Ze Comedy: Idea zimekwisha!

Kabota

Member
Aug 15, 2009
63
10
Jana nimekubali kuwa bila Masanja kama anchor kwenye Ze Komedi show inasuck! Show ya jana ilikuwa mbaya kinoma. Nilikuwa najilazimisha kucheka but sikucheka coz there was nothing to laugh at! Wale waliokuwa wanasoma wanajifanya kuongea viingereza mshenzi ndo walikuwa wanaboooooooooooooooooa! Kwa style ya jana Futuhi iko juu zaidi ya Ze Comedy yenu hiyo.
 
pole sana...kumbe una muda hata wa kuangaliaga hao watu
 
Jana nimekubali kuwa bila Masanja kama anchor kwenye Ze Komedi show inasuck! Show ya jana ilikuwa mbaya kinoma. Nilikuwa najilazimisha kucheka but sikucheka coz there was nothing to laugh at! Wale waliokuwa wanasoma wanajifanya kuongea viingereza mshenzi ndo walikuwa wanaboooooooooooooooooa! Kwa style ya jana Futuhi iko juu zaidi ya Ze Comedy yenu hiyo.

Mkuu Kabota

kwanza nakupa pole kwa kupoteza muda wako kuangalia upuuzi wa ze comedi.
Nilisema tangu mwanzo Ze Comedi walitakiwa kuwa makini sana pale walipoamua kujiunga na TBC1.

Jana nimekubali kuwa bila Masanja kama anchor kwenye Ze Komedi show inasuck! Show ya jana ilikuwa mbaya kinoma. Nilikuwa najilazimisha kucheka but sikucheka coz there was nothing to laugh at! Wale waliokuwa wanasoma wanajifanya kuongea viingereza mshenzi ndo walikuwa wanaboooooooooooooooooa! Kwa style ya jana Futuhi iko juu zaidi ya Ze Comedy yenu hiyo.

Futuhi inapaa kama KLM, HUWEZ IFANANISHA NA MAWAKALA WA RA,ze comedy, ambao wako biased, kitu ambacho ni hatari mno kwa survival yao!
 
@Ngogo: Mkuu nadhani sasa sitapoteza tena muda wa kuwaangalia! Tanzania inahitaji creative comedies sasa! Where are the actors guys?
 
Original comedi,Kwishney kabisaaaaaaaa.Kweli Usitukane wakunga na uzazi ungalipo-sasa ni zamu yao kufulia.
 
hahahahaha
mi juzi alhamisi niliipenda futuhi kama nin , wale jaam wako fiti balaa,
hawa ze comedy wanajifanya tu. ubishoo ni mwingi sana, bureeeeeee
 
ze comedy wanajaribu kuingia kwenye system isiyoyao ndo maana watapotea kabisa. huwezi kufanya comedy na wakati umebanwa na watu fulani.
 
Aisee hakuna aliyetarajia kifo chao cha ghafla,ila wakimbilie mlingotini kabla mboga haijamwaga......wanakoelekea sijui....wandhani matusi ndo komedi.....waswahili walisema sheria msumeno hukata... sasa waliofuliaaaa...ORIJINO KO M E .. coming soon
 
Hawa jama,hata akina zimbwela wa mizengwe,wanawapiga bao sasa...bora waombe wapunguziwe muda badala ya dk 50 za kipindi wapewe dk 15 tu.Wataonyesha vitu vichache lakini vya maana.La sivyo watapotea kabisa katika ulimwengu wa vichekesho.
Kwa sasa Dk hamsini za kuwaangalia the comedy,zaidi ya nusu ni mambo ya kuboa,na matangazo ya biashara.

Waangalie sana watafulia muda si mrefu,wawe wabunifu zaidi.

kuna kuna mtu wao wa karibu JF awambie waje wapate ushauri humu jamvini.
 
Original comedi,Kwishney kabisaaaaaaaa.Kweli Usitukane wakunga na uzazi ungalipo-sasa ni zamu yao kufulia.

wameshafulia, coz kile kipande kwa sasa kinawachoma ndio maana jana sikukiona kabsaaaaaaaaa. na muda pia walimaliza sijui saa moja kasoro ile?, yani ZE KOMEDI KWA SASA WAMELOWEKA HATA KUFUA BADO TENA WAMELOWEKA BILA SABUNI, Lol.
 
Laiti mdogo wangu Sekioni angekuwa anapokea Cmu zangu...!!!

Mbona mi nampata kwenye line yake ya tiGO!! Niliwahi kumwambia Seki hapo nyuma kidogo kwamba waangalie show inapoteza ladha na ubunifu unaporomoka kwa kasi. nilichojibiwa ni kwamba huo ulikuwa ni mtizamo wangu, na eti utafiti ambao si rasmi walioufanya ni kwamba wao wanakubalika zaidi kuliko kikundi chochote kile cha sanaa za maigizo/vichekesho Tanzania. Alienda mbali kidogo na kuniambia ati wao wako juu kuliko kikundi chochote cha burudani hapa Tanzania (including Bongo flavour artists na bendi za burudani)

Nikamwambia sawa, labda mimi nazeeka sasa!!!
 
In short ni kwamba hawa vijana walilewa sifa na kujisahau kama kuna kesho... wananikumbusha ile hadithi ya mtu aliyepika chele mwiingi na aliposhiba akafukia wote uliobaki, bila kukumbuka kwamba kesho yake ataumwa njaa

Vijana wanalewa sana, ni wazinzi na kibaya zaidi wamenza kudharau kila mtu hata wasiyemjua na hivyo kupunguza mvuto kabisa

Natumai watajivunja wabaki watatu waanze upya!!

MTM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom