Zawadi ya ngono

kuna binti alikuwa kaajiliwa kwenye ofisi ya kaka wa rafiki yangu ambaye ni agent washirika la ndege sasa akaja jamaa yye kaajiliwa kwenye kampuni ya ndege akamwambia yan mrembo kama ww umeajiliwa na agent acha kazi uje ofsin kwetu tuna nafasi binti kwa tamaa kaacha kazi siku hiyo hiyo jamaa kamtoa chakula cha jioni alafu akamwomba mambo flan.

binti katoa afu kamwambia aje asubuhi ofsin kwao. binti kwenda pale kakuta walushaajiri mtu jana yake na hiyo siku ndo kaanza kazi.
 
kukosa competencies, confidence, self control, self valuation na mengine yanayofanana na hayo huchangia sana kwa kushamiri kwa rushwa ya ngono. Yapaswa wanaofanya hivyo wajue thamani ya miili yao maana wengine hujirahisisha na wakati mwingine favour yenyewe hawaipati. Mfano ni kama wanafunzi wa vyuo vikuu amboa wanajirahisisha kwa ma-lecturers ili wapewe marks hususani kwa yale masomo magumu, au wakati wa kutafuta kazi mdada au mwanamke anapeleka CV yake kwa boss anammega na CV anaitupa na ikifikia kuulizia siku ya interview anaambiwa hakupita kwenye selection.
 
kuna binti alikuwa kaajiliwa kwenye ofisi ya kaka wa rafiki yangu ambaye ni agent washirika la ndege sasa akaja jamaa yye kaajiliwa kwenye kampuni ya ndege akamwambia yan mrembo kama ww umeajiliwa na agent acha kazi uje ofsin kwetu tuna nafasi binti kwa tamaa kaacha kazi siku hiyo hiyo jamaa kamtoa chakula cha jioni alafu akamwomba mambo flan.

binti katoa afu kamwambia aje asubuhi ofsin kwao. binti kwenda pale kakuta walushaajiri mtu jana yake na hiyo siku ndo kaanza kazi.

inasikitisha usikute na ukimwi kapewa
 
Hapo namba 4, inaweza husika au la, maana mtu anaweza patiwa malezi mema lakini anapofikia umri wa kujiamlia ndipo huanza kuja na hayo ya kutaka asivyoviweza kwa kutumia rushwa na hata kujiuza mwili wake ili afanikiwe kwenye hitaji lake, na wengine hutumia njia hizi hata kama anavigezo vyote, kukosa kujiamini na kutokua na msimsmo ktk maamuzi
 
Bongo lala haliwezi kulead familia,,,ukishaanza kubebwa hutaweza hata kufikiria anything and solve challenging life ahead
 
Baada ya majadiliano na rafiki yangu kuhusiana na rushwa (zawadi) ya ngono mashuleni, vyuoni na maofisini nimejikuta najiuliza maswali mengi ambayo ningependa tusaidiane kuyajibu kwasababu kwa namna moja ama nyingine matokeo yake yanaathiri hata mahusiano, ndoa na malezi.

Kwanza ni wazi kabisa kwamba mtu akishaanza ni ngumu kuacha kutokana na ukweli kwamba anakuwa amejipa ukilema wa aina fulani. Kwamba kama alifaulishwa sekondari kuna nafasi kubwa atahitaji kufaulishwa chuoni, na akifaulishwa chuoni kuna nafasi kubwa atahitaji kubebwa pale atakapokuwa kwenye mchakato wa kupata kazi na baadae kwenye kujiendeleza (kupandishwa cheo, kupata nafasi za masomo, kushirikishwa kwenye semina zinazolipa n.k).

Sasa, Je:-

1. Mtu anapoanza kuhonga mwili wake ili afanyiwe kazi yake (kusoma, kuwa na CV kali, good work ethics, experience n.k) kwanini anafanya hivyo? Ni kutojiamini (mwenyewe siwezi) au ni kuzungukwa na watu wasio na imani nae (wazazi, ndugu na jamaa wasioisha kumwambia hatofika popote)?

2. Je, kuna hatari gani mtu kutegemea mwili wake badala ya akili na uwezo unaohitajika kupata kazi, kufaulu n.k?

3. Mtu kama huyu akija kuwa mzazi atakuwaje? Ataweza kumfundisha mtoto wake kuwa tofauti na alivyo yeye?

4. Malezi yanachangia vipi kuwafanya ndugu zetu wawe hivyo?

Najua kwa kiasi kikubwa hata system yetu (kupeana kazi kwa kujuana bila kujali sana uwezo wa kazi) inachangia kwa kiasi kikubwa, maana isingekuwa inaruhusu ingekuwa ngumu kutoa na kupokea rushwa ya aina hii ila napenda kuangalia kile kinachowasukuma wahusika zaidi.
Hii inawahusu jinsia Ke
 
Cant even thnk 'bt it. Kwangu itakua km kula haram, kuchuma haram.
Muhm kujiamini tu. Ndo mana hatuendelei, utakuta mtu hata haqualify lkn anapeta kuliko mwenye uwezo. Mungu awalaani wote wanaotoa na kula rushwa especially hii ya ngono kwani wanizibia rizk wenziwao. Ameen
Its not about kuziba riziki ila yote haya yanasababishwa na maisha magumu tu. Nchi haina mifumo ya kujali raia kila kitu ni lazma ujipambanie haswa ndio utoboe. The weak hearted ones hutumia shortcuts kama hizo kufikia malengo so tusiwalaumu sana.
 
Ah, kumbe unazungumzia "zawadi"!? Sasa mtu ukipewa zaidi si huwa tunapokea? Tunakataa kupokea rushwa, lakini zawadi tunapokea. Zawadi si kama tips?
Zawadi ni Takrima😂 sio rushwa.

Tofauti ya Rushwa na Takrima ni namna ambavyo inakuwa induced.

Ikiwa mtu atatoa kitu kwa hiari yake kama shukurani hio si rushwa ni Takrima. Hii ni kama mtu kutoa Tip.

Ikiwa mtu atapewa condition kwamba ili upate au ufanikishe jambo lako toa kiasi flani au twende lodge hio ni rushwa without a doubt.
 
Back
Top Bottom