Ze Comedy Watinga Bungeni

Pamoja na yote, nadhani nia ya EATV ilikuwa kuwakomoa vijana tu! Na ilitumia nafasi ya ujinga wao wa kutojua sheria kuwakomoa.........which is not good!

Kwa hali ya Kitanzania na jinsi vijana hao walivyojitahidi kujiajiri, nadhani kwa maoni yangu EATV walitakiwa kama walikuwa na nia nzuri na vijana hao ilikuwa ni kuwaita na ku-negotiate mkataba wao upya kwa kuangalia na kuzingatia mahitaji ya wakati!!

Mr. Mengi akiwa ni mfano katika kusaidia vijana kujikwamua kimaisha......nadhani hapa una mtihani kitaifa kuonesha ukweli wako katika kusaidia vijana, na sio kutumia nafasi yako ya kipesa na katika society kuwakomoa vijana wanaotaka kwenda mbele kimaisha.

Elewa kuwa jamii kila siku huwa inajifunza kwa makosa......itaicost EATV in a way in future kama sio IPP Media kwa ujumla kwa hili litokealo!!!

Take care
 
Mbona nasikia hawa watu zi komedi eti waliwapinga mafisadi halafu mara ghafla wakabadili mawazo?
Ama na sasa wamebadili mawazo tena lakini kwa vitisho?
Kipanga MWEUPE..Hiyo ni HAKI KWELI KWA KIPANGA MWEUSI?
Nafikiri pia u take care kwani kunayo kipanga nyeusi.
 
Mkuu Kipanga Mweupe
Hakuna Kukomoana Tuondoe Ushabiki !!!!!
Ze Comedy Mali Ya Eatv!!!waende Na Kwa Raisi!!!1kama Uamini Mi Nilifwatiliaa Kwenye Baraza Lao !!!!wanapiga Porojo Hao Walikuwa Wamefwata Per Dm Uko Dodoma!!!!wanachotakiwa Amam Wakae Chini Na Eatv Wamalizane Kwa Amani Au' Kama Kweli Wanavipaji Halisi Kama Wanavyoonyesha Waunde Jina Lingine'''

''''''''''''''''''''''''''''''''ze ---------------------inviscible''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''

Mbona Jina Rahisi Tu
 
Nadhani watu waache ushabiki usio na maana kwanza. Tujadili issues kuhusu hili.

Sheria za milki ubunifu zinaeleza wazi kwamba mtu anayetengeneza kitu kutokana na ubunifu wake ndiye mmiliki! Mara nyingi huwa mbunifu napoteza haki ya kutambulika kama mwenye 'mali' hiyo inayotokana na ubunifu kama ni mwajiri kwa maana kwamba kubuni vitu kama hivyo ni kazi yake na analipwa mshahara na mafao kwa kutenda kazi hiyo. Yatakiwa lakini kuwepo na mkataba wa ajira baina ya pande mbili. Hii kitaalamu inatokana na dhana kwamba mwajiriwa anakuwa anafanya kazi ile ili kutekeleza majukumu yake na kukidhi matakwa ya mwajiri kwa maana kwamba asingefanya hivyo basi asingekuwa na manufaa kwa mwajiri wake.

Kwa kuwa hakuna mtu awaye yote kati yetu anayejua kama hawa watu kwa mujibu wa makubaliano yao na EATV walikuwa waajiriwa au hapana, tuache ku-pass judgment kuhusu EATV. Yawezekana kabisa hawa vijana wamedanganywa wakadhani wanaweza kuondoka na kila kitu wakati mkataba wao unasema vingine.

Iwapo ,kwa mfano, EATV ndiyo walikuwa waanzilishi wa kipindi kwa ku-conceive idea na kui-translate na hawa vijana wakawa walitafutwa kufanya kazi tu kwa kuingiza kipaji chao tu, uwezekano ni mkubwa kwa EATV kuwa mmiliki halali.

Kwa upande mwingine, pamoja na kuwa ndugu hawa waweza kwa mujibu wa sheria kuwa wao ndiyo waandishi na watengenezaji wa scripts na kipindi chenyewe cha Ze comedy, wakati EATV wakiwapa airtime, studio na vifaa vya kurushia na kurekodia, inawezekana kabisa walikubali kwamba kwa vile wanatumia mali za EATV kutengeneza vipindi vyao then, EATV wapewe haki miliki wakati wao wakilipwa fees tu. Kama makubaliano yapo hivyo basi haki zote zinakuwa mali ya EATV by virtue of the transfer in lieu of the fees and other things.
Kwa hiyo , ni muhimu sana kufahamu makubaliano baina ya pande mbili kabla ya kurukia issue.

Hili ni suala la kitaalamu zaidi badala ya kiushabiki. Na si kila mwanasheria anajua sheria juu ya milki ubunifu, kwa Tanzania bado wapo wachache sana ukilinganisha na mahitaji.
nafahamu kuna bush lawyers wengi sana wanaojifanya wanajua hii sehemu ya sheria, ila hawajui, na kwa kuwapa dondoo kidogo tu, advocate SWAI atachemka na vijana wanaweza kujuta kwa nini walimchukua kama wakili wao.
 
Pamoja na yote, nadhani nia ya EATV ilikuwa kuwakomoa vijana tu! Na ilitumia nafasi ya ujinga wao wa kutojua sheria kuwakomoa.........which is not good!

Kwa hali ya Kitanzania na jinsi vijana hao walivyojitahidi kujiajiri, nadhani kwa maoni yangu EATV walitakiwa kama walikuwa na nia nzuri na vijana hao ilikuwa ni kuwaita na ku-negotiate mkataba wao upya kwa kuangalia na kuzingatia mahitaji ya wakati!!

Mr. Mengi akiwa ni mfano katika kusaidia vijana kujikwamua kimaisha......nadhani hapa una mtihani kitaifa kuonesha ukweli wako katika kusaidia vijana, na sio kutumia nafasi yako ya kipesa na katika society kuwakomoa vijana wanaotaka kwenda mbele kimaisha.

Elewa kuwa jamii kila siku huwa inajifunza kwa makosa......itaicost EATV in a way in future kama sio IPP Media kwa ujumla kwa hili litokealo!!!

Take care

Kipanga hii inasond kama ni suhabiki zaidi kuliko sheria. Naona umekata na hukumu kabisa!
Tujue sheria inasemaje tu basi. Wasidanganywe na mashabiki wa Mengi/Manji.
Lakini kwa nini wasibadili jina tu na kutumia jina tofauti? kwani lazima waitwe ze comedy? si wanaweza kuitwa TBC comedy? shida iko wapi? Naona na wao watatuchosha kwa upuuzi wa kujifanya ujuaji na mwisho tutaishia kudharau hata maigizo yao kama tulivyodharau ya wengine wengi yasiyo na mashiko.
 
Back
Top Bottom