti hayo wanajulikana wakati UTAMU ameendelea kuwa katika hisia zaidi kuliko reality.

Jaribu kwenda kwenye internet cafe halafu angalia history ya waliokuwa wana-browse mtandao na utaamini kwamba wapenzi wa mambo ya ngono ni sehemu kubwa katika jamii yetu.

Chema chajiuza kibaya chajitembeza.Laiti tovuti zenye mambo yanayoonekana hayapendezi machoni mwa watu flani zisingetembelewa ni dhahiri zingejifia kifo cha asili.Tunaweza kushinda na kukesha hapa tukisherehekea kufungwa kwa UTAMU lakini ni dhahiri kwamba ikianzisha blog nyingine yenye picha za ngono itapata umaarufu kama huo wa UTAMU.Na history inatuonyesha kuwa hii ni mara ya pili kwa blog hiyo kufungwa lakini baadaye inaibuka tena.

Pengine ni muhimu pia kujiuliza kwamba baadhi ya picha na habari chafu zilizokuwa zinawekwa humo kwenye blog ya UTAMU zilikuwa zinatoka wapi kama sio kwa hao mashabiki wanaoitembelea kila siku?Sawa kuna nyingine zilikuwa zinafanyiwa usanii lakini kuna nyingi tu ambazo naamini zilikuwa zinapelekwa na akina dada walioporana wanaume.

Kupotea kabisa kwa blog kama UTAMU kutawezekana tu iwapo curiosity ya umbeya na mambo ya nyuchi miongoni mwa wanajamii itaondoka,and that sounds impossible kwa vile people vary because we differ
 
Jaribu kwenda kwenye internet cafe halafu angalia history ya waliokuwa wana-browse mtandao na utaamini kwamba wapenzi wa mambo ya ngono ni sehemu kubwa katika jamii yetu.
Hilo ni kweli mkuu! Yani asilimia kubwa ya wanaoenda internet cafe wakimaliza kusoma mails zao basi wanahamia WorldSex au kwingineko kuvuta pumzi!

Tunaweza kushinda na kukesha hapa tukisherehekea kufungwa kwa UTAMU lakini ni dhahiri kwamba ikianzisha blog nyingine yenye picha za ngono itapata umaarufu kama huo wa UTAMU.
Duh, haina haja ya kusherehekea kifo cha Utamu, kuanzisha blog kama ile ni rahisi, ni suala la kubonyeza "Create Your Own Blog" na ukiwa na Gmail account you're done! Unaanza kushusha mipicha tu! Simple sana, lakini unapoanzisha issue kama hiyo uwe fair, jaribu ku-filter comments, jaribu kuangalia kama wanaokutumia picha hizo wanatuma kwa dhamira safi ama kwa nia ya kuchafuana... Mimi kutofautiana na mume wangu au b/f wangu akaanza kupakazia kuwa nasambaza ukimwi UK au US si fair mkuu...

Sawa kuna nyingine zilikuwa zinafanyiwa usanii lakini kuna nyingi tu ambazo naamini zilikuwa zinapelekwa na akina dada walioporana wanaume.
Yeah, kuna aliyoweka akidai ni Do Me Concert, alikuwa tayari kawapaka matope walioandaa tamasha hilo... Ni tusi kubwa kwa tamasha ilhali picha ile aliitoa kwenye blog ya watu wa Afrika Kusini na ni ya mwanamuziki wa huko Bondeni!

Kupotea kabisa kwa blog kama UTAMU kutawezekana tu iwapo curiosity ya umbeya na mambo ya nyuchi miongoni mwa wanajamii itaondoka,and that sounds impossible kwa vile people vary because we differ
The red inked one... Mkuu kiswahili chako kikubwa sana... Neno hilo kwangu geni, lakini nahisi nimekusoma. Good comment either!
 
ahhh mie bwana niliijuia siku ya Jumamosi ndio maana hata kule kwenye ligi yangu na Mwanakijiji nilikuwa abit slow kwa sababu ile ya FRANK ilikuwa ndio kwanza niko kwenye maoni post number 130 out of 600!

Achiliambali yule jamaa wa benki kuu

nishai kweli i was so keen nayo jana maana kulikuwa na jamaa kibao ninaowajua kama yule mtoto wa KIMEI wa CRDB

Lakini kwa sababu ni blog i am sure itaibuka nyingine tuuu...it was ure entertainment sema mapicha mengine yalikuwa nishai na hilo nakubaliana na Invisible
 
UTAMU kama blog inaweza kwenda lakini spirit ya UTAMU bado imo katika jamii yetu. Ushahidi ni mauzo ya juu ya magazeti ya Udaku. Watu wanapenda habari za ndani za watu maarufu. UTAMU alianza vizuri lakini baadae naona akawa ameishiwa (may be kukosa muda na fedha za kufuatilia habari kikamilifu) kwa hiyo akawa anaposti picha hovyo hovyo.

Pia sina uhakika ni kwa nini imefungwa. Google (ambao ndio wamiliki wa blogspot.com) huwa wanachambua blogs na kufunga zile wanazoona hazina mantiki. Au ni kwamba wamepata malalamiko mengi labda kwa hiyo hawataki matata na wateja wao.

All in all, maadamu UTAMU amepotea nadhani hautapita muda mrefu itaibuka blog nyingine yenye maudhui ya UTAMU.
 
Invisble heshima mbele!

Huu ndiyo uzuri wa teknolojia. Globalization imetufungua macho wengi wetu humu. UNAJUA HATA SERIKALI ZETU KUNA MAMBO SASA HIVI WANAFANYA WANGETAMANI COMPUTER ZOTE ZIPIGWE MARUFUKU! Lakini wakati bado wanahangaika namna ya kudhibiti komputer..tayari Blackberry iko mtaani,.......

Hivi ni nani anayejua what is good on our behalf kama jamii? Invisible you have assumed that role. Mi naungana na Gembe. Ukiangalia ile globu ya UTAMU post moja ilikuwa inaattract comment zaidi ya mia! tell me, why blame jamaa? mi nadhani hii inaonyesha jinsi jamii yetu ilivyo na vipaumbele vyake viko wapi.

Again simtetei Utamu, personally niliwahi kuingia mara moja, ingawa sikukubaliana na jamaa. lakini hakuna aliyenilazimisha kuingia huko..na sikwenda tena! Ila swala la Ngono limeshamiri sana katika ulimwengu wa leo. Na ubaya kuna watu hapa wanamkondemn UTAMU wakati wao ndo nambari one..kupiga picha wenzao wakilala nao..kwani UTAMU picha anazitoa wapi? si anapewa na watu?

Hivi unaonaje kama lets say msichana ambaye picha yake imeanikwa pale kumdharirisha, angechukua hatua na kwenda kwenye sehemu inayohusika.. si unaona lingekuwa somo kwa watu wenye nia na mtindo wa kuwadhalilisha wenzao? (after all umesema kwamba jamaa anajulikana na barua pepe mnazifuatilia kujua ni nani...so isingekuwa taabu kumjua)..lakini sasa mlichokifanya ni kutatua tatizo kwa mda mfupi.....

Unafikiri kwa nini sisi JF jamaa alitupeleka mahakamani? si angeamua kuifuta isionekane tena? Iam sure hili si somo gumu kiasi hicho!


Mwisho invisible na wengine hapa....naomba niwaulize UTAMU amevunja sheria gani ya nchi? (kumbuka kabla ya kuingia kwenye ile globu kulikuwa na disclaimer)!!!!!
 
Hawa jamaa wa theutamu ndio zao wanajaribu kutafuta popularity wanajidai blog imefutwa kumbe wanatuzuga... mbona wamebadili jina kiaina
 
Hawa jamaa wa theutamu ndio zao wanajaribu kutafuta popularity wanajidai blog imefutwa kumbe wanatuzuga... mbona wamebadili jina kiaina
Yep, aliyeisajili hiyo blog si wa awali. Ninachomshauri aloanzisha blog hii ajaribu ku-filter matusi kwenye comments.

Namtakia mafanikio kwa kazi yake mpya...! Ni 'mtoto wa mkubwa' huyu mpya na yupo UK ndiye alikuwa anashirikiana na Shigongo!
 
mhhh hii si sawa na ile ya mwanzo...lakini kusema ukweli hawa jamaa walikuwa wanatupunguzia sana traffic huku
 
mhhh hii si sawa na ile ya mwanzo...lakini kusema ukweli hawa jamaa walikuwa wanatupunguzia sana traffic huku

Hahahahah mkuu ina maana wengi walihama hapa JF na kwenda UTAMU? this is interesting!! wacha utamu iwepo ishughulikie watoto wa mafisadi na JF inashughulikie mafisadi wenyewe katika kila angles....

Ushi
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 50 (12 members and 38 guests)
BantuGirl, Dan M, Domo Kaya, Freelancer, Jasusi, Kandambili, Mizani, mwenda_pole, paulimasao, Ushirombo

mnahusika nini?
 
JE? ULIONAJE HIZO PICHA NA HATA KUZICHAMBUA KWA KINA NA KUJUA NI REAL PICS? ULIOTESHWA NJONZI? TUACHE UNAFIKI!
Sishindwina silegei ni kwamba mimi nilikuwa msomaji mzuri saaana wa theutamu kila siku napita zaidi ya mara 3,nasema ukweli najua hata wewe ulikuwa kama mimi ila unazuga machoni mwa watu........

Blogu ilikuwa njema sana yaliwekwa mule nisema 75% ni kweli na imesaidia wengine na majambga ambayo yangetukuta.......

KUMBUKA,UNAPONYOOSHEA WENGINE KIDOLE UJUE VITATU VINAKUELEKEA WEWE MWENYEWE.
Nadhani nimeeleweka
Sipingi mimi nilikuwa mlevi wa Theutamu......hata wewe najua ulikuwa nami kule huwezi kusema blogu mbaya wakati hujaona kilichomo ndani..........content imekwambia kuna mamabo mabaya wewe bado uka click kwenda mbele kuona UTAMU uliomo......tuliza munkari kaka/dada
 
Yep, aliyeisajili hiyo blog si wa awali...
Mkuu is the same Guy......just check the Utamu hints pale chini mara ya mwisho niliangalia walikuwa wametembelea watu zaidi ya Mil 1 na leo mimi nipo wa 1069874.......waache waendeleze libeneke....
Ninachomshauri aloanzisha blog hii ajaribu ku-filter matusi kwenye comments.

Namtakia mafanikio kwa kazi yake mpya.
hapana comments ndio Utamu wenyewe wa kujing'ata.......hivi mnajua ni jinsi gani inavyosaidia blogu ile?
Mibazazi kibao Dar ilipunguza nawaambia walikuwa wanawamega sana dada/wake na mademu wetu.........
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom