Zanzibar will not sustain itself without Union –Sitta: Says currently Mainland meets most of cost in

Nje ya muungano Zanzibar ni Somalia nyingine.

MKUU ULISAHAU KAMA ZANZIBAR NI MOJA YA NCHI ZILIZOPEWA HESHIMA KUBWA NA UNITED NATION 1962 KWA KUWA NA AMANI NZURI!!! KABLA YA BABA WETU WA TAIFA LA TANGANYIKA NYERERE NA MAFIA WENZAKE KUPANGA DEAL NA KUFANYA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA AGENDA YA TANGANYIKA YETU:grouphug:
 
Muungano ni mzuri pale nchi zilizoungana zikanufaika na Muungano. Ila nina mashaka na huu muungano uliopelekea likatokea jina la TANZANIA. Kwa uelewa wangu, Tanganyika haipo tena kama nchi lakini Zanzibar inatambulika kama nchi, kwa nini? Kwa kuwa kuna nchi ya Zanzibar basi na nchi yetu ile ya mwaka 1961 ambayo ni Tanganyika iwepo. Hakuna muungano wenye Serikali mbili. Kama Zanzibar wana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) na iwepo Serikali ya Watu wa Tanganyika(SWT) na iwepo Serikali ya Muungano wa Tanzania(SMT). Kama haiwezekani basi tuwe na chaguo moja, kuutengua Muungano au Zanzibar iwe mkoa kama ilivyo mikoa mingine. Kuna nchi kama Marekani ni muungano wa nchi nyingi lakini wana Serikali moja. Ina onekana Watanganyika hatupendi kujitegemea. Historia inaeleza kwamba: muungano huu ulikuwa ni mwanzo wa kuunganisha nchi za Afrika na kuwa moja, jambo ambalo lilishindikana. Jamani Zanzibar ni nchi iliyojipatia Uhuru mwaka 1963 tuiache iwe huru. Kung'ang'ania Muungano uwepo wakati pande ya pili(Zanzibar) haitaki,hapo katikati kuna jambo limejificha. Nina mashaka na muungano wa vyama vya siasa: TANU( Tanyanyika African National Union) na ASP( Afro Shiraz Party) cha Zanzibar. Vyama hivi vya Siasa vilipelekea kuzaliwa CCM (Chama Cha Mapinduzi) mwaka 1977. Ndio maana linapoibuka suala la muungano Bungeni, wabunge wengi wa CCM wanajaribu kulikingia kifua. Hili linadhihirisha kwamba hawataki kuona CCM ikivunjika, ndio maana wana-CCM hawapo tayari kuona Zanzibar ikijitenga.
 
Sikubaliani na Sita, Zanzibar nje ya muungano itasitawi sana kwa sababu zifuatzo;
1.Wazanzibari hawana hulka ya ufisadi kama wenzao wa bara, angalia hata viongozi kwenye serekali wale wa zanzabar hakuna anayetajwa kwenye ufisadi.
2.Zanzibar ina rasilimali nyingi kama mafuta, karafuu, fukwe murua zinazovutia watalii, na uzoefu wa biashara ya kimataifa miongoni mwa wazanzibari wengi
Hivyo iacheni Zanzibar ipewe uhuru wake wenye kutamani kufisadi mafuta ya Zanzibar watafute kitu kingine huko kwao Tanganyika.
 
Hizi habari zinazungumziwa sana humu. La msingi ni Constitutional Assembly and referendum. Na hio Constitutional Assembly iwe na wajumbe sawa in terms of idadi from Tanganyika and Zanziabr. Na hio referendum, ipigiwe kura za mapendekezo Zanzibar na Tanganyika separately. Tupate maoni ya wananchi
 
Wabunge wa zanzibar na wawakilishi wanasemaje au wamefyata ? maana kawaeleza ukweli kama hawataki basi tuvunje. Sasa utasikia watakaa kimia.
 
Na Miaka 5 au 10 ijayo Tanganyika haitakuwa kama miaka ya 60, 70 au 80 ambapo ilikuwa haina pesa za maendeleo, inaonekana kuwa Oil and GAS itapatikana kwa wingi, Nchi nyingi sana zitataka uhusiano na Tanganyika na sio kuikimbia.
 
kelele zote za nini? Sita kasema bila kumung'unya maneno, uwezo wenu mdogo saana, kama hamtaki tuvunje sasa kama kweli wabunge wa Zanzibar ni jabali si wangetoka majengoni? wawakilishi nao kimi huko kwenye kakiota kao. Wazanzibar mnapenda mno kubebwa kama nyumba ndogo, safari hambembellezwi ng'o mziki moja tu, hamtaki maamuzi ya bara basi nendeni. Watu hata hamjui mnachoongelea, uchumi wa Zanzibar haufikii hata nusu ya uchumi wa wilaya ya Kahama peke yake.
Watu mnashinda mmevaa taulo hamfanyi kazi leo mnasema bara inawanyonya.
 
Pamoja na kwamba quality ya picha ni siyo nzuri nadhani ina weusi wachache au hamna kabisa, sishangai kwa nini mapinduzi yalikuwa ni lazima kwa watu asilia. Wenye kelele za kuvunja muungano ni wale wale wanaotaka kurudisha hali ilivyokuwa kabla ya mapinduzi. Watanganyika tunajua zanzibar ni mzigo kwetu lakini tutakuwa tumewasaliti waafrika wenzetu kama tutawaacha mikononi mwa mafedhuli. Zanzibar ipo afrika kwa manufaa ya waafrika period!!!

Mkuu hayo sio kweli kwani mfano mdogo wakati wa mjadala wa hivi karibuni wa Mswada wa Marekebisho ya Katiba, waliokuwa mstari wa mbele ni pamoja na Mawaziri, Watendaji Wakuu wa Serikali, Waasisi na Makamanda Wakuu wastaafu wa JWTZ ambao takriban wote ni CCM

Mmoja ni Mzee Hassan Nassor Moyo ambae tabaan unajua alikua nani ndani ya ASP, CCM, SMZ na SMT.

Mwengine ni Mheshimiwa Mansour Yuuf Himid, Waziri wa SMZ na Mjumbe wa NEC ya CCM. Pia ni mtoto wa Brigadier Yusuf Himid aliekuwa Kamanda wa JLU (Jeshi la Ukombozi) na katika Commitee of 14, walioandaa Mapinduzi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia alikuwa mstari wa mbele.

Huko nyuma, Wazanzibari waligawanyika sana kutokana na fitna za Nyerere, lakini likija suala la Utaifa wao utashangaa.
 
Ah! makaimati wee, hapo kwenye red kuna baalawy asiye mwarabu kweli au?


Huo ndio ukweli kwani Pemba kuna watu kabila lao ni Baalawy na wengine Bahassan. Hawa kwa kweli si Waarabu bali wanaitwa au kujiita Masharifu. Una mengi ya kujifunza Mkuu.

Tena katika hao Masharifu, mmoja wao amefariki leo na tumemzika jioni.
 
Mr Dash Dr Idarous Baalawy, Mohammed Shamte, Rashid Hamadi na Mkamandume ni Wapemba safi, Ali Muhsin ni Muarabu aliyechanganya na Mmanyema,Juma Aley sina uhakika ila alikuwa mweusi ti, Ibuni Saleh na Maulid Mshangama ni Wangazija - Comorians, Ameir Tajo ni Mmakunduchi na Amirali Abdurrasul ni Muhindi. Sasa hapo la ajabu lilikuwa lipi.

Kama ni Wahindi na Machotara hata Cabinet ya Tanganyika walikuwepo akina Bryecon (mzungu), Amir Jamal (Muhindi) Julie Manning (chotara). Hata Secretary wa Nyerere alikuwa Mzungu

Mkuu wako Waarabu weusi kama wale wa Saudia. Huyu ni graduate wa Oxford University na alikuwa akisema Kiingereza, huwezi amini kuwa ni Mzanzibari. Pia alikuwa bingwa wa kujulikana wa mchezo wa cricket.
 
Zanzibar na wanzanzibar ni parasites tu,muungano hauna faida kwa wabara ni mzigo.
 
Simwelewi Sitta kitu kimoja, ok, Zanzibar wanapata umeme bure, kwa hiyo ni faida ya Muungano kwa Zanzibar. Na sisi tunapata nini bure kutoka Zanzibar, karafuu?

Sitta ni mtu mzima mwenzangu na siwezi kumwita muongo lakini ntasema hasemi kweli.

Hizo 50bn/= sio deni Mkuu, bali rushwa kwa viongozi wetu wasivunje "muungano" kwa faida yao wanaofaidi.
 
Na Miaka 5 au 10 ijayo Tanganyika haitakuwa kama miaka ya 60, 70 au 80 ambapo ilikuwa haina pesa za maendeleo, inaonekana kuwa Oil and GAS itapatikana kwa wingi, Nchi nyingi sana zitataka uhusiano na Tanganyika na sio kuikimbia.


Hata sasa Mkuu, Tanganyika sio maskini, watu wake ndio maskini. Hushangai hili?

Ukweli ni kwamba viongozi wao wanaiuza nchi yao na wameshaifisidi nchi yao kwa kuendekeza ufisadi.

Wanataka wazame na Zanzibar lakini tumeshashtuka.

Hata ikiwa kila Wilaya yao itatoa mafuta na gesi, kwa uongozi walionao, watadidimia katika lindi la umakini tu.
 
Mkuu ni kweli nakiri kuwa picha imekosa ubora wa kutosha.

Pili nataka uelewe kuwa kabla ya kuundwa cabinet hio YA coalitian government, Shamte alimtaka Karume waunde GNU. Kwa kushawishiwa na Nyerere, Karume alikataa, kumbe walishapanga kuipindua mwezi mmoja baadae.

Tatu naomba ujue kuwa Zanzibar is a multi ethnic society na hao unaowaona wote ni Wazanzibari wa asili mbalimbali na cabinet ilikuwa very representative.


Nakuomba usihadalike na hivyo vilemba au rangi, iwe ya picha au ya ngozi Mkuu .

Cabinet ilikuwa na watu hawa:

Seated from left are: Dr. Idarus Baalawy, Ali Muhsin (died March 20, 2006), Mohamed Shamte, Juma Alley and Ibuni Saleh. Standing from left are: Sheikh Ameir Tajo, Amirali Abdulrasul, Rashid hamadi, Omar Hamad (Mkamandume) and Maulid Mshangama

Tafakari haya kwanza Mkuu kwa leo.

Mkaimati, naomba usiuahadae umati wa JF kwa picha tu!
The basic conflict katika mahusiano ya wazanzibari ni kati ya utawala wa waarabu na waafrika wanyonge.
Ukisema walikuwa wamoja ni uongo, maana hapangekuwapo na haja ya mapinduzi.
Na ni ukweli usiopingika kuwa waliouwawa kwa idadi kubwa wakati wa mapinduzi ni waarabu.
Na hii haikuwa by accident, ilikuwa kupindua the status quo.
Pich uilyoionyesha ni ya vibaraka wachache walionunuliwa na waarabu ili wakidhi haja zao za kisiasa.
Hebu tutajie hao waaafrika wachache waliokuwa katika cabinet ya 1963, leo wako wapi?
Bila ku address the reasons for the revolution , kwa Zanzibar , this is bound to happen again.
 
[h=1][/h]Written by Hassan10 // 11/07/2011 // Habari // No comments

Sitta avaa (?) kinga wakati kachaingia mimba.

Mimi nilishangazwa sana kumuona Samul Sitta akijiona Hiro kumbe shushu lakufutia mavi, na huku wenzake wakimpigia makofi haliyakuwa anawaaibisha na kuwazalilisha, Jee Wzanzibar muko tayari kana na kuikataa Zanzibar yenu?.
Sita asema ikirudi tena Tanganyika nibora Muungano uvunjike,ok jalia Muungano umevunjika Sita utajita Mtanzania au Mtangatanga?. sasa chakushangaza kwa ni kawaida ya muungano si kuanzia nchi mbili na kuendelea? Jee Sita huoni ufahari kujita M-Tanganyika kuliko M-Tanzania?.
Tanganyika ina samani zaidi kwakokama hujuwi Sita kuliko Tanzania ambayo imekuja from no where? ama kweli wewe sie na wote Wa-Bara wenzako waliokuunga mkono, wahiari kuza utu wa nchi yao yenu na historia ya Babu zenu na Bibi zenu na asili zenu kwasababu ya kukumbadia Zanzibar isiwatoke.
Mimi naona Mumekula hasara Sita na wenzako wote, unajaribu kuvaa kinga lakini mimba imeshaingia, hivi sasa huna vyakuwaeleza Wzanzibar kuhusu Muungano, Muungano ni fake na haukubaliki katika generation ya sasa tokea kufa kwa Tanganyika Muungano ndio ulipo kufa kinacho fanyika hivi sasa Zanzibar nikuwalazimicha viongozi wa ccm/smz wawatii na kuwa karibu na chama na sera lakini tusidanganyane Muungano haupo Zanzibar umesha vunjika Zamanii.
Kwa hio kama sita unasema mfumo wa Serekali tatu siwo basi ndio kitanzi cha Muungano kufa foroho, maana hao ccm/smz wawadanganya tu,lakini ukweli ulopo washachoka kuburuzwa kwa nguvu ya chama na kulazimishwa ku-sacrify mambo yasio ya Muungano wala chama. huwa hawawambii kweli tu huwahashua na nyiyi mukahashukwa, kifupi wamesha washtukizia kuwa lengo lenu baya, sikiliza BLW litakupa jibu la Wzanzibar?.
Hivi sasa chini ya Serekali ya GNU ambayo kikatiba ni ya Muungano wa Wzanzibar basi mumekwicha, mutashezea madongo mpaka mutajuwa kama mpoga kitoweo au majani.
 
Tunachobishana hapa ni kipi haswa. Alosema Siita au Mapinduzi ya Zanzibar!

Zanzibar inaweza kabisa kusimama pekee Kiuchumi, na hizi hadithi za kusema Bara tunalipia kila kitu ni fujo za kisiasa tu kwani walitaka Zanzibar wajilipie wakakataa? maana Zanzibar wakijilipia matumizi yao ndio kuwa huru huko wanakokukataa kwa hiyo hizi hadithi na vipande vya siasa za majitaka hazifai.

Mzee Sitta anajua fika kwamba baraza la Mapinduzi hawatataka kabisa kuona Muungano unavunjika ila wengi ni wanafiki wanapokuwa na Wazanzibar hujigamba kusimamia maslahi yao wakati ndio wao wanaokwamisha hata kura za maoni ya wananchi. Kama kweli walikuwa wanajali haya kwa nini wasifanye hivyo badala yake wakapitisha kura za maoni kuunda serikali ya mseto!

Nilisema wazi mpango wa serikali ya mseto ulikuwa wa kisiasa kuwapa viongozi nafasi za kutawala na bunge lilokwisha hadithi kubwa ilikuwa kila mtu anataka kupewa nafasi ya kuongoza. Hoja kubwa za wanawake ni kuongezwa bungeni hata bila kusema wanawakilisha kitu gani. Zanzibar nako wanataka hesabu sawa ya viongozi serikalini wasiwe wabara watupu.. yaani hakuna hata siku moja viongozi wameweka maslahi ya Watanzania mbele.

Hivyo Wazanzibar kwa kutofahamu wakaupanda mkenge, wkafurahiu sana kwamba wanarudisha utaifa wao kwa kuunda serikali ya mseto, sijui kama walielewa maana yake. Leo tena Wazanzibar wanataka kuvunja Muungano ili hali wamekubali kwa maandishi na mkataba wazi ulowekwa sahihi na wanasheria kuunda serikali ya mseto kuwa ndio njia pekee ya kuwaunganisha Wazanzibar. jamani unapoungana na CCM tayari umeihusisha bara na maadam makao makuu yako bara tayari umejifunga ktk kudumisha Muungano.

Adui mkubwa wa maendeleo nchini ni CCM na ajabu nilidhania Wazanzibar wajanja lakini nilikuja choka walipoingia Muafaka na CCM hata kabla ya uchaguzi mkuu for what mlipiga kura zenu!. Seif akakubali kushindwa na Shein hali akijua fika kwamba ameshinda uchaguzi tena kwa kura nyingi! - Haya siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama CCM kama sikosei, nikamwona Shein akisoma ilani ya chama kwa maendeleo ya Zanzibar na viongozi wote wa CUF na CCM wakakabidhiwa vijitabu vya kijani!... I mean Muislaam kapewa biblia mkononi ili kufanya ibada zake kisha bado unadai nyie waislaam? wakisema CDM mnawakana hali misalaba mmeivaa..

Jamaa zangu Wazanzibar, tuache maneno ya Sitta mbali kabisa. Wazanzibar na Wabara wote tumekosa viongozi bora. Viongozi wetu wameshindwa kuwa wazalendo na wagumu sana wa kuwa responsible maanake huu sio utamaduni wa mtu mweusi. Mtumwa hata siku moja hawi responsible bali kusukumwa kama punda na yalikuwa makosa makuibwa kufikiria ukimwachia punda mzigo ataufikisha! - Nitaendelea kuwaheshimu Abeid Karume na Nyerere kwa kuchukua maamuzi magumu ya Muungano na hata kuwa madikteta wenye nia njema! Aloyafanya Karume na Nyerere hakuna kiongozi ameyafanya na pengine hatakuja kiongozi mwingine kuwafunika!
 
Sielewi kabisa kwanini wanaotaka Muungano uvunjike hawatoki kwanza Bungeni na kwenye Baraza la Wawakilishi na kuanzisha movement ya kutaka Muungano uvunjike? Walikula kiapo kulinda Katiba hii na Muungano huu sasa wanapata wapi ujasiri wa kutaka Muungano uvunjwe? Au waliapa hawakujua wanachoapa ni kitu gani?
 
Sielewi kabisa kwanini wanaotaka Muungano uvunjike hawatoki kwanza Bungeni na kwenye Baraza la Wawakilishi na kuanzisha movement ya kutaka Muungano uvunjike? Walikula kiapo kulinda Katiba hii na Muungano huu sasa wanapata wapi ujasiri wa kutaka Muungano uvunjwe? Au waliapa hawakujua wanachoapa ni kitu gani?
tena basi wao wenyewe wamerekebisha maadhi ya ibara za katiba kuwawezesha viongozi wao kuwa na madaraka zaidi ktk Muungano sasa hili sii kujifunga ktk Muungano zaidi. Hawa wasitubabaishe CUF walipokuwa na CDM waliweka nia safi sana ya kuunda serikali tatu na ndio dawa. Federal government itaendelea kuwasaidia Zanzibar kwani ndio wajibu wa serikali kuu.
 
Huyu Sitta ananishangaza.

1. Mara anapinga ufisadi.
2. Mara Spika.
3. Mara Serikali.

KINYONGA HUYU
 
CUF wamvaa Sitta

*Wadai amewakebehi Wazanzibari kuhusu muungano
*Watakiwa kusimama bila ya woga kutetea nchi yao


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemvaa Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta kikimtaka aache kuwakebehi Wazanzibari kwa kauli alizotoa
bungeni kuhusiana na muungano.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Ismail Jussa Ladhu amesema wakati umefika kwa Wazanzibari kusimama kidete na bila ya woga kuitetea Zanzibar katika masuala mbalimbali ya Muungano.

Wiki iliyopita Bw. Sitta akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati akichangia bajti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, alipinga kuanzishwa kwa serikali tatu, akisema itakuwa ndio kuua muungano, kwa kuwa itahatarisha ustawi wa Zanzibar.

"Kuleta serikali tatu ni kumleta mbia wa kushindana na Zanzibar na hapo Tanganyika haitakubali, kwani wote watalazimika kuichangia serikali ya tatu na hapo haitakuwa na meno ... kwa sababu ya Muungano, Zanzibar inauziwa umeme kwa bei ndogo na sasa tunaidai sh bilioni 50, lakini tumekaa kimya.

"Kwa akili nyepesi kutaka serikali tatu ni kuua Muungano, kama Muungano hautakiwi semeni kistaarabu tuwe na maelewano ... tuache kusema Karume (Abeid) alikuwa mbumbumbu wakati alifanya mazuri mengi kama kujenga nyumba za Michenzani," alisema.

Pia waziri huyo, alisema wakati wa mjadala wa Muungano baina ya waasisi wake, Mzee Abeid Aman Karume alikuwa anataka uwe wa serikali moja na yeye awe Makamu wa Rais, lakini Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema ikiwa hivyo Zanzibar itamezwa, hivyo akashauri ziwe serikali mbili, kama ilivyo sasa.

Kutokana na kauli hiyo, Bw. Jusa aliyeonekana kukerwa na kauli hizo za Waziri Sitta, alisema wakati huu Wazanzibari wote wanahitaji kupata haki sawa juu ya mambo yanayohusu Muungano. Alimtaka na kuwabeza Wazanzibari wakati wanaposimama kudai haki zao.

Bw. Jussa alitoa kauli hiyo jana wakati akiwahutubia wananchi na wanachama wa chama hicho Jimbo la Bububu, Wilaya ya Magharibi Unguja.

Alisema, Bw. Sita amekuwa akitoa matamshi mabaya juu ya lengo na adhima ya muungano, jambo ambalo halileti taaswira nzuri.

"Kwenye muungano huu kila nchi inapaswa kupata haki sawa na mwenzake na mambo ambayo hayamo katika muungano yanapaswa yasiingiliwe," alisema.

Alisema kuwa Marehemu Karume na Mwalimu Nyerere walitaka kuwepo na muungano wenye maslahi bora kwa pande zote mbili.

Lakini kinyume na hilo, Bw. Sitta amekuwa akibeza muungano kwa kusema mambo ambayo hayamo katika makubaliano, huku akifanya Wazanzibari kama watu wasioelewa adhima ya muungano huo.

"Huu si wakati tena wa kutudanganya, Wazanzibari wa leo tumesoma hatudanganyiki," alisema Bw. Jussa na kupigiwa makofi na wananchi waliokuwepo.

Alisema kuwa katika Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Wazanzibari wamependekeza mambo kadhaa ambayo kutoingizwa kwake kutasababisha mswada huo kutopita.

"Kama alivyosema Mzee Karume Muungano ni sawa na koti, hivyo likitubana tutalivua," alisema.

Aidha aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imechukua ahadi kuwa itasimamia kidete kuhakikisha maslahi ya Zanzibar yanalindwa.

Akijibu malalamiko ya wabunge waliochangia kuwa suala la mafuta kuwekwa kwenye Muungano baada ya kuwa na dalili ya kupatikana Zanzibar, Bw. Sitta alisema serikali ililazimika kuliingiza kwenye Muungano, baada ya kubainika kuna uwezekano wa kupatikana mafuta baharini kwenye mpaka kati ya Tanga na Pemba.

"Hapo huwezi kujua mafuta yatapatikana wapi, hivyo kuepuka ugomvi na yasitokee kama ya Iraki na Kuwait, tukaona tuliingize kwenye Muungano," alifafanua.

Kuhusu mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 hadi 22, alisema yaliongezwa kulingana na matukio kama kulipovunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hayakuongezwa kiholela, bali Bunge lilipitisha kwa kupiga kura. Alitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni Posta na Simu; Hali ya Hewa na Ofisi ya Takwimu.

Hata hivyo, alisema, suala la elimu ya juu liliingizwa baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuiomba Serikali ya Muungano kwa barua ambayo hadi leo ipo imehifadhiwa.

Akizungumzia ushiriki wa Zanzibar kwenye masuala ya Afrika Mashariki, alisema "ushiriki wake ni wa moja kwa moja, kabla ya kwenda huwa wataalamu wa pande zote wanakutana na baadaye mawaziri tunakwenda kwenye majadiliano."

Alitaja miongoni mwa miradi ya maendeleo ya Zanzibar iliyotokana na ufadhili kupitia EAC, kuwa ni pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Karume kisiwani Pemba; bandari ya Marhubi; ujenzi wa chelezo ambapo mtu ataweza kusafiri na gari hadi Mombasa au Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom