Ze Msaada please

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Wakuu wote humu jamvini nawasalimu.

Nilikuwa na rafiki yangu mmoja anataka kufungua biashara yake sehemu fulani hapa Tanzania. Kama ilivyo ada akaenda kwa hawa jamaa wa TRA. Akawaambia lengo la kufungua biashara, yakaanza maswali kama ilivyo ada.

1- Mtaji umepata wapi
2- Kodi ya nyumba unalipa shilingi ngapi.
3- Una wafanyakazi wangapi.
4- Unategemea kuwa utakuwa unauza shs ngapi kwa siku (hapo hajafungua biashara!)
nk!nk!

Jamaa wakateremsha hesabu zao, wakamwambia kwa kuwa returns zako kwa mwaka ni zaidi ya 20m basi unatakiwa uwe na mhasibu!

Swali, Je, kuna ulazima wowote wa kuwa MHASIBU wakati huyu mwenye biashara ana uwezo wa kutunza kumbukumbu sahihi na kuziwasilisha TRA bila kupitia kwa huyu wanayemwita mhasibu?

Kuna sheria inayoagiza kuwa wafanyabiashara hawa wadogo wawe na wahasibu?

Naomba mwenye ufahamu wa hili anifafanulie tafadhali. Natanguliza shukrani zangu.
 
Kama ni kampuni,hesabu lazima zipitiwe na CPA according to Income Tax Act. Otherwise kama ni sole propriator mwenye complex operations na hesabu zake ni complex watahitaji pia uwe na CPA.
Nadhani TRA hawamaanishi jamaa aajiri kabisa Mhasibu,wanamaanisha hesabu zake lazima ziwe zinaandaliwa au zinapitiwa (baada ya yeye kuziandaa) na Certified Accountant.
Mkuu Eeka,haya mambo ni ya kiutaalam zaidi labda kama huyo mtu anayo taaluma ya uhasibu sawa.Kuna baadhi ya matumizi ambayo ni ya kibiashara kabisa,lakini huwezi kuyaorozesha kwa ajili ya tax returns kwani hayaruhusiwi according to Income Tax Act.
Mwisho ningependa kuwashauri watu wa TRA wawaelimishe wafanyabiashara kuhusu complexity ya Icome Tax Act na umuhimu wa kuwa na mhasibu and/or lawyer wa kuandaa hesabu au kuwashauri wanapotaka kufanya transaction yoyote juu ya tax consequences ya kila transaction.
Mkuu kama kuna lolote ambalo ungependa kujua au huyo entrepreneur,kuna watu wengi humu jamvini wana knowledge za kutosha wanaweza kusaidia.Mimi nimeelewesha kwa kiasi,wapo wajuzi zaidi yangu wanaweza kutusaidia.
Asante
 
Hapo TRA hawamaanisha lazima aajiri mhasibu mwenye CPA;ila anapokua anaanda hesabu zake atalazimika kumtumia huyu jamaa katika kuthibitisha hizo hesabu za kampuni yake pale anapokuwa anahitajika kupeleka TRA.
 
Hata hivyo TRA wasumbufu kwani wangeacha jamaa aanze biashara ndio wamtoze hiyo kodi ma makorokoro mengine. Hali ndio imekatisha watu tamaa ya kuanzisha biashara. Wanaleta mambo kibao bila mpango. Ukweli ukianza biashara mwaka wa kwanza bado hujajua kama itakubali na hata masuala ya masoko yatakuwa bado. Ni bora wampe minimum offre aanze shughuli.
 
Biashara zinafanywa kwa kufuata sheria za nchi,hatufanyi biashara kufuata matakwa ya mtu mmoja mmoja. Jamaa anaanza biashara,amefanya jambo la msingi kwenda TRA kufanya biashara yake ijulikane kabla hajaanza kama sheria inavyotaka.
Inatakiwa ujue implications za kuanzisha biashara at the begining of the business,sio itokee baadaye TRA wanakukadiria kodi unasema oooh,nimebambikwa na vitu kama hivyo.
Katika kuanza biashara,kitu kimoja ambacho watu wanasahau ni mambo ya kodi.Haya mambo ni muhimu sana kwana yatasababisha outflow of future economic benefits which means they will eat part of your profit or all if you don't plan well your transactions.
Watu wengi wananzisha biashara kwa kuangalia mapato na matumizi ya moja kwa moja. Kuna matumizi ambayo ukiwa katika biashara halali ni lazima utalipia tu,mojawapo ni kodi.Hivyo ni lazima ujue itakuaje mwisho mwa mwaka wa kibiashara.
Asanteni,naomba kuwasilisha.
 
Na pia mtu anapoanzisha biashara huwa anatakiwa kuwa amefanya utafiti angalau kidogo, kuhusu kiasi cha masoko/mauzo, matumizi n.k. TRA huwa wanakuuliza wewe mwenyewe ulivyokadiria, sasa kama hujui hata makadirio, basi kuna tatizo, biashara inayoanza hivyo ni ngumu kujua kama kuna dalili ya mafanikio au la.
Ni vyema unapotaka kuanzisha biashara ukatafiti yale yote yanayohitajika ili kama haifai basi usianzishe.
Mara nyingi wanataaluma wanazungumzia "Business Plan" hii si lazima iwe na makabrasha kibao lakini iwe hata kichwani mwako ili ujue wapi unakwenda, hapo mambo ya kodi, michango ya VETA, maana ya uajiri na kodi zake hayatakuwa ya ajabu.
Hayo aliyo ambiwa TRA ni ya kawaida na wala hayana tatizo lolote ili mradi umejitayarisha vizuri.
Wengine wamsaidie mwenzetu asije kata tamaa akidhani haiwezekani!!!!!!!!!!!!
 
Karibu yote yaliyosemwa hapa nakubaliana nayo. Tuwe wakweli, ni wangapi hapa kwetu wanaanzisha biashara hizi ndogondogo wanakuwa na business plan? Watu wanaofanya tafiti kuhusu biashara zao ni watu wanaotaka ku-invest kwenye biashara kubwa kubwa.
Huku jamvini kuna watu wana internet cafe, kuna wenye retail shops, maduka ya nguo na zote za aina hii. Tujiulize waliaseek hii tunayoita business plan ama hata walifanya consultation toka kwa hawa business planners?
Ninayemwongelea hapa ni mtu wa kawaida kabisa,,, alikuwa akifanya kazi mahala fulani,,, akalipwa mafao yake hayazidi milioni 10. Aka-plan biashara kuuza vyakula na vitu vya nyumbani (somesort of Grocery).
Hataki kukwepa kulipa kodi na wala hajakataa. Na alikuwa muwazi kwao pia kuwa anaweza kuuza kati ya Tshs 40,000 mpaka 80,000 Tshs kwa siku. Mheshimiwa wa TRA baada ya kufanya mahesabu yake akamwambia kuwa anatakiwa awe na mhasibu wake wa kumfanyia mahesabu. Jibu hili ndilo lilompa mashaka na kuomba msaada huu.
Kwa kiwango cha mapato haya ya huyu mjasiria mali anahitaji kuongeza mdomo mwingine wa kula haka kamtaji kake?
 
Nadhani kua wa TRA humu JF hebu tusaidieni kuelmisha wananchi wanataka kuanzisha vibiashara. TRA iwe ikimweleza kwa upana kuwa anatakiwa na Mhasibu yupi au ikwa namna gani. Kama alivyosema eeka Mangi unaongeza walaji kwa kuongeza Mhasibu.
Inanikumbusha wakati fulani Mama mmoja alilalamika kwa mtu fulani kuwa kabiashara kake kanaibiwa kidogokidogo na wafanyakazi. Basi akashauriwa na mtu mmoja waweke "internal Auditor"................malipo yake mara mbili ya hela anazoibiwa !!!!!!!!!!!! Mama akaona afadhali waendelee kuiba kidogo hivyo hivyo.

Elimu na uzoefu unaweza waokoa wengi wa wajasiria mali wanaoanza.
 
Back
Top Bottom