Zanzibar yagoma kulipa Sh40 bilioni Tanesco

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
shamuhuna.jpg


Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekataa kulipa deni la umeme la Sh 40 bilioni kwa TANESCO baada ya kupandishiwa kiwango.Waziri wa Ardhi, Maji, Makazi na Nishati wa Zanzibar , Ali Juma Shamuhuma alisema baada ya kiwango kuongezeka, serikali ya Mapinduzi Zanzibar inatakiwa kulipa kwa asilimia 168 badala ya asilimia 21 kwa uniti.

Shamhuna alikuwa akichangia katika majumuisho ya mjadala juu ya ripoti ya Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo Shamuhuna alisema, "hatukubali kulipa deni la Sh 40 bilioni kwa kiwango cha asilimia 168 asilani."

Tanesco ilipandisha viwango vya malipo kwa wateja wake tangu mwaka jana kwa asilimia 21, kwa upande wa Tanzania bara ambapo kwa Zanzibar shirika hilo la umeme limepandishwa kwa asilimia 168 na kusababisha malalamiko makubwakutoka kwa wateja.Shamhuna alisema kuendelea kwa Tanesco kudai deni hilo kunakwenda kinyume na agizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba pande zote mbili za Muungano zilipe viwango sawa vya asilimia 21.

Waziri huyo ambaye alikuwa akichangia na kupigiwa makofi na wajumbe wengine alisema ili kuepukana na utegemezi wa umeme kutoka Tanesco ambao unaigharimu SMZ fedha nyingi, serikali umeanza kuchukua hatua za kuzungumza na wawekezaji wazoefu ili kuzalisha umeme kutokana na jua na gesi utakaojitegemea.

Shamhuna aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba mradi kama huu umefanikiwa Dubai na Malaysia unaweza kuzalisha kati ya Megawati 50 na 100 ambao unatosheleza mahitaji ya sasa ya Zanzibar ya Megawati 50.



Hata hivyo, akizungumzia kuhusu madai ya baadhi ya Wajumbe wa baraza la Wawakilishi wanaotaka Zanzibar izalishe umeme kwa kutumia mawimbi ya bahari, Shamhuna alisema utafiti unaonyesha kuwa ni mradi mkubwa wenye gharama kubwa na pia haujafanikiwa katika nchi nyingi duniani.

wakichangia mjadala huo wajumbe wengine wa baraza hilo wamesema suala hilo linahitaji kuangalia vyema na serikali ya muungano kwani haiwezekani serikali hiyo kukaa kimya na baadhi yao kutaka fedha hizo kutolipwa kwani haitowezekana
 
Usishangae sana Mkuu, hawa Zenj siasa yao ya Nje/Muungano ni changu changu, chako chetu.
 
Nakumbuka wakati wa Nyerere walikuwa hawalipi hata kidogo
 
Hizo ndizo faida za muungano, mkijitenga kama mnavyolazimisha mtapata wapi jeuri ya kugoma kulipa?
 
Nadhani kabla ya kuendelea kuwalaumu tungeangalia "uhalali na ukweli wa Zanzibar kutakiwa kulipa 168% wakati TBara ni 21%"
 
Back
Top Bottom