zanzibar.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,063
115,462
kila siku huwa najiuliza..
hivi kila mwembe zanzibar umepewa jina?if so why?
yani kuna vitongoji zadi ya kumi
ambavyo vinaitwa
mwembe fulani..

mfano
mwembe mimba
mwembe ladu
mwembe tayari
mwembe madafu na kendelea.

swali langu ni je kuna siri gani iliyopelekea
kuwa hivi??kuna mtu anaejua historia yeyote
kuhusu hili?
 
Mkuu hayo yote cha mtoto tu.
Kuna:
Legeza mwendo
Mchamba wima
Dole
Makunduchi
Mgeni haji
Kilimanyege(barabara ya kuendea Matemwe hiyo...usiseme umekuja Unguja kama hujapitishwa barabara hii,ndiyo bara bara hii Mzee Karume alimpitisha Nyerere akawa anajisikia raha na mshawasha...akamuuliza Mzee karume "...ni nini hii..." Karume akamjibu kwa ile sauti yake ya kibashabasha..."...kilimanyege hicho..." safari iliendelea.
Pemba ndo utakoma mwenyewe kwa majina ya kiasili ya kupendeza hakuna Broklyn na washington huko, huko kuna:
Wambaa
Mzambarautakau
Kiuyumaziwan'gombe
Jadida(wete hapo)
chokocho
Rasi Uso wa membe(hapo hata Mlima kilimanjaro utauwona uleeeee)
Mengi tu na maana ya majina hayo yatafuatia subirini.
 
Hivi kwanini Mwembenjugu ulikatwa? Je eneo hilo bado lina sifa ya kuendelea kuitwa M'njugu?
 
Mkuu umepandwa mwengine...mikwaju ilikuwa haishi msikitini pale na wakaazi wa jirani walijikuta wakilala na vitu vya ajabu ajabu na ajali barabara ya Magomeni kuelekea Jan'gombe zilikuwa hazishi yaani hushangai Mkuu, gari la n'gombe linapinduwa daladala..."wataalam wa sayansi ya uswahili" wakaja na "teknolojia" kwa njia ya hadhari, wakawaambia watu...kuwa wamebomoa "ghorofa la watu" wenyewe hawana pa kukaa..ndo maana wamehamia majumba ya watu na waliobaki wanatembeza bakora msikitini pale...na ajali hazishi...wakakubaliana "lijengwe ghorofa jingine" na sasa ukipita pale unastawi vizuri tu.
Sawa na Mfenesi Mazizi (si unakumbuka KULI na Adam Shafi) mtaa ulikuwa haukaliki wanakufa watoto wachanga vikongwe vina "ukaba" kama kawa, "wataalamu" kama wale wa Mw'njugu, wakapendekeza mfenesi mazizi upandwe mwengine...na hali imekuwa shwari sasa...watoto wanakuwa vizuri...vijana wanacheza mpira hapo hapo sasa.
 
Acha uongo wewe! mara ya mwisho ulikwenda lini zbar. Huo mwembe umeshakatwa na hapana hata muarubaini
 
Kama ni hivyo ni bora kurudisha Mfereji wima, kwani kwenye ile junction ajali nazo hazikauki..
 
Mkuu umepandwa mwengine...mikwaju ilikuwa haishi msikitini pale na wakaazi wa jirani walijikuta wakilala na vitu vya ajabu ajabu na ajali barabara ya Magomeni kuelekea Jan'gombe zilikuwa hazishi yaani hushangai Mkuu, gari la n'gombe linapinduwa daladala..."wataalam wa sayansi ya uswahili" wakaja na "teknolojia" kwa njia ya hadhari, wakawaambia watu...kuwa wamebomoa "ghorofa la watu" wenyewe hawana pa kukaa..ndo maana wamehamia majumba ya watu na waliobaki wanatembeza bakora msikitini pale...na ajali hazishi...wakakubaliana "lijengwe ghorofa jingine" na sasa ukipita pale unastawi vizuri tu.
Sawa na Mfenesi Mazizi (si unakumbuka KULI na Adam Shafi) mtaa ulikuwa haukaliki wanakufa watoto wachanga vikongwe vina "ukaba" kama kawa, "wataalamu" kama wale wa Mw'njugu, wakapendekeza mfenesi mazizi upandwe mwengine...na hali imekuwa shwari sasa...watoto wanakuwa vizuri...vijana wanacheza mpira hapo hapo sasa.

Hivi waliukata ule mfenesi pale mbele ya Branchi ya (Gulioni )ilikuwa ya ASP kabla haijabadilishwa na ikaitwa branch ya CCM ,mzee wetu Aboud Jumbe alituwekea TVz pale watoto na watu wazima tulikuwa tunakwenda kuangalia hizo zilikuwa siku za nema siku za arba fogo wali pesa mbili na watu zanzibar walikuwa naimani za utu leo wapi visiwa vimeingizwa NAJIS kubwa.
 
Ule Mfenesi wenye mazizi makubwa haupo umekatwa...saivi pamepandwa mwengine palepale ulipokuwa ule wa awali na unastawi vizuri tu...umenikumbusha enzi zangu pale madrasa za Maalim Imam RIP na Maalim Bi.Afua zote zikipakana na Msikiti wa Simba mpaka leo zipo ila msikiti ulibomolewa na kujengwa upya...kuna Mzee(khamis kibatari,RIP) aliyekuwa mwazini mwenye sauti kali akiadhini bila ya bomba sauti yake unaisikia mpaka Mwembeladu na Mbuyutaifa...hata waadhini wa misikiti ya Salum Makka na Kwabiziredi wakimsubiri Kibatari amalize ndo waanze wao...saivi wapi?
vijana wapo na bongo flava upuuuzi mtupu...mjini.
 
mwembe lukunda na hata kule mafichoni Mwembe mchomeke.
We Balubalu Ni Muembe Rikunda. Kwani wewe ulishawahi kufika Mwembe-Mchomeke? Huko unatakiwa uwe Ngangari kweli! Ukizubaa- basi. Kama utapapatikia lile jambo bila indhari utaishia kama Mwembe unavyosema.
 
bila kusahau mwembe dezo pale maeneo ya magomeni, hapo ukikatisha na kivespa unaombwa lifti. kidongo chekundu HQ ya wenye akili nyingi.
 
Jamani na hii 'KUNDUCHI' aka *****-UCHI' kwa nn ikaitwa hivi!
Nasikia pia kuna 'MCHAMBA WIMA'. Haya utachambaje huku umesimama (wima)! Lol!
 
hahaa kweli mtu kwao mie sina mbavu majina mara bububu, mara fuoni mara kizimkazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom