Ze komedi -vs- Futuhi

utamfananishaje mamba na mjusi kafiri?wale wasiomjua mamba watadai mjusi zaidi, ze comedy wapo juu, ni wabunifu, ebu atoe mtu ubunifu wowote wa futuhi,anything new ambacho hawajaiga from ze comedy.ndo tz bwana ukianza saloon mahali mda si mrefu utajikuta umefungiwa hata njia namna saloon zitavyoenea jirani yako, ndo walichofanya hawa wasukuma na chanel ten.basi waje na usanii tofauti,tuone kitu tofauti,si kuigaiga halafu mnadai eti wapo juu.huu mjadala ufe, ze comedy wapo juu ful stop
 
Ze comedy wakieendelea na lugha zao wataangaliwa na mademu zao siku si nyingi
 
Ze comedy nao si wabunifu kwani waliiga kutoka katika kipindi cha Daily Show hurushwa CCN International,wapunguze mijitusi kwani hatuwezi kucheka bila matusi
 
Ze comedy nao si wabunifu kwani waliiga kutoka katika kipindi cha Daily Show hurushwa CNN International,wapunguze mijitusi kwani hatuwezi kucheka bila matusi
 
tena ile mbaya, wako juu sana. Nimekosa mizengwe basi wiki nzima nakuwa nahuzuni. Hao futuhi nao wanafuata siku hizi halafu zecomedi wanazidi kushuka ila wako juu pia. Ranking yangu kwa wiki iliyopita ni Futuhi then Mizengwe then Origino comedy.
 
Mimi naona mwanzo Ze Komedi walikuwa juu, lakini Futuhi siku hizi naona wanakubalika zaidi. Sababu kubwa naona Komedi wamebweteka na kufanya mambo yanayoonekana kutokuwa na ustaarabu kama kumdhihaki mwajiri wako wa zamani, kutania watu maarufu walio filisika n.k. Nadhani mtu ukianza kufanya mambo kama haya anayofanya Ze Komedi, ung'aavu wako utapotea with time hata kama una kipaji kizuri.
 
Ze comedy nao si wabunifu kwani waliiga kutoka katika kipindi cha Daily Show hurushwa CNN International,wapunguze mijitusi kwani hatuwezi kucheka bila matusi

pia kuna muvi ya kinaijeria inaitwa bird flu. Walichomoa huko kile kipande cha mtoto haram na DNA
 
Ze komedi hawana ubunifu...hata miziki wanaigiza na uigizaji wao unachusha.Siku hizi nimekoma kabisa kuwaangalia maana huwa napata kichefuchefu!Mara ya mwisho nilitaka kutapika!
Na futuhi wana vipaji natural..japo naona tatizo lao ni direction! Wao wananipa good time maana hawaimbi nyimbo za watu wala kuwadharau watu....
 
Wajameni hawa kina original comedy wanaboa hasa yule wa kufulia na yule mhaya anaye act kama tajiri.

Hawana kitu kipya na wanaonekana kama mashoga...mijiaba mizima inaact kama wanawake na wanawake wako wengi.Ahhh...bora ya futuhi wanachekesha.
 
Kwa kweli Comedy lazima wajiangalia upya, maana FUTUHI wanaangalia mapungufu yao alafu wanayafanyia kazi.... NDO MAANA WAKO juuu

COMEDY TAKE CARE, MTAACHWA SOLEMBA
 
Hivi wale wa channel Ten wanaitwaje wanaonyesha kipindi chao jumamosi no naona wanakuja juu

wale wanaitwa vimbwanga time, ila na wao sijui kama wapo kwani kuna wakati walisuasua. Hawapewi air time ya kutosha na media kama ze komedi
 
ze komedi wako juu ukiwa mfuatiliaji Futuhi wanaiga yaani ni copy and paste ya ze kometi waweke mpangilio wao. they have to be creative.
 
Back
Top Bottom