Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Hawa jamaaa ni kiboko yaani huwa nacheka mpaka basi, ni kiburudisho tosha kabisa kwa siku kama hii ya Ijumaa. Kama ukiweza SteveD tafuta moja inayomhusu Lowassa akiwa anabanjuka.
 
Sina undugu na Kajura wala Seikh Yahya, lakini haya niliyatabiri hapa...

varangati la ze comedy

KIKUNDI cha Sanaa za Maigizo ya Luninga nchini maarufu kama 'Ze Komedi' kimeulalamikia uongozi wa East Afrika Television (EATV) kwa kuwazuia kutumia majina na uhusika wa uigizaji waliokuwanao katika kituo kingine cha TV kwa madai kuwa ni hati miliki yao.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ze Komedy Production, Isaya Mwakisyala alisema uamuzi wa Cosota kukubaliana na ombi la EATV kuwa Ze Komedy ni mali yao katika barua walioiandika Juni 9 na kujibiwa na Cosota Juni 10 kuwa ni mali yao si sawa kwa kuwa wao ni kikundi kinachojitegemea.

"Hatukuanzishwa na EATV bali tulikuwa ni waigizaji kipindi kirefu kabla hata hatujaonekana huko, kinatushangaza na kustaajabisha kitendo cha EATV kudai kuwa Ze Komedy ni mali yao, sisi tuanchosema tutaendelea kuwa huru na kubakia vile vile katika uigizaji huo kama kawaida," alisema Mwakisyala.

Alisema mkataba wa uhalali wa kumiliki kikundi cha Ze Komedy waliupata Julai Mosi mwaka 2007 kwa cheti halali baada ya kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) tofauti na EATV ambao wanadai kupewa umiliki wa Ze Komedy Juni 30 mwaka huu.

Alisema endapo kutatokea kutoelewana kokote baada ya uamuzi wao wa kuingia mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) ambao uhamasishaji wa matangazo ulianza jana, watakwenda kumuona Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ikishindikana watafika kwa Waziri Mkuu na hatimae kwa Rais.

Hata hivyo kurushwa kwa vipindi vya kundi hilo TBC1 kutaanza baada ya wiki mbili zijazo kutokana na safari ya kundi hilo nchini Uingereza baada ya kuahirisha ya kwanza nchini Afrika Kusini kutokana na ghasia zilizokuwapo nchini humo.

Source:www.issamichuzi.blogspot
 
Something needs to be cleared hapa- nani anamiliki hili kundi? Siku zote nimekuwa najua kwamba hawa jamaa wanaingia mkataba na vituo vya TV tu , jambo ambalo halitakiwi liingiliane na umiliki.
 
mambo hayo baadhi ya wakati wajanja wanapenda kuwaonea wanyonge na hasa shule ikiwa ndogo


...kabisaa!!!

imagine hata Masanja hatakiwi kulitumia jina la "masanja", soon JOTI naye atakatazwa kutumia manjonjo ya ki "JOTI JOTI",

haipendezi wala haifurahishi EATV na reputation yao kung'ang'ania 'tonge' la hawa jamaa...

haipendezi!

sikuwa mshabiki wa Manji Vs Mengi saga, lakini kidogo kidogo naanza kuona "wagombanapo mafahari wawili nyasi ndizo ziumiazo!"
 

...kabisaa!!!

imagine hata Masanja hatakiwi kulitumia jina la "masanja", soon JOTI naye atakatazwa kutumia manjonjo ya ki "JOTI JOTI",

haipendezi wala haifurahishi EATV na reputation yao kung'ang'ania 'tonge' la hawa jamaa...

haipendezi!

sikuwa mshabiki wa Manji Vs Mengi saga, lakini kidogo kidogo naanza kuona "wagombanapo mafahari wawili nyasi ndizo ziumiazo!"
Hapo ndio na mie nashangaa aisee hwa EATV naona wanataka kuchukua advantage kwa hawa jamaa ili kuendeleza chuki ya Mengi na Manji.
Mfano Joti namjua akitumia jina lake toka kitambo hata hawajaanzisha kundi la Ze comedy.Masanja vile vile Mpoki nae na wengine.

Sasa jina gani hawa EATV wanataka wasilitumie hawa jamaa? ni hili Ze comedy au majina yao ya kisanii? Alafu pia nakumbuka kuwa hii Ze comedy haikuanzishwa na EATV bali walijianzishia toka mtaani wanakojua wenyewe then wakaonwa na EATV.

Aisee! yaani na style ya shtua ya JOTI aiache?
 
hahhahah eatv ovyooooooo
eti joti naye aacha kusema kudadadekiiiiii!!!
they shud fikiria mbali zaidi hawa eatv as so far wanazidi ku prove hw stupid they are!!n kuzidi kuwapa jina ze komedy!
 
..............kwa kweli mengi hapa kazidiwa kete na manji .....YAANI PAMOJA NA HAWA VIJANA KUMUINGIZIA MENGI MAMILIONI....HAJAPATA KUWAPELEKA HAATA NAIROBI!!!!....ALIKUWA ANAWAMINYA SANA ...WAKATI AMEFAIDIKA SANA NA PESA ZA MATANGAZO YA BIASHARA MBALI MBALI....SASA NINI NAIROBI ...VIJANA WAMEPIGWA KWA MAMA ...NA MANJI.....

KWA HILI MANJI KAMPIGA BAO NYUMA MENGI...KUGEUKA TU KUMPA KISOGO! GOLI!
 
kosa kubwa walilolifanya ZeComedy ni kutokujiandikisha kama kundi binafsi na kuingia mkataba mpya na EATV. Kazi yao ya uigizaji kama "Ze Comedy" haikuanza nje ya EATV na walikusanywa ndani na kwa kutumia resources za EATV.

Wanachoweza kufanya na ambacho hata wakienda mahakamani wanaweza kuonewa huruma ni kwa Manji na hiyo TV nyingine to buy rights (aidha ziwe exclusive toka kwa EATV).

Lakini kusema walikuwa waigizaji kabla ni kujidanganya. There was no "Ze Comedy" nje ya EATV unless kama wataweza kuonesha kuwa walikuwa wanatumia jina hilo kabla ya kuanza kuwa kwenye EATV au walikuwa wameandikishwa kisheria kama kundi hilo kabla ya kuanza kuonekana kuwa kwenye Luninga.

Nadhani Manji alidhani amemzidi kete Mengi.. kumbe kazungukwa.. vyombo vya habari vina umiliiki wa kazi zake original.
 
Mbona JamboForums imebadilika na kuwa JamiiForums kwa mambo hayo hayo ya copyright lakini wembe ni ule ule?

Kama wameshikwa pabaya wabadili jina, mwendo mdundo!
 
Kwani ze Comedy ni jina la kikundi au la kipindi?
Kama ni jina la kipindi basi EATV watakuwa na haki nalo, ila iwapo ni jina la kikundi kilichosajiliwa basi wanaondoka na jina lao.
Majina ya waigizaji kama Joti, Masanja n.k hayamilikiwi na EATV.
 
Kwani ze Comedy ni jina la kikundi au la kipindi?
Kama ni jina la kipindi basi EATV watakuwa na haki nalo, ila iwapo ni jina la kikundi kilichosajiliwa basi wanaondoka na jina lao.
Majina ya waigizaji kama Joti, Masanja n.k hayamilikiwi na EATV.

All of this should be in the contract.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom