Ze comedy waanza kufulia kweli ni aibu wanaomba nauli hata bia kualikwa!?

mamanalia

JF-Expert Member
Nov 7, 2009
666
146
Orijino Komedi walilia nauli

Tukio hilo lilitokea Novemba 11 mwaka huu ,Oysterbay jijini Dar es Salaam, katika viunga vya Club hiyo ambayo iliteketea kwa moto hivi karibuni.

Komedi walifika katika eneo hilo kwa ajili ya kurekodi picha za kipindi chao lakini waliacha jukumu hilo na kujichanganya kwenye mkutano wa waandishi wa habari na uongozi wa Club Maisha uliokuwa ukiendelea.

Wasanii wa kundi hilo waliotinga kiaina kwenye mkutano huo ni Emanuel Mugaya ‘Masanja,’ Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Joseph Shamba ‘Vengu’, Alex Challamilah ‘McRaegan’ na Lucas Mhuvile ‘Joti.’

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wasanii hao walivamia mkutano huo ambapo Masanja ndiye aliyekuwa wa kwanza kupenya na kwenda kukaa kwenye safu ya mapaparazi hali iliyozua mshangao.

Baada ya mkutano kwisha Masanja alimzukia mmiliki huyo Hellen Sweya na kuomba nauli ili yeye na wenzake watimue kutoka kwenye mkutano huo.

Hata hivyo, mwanamama huyo alimjibu kuwa, hawezi kumpa nauli kwa vile hali ni mbaya na hakuwa amemwita kwenye mkutano huo.

Ndipo Masanja alipoamua kukomaa: “Nimejiandikisha bwana, sijaalikwa kivipi, sasa mimi sina nauli, nipe niondoke zangu.
Akajibiwa: “We Masanja usilete utani hapa. Kama ulialikwa hapa wewe ni wandishi wa chombo gani?”

Hata hivyo, mchekeshaji huyo anayetumia nguvu kuchekesha, alizidi kukomaa kutaka apewe nauli ambapo safari hii alikwenda kuongea na bosi mwingine ambaye naye alimchukulia kama alikuwa akiigiza tu.

Wakati Masanja akikomaa kutaka apewe ‘fea’ msanii mwenzake, Vengu alifika na kuongeza nguvu ya kudai ‘masurufu’ hayo.
Mpaka mapaparazi wetu wanaondoka ukumbini hapo, haikujulikana kama wasanii hao walipewa nauli au la!

Mmefulia haooooooooooo!!!!!!!!!!!

Source: http://www.globalpublisherstz.com/2009/11/13/orijino_komedi_walilia_nauli.html
 
Mbona walikuwa na landcruiser la TBC,tena lina namba za STK ....sasa nauli ilikiuwa ya nini?au walitaka kupiga mzinga tu?

kuna habari zingien huwa hazina uhakika kabisa ndo maana mtu mmoja hapo kasema ni udaku
 
Mbona walikuwa na landcruiser la TBC,tena lina namba za STK ....sasa nauli ilikiuwa ya nini?au walitaka kupiga mzinga tu?

Nauli wanazogaiwa waandishi ni kama hongo, wengine wanafika na magari yao full tank, lakini bado wanagaiwa nauli!
 
The comedy hawajafulia kama ni issue ya kuomba nauli walikuwa wanaigiza tu.walifika kwenye eneo la tukio wakiwa na gari la kibaruani kwao kwa ajili ya kurekodi mengine ilikuwa ni mbwembwe tu.
 
Hivi utumwa huu wa waandishi wa habari kusubiri wapewe nauli ndo wakatafute habari utaisha lini? nilifikiri wana hamasa ya kujikwamua na wenye vijisenti ili wawatendee haki katika habari. kwa mtindo huu sidhani kama wanaweza kuwa na ujasiri wa kuandika kasoro zilizoambatana na mazuri katika matukio.
Hongera waandishi kwa kujitundikia kitanzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom